Hatimaye zile Km 51 zilizokuwa na vumbi zimekamilka. Sasa kutoka Dar hadi Kigoma ni lami

Hatimaye zile Km 51 zilizokuwa na vumbi zimekamilka. Sasa kutoka Dar hadi Kigoma ni lami

Kuna bonge la mbuga ya selous hapo je barabara hiyo ina umhimu wowote? Na je itakuwa lami ama vumbi?
Hata Sasa Kuna Barabara hapo ila ni ya vumbi.

Hiyo haitakuja Barabara ya kwanza kupita mbugani na in fact inatakiwa ipite hapo Kwa Ajili ya kufungua Utalii zaidi huko Kusini.
 
Hiyo naona ni Singida-Iringa-moro-Lindi-Ruvuma bonge la barabara mpya haijawahi kuwepo na itagharimu matrioni mzee, hiyo labda wajenge kizazi kijacho 2050 huko
Hakuna Cha Matrilioni yeyote hapo,pesa kama zile za Kujenga daraja la JPM linatosha kumaliza hiyo Barabara ,kimsingi ni uamzi tuu Wala haifiki hata Trilioni 1.Section ngumu ni hiyo ya Kutoka Kilolo-Morogoro-Ulanga kwingine ni tambarare na swamps ambazo zinajengeka japo inaweza kuwa time consuming.

Mimi ningekuwa kwenye vitengo vya mipango au ushauri wa Rais ninge priotise hizo Barabara maana zinafungua uchumi na kutoa relief Kwa Barabara zilizopo.
Screenshot_20241113-134043.jpg
 
Mwaka Jana niliweka mada hapa kwamba Zimesalia km 51 za vumbi Ili Barabara yote kutoka Dar Hadi Kigoma iwe Lami.

Hatimaye km za mwisho kutoka Ilunde-Malagarasi zimekamilika na Sasa Kigoma sio mwisho wa reli tena.Serikali ya Rais Samia imewakomboa watu wa Kigoma na Tabora. Soma hapa Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami

Sasa Serikali iweke Nguvu kwenye Barabara zifuatazo

-Mbeya-Tabora
-Songea-Morogoro
-Njombe-Morogoro
-Arusha-Musoma
-Mpanda-Kigoma
-Tanga-Singida
-Iringa-Morogiro-Lindi.

===

Ujenzi wa barabara ya Kaliua - Malagarasi - Ilunde (km 156) na kipande cha Kazilambwa - Chagu (km 36) umekamilika kwa asilimia 100, huku kazi za nyongeza kwenye barabara ya Ugansa - Usinge (km 7.4) zikifikia asilimia 98.5.

Barabara hii, yenye umuhimu mkubwa wa kiuchumi na kijamii, imejengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi 48.6 bilioni, ambapo Mfuko wa OPEC umefadhili asilimia 95 ya mradi huku Serikali ya Tanzania ikigharamia asilimia 5.

Mradi huu ulianza kutekelezwa tarehe 3 Agosti 2020, baada ya upembuzi yakinifu uliofanywa mwaka 2009 na kampuni ya Crowntech Consult Ltd kwa gharama ya shilingi 134.4 milioni.

Serikali ya Tanzania ilianza kufadhili ujenzi huo kwa asilimia 100, kabla ya Mfuko wa OPEC kuingia kama mfadhili mkuu mwaka 2021.

Wakazi 199 wa vijiji vya Ugansa na Malanga walilipwa fidia ya jumla ya shilingi 725.3 milioni kupisha ujenzi huo, huku gharama za usimamizi wa mradi zikifikia shilingi 2.2 bilioni kwa kipindi chote cha utekelezaji.

Aidha, mradi huu umesimamiwa na Kitengo cha Usimamizi wa Miradi cha Wakala ya Barabara Tanzania - TANROADS (TECU) kutoka Mkoa wa Tabora.

Pamoja na mafanikio ya mradi, changamoto kubwa imejitokeza ikiwemo wizi wa alama za barabarani.

Mpaka sasa, jumla ya alama 10 na mabango mawili ya mradi vimeripotiwa kuibwa, hali inayohatarisha usalama wa watumiaji wa barabara.

Katika juhudi za kudhibiti hali hiyo, vyombo vya ulinzi na usalama vikishirikiana na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora vimemkamata mtuhumiwa mmoja, Moshi Luponya, mkazi wa Kijiji cha Tarehe Moja, Kata ya Usinge. Mtuhumiwa anashikiliwa na kwa kesi ya kuhujumu miundombinu ya serikali chini ya RB Na. USNG/RB/37/2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Kaliua.

Kwa sasa, kazi zinazokamilishwa ni pamoja na ufungaji wa taa za barabarani, ujenzi wa barabara za maingilio, na upakaji rangi.

