Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Kukimbia tatizo sio suluhisho la utatuzi wake.
Bora kukaa ndani mkiwa wanne msikilize yaliyo ndani kuliko kukaa nje na kuchungulia yaliyoendelea ndani mkiwa mia mbili.
Ni heri kukubali kushindwa kwa kushindana mkiwa ndani kuliko kutokukubali kushindwa mkiwa nje.
Ukishindwa jishushe ili uwepo wako uwepo.
 
Sitaki kusikia tena hiki chama.



Kuanzia leo



1.sitakuwa na chama.

2.sipigi kura, mpaka ipatikane katiba mpya na tume huru.



Chadema mmenipa hasira isiyomithilika.
 
Kuwa mzalendo ipende nchi yako, huu mchezo hautaki hasira.
Viongozi wa upinzani huenda wamepima ujasiri wa wanachana na wapenzi wao kuona kuungwa mkono uamuzi wa maandamano ukiwa mdogo mno.
 
Swadaktaaa.....

Mapambano si kazi RAHISI....

WALIKOSEA SANA KUTANGULIZA HISIA JUU YA UHALISIA....

Kipindi Cha KUINAMA...INAMA...ukishupaza MGONGO basi UJUE utauvunja🤣🤣
 
Kumbe hakuna umuhimu wa kupiga kura Sasa Bora waseme nchi ni ya chama kimoja tu basi mambo yaende , anayetaka ubunge ajiunge CCM Basi daah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…