Hatimaye takwimu za waliopimwa COVID 19 Tanzania zatoka hadharani, wamepimwa watu 652 tu kwa muda wote!

Jana Rais analalamika mpaka pamba ile ya kuchukua kipimo inaagizwa. Wanabana matumizi. Halafu 652 kwa watu million 60 ni utani huo. Ina maana kuna wagonjwa kibao wana virus na hawajadhibitishwa.
Halafu kati ya vipimo 652 watu 480 positive.
Kazi ipo.
73.6%
 
Unafikiri kupima ni sawa na kwenda kununua bagia?
Naona umekuja kwa kasi, ungesoma vizuri ungejua nimewaondoa hofu wanao ona uwiano wa waliopima na idadi ya walio kutwa na ugonjwa ni kubwa sana.

Lakini sikusita kusema maoni yangu kwamba waliopimwa ni wachache sana.

NB: Mimi ni kati ya watu wachache walio itetea serikali kupima kwa ungalifu tusije tukamaliza vipimo baadae tukashindwa kuwapima hadi wenye dalili endapo tutaiga mass testing kwa kufuata mkumbo.
 
Hao jamaa wameshatoa mbuzi, kondoo, papai, fenesi kwale? Kama bado waambie wafanye review watoe takwimu halisi za WATU waliopimwa.
 
Wadau someni mazingira msikimbile kuandika namba bila kuzitafsiri katika mazingira husika ya kuchukuliwa vipimo.

Hiyo ni kama sakata la waliopima DNA kutambua baba wa mtoto, asilimia kubwa nadhani 40 na kitu walikutwa ni watoto wa kubambikiwa baba husika, hii ilitokana na waliojitokeza kupima ni wale tu ambao tayari kulikuwa na migogoro ya ndoa na kukosa uaminifu.
Kama wangepimwa watu randomly takwimu zingekuwa tofauti, idadi ya waliobambikiwa ingekuwa chini sana.

Vivyo hivyo wengi wa walio pimwa COVID-19 ni wale walio onesha dalili na wale waliokutana na waliokutwa na ugonjwa, kwahivyo ni lazima ionekane waliokuwa na ugonjwa kati ya waliopimwa wote ni wengi sana.
 
Jana Rais analalamika mpaka pamba ile ya kuchukua kipimo inaagizwa. Wanabana matumizi. Halafu 652 kwa watu million 60 ni utani huo. Ina maana kuna wagonjwa kibao wana virus na hawajadhibitishwa.
Halafu kati ya vipimo 652 watu 480 positive.
Kazi ipo.

Kwani wakipimwa ndo hawatakufa?, unapima watu kulingana na ukubwa wa tatizo, unaambiwa usi copy na ku paste, hata huko waliopima na kukutwa na ugonjwa, hawazuiliwi kufa kama kifo kipo, na wakishapimwa kama hawaumwi wanaambiwa wakajifungie wenyewe sasa faida ipo wapi?, kinachotakiwa kutangzwa ni vifo maana tayari ni binadamu kapoteza maisha, pia itakufanya uchukue tahadhali. Asiyejua kifo akaone kaburi,
 
Upo sawa lakini unapishana na mwenye nyumba. Mabeberu itakuwa wameweka vibaraka wao kule lab
 
Et mbona nchi za mabeberu cases ni nying. Coz wanapima watu na wako transparent. Usikute huku wafu ni wengi sana sema hatujui tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Je wakishapimwa huwa wanapewa nni wailoambukizwa? Hapo ni kujisifu ujinga tu,
Unampima mtu unamkuta ana ugonjwa na alikuwa mzima kisha humtibu unamwambia hakuna dawa anapata hofu anakufa sasa nani muuaji kama sio wewe uliyempima
 
Lengo la kumpima mtu ni ili umtenge asiambukize wengine na umfanyie matibabu vilevile pale atakapozidiwa. Hivi mbona watu hamna akili kabisa? Mkoje nyie?
 
Wewe jamaa acha uongo basi, kama unasema wapepimwa 652 kati yao 480 ni wagonjwa si karibia kila nyumba tungezika watu 2 hadi 3.

Hizi siasa za kishamba hizi zitawaua. Haiwezekani nchi mpaka leo ipime watu 652 kisha 480 wawe wagonjwa
 
Jana Rais analalamika mpaka pamba ile ya kuchukua kipimo inaagizwa. Wanabana matumizi. Halafu 652 kwa watu million 60 ni utani huo. Ina maana kuna wagonjwa kibao wana virus na hawajadhibitishwa.
Halafu kati ya vipimo 652 watu 480 positive.
Kazi ipo.
Kwa hiyo sampling Ina maana 75% ya watanzania Wana korona a very horrible observation
 
Huu ni utakuwa uongo mkubwa. Na hii dashbord ni ya kupika pia. hatuwezi kuwa tumepima watu wachache hivyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…