Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Wajukuu, Wanangu na wazee wenzangu! Heshima kwenu nyote.

Sijisikii vizuri leo naumwa kidogo.

Niende kwenye mada...

1. Love is inversely proportional to distance.

Let love be "L" and distance be "D"

So L ≈ C/D where C is proportionality constant.

But C = a,b,c,d,e,f,t,w,r

Where a = age, b = beauty, c = characteristics, d = diseases, e = education (intelligence), f = family background, t = tribe, w = wealth.

Hence L = C/D

The more the distance the less the love

Ila C "result" ikiwa kubwa huongeza L kuwa kubwa.

Hii ni topic muhimu kwa vijana wanaotaka kuoa ama kuolewa hususani kwenye kuchambua hiyo "C"

2. Kwa waislamu, sisi wanaume tumeusiwa kuoa wanawake wawili, watatu hadi wanne, lakini 'tukishindwa' (kwa sababu mbalimbali' basi tuoe mmoja

Lakini pia tumeusiwa sisi kuwaoa kwa sababu za:-
(i) Uzuri wao
(ii) Ukwasi wao
(iii) Nasaba zao
(iv) Ucha Mungu wao.

Msisitizo ukawekwa kwenye ucha Mungu na kupuuza hayo matatu ya juu maana tutaongezewa...

Lakini atakaye chagua kuoa kwa sababu tatu za juu bila kuzingatia ucha Mungu 'huenda' akaangukia pabaya baada ya sababu hizo zilizomfanya aoe kuondoka.

Hapa napo panahitaji darasa lake.

3. "Hatma ya maisha yangu ipo mikonono mwa kijana wa Buguruni" ndiyo kichwa cha simulizi.

Hatma ya maisha YAKO ipo mikononi kwa kijana wa Buguruni!

Kijana wa Buguruni keshazingua 'big time'

Je, hatma ya maisha yako sasa ipo mikononi kwa 'Caryn?!'

Je, hatma ya maisha yako ipo Mikononi mwa Baba Caryn!?

Je, hatma ya maisha yako ipo mikononi mwa maamuzi yako ya kumchaguwa Anne ama Caryn ili uendeleze uhusiano wa mapenzi!!??

Bila shaka unapenda hatma hiyo iwe yenye furaha, amani, upendo na ukwasi.

Je ukwasi unapatikana kwenye Kampuni za Baba Caryn pekee?

Je, upendo upo kwa Caryn ama Annie, au wote??!!

Je, amani unaipata ukiwa kwa Annie ama kwa Caryn?!!

Je, furaha unaipata ukiwa na Caryn au Annie?!

Kura zetu hazitasaidia sana kwenye maamuzi yako juu ya Annie na Caryn, ingawaje inaleta burudani katika kuendeleza simulizi hususani katika kipindi hiki ambacho muendelezo umesimama...

Maamuzi sahihi unayo mwenyewe kwakuwa kuna mengi ambayo hujasimulia kuhusu hao akina Annie na Caryn.


Nakuwa miongoni wa waharibu kura kwenye hili.

Hii ni comment yangu ya kwanza humu, nichukue nafasi hii kukupa kongole kwa uandishi mzuri na kutumia muda wako mwingi kwenye kusimulia hii simulizi yenye mengi ya kujifunza.

#Pigania unacho kiamini.


JBourne59
Hupingwi Babu.
 
Mm nasimama kama "X "

Ni kwamba, mwanaume huwez kumuamini 100%.

Ikiwa tayari nimeshaamua kukupa 100% uwe mume wangu nataka nijue namkabiddhi moyo wangu mtu wa aina gani.

Mimi ni mpole najijua, yule Y tocative ...kwenye mahusiano hujui nimeshadanganywa na wale hit and run wangapi. Mwanaume ananidanganya na ahadi kibao, tena unawaza huyu si angesema tu ananitamani?!😭.

Msemo wa wanaume wote ni walewale una ukweli wake, kama ambavyo ulitaka Y ule ukimbie.

Ni kweli pesa ni kipimo cha tabia ya mtu lkn je unajua ego yangu mie? Kikawaida pesa ni gear tu, brain ipoje? nikiwa na hela, nadhani ni bora uangalie uwezo wa akili kichwani. Na aakiki yako it's balance na yangu?

