Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Mkuu nilikuambia Sterling ni Kijana wa Buguruni kwa sababu kuu moja, huyo ndiye aliyenifanya nianzie huu Uzi, kama ulisoma story vizuri mwanzoni nilimchukua kijana wa Buguruni na kumsaidia ni kwasababu ya Mzee, Mzee alinitaka nifanye hivyo kwa yule kijana na kumuwezesha mtaji wa Biashara na kama endapo kijana atafaulu basi na mimi nitakuwa katika nafasi nzuri ya kusaidiwa na Mzee

Kwa akili yangu ya haraka haraka Mzee alifanya hivyo ili kutaka kuusoma uwezo wangu wa kusimamia Biashara hapo ndipo kijana wa Buguruni alitumika, kwasababu Mzee nilikuwa namuonesha Nia ya kufanya Biashara lakini kwa upande wake hakuwa na uhakika kama naweza kufanya au kusimamia Biashara coz kwa mujibu wake anasema unaweza ukawa na shauku ya kufanya Biashara lakini misingi yake ukawa huijui

Kwa mfano hapa juzi masaa machache kabla ya A day to remember nilipata hasara ya milioni 10 kwa uzembe uliotokea kazini, by that time hiyo issue inatokea Mzee alikuwa nje ya Nchi, baada ya siku mbili 3 ilibidi nimpigie na kumuelezea, wakati namuelezea situation iliyotokea ni kama alinisoma hali niliyokuwa nayo, (sikuwa sawa)

Mzee alinijibu simple sana, aliniambia "Kijana wangu relax, milioni 10 ni Hela ndogo sana, kwasasa ni mapema sana kwa wewe kuchanganyikiwa, kwasababu kwa aina ya Biashara uliyoniambia unataka kufanya, kipindi kile kupata hasara kama hiyo au na zaidi ni kitu cha kawaida sana, ndio maana nilitaka uanzie chini uzoee hio hali"

Hapa nakurudisha kwa kijana wa Buguruni, mpaka Mzee ananiambia nimfungulie huyo kijana Biashara na nimsimamie alijua tutakutana na kitu kinaitwa hasara so kwa nilivyomuelewa mimi ni kama alikuwa anataka nipate experience ya mambo mengi katika Biashara lakini pia na uzoefu wa kupata hasara ndogo ndogo na nijue jinsi ya kukabiliana nazo kabla sijaja kukutana na hizi kubwa kubwa, Kwa bahati mbaya ndio nimekuja kukutana nayo juzi

So kwa kipindi kile Kichwa Cha Uzi (title) na story yenyewe vilikuwa vinaendana na Kijana wa Buguruni alikuwa ana appear mara kwa mara lakini kadri siku zinavyoenda mambo yanabadilika

Kumbuka hii story inayoendelea kila siku, kwa mfano Leo kuna kitu kimenitokea so siku za mbeleni pengine nitakuja kukiandika, kama ingekuwa ni story iliyotokea kitambo kama unavyosema hapo sasa ndio ningekaa chini na kuchagua Heading ya Story kulingana na maudhui yake
Nashukuru kwa ufafanuzi ulionyooka, hata hivyo usichoke kutuhabarisha na kutuelewesha sie wadau wako
 
Mkuu nilikuambia Sterling ni Kijana wa Buguruni kwa sababu kuu moja, huyo ndiye aliyenifanya nianzie huu Uzi, kama ulisoma story vizuri mwanzoni nilimchukua kijana wa Buguruni na kumsaidia ni kwasababu ya Mzee, Mzee alinitaka nifanye hivyo kwa yule kijana na kumuwezesha mtaji wa Biashara na kama endapo kijana atafaulu basi na mimi nitakuwa katika nafasi nzuri ya kusaidiwa na Mzee

Kwa akili yangu ya haraka haraka Mzee alifanya hivyo ili kutaka kuusoma uwezo wangu wa kusimamia Biashara hapo ndipo kijana wa Buguruni alitumika, kwasababu Mzee nilikuwa namuonesha Nia ya kufanya Biashara lakini kwa upande wake hakuwa na uhakika kama naweza kufanya au kusimamia Biashara coz kwa mujibu wake anasema unaweza ukawa na shauku ya kufanya Biashara lakini misingi yake ukawa huijui

Kwa mfano hapa juzi masaa machache kabla ya A day to remember nilipata hasara ya milioni 10 kwa uzembe uliotokea kazini, by that time hiyo issue inatokea Mzee alikuwa nje ya Nchi, baada ya siku mbili 3 ilibidi nimpigie na kumuelezea, wakati namuelezea situation iliyotokea ni kama alinisoma hali niliyokuwa nayo, (sikuwa sawa)

Mzee alinijibu simple sana, aliniambia "Kijana wangu relax, milioni 10 ni Hela ndogo sana, kwasasa ni mapema sana kwa wewe kuchanganyikiwa, kwasababu kwa aina ya Biashara uliyoniambia unataka kufanya, kipindi kile kupata hasara kama hiyo au na zaidi ni kitu cha kawaida sana, ndio maana nilitaka uanzie chini uzoee hio hali"

Hapa nakurudisha kwa kijana wa Buguruni, mpaka Mzee ananiambia nimfungulie huyo kijana Biashara na nimsimamie alijua tutakutana na kitu kinaitwa hasara so kwa nilivyomuelewa mimi ni kama alikuwa anataka nipate experience ya mambo mengi katika Biashara lakini pia na uzoefu wa kupata hasara ndogo ndogo na nijue jinsi ya kukabiliana nazo kabla sijaja kukutana na hizi kubwa kubwa, Kwa bahati mbaya ndio nimekuja kukutana nayo juzi

So kwa kipindi kile Kichwa Cha Uzi (title) na story yenyewe vilikuwa vinaendana na Kijana wa Buguruni alikuwa ana appear mara kwa mara lakini kadri siku zinavyoenda mambo yanabadilika

