Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

We ungeweza? yaani uache kazi hujajipanga! unafanya masiala nini![emoji16] Mtaani kuna balaaa
 
Anatunga lazima story iwe n Good ending ,,, any way jifunze kwa OMUGHAKA
 
....
 
Ilipoishia

BM: "Ebu funguka sijakuelewa"

Mshkaji: "Labda nikuulize wewe, likizo yako inakaribia kuisha umeamuaje kuhusu kazi?"

BM: "Kazi nitapiga kama kawa, nitajua jinsi ya kumpanga yule mtoto (Accountant)"

Mshkaji: "Sasa acha nikupe mchoro mzima, hii ni kama ramani na uko vitani ukikosea kuisoma hii ramani unajikuta kwa adui na kumbuka huna siraha"

Muendelezo


SEASON 2 Episode 4


BM: "Nakusikiliza kiongozi"

Mshkaji: "Unajua sometimes inabidi utumie akili kwenye kufanya maamuzi, ukiweka hisia mbele kwenye kila kitu utafeli, kwanza kabisa mruhusu Demu wako aende Mwanza, usipomruhusu utajipiga pini mwenyewe"

BM: "Then nikishamruhusu?"

Mshkaji: "Ukishamruhusu utajua unaishi vipi na yule Demu wako wa Ofisini kule, unajua yule ndio amekuweka mjini, hata kama humpendi wewe igiza kumpenda hutapungukiwa chochote sana sana ndio una gain"

BM: "Huu Ushauri wako wa leo sijauelewa kabisa"

Mshkaji: "Hujauelewa kwasababu umeweka Mapenzi mbele hivyo unatumia sana hisia katika kuamua mambo, Leo upo tayari kuacha Kazi kwaajili ya mwanamke lakini nikuhakikishie mwanamke huyo huyo atakuja kukuacha wewe kwasababu huna kazi"

BM: "Sawa nimekuelewa, vipi ule mchongo wako wa mkoa, ulitiki?"

Nikachange mada makusudi, tukaendelea na story zingine hadi giza likaingia tukaagana, mimi nikarudi zangu home, nimefika mjengoni nimemkuta Annie kalala Sebuleni kwenye kochi,

Kabla sijamuamsha nikakaa kwenye kochi lingine nikakumbuka kile alichoniambia Mshkaji wangu kule Kinondoni, niliwaza sana na kuuchambua ule ushauri nikaona una make sense, nikamuamsha Annie

BM: "Vip mbona umelala mapema sana, uko sawa?"

Annie: "Niko poa, ni uchovu tu usingizi umenipitia muda sio mrefu"

BM: "Ungeenda kulala ndani, Vipi lakini Kuna chochote kitu?"

Annie: "Yeah, mimi nilishakula labda kama nakuwekea wewe tu"

BM: "Hapana, nitakula badae wewe nenda kalale tu...ila kabla hujaenda kulala Kuna jambo nataka nikuulize"

Annie: "Jambo gani?"

BM: "Kuhusu kazi uliyoniambia umepata, ni kazi gani?"

Annie: "Kazi ya Bank [emoji542]"

BM: "Ooh! Bank gani?"

Annie: "Bank flani ya Wahindi inaitwa I&M Bank"

BM: "Hii Kazi Annie umeipataje?"

Annie: "My Uncle ndio ameni connect ila yeye ananyia hapa Dar"

BM: "Ni sawa, unaweza kwenda hiyo kazi, ila utafanya kwa Mwaka mmoja tu"

Annie: "Usijali Mimi nimesha change mind siendi tena"

BM: "Kwanini!?"

Annie: "Si ulikataa wewe, kilichokufanya ukubali Sasa hivi ni nini?"

BM: "Kuna mambo mengi nimewaza nikahisi kama nilifanya maamuzi ubinafsi, unajua maisha yako pia inabidi yaendelee"

Annie: "Kweli nataka kwenda kufanya hiyo Kazi lakini nafsi yangu ghafla imekuwa nzito sijui kwanini"

BM: "Ni kawaida hiyo, we fanya maandalizi ya Kila kitu kwaajili ya safari"

Kwa mara ya kwanza kufuata ushauri wa mshkaji, maana jamaa nae miyeyusho kinoma, basi Annie akaenda zake kulala Mimi nikazuga na picha moja la Thriller ilivyoisha nikaunga tela kulala

Siku zikakatika Safari ya Annie ikakaribia hapo mm nimebakiza wiki moja tu likizo yangu kuisha, sasa ndio nikawa namlazimisha Annie kusafiri, Nakumbuka nilimkatia Ticket ya ndege nikampatia na milioni 3, nilivyompa hiyo Pesa Account yangu Balance ikasoma 4.1 m

But nilimpatia kiasi kile Cha pesa kwasababu sikutaka mshahara wake auingize kwenye kulipa Kodi ya nyumba,

Siku ya safari ikafika nikamsindikiza hadi Airport mtoto asianze kutoa machozi? nikamu hug hug kidogo nikahisi kama tuko Telemundo, mwisho wa picha Annie aliingia kwenye Air Precious

Plan A[emoji3514]

Nilivyotoka Airport straight nikaunga Kino kwa Mshkaji, unajua sikumwambia kama nimefata vile alivyonishauri, Mshkaji alinambia yupo maghetton nikamtimbia,

Nilivyofika Maghetton kwa mshkaji nikamuelezea kila kitu, nikamuambia yani hapa unavyoniona nimetoka Airport kumsindikiza Annie kaenda Mwanza, jamaa kama hakuamini akawa anaitikia Ile design ya mtu kumsapoti kile anachoongea

Alikuja kuamini Annie alivyonipigia simu kunijulisha kwamba amefika, Mshkaji ndio akaamini kumbe mchongo ni serious

