Hatimaye 'viatu vya shetani' vyaingia sokoni by Lil Nas

Cha ajabu nini sasa hapo kama mwenye viatu mwenyewe tuko naye mtaani daily..Viatu vyake wala havitushtui
 
Mungu hakutuumba tutawaliwe na vitu, bali tuvitawale vitu vyote. Kitendo cha kuogopa alama fulani au rangi fulani ni kukubali kutawaliwa na alama hizo maana tutakuwa tunaziogopa. Ipo siku tutaishiwa vitu vya kutumia kwa ajili ya kufikiria au kuaminishwa eti ni vya shetani. Kilichomo moyoni mwako ndicho dhamira yako, sidhani kama kuna madhara iwapo utavivaa huku ukiwa unatekeleza wajibu wako wa kumcha Mungu. Labda ikifikia wakati vinawakwaza watu, hapo naweza kuviepuka
 
Uko sahihi ila uwe na uwezo wa kuvunja maagano yanayoambana na hivyo vitu,hebu chukua kibuyu cha mganga anachotumia kwenye uganga halafu uanze kunywea pombe uone nini kitakukuta,vitu vingine sio vitu tu vya kawaida ila vina maagano fulani,ndio maana kuna wanyama wanatumika kichawi mfano paka nk,huyo paka ukimchukua ukamfuge unafikiri utabaki salama
 
Hii habari nimeisoma mahali hadi nikaogopa nikajua ni pye pye pye tu kumbe ni kweli? Ni noma sana.
 
Sijaelewa hapo kwenye damu halisi ya binadamu.

Unamaanisha ukinunua raba kuna mtu anachanjwa kidogo alafu wananyinyizia kwenye kiatu au
Nimeisoma hii habar bbc wanasema kua hayo matone ya damu yalichangiwa na wanachama waliohusika kutengeneza iyo buti wanachama wa kampuni ya "mschf", cjui kirefu chake.
 
Huo mzigo ndani ya dakika moja pair 666 zimeisha zote..Nimeweka order mapema kabla hawajaleta kwa awamu ya pili

Viatu vikinifikia nitapiga navyo picha kisha niweke kwenye avatar..watoto wazuri wa jf waanze kupagawa na mimi mzee wao
 
Hiphop/rap sahv imevamiwa wasanii hata hawaeleweki

Ova
 
Mjanja wa mjini huyo.
Ameshaona kuwa watu wamechoka kutajataja Mungu.
Hamna cha Ufreemasoni wala nini hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…