Unajuaje kuwa y anakulipa fadhila zako kwake?

Bado una kitendawili, unajuaje mama y ni mama mzuri mllezi was watoto
Why utoe 100% moyo wako umpe binadamu mwenye udhaifu na tamaa za kila siku. Wewe hapo mwenyewe ukipata wawili akatokea mmoja akawa yupo more advanced unawaacha Hawa wawili kabla jogoo halijawika. Huwa Hakuna upendo Bali kila kitu duniani huwa Ni TRADING.
Yaani unacheki maximize profit muda huo huo unamliza mwenzako yaani unamlalia. Unataka mahusiano ufaidike nayo,upate maisha mazuri na mme mzuri ama mke na huku wewe hujajiuliza una value gani mbali na kiungo chako na huku mwenzake naye ana kiungo.

Watu ,miti hata wanyama vinacheki palipo na rutuba ama mbolea. Usije ukaniambia mti ama magugu maji yataenda kuota jangwani kuonyesha upendo na mchanga na huku yanatakiwa yaote majini.
The same Simba asile nyati eti akale kuku kisa kuonyesha kuwa anampenda kuku haipo hiyo. Ama maji Yapande mlima yasiteremke ama sumaku isivute chuma ivute mbao eti kuonyesha eti Kuna upendo.

Huwa Hakuna upendo duniani Mana upendo upo against na nature.cheki wanyama wenyewe wanafukuzana kwenye chakula ama kifaranga ajichanganye aende kwa asiye mama yake yaani anavyoraruliwa utalielewa jiji so mbona upendo amfukuze kwa amani kuwa mama yako Ni yule.


Yani kila kitu Ni biashara Kwisha habari,mfano ukiwa hauna value ya kua add kwa mama yako ama familia yako inaonekana huna lolote sawa na jiwe tu yaani unakuwepo mtu jina.
 
Mm nasimama kama "X "

Ni kwamba, mwanaume huwez kumuamini 100%.

Ikiwa tayari nimeshaamua kukupa 100% uwe mume wangu nataka nijue namkabiddhi moyo wangu mtu wa aina gani.

Mimi ni mpole najijua, yule Y tocative ...kwenye mahusiano hujui nimeshadanganywa na wale hit and run wangapi. Mwanaume ananidanganya na ahadi kibao, tena unawaza huyu si angesema tu ananitamani?![emoji24].

Msemo wa wanaume wote ni walewale una ukweli wake, kama ambavyo ulitaka Y ule ukimbie.

Ni kweli pesa ni kipimo cha tabia ya mtu lkn je unajua ego yangu mie? Kikawaida pesa ni gear tu, brain ipoje? nikiwa na hela, nadhani ni bora uangalie uwezo wa akili kichwani. Na aakiki yako it's balance na yangu?

Unajuaje kuwa y anakulipa fadhila zako kwake?

Bado una kitendawili, unajuaje mama y ni mama mzuri mllezi was watoto
Aiseee kwa case yangu mimi X ni mtu asiyejali. Hii moja kwa moja inamdisqualify kuwa mke. Kuna muda huwa nawaza kwamba huenda ana mambo yake kichwani. Lakini mbona hanishirikishi? Sasa anadate na mimi then mambo yake yanayomuumiza kichwa anaenda kumshirikisha nani? Upuuzi.

Y naye ana madhaifu yake ila atleast naona yanavumilika.
 
Last time nimepita humu, nilikuta mnapiga kura eti kumchagulia mleta mada amuoe yupi. Mmefikia wapi?

I'm sure atamuoa mtoto wa yule mzee tajiri. Maana yule binti tayari kaonyesha kumzidi akili. By the way, kijana anakwenda kumeza ndoano ya mwisho kabisa na kua MTUMWA wa familia ya huyo mzee.

Maana uzi mzima, mzee this.... Mzee that...
Kwani hauna kwenu brother? You'll never be a king in another man's territory (mzee).

Kumkimbia yule binti kule ofisini ukizuga haupendi kitonga, then kumuacha mchumba wako wa miaka na miaka ili umuoe mtoto wa mzee ni unafki first class!


Hii sio kura, ni man to man kind of a talk. Excuse my language!
Hahaha...kwamba mzee this..mzee that....
 
