Oficial chawa
Member
- Jun 15, 2022
- 8
- 15
Let stori mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante ila jikaze uandike andikeIlipoishiaa[emoji1484]
Tukaagana mzee alinichukulia moja ya tax zilizokuwa zimepark nje ya Ile hoteli, yeye akaingia ndani ya Alphard akaondoka na Mimi nikashika njia ya kuelekea Tabata
Inaendelea [emoji1484]
Tax ilinifikisha hadi mjengoni kwangu Tabata I mean nilikopanga, (hamkawii kusema "mbona mwanzo wa story hukusema kama umejenga[emoji849]) nikaingia mjengoni, nikakuta nyumba ipo kimya, Leo nilikuwa nina jambo na Wifi/Shemeji yenu, so nilijua nitamkuta kashafika nikampigia simu ikawa inatumika, nikaachana nayo nikaenda zangu kuoga, natoka kuoga nikasikia simu inaita nikaipuuzia nikawa nachagua nguo za kuvaa, Sasa nimemaliza kuvaa nashika simu ili nimpigie wifi yenu kumbe Ile missed call haikuwa ya kwake kama nilivyodhania, Ilikuwa ni missed call ya Mzee,
Nikampigia akapokea vipi Mzee ulifika salama "yeah Nilifika muda kidogo, nilikuwa nataka kukuuliza Kuna Kitu chochote ulisahau huku au Kuna Kitu umepoteza?" hapana mzee sidhani kama Kuna Kitu nimesahau au kupoteza "Inaonekana una shida kwenye swala la kumbukumbu, Kuna bahasha hapa niliiona tangu jana, leo nimefungua ndani nimekuta Documents za TRA na nimejua ni ya kwako kwasababu nimeona Jina la Kampuni yenu" Dah kweli Mzee nilisahau kabisa nilitakiwa kumpatia Accountant ile Ijumaa lakini hakuwepo......tulimaliza kuongea na Mzee akanambia nizifuate nikipata muda sababu wiki hii yote hatokuja town wala Ofisini kwake
Nikamcheki tena Demu wangu (anaitwa Annie, really name, hii code haina madhara nikiifungua) kupiga simu bado inatumika, nikaona hii ni too much Sasa, Dakika 30 zimepita mtu bado anaongea na simu tu, nikaona nikiendelea kumuwaza nitajipa stress tu nikawasha zangu Tv nikaweka Series ya Kings of Jo'Burg Wakati na naendelea ku watch katikati ya series huko Demu ndio anapiga eti, makasiriko kama yote na ananijua akaanza kuomba msamaha, kabla hajaongea sana nikaanza kumpa lecture uzuri wa Demu wangu nikiongea yeye huwa anakaa kimya kunisikiliza hadi nimalize
Nikaanza kumsomea>>>Nimeenda kuoga nimemaliza naweza movie naangalia karibia inaisha na wewe ndio unamaliza huo mkutano wako au siku hizi umekuwa Customer care na huniambii, kama umekua Customer Care inabidi uwe special phone wenzako hawatumii hizi simu za kawaida, Simu ya mkononi ilimaanishwa kuongea 'less than 10 minutes' kwasababu 'microwave' zinazosafirishwa na simu yako ukiongea zaidi ya dakika 10 una increase level yao inakuwa troublesome kwa brain yako kwasababu hizi simu tunazotumia zipo wireless.
