Hatimaye Uchumi wa Zimbabwe Waanza Kukua tena Baada ya Wazungu Kurejeshewa Mashamba Waliyoporwa na Uwekezaji wa Migodi

Hatimaye Uchumi wa Zimbabwe Waanza Kukua tena Baada ya Wazungu Kurejeshewa Mashamba Waliyoporwa na Uwekezaji wa Migodi

Miaka ya 90's tulikuwa tukinywa sana maziwa ya SUPER MILK watoto tuliokulia mitaa ya kishua kabla ya Mugabe hajafanya yake
 
Nyerere alifanya kosa kubwa kuwapora wazungu, wahindi na waarabu mashamba, majengo na biashara zao kwa ujumla. tungekuwa mbali sana. man akipindi hicho tulikuwa mbali kuliko nchi nyingi sana ambazo leo zimetuacha mbali.
 
Nyerere alifanya kosa kubwa kuwapora wazungu, wahindi na waarabu mashamba, majengo na biashara zao kwa ujumla. tungekuwa mbali sana. man akipindi hicho tulikuwa mbali kuliko nchi nyingi sana ambazo leo zimetuacha mbali.
Wakati ninyi mkiwa mbenanishwa kwenye ujamaa na hamkuuruhusiwa hata kidogo kumiliki Mali na biashara.

Watu jamii ya Asia waliendelea kuruhusiwa kwa miaka mingi.

Mpaka leo hofu yao ni juu ya Watanganyika kuwa na nguvu kiuchumi ila hizo jamii nyingine zinalegezewa.

Wanajua hao jamaa hawana interest na political power na loyal kwa chama tawala kwa sababu uraia wao ni wa makaratasi.
 
Hakuna Mashamba waliyoporwa Wazungu hapa Tanzania.

Sema tuwape wawekeze kwenye large scale farming
Mashmba ya mkonge, kahawa chai na mashamba ya ngano. Achilia mbali majumba yaliyochukuliwa na msajili wa nyumba, usisahau mabenki. Haya yalifanyika wakati wa Azimiola Arusha. Hapo ndipo tulipodondoka kiuchumi kama Zimbabwe.
 
Chanzo Cha Zimbabwe kuporomoka kiuchumi sio ardhi waliyonyang'anywa Walowezi wa Kizungu bali ni vikwazo vyà kiuchumi.

Hii ni jamii forum ila watu wanajadili hoja kwa mpapaso wa manati badala ya kugusa mpini.

Vikwazo vyà kiuchumi imekuwa siraha kwa mataifa ya magharibi pale maslahi yao yanapoguswa ndio maana mataifa yanataka kujitenga dhidi ya Dola na mfumo mzima wa magharibi.
Pia kumbuka Mgabe alivyowatesa wapinzani na kuwaua wapinzani baada ya kuendesha uchaguzi wakati alikuwa akubaliki tena. Pia alichukua mashamba na kuwapa rafiki zake waliojulikana kama "war veteran" ambao waliyaacha bila kuyaendeleza na nchi kuanza ku import chakula na kuna wakati Tanzania iliwasaidia mahindi ya msaada.
 


Mugabe alikosea kutekeleza jambo hili la kutwaa Ardhi ya Wazungu. Aliongozwa na Mihemko, Tamaa na Chuki binafsi dhidi ya Wazungu licha ya kujua kwamba Watu weusi waliopo katika nchi hiyo hawakuwa na uwezo wa kuitumia vizuri Ardhi hiyo.

Mathalani, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe wakati huo alipokuwa anawapokonya Ardhi raia Wazungu kwenye nchi hiyo alikuja na Sera yake iliyokuwa ikisema kwamba Mtu mmoja anapaswa amiliki shamba moja tu na wala siyo zaidi, yaani: "One Man One Farm." Lakini matokeo yake yeye mwenyewe Mugabe alijitwalia na kujigawia Mashamba mengi yapatayo 28 nchi nzima hali iliyosababisha manung'uniko katika jamii na yeye Rais kuingia kwenye migogoro mikubwa na washirika wake wa karibu Sana kwenye Utawala wake kama vile Mwanasheria Mkuu wa Serikali yake na Mkuu wake wa Majeshi.
 
Back
Top Bottom