Kumbuka hii story inayoendelea kila siku, kwa mfano Leo kuna kitu kimenitokea so siku za mbeleni pengine nitakuja kukiandika, kama ingekuwa ni story iliyotokea kitambo kama unavyosema hapo sasa ndio ningekaa chini na kuchagua Heading ya Story kulingana na maudhui yake
Kuna sehemu nadaiwa pesa zaidi ya hiyo biashara ili ni do,hii imenipa moyo wa kuendelea kupambana na kupambana mpaka iwe

Sent from my SM-A507FN using JamiiForums mobile app
 
Ilipoishia

Pia katika maongezi Mzee akaniambia kuwa kwa vile ahadi za kuja kupaona kwangu zimekuwa nyingi bila mafanikio akaniahidi na kunihakikishia atakuja siku ya Pasaka kula sikukuu kwasababu siku hiyo Bi Mkubwa Yani mke wake atakuwa yupo mkoani

Hivyo Ukiachana na Annie, Mzee pia ameingia kwenye list yangu ya wageni nitakao wapokea siku ya Pasaka japokuwa Annie alisema atakuja before Pasaka

Muendelezo

(Episode 24, SEASON 2)

Hii siku nilivyorudi nyumbani nikamjulisha Caryn kuhusu Mchina (Hili Jina kalitoa member wa hapa Jf wakuitwa [emoji1542]Tajiri Kichwa) Mchina ni huyu jamaa ninayemfanyia Mpango wa kwenda China, basi nikamuambia kwamba jamaa inabidi awe anakuja ofisini pale akiwa anasubiria process za visa zianze kufanyika

Caryn: "Ofisini anakuja kama nani? na kufanyaje? majukumu yake yeye si ni huko China"

BM: "Anakuja kwa lengo la kujifunza ili akifika kule (china) at least awe anajua baadhi ya mambo"

Caryn: "Wewe ni nani aliyekuambia sisi tunaajili wanafunzi wa kuja kujifunza kazi"

BM: "Aysee, hii sio amri yangu, ni kutoka kwa Mzee"

Caryn: "Na mm ndio nakuambia hatuajiri wanafunzi, tafuteni mtu mwenye Experience"

BM: "Kama ni hivyo acha niende mwenyewe"

Caryn: "Unajua BM unapenda sana kufanya vitu kwa mazoea, hii tabia hata Dad anayo"

BM: "Hiyo tabia ya mazoea unayoiana kama ni kasoro ndio imemfikisha Mzee pale alipo"

Caryn: "Back then, kwasasa huwezi kutoboa ukiwa una apply hiyo tabia mara kwa mara"

BM: "Tatizo lako unapenda ku complicate sana mambo... anyways kwa uchache wa siku zilizobaki according to Mzee, ni Either Mimi au Jamaa"

Caryn: "What's for dinner?"

BM: "Hujaniambia msimamo wako kama ni Mimi au Mchina, kama ni Mchina nimuambie Jumatatu aanze kuja job"

Caryn: "How does that answer my dinner question"

Caryn bhana, ukiwa unabishana nae kuhusu kitu fulani na ghafla ukaona ame switch topic basi ujue ameshakubaliana na wewe, hawezi ku admit directly, ikitokea basi ni mara chache sana.

Jumatatu ya mwisho ya mwezi wa 3, nakumbuka ilikuwa date 27 kama sikosea Mchina ndio alianza kuja pale ofisini, kabla hajaja nilimpanga kabisa kuwa mtu anayekuja ku-Deal nae ni kichefu chefu so ajue namna ya kuishi nae coz akisema NO basi ujue ni NO kweli hadi Mzee anaipitisha ila kwa Mzee anaweza kukutamkia YES lakini kwa Caryn ikawa NO na Mzee akabadilisha YES yake kuwa NO kwa Caryn

Yani nilichokuwa najaribu kumuambia Mchina ni kwamba katika kuruka ruka kwake kote awe makini tu asimkanyage Caryn kwasababu ndio mambo yote, ukijua kwenda nae sawa mambo yana floo yenyewe

Mchina nikampeleka Ofisini kwa Caryn kumtambulisha, baada ya kutambuana Caryn akaanza kumfanyia Oral interview

Caryn: "Okay, tell me have you ever exported....I mean What experience do you have in exportation of goods"

Mchina: "No, I don't have any, I'm looking forward to gain some here"

Caryn: "Impressive! I really like straight forward guy like you"

Caryn baada ya kumaliza kumuulizia Mchina maswali ya yanayohusiana na kazi akaanza na Personal questions

Caryn: "Una familia?"

Mchina: "Ndio ninayo"

Caryn: "Una watoto wangapi? na uliezaa nae bado unaishi nae?"

Mchina: "Sina mtoto, kwa kifupi sijaoa"

Caryn: "Kwanini ulijibu Ndio kwenye swali langu"

Mchina: "Nilidhani una maanisha familia ya Baba, Mama na ndugu niliozaliwa nao"

Caryn: "Hiyo sio familia yako, ni familia ya Baba yako na Mama yako"

Caryn: "Wewe na BM mna muda gani tangu mfahamiane?"

Mchina: "Karibia Mwaka sasa"

Càryn: "Be specific"

Mchina: "Ni ngumu kukumbuka siku tuliyofahamiana, so I can't be specific"

Caryn: "Wow, this is the level of confidence and boldness we want to see moving forward...anyways kesho utaniletea Barua mbili za udhamini"

Kusikia hivyo nikajua 'hapa mchezo ushaisha' tulivyotoka nje nikamuambia Mchina "Mwanangu kumbe unaweza kuwa kauzu"

Mchina: "Oya, unajua ulivyoniambia tabia za demu mwenyewe nikasema piga ua hata kama Sina Confidence nitakuwa nayo tu hata kama ni ya kuigiza"

BM: "Na kama ulimsoma, Kuna maswali alikuwa anakuuliza ili tu ujikanyage"

Mchina: "Ila unajua nini mwanangu, umetisha sana, sitakuangusha, Boss wako mm nitaenda nae anavyotaka tutarekebisha mbeleni, Ujanja sio kua bora, ujanja kupata"

Jioni yake wakati tupo nyumbani Caryn akawa kama Bado ana mashaka

Caryn: "BM yule jamaa ni rafiki yako kweli? I mean mnajuana vizuri?"

