Hatimaye Yanga yakabidhiwa kwa Manji aiendeshe kama club Binafsi

Hatimaye Yanga yakabidhiwa kwa Manji aiendeshe kama club Binafsi

Nimemuelewa MANJI ana nia nzuri kitu cha muhimu ni uwazi naota kuanza kuona vitu vifuatavyo
1:YANGA FC TV
2:JEZI ZIKIUZWA KWA MPANGILIO MZURI NA WA FAIDA
3:bidhaa mbali mbali zenye logo ya YANGA FC
TIMU YETU ITATUMIKa kibiashara zaidi tuache wanao sema tuna kodisha timu ila baadaye wata tuonea wivu 25% ya faida sio mbaya kwani sasa ivi atuitumie club yetu ki biashara ila ni vema tukawekeana mkataba pia napenda tuiboreshe katika
1:mitandao website na social network page ziendeshwe na wataalamu
2:Magazeti yaongezeke
3:tuwe na kituo cha radio Jangwani fm
4:tuwekeze kwenye usafiri
5:kituo cha kulelea vipaji mbali mbali
 
Nikuulize sisi wana chama tuna faidika nini sasa hivi zaidi ya ubishi bora manji awekeze tu maana wataweza pata ajira kuliko sasa hivi
 
Kwani kabla ya kuikodisha wanachama walikuwa wana faidika na nini zaid ya kushangilia na kujifanya makocha? Wale wachache waliokuwa wanafaidika na mapato ya getini na hujuma sasa watafute kazi na sio kwenda kushinda makao makuu kufikiria uchawi na upumbavu uliopelekea timu hizi kukosa mafanikio
 
Nikuulize sisi wana chama tuna faidika nini sasa hivi zaidi ya ubishi bora manji awekeze tu maana wataweza pata ajira kuliko sasa hivi
Habari za mwanzo ni ilikua nae atoe bilioni 25 kisha achukue 50% lakini mpango huo ukavurugwa na kigogo mmoja alietaka kutoa bilioni 65 kwa asilimia hzo hzo ndo ili kumvua huyo mshindani akaamua kujikodisha, swali linakuja hivi ndani ya miaka kumi akiishusha daraja je, akiamua kuitumia yanga kukopea hela benki je, tujiulize maswali kabla ya kumkubalia
 
Shida kubwa ya hiz club zetu, ni mambo kuamuliwa na wachache kama sio mtu mmoja kabisa.

Kukodisha maana yake nin?? Tena kwa miaka kumi?!

Mimi ni Yanga, ambae naona ukurupukaji mkubwa sana hapa. Haya mambo yanapaswa yawekwe sawa mapema, tena muhim kujaribu makubaliano haya angalau kwa misim miwili kwanza.

Sina iman na viongoz wangu.
 
Am Young Dar African Sports Club,

Ila hapa naona tumeliwa mchana kweupeee, Unajua nini....?

Tunamkabidhi timu mtu for nothing..!!!, Hatujui anataka kuwekeza nini? Hatujui anataka kufanya biashara gani? Hakuna mkataba unaomfunga kwamba anatakiwa kujenga Uwanja wa Timu labda ndani ya kipindi hicho...!!!! Mkataba kwamba anatakiwa kununua angalau wachezaji wa kiwango fulani ndani ya kipindi husika hakuna...!!! Kwamba anatakiwa kuwekeza kiasi fulami kila mwaka ndani ya kipindi hicho hakuna....!!!!!!

Yaani mtu akienda huko kishumundu kutununulia kina Kibwanguso kama wachezaji wa Yanga, ni sawa tu....!!!! Hakuna cha kumbana..!!! Hapana.

Hapa tumeliwa kweupe hata jogoo hajawika!

Hii ni nafuu sana kwa watani zetu hapo ambao Mo amewaambia atawapa Bl 20. Na hata igusa hiyo wala faida yake ambayo itapatikana baada ya kukopeshwa hela hizo. Hii maana yake nini? Siku huyu mtu akiamua kuondoka Simba itakuwa imepata Bl20 na faida iliyopatikana baada ya kukopeshwa fedha hizo.

