Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Uchaguzi 2020 Hatimaye Wabunge 19 wa Viti maalumu wa CHADEMA wajitokeza kuapishwa Dodoma. Viongozi wa CHADEMA wakana kupeleka majina yao

Nchini hii raha sana,leo Kigogo anazinguana na kina Halima na Bulaya huko Twitter......maisha yanaenda kasi sana
 
Duuu inasikitikisha sanaa kama ni ya kweli. Kama ni hivyo hakuna chama cha siasa bongo ni muda wa kuachana na siasa za bongo nw nikutafuta pesa na kupambania maisha yko ninafsi

Wasaliti 20 hawawezi kuhalilisha uzito wa kauli yako.

Usaliti wa Yuda haukuhitimisha mission ya Yesu duniani.

Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi.
 
Niko imara kama kawaida, sitishwi na watu wachache kushirikiana na shetani.
Hongera MCHAMUNGU....

Alikuwa DR.SLAA mwenye vigezo vyote ADHIMU vya upambanaji....leo yuko SWEDEN🤣🤣

Unamlaumu Nusrat Hanje kwa ALIYOPITIA?!!
Mwache ALE MEMA banaa hata Kaka yake MWAIPAYA pia atayala ya dada yake.....

Komredi Said Sambala ukuje hapa tumuongelee KAMANDA NUSRAT HANJE eti naskia ni "maswahiba sanaa" na MTENDAJI MKUU pale KINOKLEIN?!!!!

🤣🤣🤣
 
Wabunge Viti Maalum kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameanza mchakato wa kusajiliwa Jijini Dodoma.

Majina yao yamewasilishwa na Katibu Mkuu wa CHADEMA

ORODHA YA WABUNGE WA VITI MAALUM CHADEMA 2020.
1. Halima Mdee
2. Grace Tendega
3. Ester Matiko
4. Cecilia Pareso
5. Ester Bulaya
6. Agnesta Kaiza
7. Nusrat Hanje
8. Jesca Kishoa
9. Hawa Mwaifunga
10. Tunza Malapo
11. Felister Njau
12. Naghenjwa Kaboyoka
13. Sophia Mwakagenda
14. Kunti Majala
15. Stela Fiayo
16. Anatropia Theonest
17. Salome Makamba
18. Conchesta Rwamlaza
19. Asia Mohammed

HOTUBA FUPI YA HALIMA MDEE KWA NIABA YA WABUNGE WA VITI MAALUM WA CHADEMA

Mheshimiwa spika, nitazungumza kwa niaba ya wenzangu wote kwa hiyo nitazungumza peke yangu. La kwanza nikushkuru kwa amabo umepelekea kiapo kikafanyika

Pili nikishkuru chama changu cha CHADEMA kikiongozwa na Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe kwasababu kupitia wao ndio sisi tumepata nafasi ya kukiwakilisha chama chetu ambacho kwa mujibu wa matakwa ya sheria za nchi kimekidhi vigezo vya kupata viti maalum, kwa hiyo viti hivi siyo hisani ila ni sehemu ndogo ya ushindi mkubwa ambao chama chetu kilipata.

Nikuhakikishie mheshimiwa spika na mimi unanifahamu vizuri, tumefanya kazi wote kwa kipindi cha miaka zaidi ya 10, tutafanya kazi kwa uaminifu kama Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na kwa uadilifu mkubwa kwa viwango vilevile ambavyo tumekuwa tukivifanya.

Lakini mwisho lakini sio kwa umuhimu, tuwahakikishie vile vile watumishi wa Bunge, kuna vijana wapya hapa wameingia, sisi kama dada zao tutahakikisha wanafanya kazi bora na nzuri kwa ajili ya Taifa hili.

Zaidi tuwahakikishie wana CHADEMA nchi nzima, tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na kwa uadilifu mkubwa sana. Baada ya kusema maneno hayo Mh Spika nirudie kukushkuru wewe, katibu wa Bunge na timu yake wewe na nikishkuru chama chetu kwa sababu kupitia

Zaidi tuwahakikishie wana CHADEMA nchi nzima, tutafanya kazi mliyotutuma kwa uaminifu na kwa uadilifu mkubwa sana, Mh Spika nikushukuru sana, wewe na chama chetu ndio tumepata fursa hii ya kuwakilisha watu wengi ambao wana imani na sisi.

SPIKA NDUGAI: Muongezeeni makofi Halima, ningependa kuchukua nafasi hii kuwapongeza wabunge wapya na kwa niaba yenu wote ningeomba tuwapigie makofi.

Kwa mujibu wa ibara ya 78, ibara ndogo ya kwanza ikisomwa na ibara ya 66, ibara ndogo ya 1(B) ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Vyama vya siasa vilivyoshiriki katika uchaguzi mkuu na kupata angalau asilimia 5 ya kura zote halali za wabunge vitapendekeza kwa tume ya Taifa ya uchaguzi majina ya wanawake kwa kuzingatia uwiano wa kura ambazo kila chama kimepata katika uchaguzi wa wabunge ili hao waliopendekezwa wawe wabunge wa viti maalum kupitia vyama hivyo.

Tarehe 20 Novemba 2020 nimepokea barua kutoka tume ya Taifa ya uchaguzi yenye maelezo kuwa imefanya uteuzi wa wabunge wanawake 19 wa viti maalum wa CHADEMA kwa mwaka 2020 ambao ni kama tulivyowaapisha hapa.

