Mafian cartel
JF-Expert Member
- Nov 19, 2021
- 3,876
- 7,118
Kuna Kampuni nilijichanganya sikusoma vizuri price list yao kwa product niliyokuwa nasafirisha ilikuwa ni $50 per pc mimi nilikariri ni $13.5 per kg so nikampa tu supplier addres yaoNimerudi kufanya kazi kwenye Kampuni ya Mzee kama Agent na sio kama muajiriwa tena,
Advantage ya kufanya kazi kazi kama Agent zipo nyingi ila moja kubwa ni kwamba unaweza kufanya kazi na makampuni mengine kwa uhuru zaidi, unaweza kufanya kazi na Kampuni hata 5 ni wewe tu na bidii yako
Halafu hawa Agent ndio wanapiga pesa zaidi kuliko hata sisi tuliokuwa tumeajiriwa. ukiajiliwa unakuwa limited, mabano mengi sana
Mfano halisi ni huu, Mimi Wakati nimeajiriwa kwa Mzee katika Utawala wa Mama hata wa Caryn nilikuwa napewa hesabu labda mzigo kilo 1 TRA usizidi 2,800 kwa kifupi nilikuwa napewa rate ambayo sitakiwi kuzidi, Sasa ukichukua 2,800 ukajumlisha na gharama zingine kama kulipa police, kupakia mizigo kwenye toroli hadi kwenye Sealink, kulipa wachukuzi, kununua tape ukija ku calculate total hadi mizigo inafika Dar hesabu inaweza kufika 3000 hadi 3,200 kwa kila kilo, kumbuka hii ndio rate ya chini zaidi,
Binafsi sijawahi kufikisha 4,000 mara zote nakuwa chini ya hapo, na hakuna Agent anayeweza kukubali kutoa mzigo kwa elfu 4 kwa kilo moja, sidhani kama wapo, Ma agent ninao wajua wote wanachezea 4,500 kwenda juu, Wanao charge chini ya hapo labda Ukute Kampuni ndio inaanza
Ukiwa kama Agent una bargain na Kampuni, Ma-Agent wengi huwa wana charge 4,500 hadi 5,000 per kilo, Sasa Kampuni ikishakubaliana na Agent kwamba itamlipa Elfu 4,500 kwa kila kilo kutoka Zanzibar hadi kuufikisha mzigo Dar, Kampuni itakachofanya itapiga hesabu ya kilo zinazotakiwa kusafirisha, tuseme labda Kampuni ina kilo elfu 2 yani Tani 2, so itachukua 2,000 × 4,500 = 9,000,000. Kampuni itampatia Agent milioni 9 baada ya hapo kampuni haitatoa pesa nyingine yeyote Kwa maana ya kwamba katika hiyo milioni 9 Agent atalipia kuanzia usharu usafirisha na takataka zote
Wakati nimeajiriwa Mimi nilishapiga hesabu huwa mara nyingi natumia 3,000 au 3,200 kwa kilo kuitoa Zanzibar hadi kuifikisha Dar, Sasa piga 3200 mara elfu mbili kilo za mzigo 3,200 × 2000 = 6,400,000 sasa Chukua Ile milioni 9 toa hiyo milioni 6 na laki nne (9,000,000 - 6,400,000) inabaki milioni mbili na laki sita, so 2,600,000 hiyo ndio pesa anayobakiwa nayo Agent kama akiweza kusafirisha kilo moja kwa 3,200, Au kama hiyo hesabu imekuchanganya unaweza kuchukua 4,500 - 3200 = 1,300 so elfu moja mia tatu ndio faida yako kwa kila kilo moja, Sasa utachukua 1,300 utazidisha kwa kilo ulizosafirisha tuseme ni hizo kilo elfu 2 so itakuwa 1,300 × 2,000 = 2,600,000
Na Uzuri wa Agent mkishaingia makubaliano na kampuni jambo kubwa huwa wanataka uwafikishie mzigo wao kwa Wakati wao hawahitaji Documents za TRA sijui waanze kupitia mchakato mzima ulioufanya hadi unapitisha mzigo Bandarini wao hiyo sio shughuli yao, lakini Ukiajiriwa Documents ni muhimu kuonesha ofisini, Ujinga wa hizi Kampuni Sasa Mfano mimi si niliwekewa rate ambayo haitakiwi kuzidi 2,800 TRA lakini nikichezesha pale TRA nikatumia 2,500 kulipia kwa kilo na kwenye document ikaonesha hivyo ukipeleka Ofisi hiyo Document kama ilivyo ujue hio 300 itauliziwa,
Sasa tufanye labda umefanya clearance ya kilo elfu moja badala ya kutumia 2,800 ukatumia 2,500 so utakuwa umeokoa Tsh 300 kwa kilo moja, piga mara kilo elfu moja 300 × 1000 = 300,000 kama ni muajiriwa hii chenchi ni lazima urudishe kwasababu kwenye document itaonesha umetumia 2,500 vingine labda ucheze na namba za uongo na kweli ili kuonesha hiyo laki 3 Mahali ulipozitumia, unaweza ukasema mzigo ulikamatwa na kuingizwa CRN, Kuna namna nyingi za kuchezesha
Turudi upande wa Kampuni namna Inavyopata faida, Kampuni nyingi huwa wanacharge Dola 12, 13 hadi 14.5 kwa kilo moja ya mzigo
Sisi tunacharge $12 per kilogram, Chukua zile kilo elfu mbili mara dollar 12, inakuja $24,000 convert hiyo Dola elfu ishirini na nne kwa pesa zetu (rate ya leo $1 = 2371) So $24,000 × 2371 = 56,904,000. Kwenye hii milioni hamsini na sita na laki tisa toa Ile milioni 9 aliyopewa Agent
56,904,000 - 9,000,000 = 47,904,000/=
Kwenye hiyo milioni 47 na laki 9 toa hiyo milioni 7 tufanye ndio mshahara wa wafanyakazi wote japo najua inaweza isifike huko, so inabaki milioni 40 na laki 9, Kwenye hiyo Tsh 40,904,000 tutoe Pesa za pango za Ofisi zote mbili ya China na ya hapa Bongo, tutoe tu hata milioni 5 katika hiyo milioni 40 inabaki milioni thelathini na tano na laki 9
Nilisahau kutoa gharama ya Airway bill, Kusafirisha mzigo kwenye ndege tu Assume ni elfu 5 kwa kila kilo (haiwezi kuzidi hiyo) So 5,000 × 2,000 = 10,000,000 So kwenye Ile milioni 35 tutoe milioni 10.
