Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Dah nimechelewa kuona hii taarifa
This is very funny. Hawa wabunge they are dangerous and foolish.
Shikamo siasa za Bongo
 
TUNDU mgombea urais Chadea 2020 alishindwa vibaya sana na John Pombe Magufuli Rais wa sasa na aliyekuwa mgombea kupitia CCM aliyemshinda vibaya sana TUNDU. Ieleweke uchaguzi ulikuwa Oktoba 28, 2020.

TUNDU alikuwa na wakili wake akijulikana Bob Amstardam, wakili huyo alitoa matamko kwa niaba ya TUNDU na kuandika barua NEC kutisha na kutaka maelezo.

Baada ya uchaguzi alisema anaenda ICC ambayo ni Mahakama ya Uhalifu wa Kimataifa. Tawi lake pia liliwahi kuwepo Arusha likishughulikia uhalifu wa Rwanda.

Sikujua chama cha upinzani kikishindwa linageuka kuwa uhalifu wa kimataifa na kupelekwa ICC the Hague. Nilikuwa naisubiri siku ya Jumatatu, Oktoba 23, 2020 siku iliyoahidiwa Robert Amstarda anafungua kesi ICC kwa kosa la mteja wake kushindwa vibaya uchaguzi na kugeuzwa uhalifu wa kibinadamu sawa na mauaji ya halaiki. Jumatatu, Oktoba 23 mara ikapita nikasikia tena viti maalum.

Mjadala wote umehamia viti maalum na suala la kesi ya mfano na ya kisanii kuendelea kufubaza akili za wafuasi wa chama limekwisha. Hakuna mtu anaweza kukumbuka kujadili na kuuliza ICC tena.

Ili kufubaza zaidi akili za wafuasi, viti maalumu vikaunganishwa na mfumo wa serikali. Kwamba serikali imeratibu viti maalumu Chadema. Sasa hapa, Mdee, Matiko na Bulaya wameratibiwa? Hawa kuna wajumbe wa vikao muhimu sana vya maamuzi ndani ya Chama mfano kamati kuu. Sasa, mjumbe wa kamati kuu anaratibiwa na mfumo w kiserikali. Mwenyekiti wa Bavicha anaratibiwa na mfumo wa kiserikali? Hii ni hatari kwa Chama.

Walid Kabour, Wilbroad Slaa, na Mashinji ni kati ya makatibu wakuu Chadema kuwahi kutokea na kuondoka. Hii nafasi imekuwa changamoto na Mnyika hivi karibuni ataondoka. Ni kwa sababu chama hakina mfumo. Juma Duni Haji mgombea mwenza wa Lowassa 2015 alisema, CHADEMA KILA MTU NI PAPA, baada ya hapo akarudi zake CUF. Katibu mkuu hapewi nafasi kutekeleza majukumu yake hasa linapokuja suala la kusimamia chama. Wakati wa Uchaguzi TUNDU na kampeni meneja wake BOB AMSTARDAM ndio walisikika zaidi kuliko Mnyika, katibu mkuu Chadema.

CHADEMA imara, ni CCM imara, na uchumi imara wa nchi. CHADEMA ijitafakari na kuondoa ubinafsi wa watu fulani ndani ya chama na kufanya kazi kama timu lakini kila mtu akitimiza wajibu wake.

Hatutegemei tena kuona akina Amstardam wakigeuka wasemaje wa CHADEMA.

Je, ikiwa kamati kuu hakuridhia kupeleka mashitaka ICC, kwanini itakiwe kuridhia viti maalumu
 
Ni wakati muafaka wa
1. Mnyika kujiuzulu
2. Halima Mdee kuhamia CCM
3. Mbowe kustaafu uenyekiti
4. CHADEMA kuanza kuwaaga wananchi kabla ya kubakia kama CUF
5. Chama kipya na kizuri chenye sera zenye mrengo wa kimaendeleo kuanzishwa..ACT na CHADEMA na CUF have died
6. Lissu kuzeeka na kuchoka kama Lipumba
7. Bashiru kupewa tuzo maalum ya ushindi. Na kurudi zake UDSM
8. Pole pole kuingia rasmi kwenye Biashara...
8. Magufuli kustaafu bila Furaha.
 
It is fair, Chadema inakufa kifo cha mende kwa sababu mwenyekiti wake ameongoza chama hiki kama mali binafsi. Angalia mlolongo wa viongozi waliopita katika wakati wake. Majeruhi wa mwisho akiwa waziri mkuu mstaafu Sumaye. Mbowe ni bogus flani hivi ambaye anaangalia maslahi yake binafsi, hongera sana waziri mkuu chini ya uongozi wa kibaraka juha TAL.
Broken record. Mko kama fisi anaesubiri mkono udondoke.

Amandla...
 