Ila hapa ndipo mziki ulipo, BM huyu Careen uli/unampenda kweli au na wewe unakuwa opportunist the 2nd?

Au ndio kila manzi anakuvusha hatua fulani ya life, maana Annie, Accountant na sasa Careen

Anyway na mimi kura yangu imeharibika [emoji28]
 
Ila hapa ndipo mziki ulipo, BM huyu Careen uli/unampenda kweli au na wewe unakuwa opportunist the 2nd?

Au ndio kila manzi anakuvusha hatua fulani ya life, maana Annie, Accountant na sasa Careen

Anyway na mimi kura yangu imeharibika [emoji28]
Ni wazi kabisa hata mm nimeshindwa kupiga kura...
 
Leo nmerudi kusoma baada ya muda mrefu

Bm alianza vizuri lakini unachokitafuta utakipata, tutakuwa apa kusoma.
 
Ndugu zangu, She's Back!

Annie amerudi jana usiku, alipanda Bus so Alifika mida mibovu sana, hamuwezi amini nilienda kumpokea na BMW X3, Akauliza "hii gari ya nani?" Nikamuambia ya mshkaji wangu

Hivi ninavyoandika bado amelala, muda sio mrefu nilikuwa nasikiliza wimbo wa Belle 9 "Amerudi" hizi nyimbo sio Burudani tu sometimes zinaongea uhalisia

Halafu kule kazini kwa Mzee nimerudi lakini sijaajiriwa kama mwanzo, badae nitakuja kuelezea namna Ninavyofanya kazi
 
Ndugu zangu, She's Back!

Annie amerudi jana usiku, alipanda Bus so Alifika mida mibovu sana, hamuwezi amini nilienda kumpokea na BMW X3, Akauliza "hii gari ya nani?" Nikamuambia ya mshkaji wangu

Hivi ninavyoandika bado amelala, muda sio mrefu nilikuwa nasikiliza wimbo wa Belle 9 "Amerudi" hizi nyimbo sio Burudani tu sometimes zinaongea uhalisia

Halafu kule kazini kwa Mzee nimerudi lakini sijaajiriwa kama mwanzo, badae nitakuja kuelezea namna Ninavyofanya kazi
Hii stori yako ina drama nyingi sana mkuu, ni FICTION STORY, kwa kiasi chake unakaribia kumfikia KIDUKULILO
 
Bro story yako niliipenda ila kwa huku unapoelekea ni kama unawavunjia heshima hawa wanawake. Haya mambo mengine yangebaki tu kuwa private. Kuleta humu hadi tuwapigie kura wanawake it means wewe mwenyewe haujui unataka nini
 
Bro story yako niliipenda ila kwa huku unapoelekea ni kama unawavunjia heshima hawa wanawake. Haya mambo mengine yangebaki tu kuwa private. Kuleta humu hadi tuwapigie kura wanawake it means wewe mwenyewe haujui unataka nini
Samahani mkuu kama nilikukwaza
 
Nimerudi kufanya kazi kwenye Kampuni ya Mzee kama Agent na sio kama muajiriwa tena,

Advantage ya kufanya kazi kazi kama Agent zipo nyingi ila moja kubwa ni kwamba unaweza kufanya kazi na makampuni mengine kwa uhuru zaidi, unaweza kufanya kazi na Kampuni hata 5 ni wewe tu na bidii yako

Halafu hawa Agent ndio wanapiga pesa zaidi kuliko hata sisi tuliokuwa tumeajiriwa. ukiajiliwa unakuwa limited, mabano mengi sana

Mfano halisi ni huu, Mimi Wakati nimeajiriwa kwa Mzee katika Utawala wa Mama hata wa Caryn nilikuwa napewa hesabu labda mzigo kilo 1 TRA usizidi 2,800 kwa kifupi nilikuwa napewa rate ambayo sitakiwi kuzidi, Sasa ukichukua 2,800 ukajumlisha na gharama zingine kama kulipa police, kupakia mizigo kwenye toroli hadi kwenye Sealink, kulipa wachukuzi, kununua tape ukija ku calculate total hadi mizigo inafika Dar hesabu inaweza kufika 3000 hadi 3,200 kwa kila kilo, kumbuka hii ndio rate ya chini zaidi,

