Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

I like the fact kwamba mzee hajamfungia bi mkubwa tracker,hiyo Ni heshima kubwa alonayo mzee.wanaume mna la kujufunza hapa.
Sijajua the logic behind kutoifungia tracker gari ya mkewe? tusaidie ulichoelewa ili tujifunze
 
Kuna wkt inaonekana kuna shughuli zake hatamani mto yyte kujua Yuko wap kwa hyo iyo gar inakuwa choice nzuri kutumia na ilivyo ni kama haijulikani HV Kwa kuwa haitok mara Kwa mara security purposes hyo gari inafaa
 
I like the fact kwamba mzee hajamfungia bi mkubwa tracker,hiyo Ni heshima kubwa alonayo mzee.wanaume mna la kujufunza hapa.
Nafikiri kwa sisi wanaume ukioa na ukawa unampenda mkeo, basi usimchunguze wala kumfuatilia kama ana cheat. Na usithubutu kumfumania, kama humuamini bora umuache tu lakini usijaribu kumfumania.

Maumivu ya kufumania kwa wanaume huwa hayaishi na ni sumu mbaya sana. Usiharibu furaha ktk maisha yako kwa kujaribu kufumania.

Na sie wanaume hakikisha haukiri kufumaniwa hata ukikutwa live...it wasn't me. The more you denied, slowly it vanishes kuliko kukubali inathibitisha maumivu kwa mwenzio. Kataa, kataa, hata kama sababu unayoshikilia kujitetea ni ya kijinga kamatia hiyohiyo kamwe usikiri.

Ni hayo tu.
 
Well said mkuu
 
Sijajua the logic behind kutoifungia tracker gari ya mkewe? tusaidie ulichoelewa ili tujifunze
Sina hakika,lakini Ni Jambo jema maana anaepuka surprises.waswahili wanasema Bora nusu Shari kuliko Shari kamili lakini hata mzee pia anaweza kuitumia kwenye issue zake za siri
 
Inawezekana, sometimes na mimi nafunguka hadi najisahau[emoji2365]

Nakuomba hiyo Code ubaki nayo mkuu. Ifanye kama Figo
Me siwezi sema mkuu, Na nimekijua hicho kitu muda mrefu kweli ila hapa ni kama ulinikumbusha tu.

Uwe na amani....
 
I like the fact kwamba mzee hajamfungia bi mkubwa tracker,hiyo Ni heshima kubwa alonayo mzee.wanaume mna la kujufunza hapa.
Hajasema kama hajafunga au kafunga tracker kwenye gari ya mkewe kwa Sabab hakukuwa na sababu ya yeye kumueleza hilo bwana BM X6, kilichokuwa muhim kwa wakat huo ni habari ya akina caryn na Michelle tuu, kwa hyo inawezekana kamfungia hta mkewe ila ikawa ni Siri yake mwenyewe bhna.
 
Huyu mzee anataka uwe na binti yake caryn na caryn anakupenda sana ila ni kauzu hawezi kufunguka na wewe BMX6 hutokuja kufunguka kamwe kwake ila itakuja kutokea mta click tu na maisha yataendelea na Kila mtu kwenye familia na cycles zenu watajua na mwishoe ndoa itafungwa.Caryn hawezi kuishi na mtu mwingine zaidi ya BMX6 kwa hizo tabia zake ni BMX6 pekee ndio anaweza ku handle hizo kashikashi na hata mzee analijua Hilo na anataka liwe hivyo ila pia mzee anachezesha mambo kwa akili sana(manipulation) Ili ije kuwa hivyo.Coz I guess mzee anawaza sana kuhusu binti yake caryn atakuja kuwa salama kwa mtu wa aina ya BMX6 tu sio kwenye mikono ya mwingine
 
Naunga mkono hoja.