BM: "Ndio, kwani kuna tatizo?"

Caryn: "Nop, hakuna tatizo, anaonekana smart kiasi chake ila confidence inambeba"

BM: "Sawa sawa Mwana saikolojia"

Caryn: "Kebehi tu lakini naongea fact"

BM: "Uko sasa ni kujishtukia mm sijakebehi mtu"

Caryn: ".....wewe una uwezo mkubwa, you're smart ila ujasiri unakuangusha"

BM: "Hii sasa ni compliment au?"

Kwenye hii Convo nilikuwa namletea Caryn masihara mengi na utani wa kutosha, watu walivyoanza kusikia njaa ilibidi utani tuuweke pembeni

Caryn: "Bro, Body warms in my stomach are already screaming"

BM: "Sasa mm nifanyaje?"

Caryn: "It's your turn to cook today"

BM: "I'm not in the mood"

Caryn: "So you're in the mood to be hungry then"

BM: "Mimi nilishaji-sort (nilishakula)

Caryn: "BM you know this is not the first time you've doing this each time is your turn to cook you choose to eat out"

Caryn: Wait... you want me to do the cooking just for myself while you continue to eating out ... right? that's what you want?"

BM: "Hiyo pia si mbaya, mm nitarudi kwa nyumba nikiwa nimejipanga kabisa"

Nikaingia zangu chumbani, ukweli ni kwamba nilikuwa sijala ila nimemjibu tu vile kukwepa kukatakata vitunguu, Wakati naingia chumbani Caryn akaingia jikoni kukorofisha mambo,

Baada ya lisaa limoja kupita nikagongewa mlango eti chakula kimeiva naitwa nikale, nikaona kabisa huu ni mtego japokuwa nina njaa lakini nikavunga, nikamuambia we tangulia nakuja, hadi yeye anamaliza kula mimi sijatoka chumbani akanifuata tena akaniambia "BM chakula kinazidi kupoa, na hakuna Microwave kusema uta warm"

Sikwenda hata kula kwa kujishtukia, asubuhi naamka nimeingia jikoni kufuata ndizi (Kila asubuhi ni lazima Nile ndizi) nikakuta chakula alichoniwekea Caryn kakifunika na sahani kumbe msosi niliwekewa kweli ila kwa ego nikaamua kulala nayo

Wiki moja kabla ya Pasaka Annie akanicheki akaniambia Mpango wake wa kuja Dar unaweza usiwezekane kwasababu kuna mfanyakazi mwenzao amefiwa na Mama yake so kama huyo mfanyakazi mwenzake akiwahi kurudi kutoka mazishi ndio anaweza akaja na kama akichelewa itabidi tu Pasaka ailie huko huko Mwanza akisubiri safari ya mwezi wa sita

Hii ilikuwa Habari njema kwangu kwasababu mwanzo nilipanga uongo ambao sikuwa na uhakika kama Annie angeniamini au lah!

Hatimaye Pasaka ilifika lakini Annie hakufika Dar, ila Mzee yeye Alifika kwangu, alikuja mapema tu yale masaa ya breakfast but Mzee hanywagi chai, nikamuandalia kahawa, Wakati naendelea kunywa chai huku Mzee akipiga kahawa yake akauliza

Mzee: "Hapa unaishi mwenyewe?"

Unajua kuna swali mtu anauliza Kwa maana ya kwamba hajui kitu anataka umfahamishe, na kuna swali mtu anauliza kutaka kujua akili yako inaishia wapi kupitia majibu yako huku yeye tayari akiwa na majibu yake, ilibidi ninyooshe maelezo huku nikiwa na wasiwasi mno

BM: "Hapana, naishi na Caryn japokuwa mara nyingi huwa anakuwa kwa Dada yake"

Mzee: "Najua kama unaishi na Caryn, niambie kitu kipya ambacho sikifahamu"

BM: "Mzee mimi nilihisi unajua, kwakudhani Caryn alikuambia"

Mzee: "Hisia zako zipo sahihi, nilikuwa najua lakini kwa njia zangu mwenyewe hata huyo Caryn hajaniambia, hata hivyo wewe ndiye uliyepaswa uniambie, ukaribu wangu Mimi na wewe unashindwa kuniambia jambo nyeti kama hili kweli? unataka mimi nikufikiriaje, ivi ingetokea huyu Binti kakufia usiku na Mimi sifahamu kama yupo kwako unadhani Mama yake angekuelewa?"