Binafsi sijawahi kufikisha 4,000 mara zote nakuwa chini ya hapo, na hakuna Agent anayeweza kukubali kutoa mzigo kwa elfu 4 kwa kilo moja, sidhani kama wapo, Ma agent ninao wajua wote wanachezea 4,500 kwenda juu, Wanao charge chini ya hapo labda Ukute Kampuni ndio inaanza

Ukiwa kama Agent una bargain na Kampuni, Ma-Agent wengi huwa wana charge 4,500 hadi 5,000 per kilo, Sasa Kampuni ikishakubaliana na Agent kwamba itamlipa Elfu 4,500 kwa kila kilo kutoka Zanzibar hadi kuufikisha mzigo Dar, Kampuni itakachofanya itapiga hesabu ya kilo zinazotakiwa kusafirisha, tuseme labda Kampuni ina kilo elfu 2 yani Tani 2, so itachukua 2,000 × 4,500 = 9,000,000. Kampuni itampatia Agent milioni 9 baada ya hapo kampuni haitatoa pesa nyingine yeyote Kwa maana ya kwamba katika hiyo milioni 9 Agent atalipia kuanzia usharu usafirisha na takataka zote

Wakati nimeajiriwa Mimi nilishapiga hesabu huwa mara nyingi natumia 3,000 au 3,200 kwa kilo kuitoa Zanzibar hadi kuifikisha Dar, Sasa piga 3200 mara elfu mbili kilo za mzigo 3,200 × 2000 = 6,400,000 sasa Chukua Ile milioni 9 toa hiyo milioni 6 na laki nne (9,000,000 - 6,400,000) inabaki milioni mbili na laki sita, so 2,600,000 hiyo ndio pesa anayobakiwa nayo Agent kama akiweza kufanya clearing ya kilo moja kwa 3,200, Au kama hiyo hesabu imekuchanganya unaweza kuchukua 4,500 - 3200 = 1,300 so elfu moja mia tatu ndio faida yako kwa kila kilo moja, Sasa utachukua 1,300 utazidisha kwa kilo ulizosafirisha tuseme ni hizo kilo elfu 2 so itakuwa 1,300 × 2,000 = 2,600,000

Na Uzuri wa Agent mkishaingia makubaliano na kampuni jambo kubwa huwa wanataka uwafikishie mzigo wao kwa Wakati wao hawahitaji Documents za TRA sijui waanze kupitia mchakato mzima ulioufanya hadi unapitisha mzigo Bandarini wao hiyo sio shughuli yao, lakini Ukiajiriwa Documents ni muhimu kuonesha ofisini, Ujinga wa hizi Kampuni Sasa Mfano mimi si niliwekewa rate ambayo haitakiwi kuzidi 2,800 TRA lakini nikichezesha pale TRA nikatumia 2,500 kulipia kwa kilo na kwenye document ikaonesha hivyo ukipeleka Ofisi hiyo Document kama ilivyo ujue hio 300 itauliziwa,

Sasa tufanye labda umefanya clearance ya kilo elfu moja badala ya kutumia 2,800 ukatumia 2,500 so utakuwa umeokoa Tsh 300 kwa kilo moja, piga mara kilo elfu moja 300 × 1000 = 300,000 kama ni muajiriwa hii chenchi ni lazima urudishe kwasababu kwenye document itaonesha umetumia 2,500 vingine labda ucheze na namba za uongo na kweli ili kuonesha hiyo laki 3 Mahali ulipozitumia, unaweza ukasema mzigo ulikamatwa na kuingizwa CRN, Kuna namna nyingi za kuchezesha

Turudi upande wa Kampuni namna Inavyopata faida, Kampuni nyingi huwa wanacharge Dola 12, 13 hadi 14.5 kwa kilo moja ya mzigo

Sisi tunacharge $12 per kilogram, Chukua zile kilo elfu mbili mara dollar 12, inakuja $24,000 convert hiyo Dola elfu ishirini na nne kwa pesa zetu (rate ya leo $1 = 2371) So $24,000 × 2371 = 56,904,000. Kwenye hii milioni hamsini na sita na laki tisa toa Ile milioni 9 aliyopewa Agent

