ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Mwaka Jana niliweka mada hapa kwamba Zimesalia km 51 za vumbi Ili Barabara yote kutoka Dar Hadi Kigoma iwe Lami.
Hatimaye km za mwisho kutoka Ilunde-Malagarasi zimekamilika na Sasa Kigoma sio mwisho wa reli tena.Serikali ya Rais Samia imewakomboa watu wa Kigoma na Tabora. Soma hapa Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami.
Sasa Serikali iweke Nguvu kwenye Barabara zifuatazo
-Mbeya-Tabora
-Songea-Morogoro
-Njombe-Morogoro
-Arusha-Musoma
-Mpanda-Kigoma
-Tanga-Singida
-Iringa-Morogiro-Lindi.
===
Ujenzi wa barabara ya Kaliua - Malagarasi - Ilunde (km 156) na kipande cha Kazilambwa - Chagu (km 36) umekamilika kwa asilimia 100, huku kazi za nyongeza kwenye barabara ya Ugansa - Usinge (km 7.4) zikifikia asilimia 98.5.
Barabara hii, yenye umuhimu mkubwa wa kiuchumi na kijamii, imejengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi 48.6 bilioni, ambapo Mfuko wa OPEC umefadhili asilimia 95 ya mradi huku Serikali ya Tanzania ikigharamia asilimia 5.
Mradi huu ulianza kutekelezwa tarehe 3 Agosti 2020, baada ya upembuzi yakinifu uliofanywa mwaka 2009 na kampuni ya Crowntech Consult Ltd kwa gharama ya shilingi 134.4 milioni.
Serikali ya Tanzania ilianza kufadhili ujenzi huo kwa asilimia 100, kabla ya Mfuko wa OPEC kuingia kama mfadhili mkuu mwaka 2021.
Wakazi 199 wa vijiji vya Ugansa na Malanga walilipwa fidia ya jumla ya shilingi 725.3 milioni kupisha ujenzi huo, huku gharama za usimamizi wa mradi zikifikia shilingi 2.2 bilioni kwa kipindi chote cha utekelezaji.
Aidha, mradi huu umesimamiwa na Kitengo cha Usimamizi wa Miradi cha Wakala ya Barabara Tanzania - TANROADS (TECU) kutoka Mkoa wa Tabora.
Pamoja na mafanikio ya mradi, changamoto kubwa imejitokeza ikiwemo wizi wa alama za barabarani.
Mpaka sasa, jumla ya alama 10 na mabango mawili ya mradi vimeripotiwa kuibwa, hali inayohatarisha usalama wa watumiaji wa barabara.
Katika juhudi za kudhibiti hali hiyo, vyombo vya ulinzi na usalama vikishirikiana na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora vimemkamata mtuhumiwa mmoja, Moshi Luponya, mkazi wa Kijiji cha Tarehe Moja, Kata ya Usinge. Mtuhumiwa anashikiliwa na kwa kesi ya kuhujumu miundombinu ya serikali chini ya RB Na. USNG/RB/37/2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Kaliua.
Kwa sasa, kazi zinazokamilishwa ni pamoja na ufungaji wa taa za barabarani, ujenzi wa barabara za maingilio, na upakaji rangi.
Wakazi wa Tabora na Kigoma wamepokea mradi huu kwa matumaini makubwa, wakiamini utaimarisha uchumi kwa kuboresha usafirishaji wa mazao, biashara, na huduma za kijamii.
View: https://youtu.be/zv0jGPj2M8c?feature=shared