Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu . ukishaona prof amekubali uteuzi wa jiwe basi piga magoti usali.Afu siku ya kujifunga Kwny huo MKATABA pale Arusha, kulikuwa na ma-prof wawili wa sheria.. Prof Luoga, gavana wa BoT na huyo Kabundi, kumbe hakuna Cha maana, duuh!
Hapo magu anauchunaaa utadhani hayupo bongo. Ahadi ni deniJamani mzee magu si alisema tunaweza tukagawana hizi korosho kila mtu akapata japo kilo mbili mbili,HNi kheri tukazila wenyewe kisha tukasubiri msimu mwingine unaokuja tutakuwa tushapata mbia wa kununua
Watavuna huko huko ghalaniDuh hizo korosho si zimeshaanza chipua ghalani?
Je, hakuna wa kuishtaki serikali kwa kuingia mikataba na kampuni hewa?Serikali imeufuta mkataba huo uliowahi kutajwa kuwa na thamani ya Shilingi za Kitanzania Bilioni 400
Mwezi Februari mwaka huu Serikali iliweka wazi kuwa imeingia mkataba na Kampuni ya kutoka nchini Kenya ya Indo Power Solutions Ltd iliyojinasibu kuwa na uwezo wa kununua Korosho tani 100,000
Serikali kupitia Waziri wa Biashara, Joseph Kakunda imesema kampuni hiyo imeshindwa kutekeleza sehemu ya makubaliano
Aidha, JamiiForums iliibua madudu ya kampuni hiyo na kuyaanika wazi mapema mwezi Februari
Kwa Uzi ulioibua madudu ya Kampuni hiyo fungus kiunganishi hiki;
Who is INDO Power Solutions na ni nani Bw. Brian Mutembei?
Unapoambia fundi seremala kawa mpishi wa Serena Hotel, mtu unaweza tilia mashaka chakula atakachopika. Nimejaribu sana ku Gogle hiyo kampuni iliyonunua korosho na huyo kiongozi wao aliyetia saini na naibu Waziri, kidogo nimeingiwa na wasiwasi. 1. Kenya kuna kiwanda kimoja tuu cha kubangua...jamii.app
Hii ndio mikataba anayoingia Profesa Kabudi. Nikashamuona Profesa Kabudi kwenye jambo lolote huwa najua kabisa hamna jipya hapo.
Sasa kwenye jambo dogo kama hili lakutambua uhalali wa uwepo wa Kampuni husika hatuwezi tutaweza kweli kupambna kwenye mikataba mikubwa na ma mafia wa ulaya na uchina?..
Serikali yetu pendwa ya wanyonge naomba tuchukue hatua kwa wahusika wote walioshiriki kwenye aibu hii pasipo kumuangalia mtu usoni, Hili lilipigiwa sana kelele humu JF na watu wakaleta mpaka very simple investigation ambayo hata mbumbumbu wa masuala ya kijasusi anaweza kung'amua.
Huyo Kabudi namjua vizuri toka zamani. Huwa anatumika sana na watawala kutengeneza sheria zao za hila.Kumbe ulimuelewa tangu zamani sana!