Wakazi wa Tabora na Kigoma wamepokea mradi huu kwa matumaini makubwa, wakiamini utaimarisha uchumi kwa kuboresha usafirishaji wa mazao, biashara, na huduma za kijamii.

1. Merarerani - Simanjiro- Kibaya - Dodoma
2. Geita - Kahama
3. Makongorosi chunya - Tabora
4. Manyoni - Itigi - Ruangwa - Makongorosi chunya
5. Dodoma - Iringa
6. Sanya Juu Kilimanjaro - Namanga
7. Matundasi chunya - Itumbi chunya
 
Bado Eneo La Kutoka Uvinza Kuelekea Tabora Halina Lami Lote
 
Hakuna Cha Matrilioni yeyote hapo,pesa kama zile za Kujenga daraja la JPM linatosha kumaliza hiyo Barabara ,kimsingi ni uamzi tuu Wala haifiki hata Trilioni 1.Section ngumu ni hiyo ya Kutoka Kilolo-Morogoro-Ulanga kwingine ni tambarare na swamps ambazo zinajengeka japo inaweza kuwa time consuming.

Mimi ningekuwa kwenye vitengo vya mipango au ushauri wa Rais ninge priotise hizo Barabara maana zinafungua uchumi na kutoa relief Kwa Barabara zilizopo.
View attachment 3218393
Hiyo barabara ni km zaidi ya 1000 sasa kama km ya vumbi hugharimu

Hapo unaongelea km 1500 na km1 huchongwa kwa 1B so km1500 = 1.5 Trilion
Hiyo hela kwa sasa hamna
 
1. Merarerani - Simanjiro- Kibaya - Dodoma
2. Geita - Kahama
3. Makongorosi chunya - Tabora
4. Manyoni - Itigi - Ruangwa - Makongorosi chunya
5. Dodoma - Iringa
6. Sanya Juu Kilimanjaro - Namanga
7. Matundasi chunya - Itumbi chunya
 
Ukisema serikali ya samia imewakomboa ni utaahira.Hizo bara bara zimejengwa kwa kiasi kikubwa na awamu zilizopita hasa JK.Toa credit kwa awamu zote
ili kuweka mambo ilitakiwa aseme hivi, "wananchi wanaishukuru serikali" au wananchi wanaishukuru serikali chini ya mh.rais dr. Samiah
 
Tanganyika tusipoamka tunapiga na mjinga mmoja ikifika 2030, tutalia machozi.
Huyu anataka Umeya,wakati alifukuzwa Umeya😳, ila anajishika naye Kila Kona.
Hali ni mbaya sana ,hakuna anayefanya KAZI ya kuleta kipato Kila mtu Kila saa, mama ,mama,mama
 
Attachments

  • IMG-20250130-WA0022.jpg
    IMG-20250130-WA0022.jpg
    129.4 KB · Views: 1
  • IMG-20250130-WA0021.jpg
    IMG-20250130-WA0021.jpg
    83.2 KB · Views: 1
  • IMG-20250130-WA0019.jpg
    IMG-20250130-WA0019.jpg
    82.4 KB · Views: 1
  • VID-20250130-WA0023.mp4
    7.4 MB
Hiyo barabara ni km zaidi ya 1000 sasa kama km ya vumbi hugharimu
Hapo unaongelea km 1500 na km1 huchongwa kwa 1B so km1500 = 1.5 Trilion
Hiyo hela kwa sasa hamna
Haifiki huo urefu na hata kama ingefika Wala hakuna tatizo Kwa sababu kama tunajenga Sgr km less than 400 inafika kuanzia Trilioni 3 na zaidi Kuna shida gani kwenye Barabara?

Kwanza Barabara Kila km 1 unayoikamilisha inaanza Kuzalisha tofauti na reli Hadi ikamilike yote ulete treni sijui nini yaani ni hasara kujenga reli kuliko Barabara.
 
Tanganyika tusipoamka tunapiga na mjinga mmoja ikifika 2030, tutalia machozi.
Huyu anataka Umeya,wakati alifukuzwa Umeya😳, ila anajishika naye Kila Kona.
Hali ni mbaya sana ,hakuna anayefanya KAZI ya kuleta kipato Kila mtu Kila saa, mama ,mama,mama
Kwani wewe umekatazwa kuweka picha za Rais na kuutaja umeya ? Una ujinga mwingi
 
Kama sio vipaombele kubadilishwa na Magufuli Kwa Sasa Nchi yote ingekuwa lami na hivyo Nguvu ingekuwa kwenye Sgr.

By the way mama anaendelea kupiga mwingi sana kwenye Barabara,kabla ya 2030 Barabara zote kuu zitakuwa na lami.
Weka na takwimu za deni la taifa
 
Back
Top Bottom