BM: "Mzee kosa ni la kwangu naomba unisahame"

Mzee: "Unajua kuna makosa unaweza ukahisi ni madogo lakini yanavunja uaminifu kwa kiasi kikubwa sana"

Hiyo kauli ya Mzee ndio ikanimaliza nguvu, sasa namna alivyojua hii issue ndio nilichoka kabisa

Iko hivi, Mzee gari zake zote kazifunga tracker kasoro Gari ya mke wake, ninaposema Gari zake zote namaanisha hadi hizi za kina Caryn na Michelle, Sasa Ile siku ananipa Jeep mm nikijua narahisishiwa usafiri kumbe ule ulikuwa mtego,

Kwanini nasema mtego, ilikuwa hivi, Wakati Mimi naondoka Mzee alikaa chini na hiyo simu yake specific kwaajili ya hizo mambo, akaona Jeep lake hadi Mahali lilipo park, aliyekuja kuharibu ni Caryn maana Mzee anajua Caryn yupo kwa Michelle na atalala huko lakini baada ya muda akaona BMW limepark maeneo yale yale lilipopark Jeep

Hapo ndipo alipoanza kupata mashaka japokuwa tulimuambia sisi ni majirani lakini kupitia alichokiona yeye mwenyewe akawa kashajijazia kichwani kwake ni kitu gani kinaendelea

Baada ya Mzee kumaliza kunielezea kilichokuwa kinaendelea nyuma ya Pazia bila Mimi kujua Mzee akaniuliza swali

Mzee: "Nakumbuka ushawahi kuniambia kama una mchumba, na hiki ndio kipindi kizuri Cha kuishi nae ili mjuane vizuri kitabia lakini badala yake unaishi na Caryn, Kwani wewe na Caryn mna mpango gani?"

Hili swali ni muendelezo wa yale maswali ya Mzee ambayo anakuuliza ili kujua akili yako inapoishia na uwezo wako wa kufikiria, ila safari hii hajaniachia gepu la kumjibu, Wakati nataka kumjibu akaniambia kitu ambacho hadi kesho nakitafakari lakini nakosa majibu

Mzee: "Unajua...ngoja nikuambie kitu kijana wangu, kwenye huu ulimwengu ukitambua wenye manufaa maishani mwako usiwape umuhimu, hawatakuumiza. Wenye umuhimu maishani mwako usiwafanye wenye manufaa, Utaumia"


Itaendelea
Manufaa ni kunufaika tu nakusepa umuhimu ni jambo linalokufaa wakati wote,
Mtu anataka kunufaika nawe tuu kwa jambo lake asepe so usimpe nafasi,
Mtu wa muhimu kwako niyule anayesimama nawe bila hata manufaa

Hivi ndivyo nmemuelewa mzee hapo mwisho
 
Hai
EPISODE 06, SEASON 1


ILIPOISHIA [emoji1484]

Caryn: "Sorry Dad, first of all I want to know where these kids came from?

Tukaanza kuangaliana na yule jamaa aliyekuwa anaendesha Gari, Wakati najipanga kujibu.....

Caryn: BM, You should answer this question

Nikamuambia wametoka Buguruni Rozana

Caryn: "Dad, I think you should change your strategy on how to help these kids

The food we're gonna give them was it gonna change their life?
So as a rich man if you think you want to help someone give them the kind of help that would transform their life not leaving them with food in my opinion"


MUENDELEZO [emoji1484]

Mzee akamuangalia Caryn halafu akaniangalia na Mimi, Akasema "Kwahiyo unashauri tufanye nini Binti yangu"

Caryn: Let me speak swahili so that they can understand me, Hawa watoto kwa umri waliokuwa nao wanatakiwa wawepo shuleni, labda mtasema mnawapatia chakula kwasababu hawajafika umri wa kujishughulisha na shughuli zozote za kujiingizia kipato, huyo Kaka yao je maana anaoneka ni mtu mzima

Caryn: "How old...ooh sorry, Una miaka mingapi kaka?"

Kijana: "Kumi na Saba"

Mzee: Kumi na Saba Bado mdogo sheria haruhusu

Caryn: Come on Dady, Kwahiyo kama sheria hairuhusu ndio abaki kuomba omba, Kuna situation ikikufika hutakiwi kuangalia Sheria inasemaje inakubidi kufanya kile unachotakiwa kufanya ili u survive, Kijana you have to do whatever it takes to survive out here in this jungle called life

Michelle: Sometimes you sound more like an adult than a teenager

Caryn: And you sound like you're better than me, and you're not

Mama: Na nyie mshaanza sasa na malumbano yenu, ebu Kuweni na adabu hata kidogo mbele za watu msiowajua

Caryn: Ambae hana adabu ni huyo mwanao mama, Watu tunaongea vitu serious yeye analeta utani, mm teenager sawa, yeye huo utu uzima umemsaidia Nini hadi sasa, Anawaza Mapenzi tu......

Mzee: "Caryn basi Inatosha, unajua huyo atabaki kuwa Dada yako inabidi umuheshimu, halafu kwanini siku hizi nyie watu hampendani?"

Caryn: "Kwasababu nimekuambia Habari za huyo bwana ake wa huko Kibaha, I told you Dady na nakuambia tena the guy is more interested in money hakuna Mapenzi hapo"

Mzee: Caryn hiyo ni topic ya siku nyingine all in all nimeipenda maoni yako kuhusu Hawa vijana wadogo

Ila Caryn hapana asee [emoji1544] yule Demu kachukua akili za Baba yake, ni PISI KALI halafu sauti yake ni kama ya Bahati Bukuku na mara nyingi anakuaga serious, nyumba nzima hapa kwa Mzee ni yeye tu ndio sijawahi kumuona akicheka

Tukamaliza kula, Mzee akawahoji wale watoto mambo kadhaa, akawapatia na Pesa halafu akanambia "BM Nadhani Ushauri wa Caryn ni mzuri, Sasa ule mtihani nililokuambia nitakupa umekaribia get yourself ready. chukueni Gari warudisheni Hawa watoto halafu na Kijana atakudrop kwako,

Basi tukaondoka, tukawadrop madogo na mm nikadropiwa, kufika kwa nyumba nikamkuta Annie nikakuta ameandaa my favorite food Wali Nazi Njegere Nazi, Asee halafu nimetoka kubonya Pilau la Kuku kwa Mzee, nikaona hapa busara ni kula hata kama ni nusu sahani, Unajua Annie anajua natoka Kazi hakujua ratiba yangu imeendaje na Wala hajui Mahali nimetoka

Akaniwekea food kwa meza nimeipiga kama vijiko vitatu ivi nikamuuliza "Are you sure it's not Christmas yet?"

