Wanasayansi wabobezi katika chuo kimoja huko mashariki ya mbali ambacho kinaheshima kubwa sana duniani.. wameibuka na utafiti uliowashangaza wengi.. kua timu ya Simba S.C ya msimu huu ni tiba ya kila kitu.
Katika utafiti wao wamegundua mambo mengi.. Mfano;
1. Kama una stress.. Mnyama Simba ni dawa ya kuondoa stress.
2. Kama umedhoofu mwili.. Hauna haja ya kula mavyakula kibao ili urudishe afya.. Wewe anza tu kushabikia Simba S.C.
3. Kwa wale wazee wa kubet.. Simba S.C imewapa utajiri wa kutosha.. Wana manyumba, magari n.k na hii ni kutokana na kila mzigo wanaoweka.. Mnyama hawaangushi.
Baadhi ya wapenzi wa soka waliohojiwa.. walikiri Simba S.C ya msimu huu.. imebadili kila kitu katika maisha yao,.. Mfano;
Kuna mwingine ambae watafiti hao hawakumtaja jina lake alinena haya... "namshukuru sana Mnyama kwa kunipa utajiri kwani kila mwisho wa wiki nina uhakika wa kuingiza si chini ya milioni 3.7 kupitia kubet.
Ila kwa kila mashabiki wa soka aliokaidi ushauri aliopewa wa kuanza kumshabikia Mnyama mkali pengine kuliko wote mwituni.. Makubwa humkuta.. Mfano ni huyu ndugu yetu;
Simba hiyo mechi ilishinda sasa hivi jamaa hana tena mkono [emoji20] [emoji20]
Katika kuhitimisha utafiti wao.. Wanasayansi hao wabobezi, wamewaomba wapenzi na wasio wapenzi wa soka duniani.. Kuanza kuishabikia Simba S.C haraka iwezekanavyo kwa furaha ya milele.
NOTE;
Wanasayansi hao wanadai bado wamejifungia maabara usiku na mchana wakijadili goli alilofunga Shiza Kichuya mnamo 01.10.2016.. Wanasema japo walitoa mchoro wa goli hilo.. Bado wanajiuliza iliwezekanaje.. Wanadai mambo yakienda vizuri mwakani ndo wanaweza kuja na ripoti kamili ya goli hilo.