Kwasababu Kuu moja, kama ambavyo BM X6 ametuambia hapa kwamba mzee anamuamini sana Caryn kuliko wote kwenye familia yake,hivyo ni lazima ahakikishe anamuacha Binti yake kwenye mikono salama ili familia na utajiri alioutafuta uendelee kumea.
Ukizungatia mzee hajabahatika kupata mtoto wa kiume, hivyo BM X6 ndio kipaumbele kikubwa sana kwa sasa.
Michelle kashafeli kwenye kusaka mtu sahihi wa kufikia viwango ambavyo mzee anavihitaji. Hivyo anaona bora abet vema kwa Caryn kama jicho lake kuliko Michelle.
 
Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni , awali niliwahi kuuliza " sterling " wa story hii ni nani nikajibiwa ni huyo kijana wa Bugurun...hivyo basi BM x6 anafahamu mwanzo mwisho wa story hii na pengine ,kuandika kwake kwa story anajikumbusha alimopitia hadi kufikia hapo alipo ,,uhusika wa kijana wa Buguruni hadi BM x6 aseme hatma yake ya maisha ipo mikononi wa kijana wa Buguruni binafisi sijaupata ni sehem ipi navuta subira nifahamu Kijana wa Buguru i alihusika vipi hadi BM x6 ampigie magoti
 
Mkuu nilikuambia Sterling ni Kijana wa Buguruni kwa sababu kuu moja, huyo ndiye aliyenifanya nianzie huu Uzi, kama ulisoma story vizuri mwanzoni nilimchukua kijana wa Buguruni na kumsaidia ni kwasababu ya Mzee, Mzee alinitaka nifanye hivyo kwa yule kijana na kumuwezesha mtaji wa Biashara na kama endapo kijana atafaulu basi na mimi nitakuwa katika nafasi nzuri ya kusaidiwa na Mzee

Kwa akili yangu ya haraka haraka Mzee alifanya hivyo ili kutaka kuusoma uwezo wangu wa kusimamia Biashara hapo ndipo kijana wa Buguruni alitumika, kwasababu Mzee nilikuwa namuonesha Nia ya kufanya Biashara lakini kwa upande wake hakuwa na uhakika kama naweza kufanya au kusimamia Biashara coz kwa mujibu wake anasema unaweza ukawa na shauku ya kufanya Biashara lakini misingi yake ukawa huijui

Kwa mfano hapa juzi masaa machache kabla ya A day to remember nilipata hasara ya milioni 10 kwa uzembe uliotokea kazini, by that time hiyo issue inatokea Mzee alikuwa nje ya Nchi, baada ya siku mbili 3 ilibidi nimpigie na kumuelezea, wakati namuelezea situation iliyotokea ni kama alinisoma hali niliyokuwa nayo, (sikuwa sawa)

Mzee alinijibu simple sana, aliniambia "Kijana wangu relax, milioni 10 ni Hela ndogo sana, kwasasa ni mapema sana kwa wewe kuchanganyikiwa, kwasababu kwa aina ya Biashara uliyoniambia unataka kufanya, kipindi kile kupata hasara kama hiyo au na zaidi ni kitu cha kawaida sana, ndio maana nilitaka uanzie chini uzoee hio hali"

Hapa nakurudisha kwa kijana wa Buguruni, mpaka Mzee ananiambia nimfungulie huyo kijana Biashara na nimsimamie alijua tutakutana na kitu kinaitwa hasara so kwa nilivyomuelewa mimi ni kama alikuwa anataka nipate experience ya mambo mengi katika Biashara lakini pia na uzoefu wa kupata hasara ndogo ndogo na nijue jinsi ya kukabiliana nazo kabla sijaja kukutana na hizi kubwa kubwa, Kwa bahati mbaya ndio nimekuja kukutana nayo juzi

So kwa kipindi kile Kichwa Cha Uzi (title) na story yenyewe vilikuwa vinaendana na Kijana wa Buguruni alikuwa ana appear mara kwa mara lakini kadri siku zinavyoenda mambo yanabadilika

Kumbuka hii story inayoendelea kila siku, kwa mfano Leo kuna kitu kimenitokea so siku za mbeleni pengine nitakuja kukiandika, kama ingekuwa ni story iliyotokea kitambo kama unavyosema hapo sasa ndio ningekaa chini na kuchagua Heading ya Story kulingana na maudhui yake
 
Back
Top Bottom