Hatimaye: Serikali ya Tanzania yafuta mkataba wake na Kampuni ya Kenya (Indo Power Solutions LTD) iliyojinasibu kununua Korosho kwa Bil 400

Hatimaye: Serikali ya Tanzania yafuta mkataba wake na Kampuni ya Kenya (Indo Power Solutions LTD) iliyojinasibu kununua Korosho kwa Bil 400

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Serikali imeufuta mkataba huo uliowahi kutajwa kuwa na thamani ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 400

Mwezi Februari mwaka huu Serikali iliweka wazi kuwa imeingia mkataba na Kampuni ya kutoka nchini Kenya ya Indo Power Solutions Ltd iliyojinasibu kuwa na uwezo wa kununua Korosho tani 100,000

Serikali kupitia Waziri wa Biashara, Joseph Kakunda imesema kampuni hiyo imeshindwa kutekeleza sehemu ya makubaliano

Aidha, JamiiForums iliibua madudu ya kampuni hiyo na kuyaanika wazi mapema mwezi Februari

Kwa Uzi ulioibua madudu ya Kampuni hiyo fungus kiunganishi hiki - Who is INDO Power Solutions na ni nani Bw. Brian Mutembei?
 
Walitaka kuzungusha pesa kutoka mkono wa kulia nyuma ya mgongo kwenda mkono wa kushoto waseme mkono wa kushoto umenunua kumbe ni wao mkono wa kulia lengo ni kuficha aibu ya kutonunuliwa korosho na wangenunua kwa mkono wa kulia watu wangeuliza kwanza pesa mmetoa wapi, bajeti ipi na baada ya kununua kinachofuata ni nini? Uzuri wenye uelewa na mapenzi ya nchi wakashtuka wakaanika mambo. Nadhani CAG hapa angekagua angekutana na madudu, mtu mzima kaamua kuchutuma. Hataree
 
Afu siku ya kujifunga Kwny huo MKATABA pale Arusha, kulikuwa na ma-prof wawili wa sheria.. Prof Luoga, gavana wa BoT na huyo Kabundi, kumbe hakuna Cha maana, duuh!

Kwa ujumla Kabudi ni mjinga fulani, huyu Kabudi ndio alikuwa kwenye majadiliano na wazungu wa Barrick, alitoka kwenye ule mkutano na maelezo ya uongo, mara sijui tutalipwa kishika uchumba, mara sijui wanapitia deni letu. Yaani hadithi kibao.
 
Serikali imeufuta mkataba huo uliowahi kutajwa kuwa na thamani ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 400

Mwezi Februari mwaka huu Serikali iliweka wazi kuwa imeingia mkataba na Kampuni ya kutoka nchini Kenya ya Indo Power Solutions Ltd iliyojinasibu kuwa na uwezo wa kununua Korosho tani 100,000

Serikali kupitia Waziri wa Biashara, Joseph Kakunda imesema kampuni hiyo imeshindwa kutekeleza sehemu ya makubaliano

Aidha, JamiiForums iliibua madudu ya kampuni hiyo na kuyaanika wazi mapema mwezi Februari

Kwa Uzi ulioibua madudu ya Kampuni hiyo fungus kiunganishi hiki;

Huyo jamaa alikuwa tapeli kabisa, sijui waziri aliingiaje chaka
 
Sasa kwenye jambo dogo kama hili lakutambua uhalali wa uwepo wa Kampuni husika hatuwezi tutaweza kweli kupambna kwenye mikataba mikubwa na ma mafia wa ulaya na uchina?..

Serikali yetu pendwa ya wanyonge naomba tuchukue hatua kwa wahusika wote walioshiriki kwenye aibu hii pasipo kumuangalia mtu usoni, Hili lilipigiwa sana kelele humu JF na watu wakaleta mpaka very simple investigation ambayo hata mbumbumbu wa masuala ya kijasusi anaweza kung'amua.
 
Back
Top Bottom