Akajibu kwa upole "Sawa umeeleweka Boss lakini mimi nilikuwa nakuomba msamaha kwa kuchelewa kuja huko, aliyekuwa anaongea na simu sio Mimi ni rafiki yangu alikuwa anaongea na bwana ake ndio nilikuwa namsubiria amalize ili nikupigie" Okay mambo yasiwe mengi wewe kama unakuja we njoo ila hakikisha umebeba chakula Cha Supper kabisa (mida hiyo ilikuwa around 6:+PM)
Kweli bhana mchuchu kwenye saa mbili mbili hivi akawasili, tukapiga misosi watu wakashiba, Sasa Demu wangu nikiwaga nae ni lazima ashike simu yangu huwaga siwekagi password Sasa akiwa nayo yeye moja kwa moja anaenda kwenye messages kuangalia Jina la H....Accountant kuangalia kama kuna chats zote akikosa anaenda kwenye Call Logs anaangalia kama nilimpia au alinipigia akikuta vyovyote vile anaangalia muda tuliotumia kuzungumza akikuta zimezidi dakika 3 tu, basi anajua hayo maongezi hayakuwa ya kawaida, Sasa Leo katika kupekua akakuta nimeongeza na H.....Accountant kwa dakika 11 kesi ikaanzia hapo "kweli hizi Dakika zote mlikuwa mnazungumzia kazi tu au ndio hivyo tena nijihesabie Sina changu" Nikaona huyu kashaanza kesi zimeanza kufufuliwa upya
Iko hivi, kwenye hii Kampuni ninayofanya kazi sasa hivi nilipata kazi kupitia huyu H...Accountant ambaye nilisoma naye na nilikuwa namsaidia mambo kadhaa yanayohusiana na taaluma, Sasa huyu Demu bana tangu tupo chuo ananipendaga sema alikuwa anashindwa kunichana Sababu ya misimo yangu, ila mm simuelewi (kipindi hiki ndio nilianza Mahusiano na Annie) Sasa tulivyomaliza chuo Mimi nilivyoona ramani hazisomeki nikajikataa zangu nikaibukia Nairobi, hustle sana huko ngoma bila bila,
Nakumbuka Siku moja nimetoka Bypass ya Ruai naelekea Utawala kwa Chief (Quick mart) nimepanda matatu (Daladala) Ile matatu ilikuwa na wi-fi password wameandia chini ya screen, nikatumia fursa ili pesa ya Bando ikafanye mambo mengine, Sasa ile nimeconnect tu message ya kwanza Whatsapp ni ya huyo H....Accountant (wakati huo nilimsave tu H.....hiyo 'Accountant' haikuwepo) Ile msg ilikuwa inasema "BM Kuna nafasi ya kazi ya ***** kama itakufaa nambie nikulindie nafasi" Sasa wakati tunafanya Conversation ilibidi nisishuke stage (kituo) niliyokuwa nashuka kwasababu ya Wi-fi, nilienda kushukia Shutazi (Shooters) ikabidi nitembee kutoka Shutazi hadi mahali nilikuwa naenda kwa Chief
Sasa katika Yale mazungumzo kwakifupi tu ni kwamba nilikubali Offer nikamwambia Accountant najianda siku mbili tatu wiki ijayo Niko Dar es salaam, Hapo ndio nilipoachana na jiji la Stress, ule mji acha tu ningekua muandishi ningetoa kitabu kabisa
Mtu mzima nikaingia Daslam kubadilisha upepo, nilijoin kwenye Kampuni fresh na Kazi ikachapwa ikachapika, nikamuona huyu Demu (Accountant) kabadilika kabadilika Yani zile Fujo za chuoni kule simuoni nazo tena nikajua kakua maana wanasema vitu vingine vinasababishwa na utoto, kumbe Binti ananivutia Kasi ananizoom tu hakutaka papara, unajua hii Kampuni ni yao yeye ndio Muhasibu nahisi alikuwa anacheza na timing
Kuna siku hiyo bhana sitoisahau aliniita Ofisini kwake, nikaketi "naona siku hizi unanawili tu kijana jiji linakupenda hili lakini wewe hulitaki unajifanya kupenda nchi za watu, hivi ni Kwanini wanaokupenda huwapendi?" nikamuuliza unamaanisha nini? "Ukiwa Dar uHandsome wako ndio unakuwa kwenye ubora wake tofauti na ulivyokuwa Nairobi pengine hili ulikuwa hulijui, lakini nina uhakika unajua kwamba Mimi nakupenda. ndio maana nikasema wanaokupenda unawapuuzia!" nikaona huyu kumbe hajaacha mambo yake tu, Nikamwambia swala Dar sijui Nairobi hilo lipo kimaisha zaidi Sababu Nairobi sijaenda kama mtalii nikimaanisha kwamba sijaenda kwa kupenda bali kutafuta maisha, Sasa nilivyomjibu hivyo nikawa ndio nimeharibu kabisa[emoji1544]
"Kwahiyo Mimi kukupenda sio swala la kimaisha, hivi nikuulize unadai kwamba ulienda huko Nairobi kutafuta maisha, hayo maisha uliyapata? badala yake maisha umekuja kuyapatia Dar na hiyo yote ni kwasababu ya Upendo wangu kwako, Yani kama sio Upendo usingekua hapa Upendo wangu unaoudharau ndio unakupa maisha, hivi unajua kwamba Mtu anaweza kukusaidia viatu na bado akakukata Miguu. tunaishi kwenye Dunia yenye Unafki Sasa mm sijataka kuwa mnafki kwako nimekuambia ukweli" hii kauli yake ikazidi kunichanganya, kwanza huu ujasiri ameutolea wapi huyu, nikajisemea tu moyoni Leo ndio Ile siku, mara akaingia mama yake ambaye kwa hapa Tanzania yeye ndio anaiongoza Kampuni, ilibidi maongezi yaishie pale, na huyu Mama ananikubali sana nitakuja kueleza huko mbele ni kwasababu gani
"Tutaongea badae BM" alinambia hivyo yule Demu Mimi nikaondoka zangu....