35,904,000 - 10,000,000 = 25,904,000
Katika hiyo Milioni 25 na laki 9 tutoe hiyo milioni tano na laki tisa kwa emergencies zozote, inabaki milioni 20 kamili ambayo hiyo ndio faida ya Kampuni, na inaweza kuwa zaidi ya hapo kwasababu nimefanya makadirio makubwa kwenye mahesabu kama hapo kwenye Airway bill huwa ni chini ya hiyo elfu 5
Kumbuka hiyo ni hesabu ya trip moja, kwa Kampuni ya kawaida kama ya Mzee hizo kilo elfu 2 na zaidi huwa zina safirishwa kwa mara mbili kwa wiki
Sasa tufanye makadirio ya chini kabisa Kampuni ya Mzee kwa wiki inasafirisha kilo elfu 3, Mwezi una wiki nne so 3000 × 4 = 12,000
Tani 12 Yani kilo 12,000 × $12 = 144,000
144,000 kwa pesa ya kiBongo tukipiga kwa rate yetu Ile Ile ya 2371 inakuja 340,560,000
Hiyo milioni mia tatu ndio hesabu ya mwezi na kumbuka hayo ni makadirio ya chini kabisa lakini pia kumbuka hiyo sio faida kuna gharama za kuendesha Kampuni bado hatujatoa zile Pesa za Agent zipo humo humo kwenye hiyo mia tatu Airway bill na kila kitu
Turudi kwenye hesabu yetu ya kilo elfu mbili, tufanye kila wiki Kampuni inasafiri Tani 2 tu, hesabu yake si tulishaipiga na tukapata faida ni milioni 20 halafu kwenye hii milioni 20 tulishawalipa wafanyakazi na tulishalipa rent ya Ofisi zote mbili so ukipiga mara wiki 4, itakuwa milioni 80+ hiyo ni faida ushatoa kila kitu na kuwalipa wafanyakazi
Inakuja Milioni 80 + kwasababu kuna gharama za kuendesha Kampuni hazijirudii Kila wiki, kama kulipa wafanyakazi au kulipa pango la ofisi
Binafsi kwa wiki tu nilikuwa nakimbiza hadi tani 5, lakini sasa huwa sio Guarantee, wiki hii ukipiga Tani 5 wiki ijayo unaweza piga Tani moja na kilo kadhaa
Halafu kwenye hiyo rate ya Dollar 12 kuna kitu nimesahau, sio mizigo yote inachajiwa kwa rate hiyo vitu kama simu laptops zina charges zake, halafu kwenye story mnakumbuka ile Kampuni niliyopoteza mzigo wao, wale wanachajiwa zaidi ya Dola 12, kwasababu wale wenyewe wateja wao wanawalipisha dollar 18.5
Kwa kifupi Mzee Kwa mwezi faida yake inaanzia Milioni 100 na kuendelea, ninaweza kusema hii kama sio Kampuni ya kwanza basi ipo nafasi ya pili katika zile Kampuni ambazo Mzee zinamuingizia Pesa ya kutosha
Nihitimishe kwa kusema kwamba hizi Air Cargo Companies zinalipa sana na kwa sisi wafanyakazi itakulipa zaidi kama ukiwa Agent maana unaweza kufanya kazi na makampuni mengi kwa kadri uwezavyo lakini hata kama ukifanya na Kampuni moja kama Ina kilo za kutosha bado upo mbele
Welcome to the world of $1 a day, if you make it good for you otherwise it's your fucking problems
Siku nilvyotumiwa invoice ndo nikagundua nimeyakanyaga na nilikua na pc kama 6 hivi [emoji3]