Hatimaye zile Km 51 zilizokuwa na vumbi zimekamilka. Sasa kutoka Dar hadi Kigoma ni lami

Mwaka Jana niliweka mada hapa kwamba Zimesalia km 51 za vumbi Ili Barabara yote kutoka Dar Hadi Kigoma iwe Lami.

Hatimaye km za mwisho kutoka Ilunde-Malagarasi zimekamilika na Sasa Kigoma sio mwisho wa reli tena.Serikali ya Rais Samia imewakomboa watu wa Kigoma na Tabora. Soma hapa Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami.
View attachment 3218390

Sasa Serikali iweke Nguvu kwenye Barabara zifuatazo

-Mbeya-Tabora
-Songea-Morogoro
-Njombe-Morogoro
-Arusha-Musoma
-Mpanda-Kigoma
-Tanga-Singida
-Iringa-Morogiro-Lindi.
View attachment 3218389

View attachment 3218321
===

Ujenzi wa barabara ya Kaliua - Malagarasi - Ilunde (km 156) na kipande cha Kazilambwa - Chagu (km 36) umekamilika kwa asilimia 100, huku kazi za nyongeza kwenye barabara ya Ugansa - Usinge (km 7.4) zikifikia asilimia 98.5.

Barabara hii, yenye umuhimu mkubwa wa kiuchumi na kijamii, imejengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi 48.6 bilioni, ambapo Mfuko wa OPEC umefadhili asilimia 95 ya mradi huku Serikali ya Tanzania ikigharamia asilimia 5.

Mradi huu ulianza kutekelezwa tarehe 3 Agosti 2020, baada ya upembuzi yakinifu uliofanywa mwaka 2009 na kampuni ya Crowntech Consult Ltd kwa gharama ya shilingi 134.4 milioni.

Serikali ya Tanzania ilianza kufadhili ujenzi huo kwa asilimia 100, kabla ya Mfuko wa OPEC kuingia kama mfadhili mkuu mwaka 2021.

Wakazi 199 wa vijiji vya Ugansa na Malanga walilipwa fidia ya jumla ya shilingi 725.3 milioni kupisha ujenzi huo, huku gharama za usimamizi wa mradi zikifikia shilingi 2.2 bilioni kwa kipindi chote cha utekelezaji.

Aidha, mradi huu umesimamiwa na Kitengo cha Usimamizi wa Miradi cha Wakala ya Barabara Tanzania - TANROADS (TECU) kutoka Mkoa wa Tabora.

Pamoja na mafanikio ya mradi, changamoto kubwa imejitokeza ikiwemo wizi wa alama za barabarani.

Mpaka sasa, jumla ya alama 10 na mabango mawili ya mradi vimeripotiwa kuibwa, hali inayohatarisha usalama wa watumiaji wa barabara.

Katika juhudi za kudhibiti hali hiyo, vyombo vya ulinzi na usalama vikishirikiana na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora vimemkamata mtuhumiwa mmoja, Moshi Luponya, mkazi wa Kijiji cha Tarehe Moja, Kata ya Usinge. Mtuhumiwa anashikiliwa na kwa kesi ya kuhujumu miundombinu ya serikali chini ya RB Na. USNG/RB/37/2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Kaliua.

Kwa sasa, kazi zinazokamilishwa ni pamoja na ufungaji wa taa za barabarani, ujenzi wa barabara za maingilio, na upakaji rangi.

Wakazi wa Tabora na Kigoma wamepokea mradi huu kwa matumaini makubwa, wakiamini utaimarisha uchumi kwa kuboresha usafirishaji wa mazao, biashara, na huduma za kijamii.

Arusha to Musoma n ngumu hizo vipande vya hifadhi ya Serenget na Ngorongoro walitaka kuweka mamlaka zilikataa kwa sababu ya nature ndy maana imebaki mpaka sasa
 
Hawajakataa popote na hata kama walikataa hawatupangii na ujenzi unaendelea.

Kwani Kuna zuia nini hapo kuweka fence na vivuko vya wanyama?

Na zile sehemu zingine ambazo Hazina fence kujenga Kwa teknolonia ya mawe Ili kudhibiti speed?

Watu hawajaishiwa akili.
 
N kwl ila walitowa sababu lukuki kuwa cha kwanza kupoteza asili wanyama kuhama pia barabara ipo ya kupitia mwanza so ile n kama ya ziada
 
Binadamu hajaishiwa maarifa hizo ni propaganda za Wakenya kuzuia maendeleo ya Utalii wa Tanzania.

Serikali itajenga Kwa modelity niliyokueleza au laa wata divert sehemu ambazo haikatishi Kwa urefu hiyo Barabara na ujenzi unaendelea huko.

Tena sio Barabara tuu Hadi reli Iko mbioni .
 
🤣🤣🤣 tusubr
 
Pia naomba ile inayotoka tanzania kwenda jehanamu itengenezwe ile kuwarahisishia ccm kwenda kuungua jehanamu
 
ili kuweka mambo ilitakiwa aseme hivi, "wananchi wanaishukuru serikali" au wananchi wanaishukuru serikali chini ya mh.rais dr. Samiah
Wanaishukuru serikali kwa lipi, kwani hizo barabara si zinajengwa kwa kodi zetu na kama ni mikopo si ni sisi wananchi ndio tutazilipa kwa kodi zetu.

