Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni , awali niliwahi kuuliza " sterling " wa story hii ni nani nikajibiwa ni huyo kijana wa Bugurun...hivyo basi BM x6 anafahamu mwanzo mwisho wa story hii na pengine ,kuandika kwake kwa story anajikumbusha alimopitia hadi kufikia hapo alipo ,,uhusika wa kijana wa Buguruni hadi BM x6 aseme hatma yake ya maisha ipo mikononi wa kijana wa Buguruni binafisi sijaupata ni sehem ipi navuta subira nifahamu Kijana wa Buguru i alihusika vipi hadi BM x6 ampigie magoti
Mkuu nilikuambia Sterling ni Kijana wa Buguruni kwa sababu kuu moja, huyo ndiye aliyenifanya nianzie huu Uzi, kama ulisoma story vizuri mwanzoni nilimchukua kijana wa Buguruni na kumsaidia ni kwasababu ya Mzee, Mzee alinitaka nifanye hivyo kwa yule kijana na kumuwezesha mtaji wa Biashara na kama endapo kijana atafaulu basi na mimi nitakuwa katika nafasi nzuri ya kusaidiwa na Mzee
Kwa akili yangu ya haraka haraka Mzee alifanya hivyo ili kutaka kuusoma uwezo wangu wa kusimamia Biashara hapo ndipo kijana wa Buguruni alitumika, kwasababu Mzee nilikuwa namuonesha Nia ya kufanya Biashara lakini kwa upande wake hakuwa na uhakika kama naweza kufanya au kusimamia Biashara coz kwa mujibu wake anasema unaweza ukawa na shauku ya kufanya Biashara lakini misingi yake ukawa huijui
Kwa mfano hapa juzi masaa machache kabla ya
A day to remember nilipata hasara ya milioni 10 kwa uzembe uliotokea kazini, by that time hiyo issue inatokea Mzee alikuwa nje ya Nchi, baada ya siku mbili 3 ilibidi nimpigie na kumuelezea, wakati namuelezea situation iliyotokea ni kama alinisoma hali niliyokuwa nayo, (sikuwa sawa)
Mzee alinijibu simple sana, aliniambia "Kijana wangu relax, milioni 10 ni Hela ndogo sana, kwasasa ni mapema sana kwa wewe kuchanganyikiwa, kwasababu kwa aina ya Biashara uliyoniambia unataka kufanya, kipindi kile kupata hasara kama hiyo au na zaidi ni kitu cha kawaida sana, ndio maana nilitaka uanzie chini uzoee hio hali"
Hapa nakurudisha kwa kijana wa Buguruni, mpaka Mzee ananiambia nimfungulie huyo kijana Biashara na nimsimamie alijua tutakutana na kitu kinaitwa
hasara so kwa nilivyomuelewa mimi ni kama alikuwa anataka nipate experience ya mambo mengi katika Biashara lakini pia na uzoefu wa kupata hasara ndogo ndogo na nijue jinsi ya kukabiliana nazo kabla sijaja kukutana na hizi kubwa kubwa, Kwa bahati mbaya ndio nimekuja kukutana nayo juzi
So kwa kipindi kile Kichwa Cha Uzi (title) na story yenyewe vilikuwa vinaendana na Kijana wa Buguruni alikuwa ana appear mara kwa mara lakini kadri siku zinavyoenda mambo yanabadilika
Kumbuka hii story inayoendelea kila siku, kwa mfano Leo kuna kitu kimenitokea so siku za mbeleni pengine nitakuja kukiandika, kama ingekuwa ni story iliyotokea kitambo kama unavyosema hapo sasa ndio ningekaa chini na kuchagua Heading ya Story kulingana na maudhui yake