Annie: "of course it's not"

Maana sio utamu huu wa msosi, saa hiyo mm nikiendelea kula Annie alionyesha kuwa na mawazo, nikamuuliza nini mbaya?

Annie: "You know what BM, now i believe that circumstances change people"

Me: "Unamaanisha nini?"

Annie: "Hadi hapa tulipofikia life has taught me not to plant my seed in other people's garden"

Nikawa nishajua alichokuwa anamaanisha, TURUDI NYUMA Kidogo ili na wewe umuelewe Annie

Ukisema "Table turns" Mtu wa kwanza kuelewa ni Annie, niulize kwanini? Okay ilikuwa hivi, Miaka mitano nyuma Annie alikuwa mtoto wa kishua nikisema wakishua wakishua haswa haya maisha acheni nyie,

Natamani niandike mengi kuhusu Annie lakini haitawezekana kwasababu code yake nimeifungua, ndio muhusika pekee Jina lake ni halisi kwenye hii story wengine wote nimetunga majina na baadhi yao niliishia kuwaita Mzee, Mama, Jamaa nk

Ila kwa kifupi ni kwamba Annie alipiga taff sana enzi hizo wakiwa bado wako vizuri, Alinilipia hadi ada ya mwaka wa mwisho chuoni. Baba yake alikuja kupata matatizo flani kipindi Cha awamu ya 5, na Annie Mama yake Alishaaga kitambo so alibaki na Baba, Baba nae ndio hivyo akapotezwa, acheni asee kila nikikumbuka roho inaniuma ndio maana nakuwa mzito kumuachia huyu mwanamke

LEO

Nikamwambia Najua unachoniwazia ila nikwambie tu unaniwazia vibaya, acha nikuambie ukweli pengine utakuumiza ila ni Bora kuliko kudanganyana, inawezekana nimekucheat lakini sio kwa mazingira niliyoyaandaa, Najua nilishakuambia mengi kuhusu yule mwanamke (Accountant) lakini hili la kucheat nilikuficha kwasababu sikudhamilia mimi na kuhusu swala la kuacha kazi ili kumkwepa yule mwanamke sidhani kama ni sahihi kwasababu unajua hali halisi ya maisha ilivyo Mimi nakuomba tu uridhie Mimi kundelea kufanya kazi Mimi nitajua tu jinsi ya kudeal na yule mwanamke na nakuahidi sitarudia kosa, Nakuomba usikatae, ni swala la muda tu nikakamilisha malengo yangu flani naachana rasmi na Ile Kampuni

Annie: "Okay! i trust you BM, you can go ahead, but remember not everyone in this life gets a second chance to write their wrongs"

BM: "Nakuahidi haitojirudia, na nakupenda sana japokuwa ww mara nyingi husemi kwa Mdomo kama unanipenda"

Annie: "Ushaanza, listen BM 'I trust you' is better compliment than 'I love you' because you may not always trust the person you love but you can always love the person you trust"

BM: "Wow! thanks, i didn't even know that"

Basi Mama lao akatoa vyombo pale, Leo hajaachwa mtu Sebuleni, Najua mshaelewa. siku zilikatika mambo yalikuwa mswano na Annie

Asubuhi ya Jumamosi moja nimeamka nimechelewa sana kwenda job, nikajiandaa fasta nikasepa nikafika eneo langu la kazi Sasa wakati naingia Ofisini nikamkuta Accountant kakaa kwenye kiti changu ni kama alikuwa ananisubiri kwa hamu, nikamsalimia akaitikia halafu akanambia

Accountant: "Naona maisha yako yanaenda kuwa mazuri ila endapo tu utafanya Maamuzi sahihi"

BM: "Nikamuuliza Maamuzi gani?"

Accountant: "Usiwe na haraka BM, Mama alikuwa anakuulizia amesema ukifika tu nikwambie uende Ofisini kwake so we nenda kaonane na Mama"

Nikawa najiuliza Kuna jipya gani maana Accountant anafuraha kupita maelezo na si kawaida yake, basi Mimi nikaelekea ofisini kwa Mama, nikasalimia nae halafu nikakaa kwenye kiti

Mama: "Mwanangu si kawaida yako kuchelewa kazini, Leo imekuaje?"

BM: "Jana nilichoki sana Mama, hali iliyosababisha kupitiwa na usingizi Leo na kuchelewa kuamka"

Mama: "Ooh, halafu hata hivyo hukuwahi kuchukua likizo ya kueleweka tangu uanze kufanya kazi kwenye hii Kampuni"

BM: "Yeah ni kweli Mama lakini sikuona ilazima huo"

Mama: "Sasa Mimi nakupa likizo ya mwezi mmoja ya lazima hata kama hutaki, japokuwa hapa nilikuitia jambo lingine lakini Nadhani tutapata nafasi Nzuri zaidi ya kulijadili hilo jambo akili yako Ikiwa refreshed"

BM: "Ni jambo gani hilo Mama?"

Mama: "Nilijadili na mwenzako lile swala la wewe kurithi hii nafasi yangu, amefurahi sana lakini ametaka mvishane kwanza Pete ya kabla ya kukalia hiki kiti, na Mimi Nadhani ni jambo zuri so nilikuitia hapa ili tupange siku ya kufanya zoezi hili, lakini wewe nenda kwanza likizo ukirudi tutapanga vizuri"

Nikamuitikia tu "Sawa Mama" huku nikimuwaza Accountant, ndio kashaanza kuchezesha Karata zake kama alivyoniahidi, Basi mm Nikatoka Ofisini kwa Mama, nilimkuta Accountant Bado yupo pale kwenye kiti changu, Nilifika tu nakumwambia kwa userious wa hali ya juu "nipishe Mimi niendelee na Kazi"

Accountant: "I hope umefanya Maamuzi ya kiume, halafu kumbe huwa mnaongeaga mambo mengi na Mama bila kunishirikisha, ivi unajua maamuzi mengi anayoyafanya mama juu yako ni kwasababu anajua Mimi na wewe ni wapenzi, Sasa isije ikawa umeshaharibu mambo huko"

BM: "Sikiliza **** (Accountant) naomba kwasasa uende kwenye ofisi yako, Nina mambo mengi ya kufanya, sitakiwi kuacha kiporo Cha aina yoyote kwasababu kuanzia Jumatatu siji kazini"

Accountant: "Unasemaje wewe?"

