Fahamu: tatizo si kupeleka wabunge, tatizo ni kwa nini halikujadiliwa wazi na wanachama? Kwa nini limefanywa kinyemela? Hii inaonesha wazi hakuna maslahi ya upinzani yatahifadhiwa huko.
Ni wazi CCM ina shinikizo kubwa la dunia, na ndiyo maana ikataka 'upinzani' uwepo bungeni. Ingekuwa wanasiasa wa upinzani wana akili (maana hawana, uchu tu) wangelazimisha Fidia kubwa kwa CCM. Fidia si fedha, bali siasa na misimamo ya kidemokrasia. Wangelazimisha hawata 'sign up', mpaka ikubalike Katiba mpya, Tume Huru na maovu yanayofanyiwa upinzani yakomeshwe, nk nk. Tena haya yasingewekwa siri. Yangejadiliwa wazi na wanachama walioumia sana katika uchaguzi uliopita. Lakini wamekubali kununuliwa kwa vijisenti vichache. Kwani hata ikiwa ni mabilioni, CCM wanazo Zaidi!
Lakini bado naona kiwingu kimefunika, kwa sababu jina la Tanzania limeshachafuliwa, na ni vigumu vitendo hivi vya kuwadanganya 'naive' Watanzania vitaweza kuwadanganya hao wanaoogopewa!