56,904,000 - 9,000,000 = 47,904,000/=
Kwenye hiyo milioni 47 na laki 9 toa hiyo milioni 7 tufanye ndio mshahara wa wafanyakazi wote japo najua inaweza isifike huko, so inabaki milioni 40 na laki 9, Kwenye hiyo Tsh 40,904,000 tutoe Pesa za pango za Ofisi zote mbili ya China na ya hapa Bongo, tutoe tu hata milioni 5 katika hiyo milioni 40 inabaki milioni thelathini na tano na laki 9

Nilisahau kutoa gharama ya Airway bill, Kusafirisha mzigo kwenye ndege tu Assume ni elfu 5 kwa kila kilo (haiwezi kuzidi hiyo) So 5,000 × 2,000 = 10,000,000 So kwenye Ile milioni 35 tutoe milioni 10.

35,904,000 - 10,000,000 = 25,904,000
Katika hiyo Milioni 25 na laki 9 tutoe hiyo milioni tano na laki tisa kwa emergencies zozote, inabaki milioni 20 kamili ambayo hiyo ndio faida ya Kampuni, na inaweza kuwa zaidi ya hapo kwasababu nimefanya makadirio makubwa kwenye mahesabu kama hapo kwenye Airway bill huwa ni chini ya hiyo elfu 5

Kumbuka hiyo ni hesabu ya trip moja, kwa Kampuni ya kawaida kama ya Mzee hizo kilo elfu 2 na zaidi huwa zina safirishwa kwa mara mbili kwa wiki

Sasa tufanye makadirio ya chini kabisa Kampuni ya Mzee kwa wiki inasafirisha kilo elfu 3, Mwezi una wiki nne so 3000 × 4 = 12,000

Tani 12 Yani kilo 12,000 × $12 = 144,000
144,000 kwa pesa ya kiBongo tukipiga kwa rate yetu Ile Ile ya 2371 inakuja 340,560,000

Hiyo milioni mia tatu ndio hesabu ya mwezi na kumbuka hayo ni makadirio ya chini kabisa lakini pia kumbuka hiyo sio faida kuna gharama za kuendesha Kampuni bado hatujatoa zile Pesa za Agent zipo humo humo kwenye hiyo mia tatu Airway bill na kila kitu

Turudi kwenye hesabu yetu ya kilo elfu mbili, tufanye kila wiki Kampuni inasafiri Tani 2 tu, hesabu yake si tulishaipiga na tukapata faida ni milioni 20 halafu kwenye hii milioni 20 tulishawalipa wafanyakazi na tulishalipa rent ya Ofisi zote mbili so ukipiga mara wiki 4, itakuwa milioni 80+ hiyo ni faida ushatoa kila kitu na kuwalipa wafanyakazi

Inakuja Milioni 80 + kwasababu kuna gharama za kuendesha Kampuni hazijirudii Kila wiki, kama kulipa wafanyakazi au kulipa pango la ofisi

Binafsi kwa wiki tu nilikuwa nakimbiza hadi tani 5, lakini sasa huwa sio Guarantee, wiki hii ukipiga Tani 5 wiki ijayo unaweza piga Tani moja na kilo kadhaa

Halafu kwenye hiyo rate ya Dollar 12 kuna kitu nimesahau, sio mizigo yote inachajiwa kwa rate hiyo vitu kama simu laptops zina charges zake, halafu kwenye story mnakumbuka ile Kampuni niliyopoteza mzigo wao, wale wanachajiwa zaidi ya Dola 12, kwasababu wale wenyewe wateja wao wanawalipisha dollar 18.5

Kwa kifupi Mzee Kwa mwezi faida yake inaanzia Milioni 100 na kuendelea, ninaweza kusema hii kama sio Kampuni ya kwanza basi ipo nafasi ya pili katika zile Kampuni ambazo Mzee zinamuingizia Pesa ya kutosha

Nihitimishe kwa kusema kwamba hizi Air Cargo Companies zinalipa sana na kwa sisi wafanyakazi itakulipa zaidi kama ukiwa Agent maana unaweza kufanya kazi na makampuni mengi kwa kadri uwezavyo lakini hata kama ukifanya na Kampuni moja kama Ina kilo za kutosha bado upo mbele

Welcome to the world of $1 a day, if you make it good for you otherwise it's your fucking problems
 