Alivyosikia "Kuanzia Jumatatu siji kazini" alipagawa sijui alidhani nimeshaacha kazi, Alitoka mbio sijui kaelekea wapi ila itakua tu kwa Mama yake bila shaka

Nimekaa kidogo akarudi akanambia "Inawezekana wewe ndio umeomba hii likizo ili ukajipange maana inaonesha Kazi unaitaka lakini mwenye kazi humtaki, Sasa Mimi nakuambia hivi, we nenda hiyo likizo lakini siku utakayorudi hapa uwe umeshaamua jambo moja kati ya haya mawili, UNIOE au uandike barua ya kuacha kazi, Sitakubari uwe Director wa hii Kampuni a halafu raha unakula watu wengine" alivyomaliza hakutaka nimjibu akaondoka

Aliniacha na mawazo, kusema ukweli hii nafasi naitaka ili niweze kufikia malengo yangu lakini ndio hivyo tena ili ni qualify kwenye hiyo nafasi basi nilazima nimuoe Accountant, nikifanya hivyo Annie wangu nitamuweka katika nafasi gani na Jana tu tumetoka kula kiapo, na huyu Accountant mwenyewe hana sifa hata moja ya wife ila kitandani kwakweli yupo vizuri japokuwa ilikuwa ni mara moja na kwa bahati mbaya na hiyo dhambi nishaimbea msamaha kwa Annie na kanisamehe kwa kumuahidi kutorudia tena

Siku ikaisha na ndio ikawa nimeianza likizo yangu ya mwezi mmoja rasmi, lakini ya mawazo kwasababu natakiwa kufanya uamuzi sahihi, hapa kichwa kiliniuma zaidi kwasababu ya mtihani wa Mzee niliopewa,

Wakati naandika huu Uzi nilikuwa Bado sijapewa likizo, Uzi nimeuanza kuaandika jumatano ya tarehe 6/7/2022 na likizo nimepewa juzi Jumamosi tarehe 9/7/2022 hii siku kama mnakumbuka nilicomment hapa hiyo comment ipo namba 272 kama sikosei nilitoa maelezo kwanini hii story imekua ndefu Sasa siku hii ndio nilipewa likizo ya lazima so hili tukio ndio nimeliunganisha kwenye Uzi.

Na Uzi ulikuwa una muhusi Mzee ila niliongea story zingine kwasababu ili kufaulu mtihani wa Mzee inategemea pia mm kuendelea kubaki kazini

Inatakiwa Utulivu wa hali ya juu kuelewa, TURUDI NYUMA KWENYE MTIHANI NILIOPEWA NA MZEE

Ilikuwa Alhamisi, saa nne na dakika thelathini na saba sekunde ya sita simu ya Mzee iliingia nikiwa Ofisini najiandaa kwenda Zanzibar na Boti ya mchana

Mzee: [emoji338]"Kijana wangu hujambo?"

BM: "Sijambo Mzee, Shikamoo"

Mzee: "Marhaba, Sasa nataka kukujuza kwamba siku ya Jumapili jioni nasafiri hivyo nakuomba tuonane siku hiyo kabla sijaondoka

BM: "Sawa Mzee Haina shida"[emoji3513]

Basi nilienda Zanzibar nakurudi kesho yake, Jumapili Ikafika nikajua kabisa LEO NDIO ILE SIKU, Ile siku ya kupatiwa mtihani, Nakumbuka nilienda kwa Mzee mida ya saa sita mchana, nimeingia kwenye Ile nyumba harafu za misosi tu ndio zimetamalaki,

Kama kawaida chimbo langu na Mzee ni Backyard tukaongea sana mambo mengi, Sasa bhana safari yenyewe kumbe ni ya nje ya nchi, Mimi nilijua ni zile safari zake za mkoani kumbe Mzee anaenda United Kingdom (Uingereza) na atakaa huko kwa muda wa miezi miwili na nusu

Acha nifungue code kwenye Biashara moja ya Mzee, Ni hivi, Mzee ana mabiashara mengi ila moja ya hizo Biashara ni maduka ya Ex UK, Sasa huko UK alikua anaenda kibiashara zaidi, Sasa Mzee alinambia kwa muda wote. huo ambao atakuwa nje ya nchi niwe natembelea familia yake mara kwa mara, muda wa msosi ukafika tukakutana wote mezani yani Mimi, Michelle, Caryn, Mama na Mzee, Wakati tunaendelea kula mazungumzo nayo yaliendelea

Mama: "BM usipotee sana kwasababu Baba hayupo, uwe inakuja nyumbani tena mara kwa mara zaidi

Mzee: "Nimeshamsisitizia hilo, halafu BM kuhusu ule mtihani niliosema nitakupatia maelezo yote anayo Caryn, So ni wewe Tu kutafuta muda ukae chini na Caryn akuelezee

Nikajibu "Sawa Mzee" (huku nikimuangalia Caryn na yeye akinipiga jicho la kimtindo)

Michelle: "Baba kwani ni mtihani gani huo?"

