Hatma ya maisha baada ya tukio hili

Hatma ya maisha baada ya tukio hili

fundinaizer

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2016
Posts
1,758
Reaction score
2,713
Wahenga walisema mficha uchi hazai.
Mie ni kijana wa mwaka wa kwanza niliepata nafasi ya kujiunga na masomo ya elimu ya juu katika chuo flani kikubwa hapa jijini DSM, Sina muda mrefu tangu nikamilishe usajili/bado mgeni.
Kutokana na ukarimu na kupenda kucheka na watu nilifanikiwa kufahamika na wanafunzi wenzangu wa mwaka wa kwanza ndani ya muda mfupi mpaka siku ya ijumaa iliyipita nikiwa nimepitiwa usinginzi ndani ya lecturing room nikajikuta nimetoa hewa chafu/kujamba bahati mbaya ni kwa sauti kubwa.
Kiufupi Rinda liko vizuri ila ni kutokana na udhaifu wa kibinadamu nikajikuta nachekwa sana baada ya kipindi kuisha.
Nazungumza nikiwa Hostel sijatoka tangu juzi na mbaya zaidi vipindi vinaendelea, najaribu kujikaza niende maana Fame ndo imeniponza.
Nakaribisha ushairi na maoni yenye kunijaza ujasiri kesho niingie kipindi.
My take: Rinda liko fiti.
 
[emoji16] [emoji16]
Zuga mpaka uzoee tu mkuu, wakikutania we kubali huku unachukulia utani tena unahadithia kwa kuikuza story,

Ikiwezekana anaekuangalia tu unaropoka vip nitoe kingine uhame na leo nimekula magarage mabichi? Utazoea
 
Zuga mpaka uzoeen tu mkuu, wakikutania we kubali huku unachukulia utani tena unahathia kwa kuikuza story,

Ikiwezekana anaekuamgalia tu unaropoka vip nitoe kingine uhame na leo nimekula magarage mabichi? Utazoea
Ushauri uliotukuka, Ngoja nipasi nguo kabisa
 
Mbona kitu cha kawaida mkuu. Kwani ndo mala yako ya kwanza kusikia?
 
Wewe ungekuwa na elimu unayojinasibishanayo usingeandika upuuzi huu.
 
Hahahaha darasani Makete, Mwakavuta Secondary School, A Level.
Kijana mtata kabisa sitamtaja jina ila ni mweusiiiii anatokea mkoa wa Mara anaachia bonge la shuzi mpaka mwalimu akafikiri kuna mtu karusha jiwe juu ya bati.

Shule pale kuachia shuzi tulikua tunaita kukata nyuzi, sasa ndugu yetu alikua amekata jinyuzi.
 
Kawaida. Iliwahi nitokea nikiwa la5, kwa aibu nikamfokea dada wawatu, kumbe mwalimu ameshaniona. Mwalimu alichek hadi mwisho. Nilitokwa na jasho.
 
Back
Top Bottom