BM X6
JF-Expert Member
- Nov 24, 2020
- 1,376
- 4,222
- Thread starter
-
- #3,261
ANNIE & CARYN, We have lost another vote hereNdugu yangu BM X6 wanasema
"Love is a complicated journey strictly to those who are ready to endure heart broken"
Katika hili vyovyote iwavyo lazima kuna mmoja kati yako wewe, Annie na Caryn moyo wake utakuwa broken [emoji174]. That is another case, itashughulikiwa kwa namna yake pindi itakapojitokeza kwa wakati wake. Ni sawa na kusema ili ule yai ni lazima ulivunje kwanza ndipo upate kiini cha kukaanga. Katika hili maumivu ni lazima, na hayakwepeki.
Niungane na wengine ambao hawakuweka wazi kura zao wanampa nani kati ya Annie na Caryn (ingawaje nafsini ninaye candidate ninayem-prefer kati ya hao wawili) Naamini kupitia maoni ya tusio na upande na hata ya wengine bila kujali kama wana upande au la yanaweza kutoa mwanga na nguvu ya maamuzi, na pengine yakawa na kura ya VETO. Mawazo yangu ni kama ifuatavyo:-
1. Wakati mwingine ili kufanya maamuzi sahihi juu ya hatma ya maisha yetu au jambo tunalolitamani na kulihitaji yafaa kutumia akili zaidi kuliko hisia.
2. Annie na wewe mmekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu, mmepitia ups and down kwa kiasi chake. Hivyo umemsoma vya kutosha. Hata hivyo umbali uliopo kati yenu kwa namna moja au nyingine umefifisha ile bond iliyopo baina yenu. Haiyamkuniki uende Mwanza zaidi ya mara moja, kisha ushindwe japo kuonana naye kwa salamu. Hivi Mzee ulishindwa japo kumwomba ridhaa kwenda kawasalimu jamaa zako, ili upate nafasi ya kuonana naye? Plus ulivyomkwepa kuja Dar kukutembelea. Yawezekana hapa napo nafasi ya upendo wako kwake ilianza/ iliendelea kufifia (who knows)
3. Caryn hujawa nae kwa kipindi kirefu kulinganisha na Annie, lakini wewe na yeye mmepata muda mwingi wa kuwa pamoja kwa karibu zaidi na hivyo kila mmoja kumsoma mwenzie. Licha ya hayo, napata hisia kwamba bado hujahitimu kumsoma Caryn, hasa kutokana na tabia yake ya kutotabirika au hali yake ya kujiamini kupita kiasi pengine ni kwa ajili ya financial stability yake au feminist character aliyonayo. Nahisi kuna jambo la ziada yanafaa ujiridhishe vya kutosha kabla hujafikia uamuzi wa mwisho kwake.
4. Wazo la wewe kusimama mwenywe kwa uwekezaji, sitalirejea. Limesemwa ipasavyo na wewe tayari uko na mawazo hayo. Na-cement kwa kukutaka uongeze juhudi kwenye hili.
5. Ingekuwa kwa kutumia akili za "kifyatu" ningeweza kukushauri uwezekano wa kuwajaza mimba wote wawili. Then hatma nyingine ingejulikana mbeleni. Katika hali ya halisi wazo hilo si jema, na si jambo la kiungwana kulifanya achilia mbali kuliwazia.
6. Maandiko ya Dini zote yametuelekeza kumtegemea Mungu kwa kila jambo. Yawezekana spiritual connection yako na "Sir God" iko down, lkn katika hili ni muhimu kumuomba na kumtumainia yeye. Naelewa kuwa yeye hawai wala hakawii katika kujibu maombi. Tena anajibu katika namna apendavyo. Zaidi sana anaujua mwanzo na mwisho wa maisha yetu. Inawezekana hapa tunajadili suala lako wewe na Annie na Caryn lakini Mungu amekupangia Fatuma wa Kwa Msisi Tanga[emoji12] (mtu tofauti kabisa). Kumbe basi, ni vyema pia kumshirikisha na kumtegemea Mungu ili akuvushe katika namna ya Ki-Mungu. Maana ni bayana kuwa jambo hili na hata hayo mengine unayoyapitia ni magumu na pengine hayawezekani kwa akili za kibinadamu pekee.
7. Nakutakia heri wakati wote.
Wasalaam.
Eniwei! Hiyo namba 2 inaonesha kabisa kura yako ilikuwa inaenda kwa nani, lakini muhimu zaidi ni namba 6 nimeichukua na kuihifadhi itanisaidia hivi karibuni