Serikali yoyote iliyopo madarakani ni lazima itajenga hizo barabara. Kwani mnafikiri wananchi ni wajinga tu siku zote. Acheni kuleta siasa za kijinga.
 
Sasa ww taahira umesema section ya mwisho ndio ilianza 2022 ,maana yake hizo section nyingine zilijengwa na makalio yako?
Hizo section nyingine zina KM ngapi ukilinganisha na hiyo ya mwisho?
Akili yako ni finyu sana
Baada ya vizee vichawi vingi Kigoma kufariki dunia sasa maendeleo yameanza kuonekana kigoma
 
Mkuu hauna update za mradi wa rami kutoka Namanyere mpaka kirando ili kuweza kuunganisha Bandari ya kipiri ? Maana njia hii ni muhimu kwa uchumi wa wilaya ya Nkasi na mkoa kwa ujumla wake.
Kwa kuzingatia kichwa cha habari ,hii taarifa unayotoa hapa si sahihi.Kipande cha kibaoni uvinza mpaka kijiji cha chakuru bado
 
Mwaka Jana niliweka mada hapa kwamba Zimesalia km 51 za vumbi Ili Barabara yote kutoka Dar Hadi Kigoma iwe Lami.

Hatimaye km za mwisho kutoka Ilunde-Malagarasi zimekamilika na Sasa Kigoma sio mwisho wa reli tena.Serikali ya Rais Samia imewakomboa watu wa Kigoma na Tabora. Soma hapa Bado Km 51 ili Kigoma-Dar iwe lami. Rais Samia anaenda kuunganisha mikoa yote kwa lami.
View attachment 3218390

Sasa Serikali iweke Nguvu kwenye Barabara zifuatazo

-Mbeya-Tabora
-Songea-Morogoro
-Njombe-Morogoro
-Arusha-Musoma
-Mpanda-Kigoma
-Tanga-Singida
-Iringa-Morogiro-Lindi.
View attachment 3218389

View attachment 3218321
===

Ujenzi wa barabara ya Kaliua - Malagarasi - Ilunde (km 156) na kipande cha Kazilambwa - Chagu (km 36) umekamilika kwa asilimia 100, huku kazi za nyongeza kwenye barabara ya Ugansa - Usinge (km 7.4) zikifikia asilimia 98.5.

Barabara hii, yenye umuhimu mkubwa wa kiuchumi na kijamii, imejengwa kwa kiwango cha lami kwa gharama ya shilingi 48.6 bilioni, ambapo Mfuko wa OPEC umefadhili asilimia 95 ya mradi huku Serikali ya Tanzania ikigharamia asilimia 5.

Mradi huu ulianza kutekelezwa tarehe 3 Agosti 2020, baada ya upembuzi yakinifu uliofanywa mwaka 2009 na kampuni ya Crowntech Consult Ltd kwa gharama ya shilingi 134.4 milioni.

Serikali ya Tanzania ilianza kufadhili ujenzi huo kwa asilimia 100, kabla ya Mfuko wa OPEC kuingia kama mfadhili mkuu mwaka 2021.

Wakazi 199 wa vijiji vya Ugansa na Malanga walilipwa fidia ya jumla ya shilingi 725.3 milioni kupisha ujenzi huo, huku gharama za usimamizi wa mradi zikifikia shilingi 2.2 bilioni kwa kipindi chote cha utekelezaji.

Aidha, mradi huu umesimamiwa na Kitengo cha Usimamizi wa Miradi cha Wakala ya Barabara Tanzania - TANROADS (TECU) kutoka Mkoa wa Tabora.

Pamoja na mafanikio ya mradi, changamoto kubwa imejitokeza ikiwemo wizi wa alama za barabarani.

Mpaka sasa, jumla ya alama 10 na mabango mawili ya mradi vimeripotiwa kuibwa, hali inayohatarisha usalama wa watumiaji wa barabara.

Katika juhudi za kudhibiti hali hiyo, vyombo vya ulinzi na usalama vikishirikiana na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tabora vimemkamata mtuhumiwa mmoja, Moshi Luponya, mkazi wa Kijiji cha Tarehe Moja, Kata ya Usinge. Mtuhumiwa anashikiliwa na kwa kesi ya kuhujumu miundombinu ya serikali chini ya RB Na. USNG/RB/37/2024 katika Mahakama ya Wilaya ya Kaliua.

Kwa sasa, kazi zinazokamilishwa ni pamoja na ufungaji wa taa za barabarani, ujenzi wa barabara za maingilio, na upakaji rangi.

Wakazi wa Tabora na Kigoma wamepokea mradi huu kwa matumaini makubwa, wakiamini utaimarisha uchumi kwa kuboresha usafirishaji wa mazao, biashara, na huduma za kijamii.

Sawa,ngoja nikusanye hela ya mafuta Krimass nikalie Kigoma...
 
Wanaishukuru serikali kwa lipi, kwani hizo barabara si zinajengwa kwa kodi zetu na kama ni mikopo si ni sisi wananchi ndio tutazilipa kwa kodi zetu.

Serikali yoyote iliyopo madarakani ni lazima itajenga hizo barabara. Kwani mnafikiri wananchi ni wajinga tu siku zote. Acheni kuleta siasa za kijinga.
Kama zinajengwa Kwa Kodi zako ndio hawapaswi kunishukuru Serikali?
 
Back
Top Bottom