Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Kwahiyo Kazini kule nisiwaze sio....haya je ikitokea kama ulivyosema kati ya Annie na Caryn unadhani wapi ni chaguo sahihi?
 
Kusema ukweli sijajipanga kihivyo kuingia kwenye Biashara ndio maana sitaki kuharakisha kuacha kazi pale Ofisini japokuwa ndio hivyo mambo yameingiliana

Inawezekana pia Mzee anataka kusoma utayari wangu kupitia huyu Dogo, na ubaya muda ni mchache wa kupanga na kupangua mambo kabla Mzee hajarudi, ili hata akirudi at least aone Kuna Progress

Kuhusu namba ya Caryn ebu subiri kwanza mkeka utiki
 
I hope hutofeli mtihani mdogo namna hiyo, na kabla ya kumfungulia biashara huyo dogo ni lazima umjenge kisaikolojia ili ajue ndio anaenda kuanza maisha yake na kusaidia ndugu zake.
 
Mkuu kwanini hutaki "kulipia" vitu vizuri ?
Hujui kwamba uandishi ni talanta ambayo inapaswa kumlipa yule aliyejaaliwa nayo...

Kama una kipaji, kwanini ufe na njaa
Waandike vitabu tununue sio mtindo huo wa online stories..
 
Sikiliza kuna mtu kukushauri biashara nzuri tu hapo juu, amesema fungua duka la spare za pikipiki na bajaji, tafuta mafundi wazuri hata wawili kwenye hii biashara mafundi huwa wanajilipa kwa kufanya ufundi ila wewe unauza spare, sasa mi naongezea kwenye hili wazo kalifanye njee ya mji kidogo, kule unapanga nyumba nzima mbele ya nyumba utaweka kiosk cha hiyo biashara, pili utakuwa hiyo nyumba unalaza bajaji na pikipiki so utamwajili mlinzi , na ukipata kaeneo kaziada hapo mbele ya nyumba unaongezaa na mashine ya kuosha pikipiki na bajaji.

Upande wa mapenzi tumia formula inaitwa delay method, yaani unaendelea kubuy time huku unasongesha goals zako, Ongea na Mama yake Accountant kuwa kuna mambo unataka kuweka sawa ndio umvalishe pete, omba akupe muda kidogo, huo muda ukipita unaangalia jambo lingine la kulata delay, siku zote visingizio haviishi mkuu, utakuwa unatengeneza visingizio mpaka mwaka unaisha.

Hii ndo delay method.
 
Teenager ni 13-19..

Umri huo huwa wanakua shule na vyuoni..
 
Dah! Asante mkuu umenisaidia kuwazaa hasa katika hili la Caryn, Yani umelenga mule mule, akiongea kamaliza halafu harudii x2 na kukuambia ukweli kwake hawazi

Kuhusu Accountant ana point zake muhimu tu tena 3 ila kiukweli sio wife material kabisa
 
Sawa mkuu, ndio nimeianza kusoma maoni yako, acha nisome na maoni ya wengine nione wanasemaje katika hili, Muda upo wa kutosha sina sehemu ya kwenda

Hey
Achana na huyo accountant, kakufanya slave wake kisa una shida.mwambie mapenzi hayaendi hivo.na pia umuweke mbali Annie wako maana anaweza mdhuru bure.
Kwa hii likizo komaa na huyu kijana,hata biashara ya chakula inalipa.hata chipsi zinalipa.kikubwa kaa nae na wadogo zake waeleze ukweli waambie nini wanatakiwa kufanya.halafu wafanye ndugu zako,wadogo zako na jukumu lako maana kufanikiwa kwao ni kufanikiwa kwako.pia kijana afanye kile anachokifurahia atafanikiwa.

Pia kama na Annie mweleze mkanda wote mwanzo mwisho aujue ukweli kutoka moyoni maana unavyomficha nae anabaki njia panda.MPE ukweli na ushirikiane nae kama unamuhitaji kwa safari yako ya mbele.kuanzia mambo ya office yalokukuta mpaka mzee.hata ikitokea ukaacha kazi na kwa mzee pakawa pagumu akuelewe its for her.mpe mkanda halisi na vitisho vyote unavyopewa.

Ila hakikisha kwanza mpango wa kijana buguruni unatick ndipo uanze kufanya maamuzi ya office!komaa na vijana kwanza kwenye hii likizo.
 
Maono yangu.

BM X6 una kipaji kizuri cha kutunga hadithi na kuipangilia vizuri. Hakika imeburudisha wengi, japo kwangu haina uhalisia.

1. Hali ya kujiamini kupita kiasi cha bint Caren imenipa wasiwas yeye ni teenager japo wanauwezo alipaswa kuku respect kama kaka yake.