Ilipoishia

Pia katika maongezi Mzee akaniambia kuwa kwa vile ahadi za kuja kupaona kwangu zimekuwa nyingi bila mafanikio akaniahidi na kunihakikishia atakuja siku ya Pasaka kula sikukuu kwasababu siku hiyo Bi Mkubwa Yani mke wake atakuwa yupo mkoani

Hivyo Ukiachana na Annie, Mzee pia ameingia kwenye list yangu ya wageni nitakao wapokea siku ya Pasaka japokuwa Annie alisema atakuja before Pasaka

Muendelezo

(Episode 24, SEASON 2)

Hii siku nilivyorudi nyumbani nikamjulisha Caryn kuhusu Mchina (Hili Jina kalitoa member wa hapa Jf wakuitwa [emoji1542]Tajiri Kichwa) Mchina ni huyu jamaa ninayemfanyia Mpango wa kwenda China, basi nikamuambia kwamba jamaa inabidi awe anakuja ofisini pale akiwa anasubiria process za visa zianze kufanyika

Caryn: "Ofisini anakuja kama nani? na kufanyaje? majukumu yake yeye si ni huko China"

BM: "Anakuja kwa lengo la kujifunza ili akifika kule (china) at least awe anajua baadhi ya mambo"

Caryn: "Wewe ni nani aliyekuambia sisi tunaajili wanafunzi wa kuja kujifunza kazi"

BM: "Aysee, hii sio amri yangu, ni kutoka kwa Mzee"

Caryn: "Na mm ndio nakuambia hatuajiri wanafunzi, tafuteni mtu mwenye Experience"

BM: "Kama ni hivyo acha niende mwenyewe"

Caryn: "Unajua BM unapenda sana kufanya vitu kwa mazoea, hii tabia hata Dad anayo"

BM: "Hiyo tabia ya mazoea unayoiana kama ni kasoro ndio imemfikisha Mzee pale alipo"

Caryn: "Back then, kwasasa huwezi kutoboa ukiwa una apply hiyo tabia mara kwa mara"

BM: "Tatizo lako unapenda ku complicate sana mambo... anyways kwa uchache wa siku zilizobaki according to Mzee, ni Either Mimi au Jamaa"

Caryn: "What's for dinner?"

BM: "Hujaniambia msimamo wako kama ni Mimi au Mchina, kama ni Mchina nimuambie Jumatatu aanze kuja job"

Caryn: "How does that answer my dinner question"

Caryn bhana, ukiwa unabishana nae kuhusu kitu fulani na ghafla ukaona ame switch topic basi ujue ameshakubaliana na wewe, hawezi ku admit directly, ikitokea basi ni mara chache sana.

Jumatatu ya mwisho ya mwezi wa 3, nakumbuka ilikuwa date 27 kama sikosea Mchina ndio alianza kuja pale ofisini, kabla hajaja nilimpanga kabisa kuwa mtu anayekuja ku-Deal nae ni kichefu chefu so ajue namna ya kuishi nae coz akisema NO basi ujue ni NO kweli hadi Mzee anaipitisha ila kwa Mzee anaweza kukutamkia YES lakini kwa Caryn ikawa NO na Mzee akabadilisha YES yake kuwa NO kwa Caryn

Yani nilichokuwa najaribu kumuambia Mchina ni kwamba katika kuruka ruka kwake kote awe makini tu asimkanyage Caryn kwasababu ndio mambo yote, ukijua kwenda nae sawa mambo yana floo yenyewe

Mchina nikampeleka Ofisini kwa Caryn kumtambulisha, baada ya kutambuana Caryn akaanza kumfanyia Oral interview

Caryn: "Okay, tell me have you ever exported....I mean What experience do you have in exportation of goods"

Mchina: "No, I don't have any, I'm looking forward to gain some here"

Caryn: "Impressive! I really like straight forward guy like you"

Caryn baada ya kumaliza kumuulizia Mchina maswali ya yanayohusiana na kazi akaanza na Personal questions

Caryn: "Una familia?"

Mchina: "Ndio ninayo"

Caryn: "Una watoto wangapi? na uliezaa nae bado unaishi nae?"