Mzee: "Hili halikuhusu Michelle, wewe si ulishafeli wa kwako, Majukumu anayofanya Caryn ulipaswa kufanya wewe. Na Caryn zidisha umakini katika kumsaidia Mama yako majukumu ya Ofisini, Kuna baadhi ya mambo Mama yako anasahau"

Caryn: "Okay Dady, we will miss you"

Eeh!!! nilishangaa, kumbe Caryn ndio anapewa majukumu makubwa kiasi hiki, basi tulimaliza kula tukakaa kama 1 hour tukaanza safari ya kuelekea Airport, hii ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kupanda 'Jeep Wrangler' halafu Mzee akaniambia nikae mbele, Guess Sasa nani anaendesha? ni Caryn jamani dah!

Tukafika Airport Wakati tunamuaga Mzee akanambia "BM nikirudi nikukute ushapata Driving Licence" Nikamwambia "nitajitahidi Mzee" Basi ndio hvyo tena Mzee akaingia kwenye kale ka mlango kalikoandikwa DEPARTURE sisi tukaenda kwenye Gari na kurudi nyumbani,

Wakati tumefika Tazara tunacross kuelekea Buguruni Nikamwambia Caryn "Mimi mtanidrop hapo Tabata"

Caryn: "Okay, I will text you, Dady gave me your number"

Tukafika Tabata wakanishusha nikatafuta Daladala la kuelekea Tabata Kimanga

Blue Monday mapema kabisa nimeamka kwaajili ya kwenda kazi, nashika simu kuangalia muda naona meseji ya namba ngeni kuifungua "Hey! Mornie, It's me Caryn" Nika reply "I got you" then nikasave namba yake

Wakati nipo Ofisini Caryn akanipigia akanambia kuwa yupo ofisini kwa Baba yake atatoka jioni na kuelekea **** ni Ile Hotel ambayo nilikutana na Baba yake, hivyo akaniambia nimkute hapo

Sasa yeye aliwahi sana kutoka siunajua wao ndio mabosi so wanajiamulia muda wa kutoka, mm ilibidi nisubiri Hadi ifike angalau saa kumi na nusu, Mida ikafika ya kutoka kazi moja kwa moja nikaelekea Hotelini lakini hiyo foleni niliyokutana nayo Njiani siyo ya kitoto, nikajua yule mtoto (Caryn) alivyo serious katika Kila Kitu sidhani kama nitamkuta, Mungu alisaidia nikamkuta Ile nimefika tu nikakaribishwa na

Caryn: "why are you late, you kept me waiting almost 2 hours?"

BM: "It wasn't deliberate the traffic was crazy it was terrible"

Caryn: "That is the senseless excuse"

BM: "Ok, let's discuss what brought us here"

Caryn: "let me start by asking you a question, Have you ever...."

BM: "Wait pls, Sijawahi kusikia ukitumia kiswahili japo kwa sentensi 3 mfululizo, naomba Leo tutumie kiswahili kwenye haya mazungumzo"

Caryn: "Ni sawa tu, as you wish"

Nikasema 'Yes' maana Nisingemuwahi huyu angenitemea Yai[emoji1639] hapa mwanzo mwisho na hata misamiati mingine nisingeielewa"

Caryn: "Umeshawahi kufanya Biashara?"

BM: "Kama Biashara gani labda?"

Caryn: "Typical Tanzanian man you're answering questions for questions"

BM: "Madam anayejibu swali kwa swali mwisho wa siku jibu lake linakuwa la uhakika, yani hiyo ni njia ya kulielewa swali vizuri zaidi, ila na wewe Kingereza unakipenda sana bhana"

Caryn: "Okay, Just any Business hata kama ya kuuza chupi"

BM: "Hapana, sijawahi Fanya Biashara"

Caryn: "Interesting, kama ni hivyo hukuwa katika nafasi ya kujibu Swali kwa swali kama ulivyofanya"

BM: "Nimekosa mimi, twende kwenye Point"(Nikajisemea moyoni Leo kazi ninayo)

Caryn: "Ebu kwanza nieleze kuhusu yule kijana aliyekuja na wadogo zake pamoja na watoto wengine"

BM: "Nikueleze nini?"

Caryn: "Ooh shit! same mistake, Are sure you will handle this?"

BM: "You wasn't specific enough, ukiuliza swali jaribu kuwa specific zaidi"

Caryn: "You're not smart enough as I expected, I see that you're even worse than i imagined"

BM: "Madam mimi naomba niende tu, maana naona Sasa umekuja kunichora tu"

Nikanyanyuka kwenye kiti, kabla sijapiga hatua akanambia "Ebu acha utoto Kaa chini na unisikilize kwa Makini, naku challenge kidogo na wewe umejaa kweli"

Nikakaa chini moyoni namsema huyu mtu inabidi nimsome akili yake ndio nitaenda nae sawa lasivyo atanitoa knock out

BM: "Caryn jaribu kuwa serious kidogo, unajua kama ningekuwa na Mzee hapa tungekuwa tushamaliza maongezi"

Caryn: "Thus why I am not Mzee, you know what BM, kwa muda huu mchache tuliokaa hapa Kuna Kitu nishakisoma kutoka kwako

BM; "Kitu gani?"

Caryn: "Unakosa some confidence pengine hasa ukiwa na mtu ambae hujamzoea, kwa Mfano kwenye swala la Kingereza sidhani kama ww hujui Kingereza, unakijua vizuri tu lakini ukataka niongee kiswahili, chaajabu nikawa naongea Kingereza makusudi na wewe unanijibu Kingereza, hiyo maana yake Nini?"

BM: "Sawa nimekusikia, nitayafanyia kazi si ni hayo tu?" (Katika siku ambayo nimejihisi mdhaifu ni leo)

Caryn: "Hapana! sio hayo tu, Pia una shida katika kuongea japokuwa tuko pale pale kwenye confidence, nimekusoma wewe ni mjanja ambae huna confidence, Sasa ukiongea mbele ya mtu ambae hayupo Makini atajua una confidence kumbe ni ujanja tu, So you should talk like gentleman with confidence"

BM: "Dah! Leo kazi ninayo, kama mambo yenyewe ndio haya nyumbani kule si wanapata shida sana?"