2. Wew una zali gani mpaka upendwe na watoto wa familia bora tu na tena waliozaliwa peke yao kwa wazazi wao?. Mtoto wa bosi wako (Accountant) umesema ni mtoto wa pekee na ni familia bora. Pili mpenzi wako Annie pia umesema ni mtoto wa pekee kwao na walikuwa familia bora sana kiasi cha kuweza kukusaidia baadh ya stuffs ulipokuwa unasoma.

3. Nyumbani kwa mzee ambako ni nyumba ya kisasa, ina maana hakuna mtu yeyote zaidi ya wanafamilia?. Yaan Mzee, mama na na mabint zake wawil?. Ambao kuna muda pia wanakuwa hawapo, kwa maelezo yako wanakuwa Kibaha. Sasa walakini wangu upo katika

a. Suala la ulinzi katika hayo mazingira, japo kuna CCTV lkn pia kuwa kwa mtu wa ziada ni muhimu kwan kuna muda umesema nyumba huwa inabaki bila mtu.

b. Mfanyakazi wa kusaidia usafi wa ndan na nje. Ni ngumu sana kwa familia bora ukute wao ndio wanapiga deki, kufagia uwanja na hata kufyeka majani.

Ni hayo tu mkuu, nakutakia likizo njema😄😄
 

Kuna mawazo mengi ya biashara ambayo nadhani unaweza yaangalia lakini kabla hatujafika huko kuna moja mbili tatu za kuangalia otherwise utafail (kumbuka akifail kijana nawe umefail)
Kwa mawazo yangu, u will need the following

1. Kumtrain kijana his mind iamini kuwa anaweza kufanya kazi na kupata pesa badala ya kutegemea kuomba (mtihani muhimu sana huu katika Zoezi lako)

2. Kumfanya azoee pesa (asichachawe na hela, kumbuka hajawah kushika laki kwa mara moja )

3. Ufahamu yeye kwa mizunguko yake ya hapo buguruni nini amekipenda na anaona kinaweza mletea hela( u real to hear also from him )

3. Management, management, management….my friend nimerudia hilo neno three times kuonyesha umuhimu wake! Lazima wewe kama wewe uwe na visibility ya anachokifanya na lazima uwe na uelewa kutambua kama mnaenda kwenye right track au mshapishana na future!

Nitaendelea na ushauri nikipata tena muda wa kuandika mkuu!
Good luck 👍
 
Mbona kama wewe ndio umeniweka katika Wakati mgumu zaidi kama haya unayoyaeleza yataenda kuwa kweli, ila Caryn kweli ana kadharau flani nadhani inasababishwa na overconfidence
 
Mtihani pamoja na Story yote havina muda mrefu, Wakati naandika heading ya Uzi nilikuwa nishapewa mtihani, ila tukio lililonitokea nikiwa nishauandika Uzi ni la ofisini la kupewa likizo
 
Ila kweli, unajua mtu mwingine anaweza kuwaza kupiga U-turn halafu mwisho wa siku ndio akaharibu kabsaa
 
Unaweza kuwa mwandishi mzuri wa scripts na muongozaji mzuri.

Fanyia kazi hili mkuu
 
Mtihani pamoja na Story yote havina muda mrefu, Wakati naandika heading ya Uzi nilikuwa nishapewa mtihani, ila tukio lililonitokea nikiwa nishauandika Uzi ni la ofisini la kupewa likizo
Mkuu tuendelee na story ninaifurahia na ina kitu cha kujifunza. Lkn sio halisi, hili niachie mimi naomba nisikutoe kwenye reli.
 
Ila kweli, unajua mtu mwingine anaweza kuwaza kupiga U-turn halafu mwisho wa siku ndio akaharibu kabsaa
Naam hata kujaribu namna gani kukuoa nafasi ya kuwa na Caryn ujue ndio mwisho wa imani yake kwako.
 
Hapo kwa Caryn kujenga hoja kama mtu mzima mi pia ilinifikirisha sana.

Anyway anajua kutunga na tumepata mawili matatu kama mafundisho katika maisha. Ngoja tuone huko mbeleni muendelezo wake utavyokua.
Caryn mbona ni mkubwa tu jamani, kwann wengi mnafikiria Caryn ni mdogo sana?
 
Si utarudi tena baada ya miezi miwili utuambie ndugu yangu??
 
Tafuta fundi mzuri wa pikipiki na bajaji, location safi kutokana na experience ya fundi, fungua kiduka kidogo cha spares za hivyo vyombo vya usafiri tajwa hapo juu. Muweke dogo asimamie chini ya uangalizi wako wa karibu sana.
Hii pia naiweka kwenye list mkuu, shukrani [emoji1545]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…