Mchina: "Sina mtoto, kwa kifupi sijaoa"

Caryn: "Kwanini ulijibu Ndio kwenye swali langu"

Mchina: "Nilidhani una maanisha familia ya Baba, Mama na ndugu niliozaliwa nao"

Caryn: "Hiyo sio familia yako, ni familia ya Baba yako na Mama yako"

Caryn: "Wewe na BM mna muda gani tangu mfahamiane?"

Mchina: "Karibia Mwaka sasa"

Càryn: "Be specific"

Mchina: "Ni ngumu kukumbuka siku tuliyofahamiana, so I can't be specific"

Caryn: "Wow, this is the level of confidence and boldness we want to see moving forward...anyways kesho utaniletea Barua mbili za udhamini"

Kusikia hivyo nikajua 'hapa mchezo ushaisha' tulivyotoka nje nikamuambia Mchina "Mwanangu kumbe unaweza kuwa kauzu"

Mchina: "Oya, unajua ulivyoniambia tabia za demu mwenyewe nikasema piga ua hata kama Sina Confidence nitakuwa nayo tu hata kama ni ya kuigiza"

BM: "Na kama ulimsoma, Kuna maswali alikuwa anakuuliza ili tu ujikanyage"

Mchina: "Ila unajua nini mwanangu, umetisha sana, sitakuangusha, Boss wako mm nitaenda nae anavyotaka tutarekebisha mbeleni, Ujanja sio kua bora, ujanja kupata"

Jioni yake wakati tupo nyumbani Caryn akawa kama Bado ana mashaka

Caryn: "BM yule jamaa ni rafiki yako kweli? I mean mnajuana vizuri?"

BM: "Ndio, kwani kuna tatizo?"

Caryn: "Nop, hakuna tatizo, anaonekana smart kiasi chake ila confidence inambeba"

BM: "Sawa sawa Mwana saikolojia"

Caryn: "Kebehi tu lakini naongea fact"

BM: "Uko sasa ni kujishtukia mm sijakebehi mtu"

Caryn: ".....wewe una uwezo mkubwa, you're smart ila ujasiri unakuangusha"

BM: "Hii sasa ni compliment au?"

Kwenye hii Convo nilikuwa namletea Caryn masihara mengi na utani wa kutosha, watu walivyoanza kusikia njaa ilibidi utani tuuweke pembeni

Caryn: "Bro, Body warms in my stomach are already screaming"

BM: "Sasa mm nifanyaje?"

Caryn: "It's your turn to cook today"

BM: "I'm not in the mood"

Caryn: "So you're in the mood to be hungry then"

BM: "Mimi nilishaji-sort (nilishakula)

Caryn: "BM you know this is not the first time you've doing this each time is your turn to cook you choose to eat out"

Caryn: Wait... you want me to do the cooking just for myself while you continue to eating out ... right? that's what you want?"

BM: "Hiyo pia si mbaya, mm nitarudi kwa nyumba nikiwa nimejipanga kabisa"

Nikaingia zangu chumbani, ukweli ni kwamba nilikuwa sijala ila nimemjibu tu vile kukwepa kukatakata vitunguu, Wakati naingia chumbani Caryn akaingia jikoni kukorofisha mambo,

Baada ya lisaa limoja kupita nikagongewa mlango eti chakula kimeiva naitwa nikale, nikaona kabisa huu ni mtego japokuwa nina njaa lakini nikavunga, nikamuambia we tangulia nakuja, hadi yeye anamaliza kula mimi sijatoka chumbani akanifuata tena akaniambia "BM chakula kinazidi kupoa, na hakuna Microwave kusema uta warm"

Sikwenda hata kula kwa kujishtukia, asubuhi naamka nimeingia jikoni kufuata ndizi (Kila asubuhi ni lazima Nile ndizi) nikakuta chakula alichoniwekea Caryn kakifunika na sahani kumbe msosi niliwekewa kweli ila kwa ego nikaamua kulala nayo

Wiki moja kabla ya Pasaka Annie akanicheki akaniambia Mpango wake wa kuja Dar unaweza usiwezekane kwasababu kuna mfanyakazi mwenzao amefiwa na Mama yake so kama huyo mfanyakazi mwenzake akiwahi kurudi kutoka mazishi ndio anaweza akaja na kama akichelewa itabidi tu Pasaka ailie huko huko Mwanza akisubiri safari ya mwezi wa sita

Hii ilikuwa Habari njema kwangu kwasababu mwanzo nilipanga uongo ambao sikuwa na uhakika kama Annie angeniamini au lah!