Mimi kama spika nawaahidi kuwapa kila aina ya ushirikiano, najua kambi yenu itakuwa ni ya wabunge wachache, wajibu mmojawapo wa spika ni kuwalinda wale walio wachache, nitajitahidi sana kuwalinda, nitajitahidi kuwapa haki, nitajitahidi kuhakikisha kwamba mnatekeleza majukumu yenu kikamilifu katika kuwatetea watanzania, kuwasemea watanzania na kufanya kila lile ambalo linawapasa katika kazi za kibunge ili muweze kufanikisha jukumu hili la kikatiba.

View attachment 1633801
View attachment 1633976
Wabunge wa Viti Maalum(CHADEMA) wakiwa na Spika Ndugai​

Suala hili lilizungumziwa na mwanaJF hapa > Suala la Viti Maalum kuna usaliti unaotaka kufanywa na wanawake wa CHADEMA

CHADEMA yakanusha kupeleka majina > John Mnyika: Hatujateua majina ya wabunge Viti Maalum, tunafuatilia Ofisi ya Spika na tukithibitisha hujuma au usaliti hatutasita kuchukua hatua
Nakala kwa Salary Slip, Return of Undertakers, G.Sam, Minyoo, Lord....na wengine wasiojua siasa za Chadema. Tuliwaambia mtaumia sana kisaikolojia na bado.
 
Chadema hata wakiwafukuza hao wamama namuona Ndugai akiwarudisha kwa Style ya Cecil Mwambe. Swala la Kufuata katiba tuko nyuma sana aisee
Sawa mkuu hiwe itakavyo kua Cha msingi ni kufutilia mbali kwenye chama mengine watajijua, chama hakiwezi shindwa timiza wajibu wake kwa kuogopa,Mambo madogo Kama haya,chadema hata ikifukuza wanachama elfu moja,ni sawa na tone moja kwenye bahari, chama kina mizizi ya kutosha kwa Sasa hakuna kuruhusu mtu yoyote chezea chama,
 
Mhutu mtu wa ajabu sana , katumia nguvu kubwa Sana kuzuia wapinzani wasipate ubunge , leo huyohuyo katumia pesa , vitisho na masharti kwa baadhi ya viti maalum kuwatoa rumande ili waingie bungeni .Ningekuwa simjui Mhutu ningeshangaa kwa haya , ila kwa kuwa namfahamu sishangai mtu anayetenda kwanza halafu anafikiri baada ya kutenda , badala ya kufikiri kabla ya kutenda.
 
Sijawahi kuwa na fikra za kijamaa, na wala sintokaa niwe na fikra hizo. Sitamani kwenda ccm na wala sintokaa natamani.
🤣🤣🤣
Kamanda eee hebu shusha RUCKSACK mgongoni utoe KIBUYU CHA KIJIVU unywe maji koo lilainike si unajua unapanda ile milima ya MONDULI pale TMA 🤣🤣
 
Nawashangaa wanaoishangaa CHADEMA leo!
CHADEMA ya principles iliondoka na Dr. Slaa toka 2015!

Tuliposema CHADEMA imekufa wengi hawakuelewa, kufa ni process, ila turning point ilikuwa 2015 'kugeuza gia angani'

Kwa hiyo matendo, matukio na matokeo mbalimbali yaliyoendelea baada ya 2015 ndiyo kifo chenyewe, uchaguzi wa 2020 umethibitisha hilo.

-Kumkumbatia na kumsafisha 'fisadi' Lowasa, tena kwa kumpa tiketi ya Urais! Alafu BAVICHA wanaimbishwa kwamba ni bora kushirikiana na shetani ili kuingia ikulu!

-Kufumbia macho udikteta wa Mbowe kwa kutoa maamuzi yake binafsi badala ya taratibu za chama! Alafu BAVICHA wanaimbishwa kwamba. hanunuliki!

-Mtu moja kung'ang'ania uenyekiti kwa miaka 20! Chama kinachojinasibu cha demokrasia! Na kufukuza au kupelekea kujitoa wote waliothubutu kuonyesha nia ya kugombea uenyekiti wa taifa, alafu BAVICHA wanaimbishwa kwamba hao ni wasaliti!

-Ubadhirifu wa mali za chama wa mwenyekiti alafu BAVICHA wanaimbishwa kuwa huyu ni mwamba na haongeki!

-Wabunge, madiwani, viongozi wa ngazi mbalimbali kujitoa kwenye chama kwa kueleza mapungufu makubwa ya mwenyekiti! Alafu BAVICHA wanaimbishwa kwamba wamenunuliwa!

-Kubwa zaidi chama kuziacha sera zilizovuta watu Kama kupinga ubadhirifu, rushwa, kuahidi kuleta maendeleo, kujenga barabara, reli, kuimarisha usafiri wa anga, Bandari, kupeleka na kupunguza bei ya umeme kwa wananchi wengi, kuimarisha matibabu! Alafu kinageuka kuwa watetea mafisadi, watumishi wazembe, wezi na wahujumu uchumi na KUPINGA MAENDELEO eti ni MAENDELEO YA VITU! Alafu mnategemea mtachaguliwa na wananchi! Wananchi siyo wapumbavu kiasi hicho! Kwa ufupi CHADEMA imejiua yenyewe!, hakuna sera inavuta watu CCM kwani wizi upo ufisadi upo CCM ni ile ile ukoo wa panya
Hakuna maendeleo yameletwa na CCM miradi yote mikubwa imejaa ufisadi mkubwa kuna 10% ununuzi wa Ndege, SGR bwawa la umeme flyover na miradi yote mikubwa, Dr Slaa hakuondoka chadema kwa kupenda alinunuliwa kwa dola milion 2 na kupewa nyumba canada hana mfano wa kuigwa hata mmoja ni mwizi kama wezi wengine huko CCM,
 
Back
Top Bottom