Hatimaye Wamekiri bayana: Kumchukulia poa Urusi ni kujipeleka kwenye kipigo


..Putin anashambulia.

..Zelensky anajihami.

..Au wewe unaonaje?
 
..Putin anashambulia.

..Zelensky anajihami.

..Au wewe unaonaje?
Ninavyoona mimi:
1. Putin anashambulia kiholela - hana malengo e.g. anaposhambulia shule za chekechea au viwanja vya kuchezea watoto ni ili iweje? Lakini akipiga madaraja ni sahihi kwa sababu anazuia askari na vifaa-vita kusafirishwa kupitia hapo.
2. Zelensky anajihami kwa sababu adui(aliyevamia) yupo ndani nchini Ukraine. Kwa hiyo Zele hana jinsi - Analazimika yan anapigania uhai wake; vinginevyo asipopambana kufa na kupona atakwenda na maji i.e.ataangamizwa jumla.
Lakini yote kwa yote;
Putin hii vita imemuweka pabaya - imemshushia Hadhi na Heshima yake kama Taifa kubwa mbele ya mataifa (Supa pawa)kwa kujiingiza kupigana vita na kanchi kadogo vile halafu bado kanamtesa hajamudu kukanyamazisha. Mataifa yalitegemea kuwa Urussi angebaki kuwa ni mzee wa kusuluhisha vitaifa vidogo-vidogo vingine vinapogombana au kuhitilafiana kumbe sasa yeye ndo kaingia kupigana.Ameonesha mfano mbaya kabisa. Ni sawa na baba nyumbani anapokuwa yeye ndio mwanzisha ukorofi / ugomvi katika familia.
 
👏👏👏👏👏👏👏👏👍👍👍👍👍🤝🤝🤝🤝Point hii pro NATO Huwa hawataki kbs

Waache waendelee kupigwa na upofu. Lakini wajue kwa mwenzao kunateketea.
 
Attn: JokaKuu

Utishio wa Ukraine kwa Russia uko katika picha hii. Kuna watu wanapigana na Russia kupitia Ukraine. Kwa hiyo, hicho kichapo anachochezea Ukraine kuna watu kibao wanaumia na kulia. Bila shaka na wewe unawaona.
Umenena vyema. Ila lakini na wewe uuone ukweli huu kwamba Urussi nako hakujawa Shwari. Wapo watu/Raia wanaoteseka na wengine wamefikia hata hatua ya kujiua kuliko kuendelea kuishi hivyo. Raisi wa Urussi naye anahangaika huku na huko (e.g. NKora, Iran, Belarus, Wagner group etc)anakusanya watu mitaani(kamata-kamata) anawarubuni wafungwa waingie jeshini n.k. n.k. Hii yote ni ili vita hii isimwelemee mno Mrussi.Kwa hiyo ukisema kuna watu kibao wanaoumia na kulia mbona wanapatikana/wanakutilizwa pande zote husika katika vita hii.
 
Kama nilivyosema hapo awali, anachofanya ni kuwakomoa wale ambao wako nyuma ya Ukraine.
Urussi amefikia mahali akagundua kwamba kuna mahali alibugi stepu lakini kwa sasa ni too late hawezi kurekebisha tena hali na hata akikomalia mapigano hakuna tena maslahi kwake. Kwa mantiki hiyo anahakikisha anawaachia Waukraine maumivu makali (magofu/uharibifu, simanzi na masononeko kwa kufiwa na wapendwa wao n.k). Mrussi hahitaji tena kushinda vita; hana tena sababu au mpango wa kushinda Vita hiyo ambayo haina maslahi kwake.Anachafanya ni kuvunja-vunja, kupasua-pasua haribu na kila vurugu anayoweza.
 
Wangewachukulia poa si wangeshapigwa? Au huelewi context ya alichoongea huyo Jenerali? Russia ndio aggressors, wao ndio wanatakiwa wakiri kwamba vita ni ngumu kuliko walivyotegemea. Toka March mpaka leo hakuna chochote cha maana walicho- achieve.
 
Wangewachukulia poa si wangeshapigwa? Au huelewi context ya alichoongea huyo Jenerali? Russia ndio aggressors, wao ndio wanatakiwa wakiri kwamba vita ni ngumu kuliko walivyotegemea. Toka March mpaka leo hakuna chochote cha maana walicho- achieve.

Sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…