Huyu bwana ni mtu mjanja sana, Aliwekeza bure kabisa kwenye Club kwa kipindi cha karibu miaka sita sasa akilenga kupata hiki anachoomba leo, Ambacho binafsi ninaamini ni kikubwa kulinganisha na kile tutachopata kwa miaka hiyo kumi. Nembo tu ya Club inazaidi ya thamani ya trilioni moja...!!!!

Unajua nini......
Akimua kuuza maji tu yenye nembo ya club ya yanga angalau kwenye mechi moja tu ya club ya Yanga huku akifungia maji mengine kuuzwa kwenye mechi husika unajua fedha itakayopatikana? Achia mbali hilo akiamua kuuza tu Opener za soda zenye nembo ya club ya Yanga kwa miaka hiyo kumi unajua itapatikana bei gani?

Hapa sijazungumzia Jezi, Skafu, Soksi, Kofia, Miruza, Laba, Six........ Oooopssss

Ngoja niishie hapa mimi........!!!!!

BACK TANGANYIKA

Hujui unachoongea,
Hao wanachama kwa miaka zaidi ya 50wameshindwa kufanya ayo unayoyasema.
Wameshindwa kudhibiti nembo inatumika ovyo, jezi,.

Sasa acha apewe mtu ambae atadhibit kibiashara,
CHA msingi ni mikataba ikae sawa tu
 
Nimemuelewa MANJI ana nia nzuri kitu cha muhimu ni uwazi naota kuanza kuona vitu vifuatavyo
1:YANGA FC TV
2:JEZI ZIKIUZWA KWA MPANGILIO MZURI NA WA FAIDA
3:bidhaa mbali mbali zenye logo ya YANGA FC
TIMU YETU ITATUMIKa kibiashara zaidi tuache wanao sema tuna kodisha timu ila baadaye wata tuonea wivu 25% ya faida sio mbaya kwani sasa ivi atuitumie club yetu ki biashara ila ni vema tukawekeana mkataba pia napenda tuiboreshe katika
1:mitandao website na social network page ziendeshwe na wataalamu
2:Magazeti yaongezeke
3:tuwe na kituo cha radio Jangwani fm
4:tuwekeze kwenye usafiri
5:kituo cha kulelea vipaji mbali mbali
Endelea kuota tu kwani ile Raman ya uwanja iliishia wapi mkuu!?
 
Ya Yanga ni Bora Kuliko ya Simba.

Kukodisha ni bora kuliko kuuza. Ingekuwa kiwanja au nyumba sawa unaweza ukauza ukanunua au ukajenga tena. Ila timu ya mpira huwezi kutengeneza nyingine.

Cha kuchekesha ni kwamba Simba hawajui kama timu yao ndo inauzwa. Nikiwaambia wanasema anachukua 51% tu. Hawajui 51% maana yake ndo mmiliki na mwenye sauti ya mwisho.

Manji ili awe na sauti ya mwisho bado anahitaji kuwa Mwenyekiti wa Yanga. Akipoteza Uenyekiti wa Yanga amepoteza sauti. Na ili aendelee kuwa Mwenyekiti wa Yanga ni lazima ahakikishe Simba haiifungi Yanga. Ushindi wa ligi kuu na makombe mengine hauna maana bila kuifunga Simba.

Ila kwa watani zetu wa Simba wakikubali kumuuzia Mo 51% wajue ndo basi tena. Wafungwe au wasifungwe Mo ataendelea kuwepo tu.

Mengine ya mgao wa asilimia za faida ya ukodishaji naamini Wadhamini wa Yanga watahakikisha yanakaa vizuri.

Muhimu ni kwamba Club haitauzwa, Manji akiboronga ruksa kumtimua. Ila Club inahitaji mawazo mapya kama haya. Yanaweza kuwepo mawazo mengine bora zaidi, lakini angalau kwa hili yupo mtu ambaye yuko tayari kulitekeleza.
 