Turudi Leo,>>>hiyo Sasa ndio sababu ya huyu Demu wangu kuwa na wivu sana sasa Visa vyote nilimuhadithia yani amefikia hatua ananiambia niache kazi[emoji849] ni kama hajiamini anajua muda wowote meza inapinduliwa na Accountant ila kiukweli kabisa Demu wangu ni PISI KALI nyie acheni tu, nampenda sana japokuwa hata Accountant ni Pisi lakini hajamfikia Mama lao,
Nikamwambia Annie kama umechoka nenda kalale hatuwezi kujadili jambo moja kila siku, akaniangalia machoni kwa sekunde kadhaa akaenda Bedroom kinyonge sana, Asee nilibaki naiangalia Ile series lakini haipandi nahisi kama nimemjibu kimkato sana manzi angu, nilizima Tv nikaingia chumbani, nikamkuta wifi yenu amelala lakini yupo macho kama ana waza kitu nikawa najiuliza huyu anawaza ya kwake au ni Yale Yale ya Sebuleni? nikajidai kuzuga nikamuuliza hivi umekuja na funguo zako au itabidi kesho nikuachie za kwangu nikitoka?.....kimya!!![emoji849] nikaona hapa vinyongo vishaanza wale wenye vipaji vya kubembeleza hapa ndio wanahitajika, Nikamwambia Annie unanijua kabisa Mimi upande wa kubembeleza sipo vizuri, naomba niambie tu wewe mwenyewe kama nimekukwaza nijue kama nilikuwa sahihi kukukwaza au nimekuonea "na sitaki unibembeleze ndio maana nilikuacha sitting room" nikamwambia sawa lakini mimi sitaki vinyongo kama Kuna sehemu hujapenda nilivyokuongelesha we nambie, Annie akanipiga jicho flani nikawa nishagundua Kitu
Mimi nipo hivi nikafanya kosa (hasa katika Mahusiano ya kimapenzi) siwezi kukiri tu mwenyewe kwamba nimekosea, hadi uniambie mwenyewe, Sasa lile jicho la Annie ni kama alikuwa anasema ("Yani wewe sijui ukoje") Mwanaume nikakaza nikazima taa nikalala
Asubuhi ikafika mida ya kwenda kazi ikafika ila nikajidai kupitiwa na usingizi kuna nilikuwa nataka kujua, Annie akilala kwangu Asubuhi ni lazima aniamshe hata kama sio siku ya kazi ila kama hajaniamsha Najua Kuna jambo, na kawaida yake huwa anaamka mapema sana, hata kama hana kazi utamkuta anaangalia Movie, halafu aina za Movie au Series anazoangaliaga sasa ni zile za ki Gangster kama Ile Kings of Jo'Burg yeye ndio kaileta,
Sasa zimepita kama Dakika 10 naona siamshwi, nikajua tu huyu mwanamke yale ya Jana bado hayajaisha ninachokipima hakipimiki, nikajiamsha mwenyewe chooni hamna mtu naenda sebuleni sikuti mtu mazingira yakaonesha kwamba huyu mtu hayupo hiyo ni saa moja kasoro Asubuhi, nikaenda zangu kuoga nimeshajianda nachukua simu nitoke kucheki Kuna Messages 2 moja ya Annie nyingine ni ya Mzee,
Ya Annie ilikuwa inasema "Naweza nisiwe mwema leo lakini isikufanye usahau wema wangu wa jana, tumia wema wangu wa jana kunirekebisha ili niwe mwema zaidi, Najua makosa ni ya kwako lakini naomba msamaha Mimi, Naomba nisamehe kama nilikukwaza jana".
Na meseji ya Mzee ndio ikanivuruga zaidi, ilibidi kwanza nikae chini aliandka "kila unapocheka hakikisha unaandaa mazingira ya utakapolilia"
INAENDELEA
So Leo ndo basi hvo?Madam, Kesho nakuja na The Guardian [emoji2786]
Maliza mzigo..Madam, Kesho nakuja na The Guardian [emoji2786]
Asante bro kwa mwendelezo, lakini mbona inaonyesha itaendelea sana tofauti na ulivyosema jana?Ilipoishiaa[emoji1484]

Bonge la Msamiati“Ni ngumu kuyafanya maisha magumu kuwa rahisi ila ni rahisi kuyafanya maisha rahisi kuwa magumu”
“Ni rahisi kuutibu ugonjwa unapoanza ingawa ni ngumu kuugundua, ni ngumu kuutibu ugonjwa uliokwisha kua ingawa ni rahisi kuugundua”
Hiyo inaitwa kuwashughulisha wasomaji ili wasitembee haraka na uzi.Hivi hilo neno "wifi yenu" unamanisha wasomaji wote wa riwaya yako ni jinsia ya ke?
Picha ya annie pls hata mkono tu