The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 458
- 1,280
Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kimekosoa kauli ya Dk. Damas Ndumbaro, Waziri wa Katiba na Sheria; na kusema chama hicho kiko imara na kitaendelea kuishauri Serikali, Bunge na Mahakama katika masuala anayohusu sheria, kukosoa kwa maslahi ya umma bila woga, hofu wala upendeleo,
Aidha, kimesema pamoja na kwamba TLS inaheshimu uhuru wa kila mtu kutoa maoni, kauli ya Waziri Ndumbaro haiakisi uhalisia wa utendaji wa taasisi hiyo.
Taarifa ya Baraza la uongozi la TLS, iliyosainiwa na Rais wa chama hicho, Boniface Mwabukusi, iliyotolewa Dar es Salaam 17 Desemba 2024, imesema TLS itaendeleza uhusiano wake na Mahakama, Serikali, Bunge, wadau wa maendeleo (DPs) na wananchi kwa ujumla kwa maslahi mapana ya Taifa.
“TLS inapenda kuwahakikishia wanachama wake na wananchi kwa ujumla kwamba, TLS iko imara na haitayumba wala kuhama kwenye misingi yake ya kisheria ya kushauri Serikali, Bunge na Mahakama katika masuala anayohusu sheria, na pale itakapolazimika, kukosoa kwa maslahi mapana ya umma na Taifa kwa ujumla bila woga, hofu wala upendeleo,” amesema Mwabukusi katika taarifa hiyo.
Chama hicho kimetoa ufafanuzi huo kufuatia kauli ya Waziri Ndumbaro aliyoitoa tarehe 16 Desemba, 2024 wakati wa kusaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU), kati ya TLS na Wizara hiyo, ambapo pamoja na mambo mengine, Waziri Ndumbaro alisema “kama kuna kitu ambacho serikali haipendi kabisa ni yale matamko ya kukurupuka kutoka TLS.”
Mwabukusi amesema kauli hiyo ya Waziri imeleta taharuki ndani ya TLS na umma, kuhusu hadhi na heshima ambayo mawakili wameijenga kwa miaka mingi.
Amesema chama hicho kilianzishwa na Sheria ya Bunge Sura No. 307 na Majukumu yake yameainishwa kwenye kifungu cha nne (4) cha Sheria hiyo, ambayo ni kuwawakilisha, kuwalinda na kuwasaidia wanachama wa TLS katika masuala yanayohusiana na taaluma ya sheria na utendaji kazi wao; kuishauri Serikali, Bunge na Mahakama kwenye masuala yanayohusu Sheria, Katiba, Haki za Binadamu na Utawala Bora.
Amesema tangu taasisi hiyo ilipoanzishwa, imekuwa ikifanya kazi zake kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria na haijawahi kukurupuka kutoa tamko.
“Matamko yamekuwa yakitotolewa baada ya kufanya utafiti wa kina.