Caryn: "Nadhani utakuwa umenielewa, acha niende straight tu the point, Japokuwa nilikuuliza swali mara ya kwanza ila ukaleta ujuaji, Yule kijana uliyemleta siku ile nyumbani na wadogo zake, Mzee kasema kamtafutie nyumba umpangie halafu utaniambiaa Kodi ni kiasi gani nikupatie pesa ya Kodi ya miezi sita, hiyo ni moja mbili Sasa, Amesema umpatie pesa ya mtaji afanye Biashara na uhakikishe katika hiyo Biashara atakayofanya huyo kijana ndani ya miezi sita iwe imeshasimama na waweze kujilipia Kodi,"

BM: "Biashara gani sasa na mtaji kiasi gani?

Caryn: "Hapo kwenye Biashara amesema wewe ndio utakayemchagulia na mtaji pia hajakuwekea limitation kwasababu wewe ndio utakayetoa hiyo pesa ila ameweka vigezo katika nyumba utakayo watafutia, Amesema Nyumba isiwe chini ya shilingi laki 1"

BM: "Dah! Baba yako sijamuelewa hapo kwenye swala la nyumba tu, kwasababu kama mm mtu ambae najiweza nakaa nyumba ya laki na nusu iweje yule kijana tumtafutie nyumba ya pesa yote hio Ikiwa ndio anaanza maisha?"

(Kabla ya kujibu Caryn akacheka kwanza)

Caryn: "I'm so proud to have him as my Dady, Sasa acha nikuambie ni Kwanini amekuwekea vigezo hapo kwenye nyumba, Cha kwanza hapo Dady ameshaku limit katika upande wa kuchagua Biashara, kwasababu asingefanya hivyo ungemtafutia tu yule kijana chumba Cha elfu 10 halafu ungempa na mtaji wa Biashara ya karanga"

BM: "Mbona kama mtihani wenyewe nishafeli, kwasababu ili mtu aweze kula na kufanya mambo mengine na aweze kulipa Kodi ya laki moja kwa mwezi basi hiyo Biashara mtaji wake usiwe chini ya milioni 1"

Caryn: "What do you mean? huna hiyo pesa?

BM; "Tatizo sio Pesa, nawaza ni Biashara gani hiyo yule kijana ataimudu kuendesha ya kiwango hicho Cha pesa"

Caryn: "Ndio maana mwanzo nilikuambia nieleze kuhusu kijana ili nikishakupa haya maelezo niweze kukushauri lakini ukajifanya mjuaji"

BM: "Yule kijana kwanza kaishia form 3, katika kumuhoji kanambia hajawahi kufanya hata Biashara ya mtualikua anaishiaga kupata vibarua vya kawaida tu"

Caryn: "Too late, hili swali ulitakiwa ulijibu pale pale nilivyokuuliza, kwasababu unaweza kuulizwa swali Dar ukiwa unaelekea Mwanza na usione mantiki kwenye swali uliloulizwa ila ukifika Mwanza sasa ndio akili inakukaa sawa na hapo inakuwa too late, So next time uwe Makini ukiwa unazungumza na Mimi"

BM: "Kwahiyo unanisaidiaje katika hili?"

Caryn: "Cha kukusaidia labda nikupe maelezo ya mwisho ambayo ndio ya umuhimu zaidi, Baba Amesema ukifaulu kwenye huu mtihani basi na wewe utakuwa katika nafasi ya kutaja kiasi chochote cha pesa as mtaji wa kufanyia Biashara

BM: "Caryn! some jokes are too experience, you don't meat it.... right?"

Caryn: "I am serious but don't cheat on this, I know my Dady....have a wonderful night"

Caryn ndio ameenda hivyo, na mazungumzo yakaishia hapo


Nakumbusha huu mtihani nilipewa kabla sijapewa likizo ya lazima, so Wakati nikitafakari vile nitafanya ili kufaulu mtihani wa Mzee ndio stress nyingine ya Ofisini ikaja

Wadau natoboa kweli hapa kwenye Situation zote mbili? TRUE STORY



MWISHO To be continued (SEASON 2)
Haijaendelea tu hapo kwa SEASON 2..??
 
Huu uzi ni upuuzi tu. Anyway BM hakuna msala mpya tukupe hela ukalipe? Nina shida though, eti unalala nyumba moja na binti halafu bilabila . Una tatizo! Mara oohh demu wangu haji pasaka mara oohh nilikwenda Mwanza ila sikuonana nae, ujinga tu. Anyway lete upuuzi zaidi maana wengi humu ni aina yako
 
Huu uzi ni upuuzi tu. Anyway BM hakuna msala mpya tukupe hela ukalipe? Nina shida though, eti unalala nyumba moja na binti halafu bilabila . Una tatizo! Mara oohh demu wangu haji pasaka mara oohh nilikwenda Mwanza ila sikuonana nae, ujinga tu. Anyway lete upuuzi zaidi maana wengi humu ni aina yako
Aysee! hebu niache kwanza tafadhali...niache tu na upuuzi wangu
 
Huu uzi ni upuuzi tu. Anyway BM hakuna msala mpya tukupe hela ukalipe? Nina shida though, eti unalala nyumba moja na binti halafu bilabila . Una tatizo! Mara oohh demu wangu haji pasaka mara oohh nilikwenda Mwanza ila sikuonana nae, ujinga tu. Anyway lete upuuzi zaidi maana wengi humu ni aina yako
Mkuu huwezi kuishi nyumba moja na msichana bila kumgusa?
Mbona hili linawezekana tu?
Mapenzi ni hisia
 
Back
Top Bottom