Ni vyema kwa wana CHADEMA kufikia maamuzi hayo hata kama ni ishara ya ku kubaliana na matokeo ya uchaguzi. Tuki jaribu ku tathmini hayo ni vizuri kufahamu umuhimu wa Chama hicho kuwa na uwakilishi wa aina fulani bungeni baada ya kupoteza majimbo mengi kwenye uchaguzi.

Ongezeko la wabunge wa viti maalum wa CHADEMA inaweza kuwa njia nzuri kwa wao kuwasilisha hoja zao na kujipanga upya katika kipindi ambacho nikigumu haswa katika kubadilisha matokeo ya uchaguzi.
 
Habari ndugu wana JF. Bila shaka muda unakimbia kwa kasi na mambo ni mengi sana. Baada ya danadana nyingi kuhusu sintofahamu ya Viti Maalum, sasa Halima Mdee kama Mwenyekiti wa BAWACHA amejitoa mhanga kwa niamba ya wenzake kusogea mbele ya kuhani na kula kiapo cha ukubali wa uteuzi wa nafasi husika.

Mara tu baada ya kuapishwa, Mdee na wenzake walitaja kuwa viti hivyo sio hisani bali ni matakwa ya sheria. Kwamba ni miongoni mwa ushindi mdogo kati ya ule mkubwa uliopatikana. Na kwamba watashirikiana na Spika wa Bunge kuunda Kambi rasmi ya upinzani bungeni itakayofanya kazi kwa viwango vilevile.

Siku chache baada Halima Mdee alisikika akijibu hoja za Mnyika kuwa yeye anachojua ametimiza vigezo vya kuwa Mbunge viti maalum. Binafsi nimeona utetezi wa Halima na wenzake una matundu mengi;

1. Hata kama ni kweli wana vigezo na sifa za Uviti maalum, Je kwa mujibu wa katiba ya Chadema BAWACHA ndio wanapendekeza majina ya viti maalum kwa Tume ya Uchaguzi?

2. BAWACHA wametumia vigezo gani katika uteuzi wa viti vyao, Je sio kwamba ni kikundi cha watu wachache ndani ya BAWACHA wamejichagua bila taratibu za vikao au mashauriano yeyote?

3. Halima Mdee akiwa mjumbe wa Kamati kuu ya Chadema, anaweza kueleza bila kupepesa macho juu ya historia ya uteuzi wa viti maalum katika chaguzi zote za nyuma, na hiki ambacho yeye anatetea na kusimama nacho kwa sasa?

4. Spika wa Bunge ( Ndugai) na Mamlaka za Serikali kusimama na Halima Mdee na wenzake, na kuwatetea ili wasihukumiwe na chama chao inatuma ujumbe gani kwa wanachama wa chadema?

5. Je Halima na wenzake wanataka kwenda Bungeni kusimamia nini ? Maadili ? Tume huru ? Ukiukwaji wa sheria na katiba za nchi ? - ipo legitimacy ya kutenda hayo ?

MWISHO KABISA NIOMBE CHADEMA KUCHORA MSTARI KATIKA HILI. NI HATUA MUHIMU KUELEKEA UJENZI WA TAASISI IMARA. CHADEMA INA ZAIDi YA WAPENZI MILIONI 3 , KUSUMBULIWA NA WABUNGE 19 AMBAO WAMEPOTEZA UHALALI WA KISIASA NI SAWA NA KUJICHIMBIA KABURI.

MAAMUZI NI SASA.
 
Habari ndugu wana JF. Bila shaka muda unakimbia kwa kasi na mambo ni mengi sana. Baada ya danadana nyingi kuhusu sintofahamu ya Viti Maalum, sasa Halima Mdee kama Mwenyekiti wa BAWACHA amejitoa mhanga kwa niamba ya wenzake kusogea mbele ya kuhani na kula kiapo cha ukubali wa uteuzi wa nafasi husika...
Majibu yote ya maswali yako anayo mh Mbowe!
 
Wadau, Ni vema tuangalie upande mwingine wa shilingi, haiwezekani mdee kutisha na kuamrishwa kufanya Yale watakayo na watu wa maagizo kutoka juu?

Kwani mpaka sasa hawa wamama wako wapi? Wanafanya nini? Je wanaonana na familia zao?

Kwa jinsi nilivyomjua Halima sauti ya zege, asingeweza kujitosa kiasi hicho maana anajua yeye bado ni kijana mdogo lakini pia pamoja na kumjua haiondoi kwamba hawezi kusaliti, nachoamini ni tujiridhishe na majibu hapo juu.

Swelana.
 
Yule Matiko alipigwa dole la Kundu na Yule poti na amesalimu amri,taratiiiiiiiiiiiiiiiiiiibu.
 
Kanuni ya Chadema ukitishwa unakimbilia Kenya ama ubalozi wowote wa nchi za E.U.
kama walivyofanya wakina Lema,Nyarandu na Lisu the great.
 
Back
Top Bottom