Hatimaye Pasaka ilifika lakini Annie hakufika Dar, ila Mzee yeye Alifika kwangu, alikuja mapema tu yale masaa ya breakfast but Mzee hanywagi chai, nikamuandalia kahawa, Wakati naendelea kunywa chai huku Mzee akipiga kahawa yake akauliza

Mzee: "Hapa unaishi mwenyewe?"

Unajua kuna swali mtu anauliza Kwa maana ya kwamba hajui kitu anataka umfahamishe, na kuna swali mtu anauliza kutaka kujua akili yako inaishia wapi kupitia majibu yako huku yeye tayari akiwa na majibu yake, ilibidi ninyooshe maelezo huku nikiwa na wasiwasi mno

BM: "Hapana, naishi na Caryn japokuwa mara nyingi huwa anakuwa kwa Dada yake"

Mzee: "Najua kama unaishi na Caryn, niambie kitu kipya ambacho sikifahamu"

BM: "Mzee mimi nilihisi unajua, kwakudhani Caryn alikuambia"

Mzee: "Hisia zako zipo sahihi, nilikuwa najua lakini kwa njia zangu mwenyewe hata huyo Caryn hajaniambia, hata hivyo wewe ndiye uliyepaswa uniambie, ukaribu wangu Mimi na wewe unashindwa kuniambia jambo nyeti kama hili kweli? unataka mimi nikufikiriaje, ivi ingetokea huyu Binti kakufia usiku na Mimi sifahamu kama yupo kwako unadhani Mama yake angekuelewa?"

BM: "Mzee kosa ni la kwangu naomba unisahame"

Mzee: "Unajua kuna makosa unaweza ukahisi ni madogo lakini yanavunja uaminifu kwa kiasi kikubwa sana"

Hiyo kauli ya Mzee ndio ikanimaliza nguvu, sasa namna alivyojua hii issue ndio nilichoka kabisa

Iko hivi, Mzee gari zake zote kazifunga tracker kasoro Gari ya mke wake, ninaposema Gari zake zote namaanisha hadi hizi za kina Caryn na Michelle, Sasa Ile siku ananipa Jeep mm nikijua narahisishiwa usafiri kumbe ule ulikuwa mtego,

Kwanini nasema mtego, ilikuwa hivi, Wakati Mimi naondoka Mzee alikaa chini na hiyo simu yake specific kwaajili ya hizo mambo, akaona Jeep lake hadi Mahali lilipo park, aliyekuja kuharibu ni Caryn maana Mzee anajua Caryn yupo kwa Michelle na atalala huko lakini baada ya muda akaona BMW limepark maeneo yale yale lilipopark Jeep

Hapo ndipo alipoanza kupata mashaka japokuwa tulimuambia sisi ni majirani lakini kupitia alichokiona yeye mwenyewe akawa kashajijazia kichwani kwake ni kitu gani kinaendelea

Baada ya Mzee kumaliza kunielezea kilichokuwa kinaendelea nyuma ya Pazia bila Mimi kujua Mzee akaniuliza swali

Mzee: "Nakumbuka ushawahi kuniambia kama una mchumba, na hiki ndio kipindi kizuri Cha kuishi nae ili mjuane vizuri kitabia lakini badala yake unaishi na Caryn, Kwani wewe na Caryn mna mpango gani?"

Hili swali ni muendelezo wa yale maswali ya Mzee ambayo anakuuliza ili kujua akili yako inapoishia na uwezo wako wa kufikiria, ila safari hii hajaniachia gepu la kumjibu, Wakati nataka kumjibu akaniambia kitu ambacho hadi kesho nakitafakari lakini nakosa majibu

Mzee: "Unajua...ngoja nikuambie kitu kijana wangu, kwenye huu ulimwengu ukitambua wenye manufaa maishani mwako usiwape umuhimu, hawatakuumiza. Wenye umuhimu maishani mwako usiwafanye wenye manufaa, Utaumia"


Itaendelea
...

Sent from my V2204 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom