Hatimaye Samsung na LG wasitisha kuiuzia Huawei vioo 'screen panel displays'

Ahsante kwa kunijibu.
 
Sasa pesa ya china utaifananisha na Doller?,Dollaer ni exchange standard ya dunia,so haiwezekani leo mmarekani atoke tu na kushusha pesa yake dhamani bila sababu za msingi.Mchina yeye anatake export kwa wingi ndio maana pesa yake anahakikisha inakuwa chini ya doller ya marekani as possible.Assets kibao za dunia hii ziko valued interms of USD,unatataka doller ichezewe tu kama anavyofanya mchina?.
Kipindi cha kuisha kwa vita ya korea 1953 marekani aliikalia korea ya kusini na ndio hapo mifumo ya uchumi ya kibepari ilianza kuota nchini korea na ndio hadi leo unawaona hivyo walivyo wako mbali kuliko wenzao wa North,Ile ni Amarican economic model (Ubebari) hakuna jina lingine unaweza ipa.Wafaransa,waingereza,wahindi wote hao wana uchumi wa kibebari,bepari kumpita bebari mwenzie its not a big deal,hata vidole vyako haviko sawa.
Hao wachina wenyewe wanatumia political economy,yaani serikali ya ki communist lakini uchumu unaendeshwa kwa element za kipepari,wangeng'ang'ania ma model kama yale ya Cuba na North Korea wasingekuwa hapo walipo.
 
Ni sababu ya msingi ndiyo maana uchumi wake ni mkubwa ukiwa wa pili nyuma ya USA.
Lakini pamoja na influence waliyo nayo Marekani ndani ya Korea, bado China ana uchumi mkubwa maeneo hayo na jeshi kubwa zaidi.
Kwanini unaipa America kama vile ndiye alianza kuwa na capitalized economy akiwa nchi ya kwanza mpaka uhisi mchina anamcopy Muamerika? Capitalism hakuanzia Marekani.
Kwani shida iko wapi akiwa na serikali ya Kikomunist na uchumi wa Kipebari? Kuna shida hapo, as longer as kwake ime work na kuwapita hao wote kutoka kuwa nchi tuliyokuwa nayo level sawa miaka ya 60 mpaka kuwa nchi yenye uchumi mkubwa wa pili, mbona sisi models tunazocopy haziwork?
 
Tatizo mentality ya watu imekalia kuwa USA ndio Baba wa dunia. Kama nchi zote zinakubaliana kuachana na upumbavu wake atakuwa hawara wa dunia tu.

Mbona Google na Facebook wanaiba na kuuza data za watu hadi leo na hakuna anaesema kuwa wawekewe vikwazo? Mbona USA imefumwa na ikidukua mawasiliano ya raia wake bila idhni ya wenyew na tena Snowden alivo expose wao bado waliendelea kukanusha. Mbona USA imefumwa inadukua mawasiliana ya Merkel? kwanini wasiwekewe vikwazo wao na kampuni zao? au ndio Dunia watu wake wamekubali kuwa wajing.a?

Huawei ikifa basi ni ujinga wa serikali ya china. Hii ngoma ilikuwa ichezwe tit for tit. Piga ban apple products, piga ban everything google piga ban everything USA. Nchi ina watu Bilioni 1+ hio ni big market.
 
China hana uwezo kupiga chini products za kimarekani kwa sababu ya joint Ventures na makampuni ya kichina. Makampuni mengi ya China yanategemea makampuni ya kimarekani kwa ajili ya teknolojia, mitaji na kila kitu.

Huoni sasa hivi hayo makampuni yanahama? China ingekua ndio soko la Dunia basi wasingehama. Miaka 5 ijayo makampuni mengi yatakua India ama nchi nyingine za south asia.

Kuungana kuachana na USA ni ndoto za mchana. Mfano Tanzania tuachane na USA si njaa itatuua?

Marekani angalau ni reliable, kuna clear checks and balances, sio China. Angalia isingekua ujinga wa China tusingekua tunaishi haya maisha leo. Walificha ficha sana kuhusu corona ona walipotufikisha sasa na hili ni kirusi lao.
 
Hakuna sehemu nimesema China kuwa na political economy kuna shida.
Kuhusu Korea nimekujibu kwamba ni kwa nini ana fungamano na marekani sababu mwaka 1953 ndipo misingi na direction ya uchumi wa korea vilianza.
Sisi models tulizo copy hazi work kwa sababu hatujui hasa tuko na model gani,na vile vile hatujui tuanze na kipi ili hizi model zifanye kazi vizuri.China walianza kuinvest kwenye akili za watu wake kwanza kable ya kitu chochote.sis huku hatueleweki hata kipaumbele chetu ni kipi.Tutabaki kuwa washangiliaji wa china na marekani tu mpaka hapo akili za viongozi wetu ziakaa sawa na wazitumie vizuri.
 

Hapo mwisho mzee, lawama unamtupia mchina peke yake, lakini unasahau kuwa WHO ndio ilisema kuwa virusi ivo haviambukizwi kwa njia ya hewa? Hio lab ilio originate icho kirusi kama inavokuwa alleged tunaambiwa kuwa ilikuwa ina receive funds kutoka kwa USA. Sasa kama ni kweli huoni kama na wao USA pia ni irresponsible?

Mentally hio kuwa Tanzania tuachane na USA njaa itatuua, ndio inatufanya Africa tunaendelea kuwa slaves bado. mimi nashangaa 21st century, bara limejaa utajiri wa Mafuta, madini, ardhi yenye rutba, eti tunasaidiwa chakula kutoka nje? huoni tatizo tulilokuwa nalo?

Yaani ni kama mchezo flani unachezwa hapa duniani kuaminishwa upuuzi wakati ukweli uko mbele ya macho yetu.
 
Sasa hivi kiujumla USA imeshikwa pabaya sana,kinachofuata ni kutumia ubabe wa waziwazi,ila kwa China wamechelewa sana,na akijaribu kuanzisha mkono atajuta kuzaliwa...
 
Labda tumecopy kitu ambacho hakiendan na mazingira yetu au labda tumecopy tusichokiweza
 
Hii ni katika orodha ya simu zenye camera bora sana duniani,katika hiyo list Apple iphone 11 pro max imekamata namba 14. Nadhani itapotoka iphone 12 itakuwa katika mazingira mazuri ya kuwepo katika nafasi za juu. Ingawa na makampuni mengine nayo pia soon yanaachia matoleo mapya mfano huawei mate 40 series nk,Nimejua kwanini USA ina hasira sana na Huawei... Orodha ya Simu 10 bora kwa camera
 
Hapa ndio tofauti ya china na marekani ilipo. China anafanya manufacturing sana ya bidhaa lakini ana upungufu wa technology mbalimbali zinazotumika kutengenezea hivyo vitu na hii ndio inayomcost sana, maana USA amezuia kampuni yoyote inayotumia technology yake either upande wa software au hardware kumuuzia au kumtengenezea Huawei microchips. Naona hizi flagship za huawei zitapotea maana wachina semiconductors industry zao bado haziwezi kutengeneza chips zenye manufacturing nodes chini ya 14nm wakati competitors wao wanaingia kwenye 5nm hapo itakuwa ngumu sana kushindana nao.
 
Tumzungumzie Huawei mobile ambae ana bifu na USA. China wamepatwa na changamoto sana
 
Tumzungumzie Huawei mobile ambae ana bifu na USA. China wamepatwa na changamoto sana
Ofcourse kampuni yoyote ingepata changamoto, maana ghafla unapigwa marufuku kutumia OS, mara vikwazo vya kufanya biashara na waliokuwa wanakuuzia vifaa, mara vikwazo kwa makampuni yatakayonunua technology yako ya 5G, vyote ndani ya muda mfupi lazima iwe changamoto.
 
Kuvunjika kwa pakacha sio mwisho wa mchukuzi sio kwa sababu huawei imekufa kwahiyo samsung atapata hasara lazima yatatokea makampuni mbadala.
Inawezekana unavyofikiria wewe ikawa hivyo lakini sio Samsung.
Samsung wamelazimika kuomba tena license ya kufanya biashara tena biashara na huawei.
Samsung Display seeks license to supply Huawei: Reuters

Hasara anayotengeneza samsung ni kubwa, makampuni mengi ya china yapo alert kwa sasa.
Serikali ya China haijakaa tu kizembe, Tayari wana plan ya Made in China 2025, Wametenga funds nyingi ku-boost uzalishaji wa processor(chip) ili kupunguza importation ya chips kwa 75%.

Wakati USA inaikaba china kimtindo huo, China pia inajaribu kupiga hatua kwa namna inayowezekana. Miaka ya nyuma China walikuwa na uwezo wa kuunda chips za 45nm(processor ina transistor chache) lakini leo china wanauund chips za 14nm ni swala la muda tu china kufikia 7nm ambayo ndio standard ya dunia ya leo.
 
Marekani anaitengeneza HUAWEI kuja kuwa kampuni kubwa kuliko duniani bila kujua..
Maana kila anachomzuia HUAWEI wanaanza kuzalisha vyao wenyewe mwisho wa mchezo HUAWEI atakua anajitosheleza full bila kutegemea vfaa toka co. Nyngne.. Period
 
Marekani anaitengeneza HUAWEI kuja kuwa kampuni kubwa kuliko duniani bila kujua..
Maana kila anachomzuia HUAWEI wanaanza kuzalisha vyao wenyewe mwisho wa mchezo HUAWEI atakua anajitosheleza full bila kutegemea vfaa toka co. Nyngne.. Period
Mnashindwa kuelewa kwamba huyo Huawei mobile anatumia Android system software ya Mmarekani
 
Ww acha ugonjwa, China hana uwezo wa kupiga burn products za marekani nani kakwambia, acha umahaba
 
Hii Huawei Mate 40 mkuu imetoka juzi, nimeshaeka mkwanja nataka kuichukua, sasaivi natumia Honor X8 (mke wa Huawei)
 
Ww acha ugonjwa, China hana uwezo wa kupiga burn products za marekani nani kakwambia, acha umahaba
Marekan anapiga ban kwa kujilipua lkn China Ni mjasiriamal bidhaa za usa zikiingia kwake Kuna mapato anaingiza anachofanya Ni kuajast kod
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…