Nimefurahishwa Na Wanachama wa Yanga kumkubalia Manji kujikopesha Klabu ya Yanga Kwa asilimia 75% huku wanachama wakibaki kuhudhuria mechi tu ambazo klabu yao itakuwa inacheza na kushangilia ikishinda au kuzomea ila hawatakuwa Na sauti hata kidogo ya mwenendo wa klabu yao.Manji akiamua Yanga ipate matokeo mabaya hakuna wa kumpinga, kwani wanachama hawatakuwa Na sauti.Nilitegemea wanachama wa Yanga wangekubaliana kuwa Manji auziwe hisa tena Asilimia 50% Na Zilizobaki ziwe za wanachama ili pande zote mbili zishiriki kwenye maamuzi ya Klabu, lakini Kwa utaratibu wa kumkopesha Manji Kwa asilimia 75% Wanayanga make mkao wa kulia tu hamtakuwa Na maamuzi Kwa miaka 10 bora mngempa hata miaka 5 kwanza ya majaribio.

Mitano ya nini! Wangempa miwili kwanza kwa 50% waangalie ufanisi na changamoto lakini 75%! Wameula wa chuya, watakuja kutoana macho hawa! Wakati ukuta!
 
Hivi hapo kwenye hesabu ya faida ya 75% anachukua yeye na 25% ni wanachama, ina maana wanachama wameshindwa kugundua kama timu yao ina thamani hata kama wameshindwa kuiendesha kiuweledi, ni sawa na mie nina hekari 100 zenye rutuba ila nyenzo za kulimia shamba lote sina hivyo anakuja kukodisha mwekezaji nusu ya shamba. Lazima atanipa kiwango kadhaa cha fedha kabla ya kuanza kazi au kama ni hekari 100 zote napo atatoa kiwango kadhaa na kukubaliana mgawanyo wa faida. Sasa hapo Yanga imekodishwa bure yaani jamaa anaanza kuwekeza bila kulipa kwanza ela kukodisha? Ambayo ndo itakuwa mtaji just in case ameshindwa kupata faida
 
Habari za mwanzo ni ilikua nae atoe bilioni 25 kisha achukue 50% lakini mpango huo ukavurugwa na kigogo mmoja alietaka kutoa bilioni 65 kwa asilimia hzo hzo ndo ili kumvua huyo mshindani akaamua kujikodisha, swali linakuja hivi ndani ya miaka kumi akiishusha daraja je, akiamua kuitumia yanga kukopea hela benki je, tujiulize maswali kabla ya kumkubalia
Benki gani itakubali kumkopesa manji kwa mali ambazo si zake ?
 
Nimefurahishwa Na Wanachama wa Yanga kumkubalia Manji kujikopesha Klabu ya Yanga Kwa asilimia 75% huku wanachama wakibaki kuhudhuria mechi tu ambazo klabu yao itakuwa inacheza na kushangilia ikishinda au kuzomea ila hawatakuwa Na sauti hata kidogo ya mwenendo wa klabu yao.Manji akiamua Yanga ipate matokeo mabaya hakuna wa kumpinga, kwani wanachama hawatakuwa Na sauti.Nilitegemea wanachama wa Yanga wangekubaliana kuwa Manji auziwe hisa tena Asilimia 50% Na Zilizobaki ziwe za wanachama ili pande zote mbili zishiriki kwenye maamuzi ya Klabu, lakini Kwa utaratibu wa kumkopesha Manji Kwa asilimia 75% Wanayanga make mkao wa kulia tu hamtakuwa Na maamuzi Kwa miaka 10 bora mngempa hata miaka 5 kwanza ya majaribio.
Mijitu ya Yanga haina uwezo wa kufikiri..
Kwanza aliwaua njaa,kwa kukataa mikataba yote
Manji kama ana hela si aanzishe timu yake!
 
Kukodisha na kupata chochote na kumpa bure kipi bora?
Hizo hisa alizonunua Mo, hela kapewa nani? Bado zipo kwake! Kachukua timu bure kuwa mali yake bado watu wanakenua meno.
Bei kajipangia na bado hela atakuwa nayo yeye mwenyewe.
Jengo na uwanja Bunju vitakuwa mali yake.
Ili Yanga au Simba ziwe kampuni Ilikuwa lazima kubadili katiba kwanza ili akina Mo wanunue hisa toka kwa wenye kampuni yaani wanachama!
 
Huyu jamaa ujue ni mfanyabiashara mkubwa na mfanyabiashara siku zote yeye anatafuta faida tena kubwa, wana yanga apa mjue tumeliwa huyu amekua mwenyekiti kwa muda mrefu hivo ashajua faida ya timu hii kubwa, tusiwe maskin wa akil jaman
 
Back
Top Bottom