Mshkaji: "Mimi nikajua unatania kumbe Demu ameng'oa kweli, Sasa hapa unaweza kufanya mambo yako fresh mwanangu"

BM: "Ila haya maamuzi nimefanya kwa kukurupuka sana, sikupata muda wa kutafakari vizuri"

Mshkaji: "Muda wa kutafakari ulishapita, Sasa hivi Cha kufanya mcheki Demu wako ****(Accountant) Anza kumsogeza taratibu hiyo ndio kazi iliyobaki"

Kwahiyo Plan B ilikuwa ni kumsogeza Accountant karibu, yani nianze kujibebisha kwake mbaya zaidi sikuwahi kumtafuta tangu nimeondoka pale ofisini na Cha ajabu yeye pia hajawahi hata kunibeep kitu ambacho sio kawaida yake

Basi Mshkaji akanipanga mambo ya kufanya, design sasa ikawa kama namsikiliza yeye kwa kila kitu,

Siku isiyokuwa na Jina nimeamka na mood Nzuri si nikampigia simu Accountant, hapo zimebaki siku 5 tu nirudi job ila kabla ya kurudi inabidi niwe nimefanya maamuzi ya kumkubali Accountant kimapenzi ili niendelee na Kazi (nimkatae Annie) au niache kazi nimkatae Accountant nibaki na Annie

BM: [emoji338]"Mambo"

Accountant: "Finally...hii simu nilikuwa naisubiria kwa hamu"

BM: "Ooh! uko wapi?"

Accountant: "Kazini"

BM: "Tunaweza kuonana Leo baada ya masaa ya kazi?"

Accountant: "Wewe tu"

BM: "Sawa basi nitakujulisha Mahali tutakapokutana"

Masaa nayo kwani yanakawia basi, jioni ndio hiyo Accountant nilishamtumia Location, tukakutana tena Mimi ndio nilimkuta yeye tukaagizia vinywaji story zikaanza, Wakati nampigisha story zingine nikawa nawaza jinsi ya kuingizia agenda yangu

BM: "Ivi ni Jumanne ndio likizo yangu inaisha eeh?"

Accountant: "Yeah, kwani unakuja kazini?"

BM: "Sasa kwanini nisije, si likizo imeisha"

Accountant akaniangalia kwa sekunde kadhaa Nikamuuliza "vipi kuna tatizo?"

Accountant: "Kuna Kitu una maanisha ila hutaki kufunguka, kama unakuja kazini ina maana umekubaliana na mimi yale matakwa yangu, right?"

BM: "Hayo mambo Tutaongea vizuri siku nyingine wala usijali"

Accountant: "Sasa hapa umeniitia Nini? umekuja kunipotezea muda wangu tu"

BM: "Okay! Relax, sasa hivi nimeamua kutulia na wewe lakini huku kupanic kwako ni moja ya sababu iliyonifanya nichelewe kufanya haya maamuzi"

Accountant: "Vipi kuhusu kidemu chako?"

BM: "Huyo nishaachana nae, ni Bora hata hili limetokea mapema maana nilikuwa tayari kuacha Kazi kwaajili yake"

Accountant: "Ooh, now I got your point, so mimi nipo hapa kama Option"

BM: "Hilo sasa umelisema wewe, ninachojua tu Mimi kwasasa nimefanya maamuzi sahihi katika Wakati sahihi"

Accountant: "But you guys mlikuwa mnapendana sana kiasi kwamba nilijua hamtoachana"

BM: "You know Love can be really without being forever"

Accountant: "Bado ni ngumu kuamini, there something fish"

Nilivyomtamkia Accountant kwamba nataka kuwa nae alifurahi sana lakini Bado hakuamini kama ni kweli nimeachana na Annie ila nikaendelea kumpiga kiswahili hadi akanielewa

Nikaachana na Accountant pale kila mtu akielekea njia yake Wakati tunaagana eti akataka kuja kulala kwangu ili a confirm kama ni kweli Annie nimeachana nae, nikamkataa kiaina bila ya kumkwaza maana Sasa hivi ni mwendo wa kula na kipofu

Weekdays zikapita, Weekend ikaanza nakumbuka siku ya jumapili mapema sana Sister Michelle akanicheki akaniomba niende home kuonana nae after church,

Ilivyofika saa Saba Mimi ndio huyo mdogo mdogo hadi kwa Mzee, nilivyofika Kona ya mwisho ya kuelekea nyumbani kwa Mzee kwa mbali naliona Jeep, nikajua tu huyu atakuwa ni Caryn bila shaka na kweli alivyonikaribia akasimamisha Gari

Caryn: "Hata kama ni ubahili hapana aise, BM umekosa hata elfu 2 ya pikipiki kweli?"

BM: "Nipatie hiyo elfu 2 nirudi highway nikapande hiyo bodaboda"

Caryn: "Nyumbani unaenda kufanya nini Sasa watu wenyewe hawapo, aliyekuwa amebaki ndio huyu anaishia"

Sasa Michelle Atakuwa na Akili gani ya kuniita halafu tena atoke, nikajisemea tu mwenyewe moyoni, Basi Caryn akanilazimisha niingie kwenye Gari, sisi hao breki Sinza Dukani kwake

Caryn: "BM Ivi ni maeneo gani mazuri ya kununua viwanja?"

BM: "Maeneo ninayoyajua Mimi kwasasa ambayo ni potential ni Kigamboni na Bagamoyo"

Caryn: "Bagamoyo hapana, nataka eneo ambalo naweza kufanya makazi"

BM: "Basi Kigamboni pata kufaa, hata Mimi nataka kuhamia huko"

Caryn: "Umeshajenga Kigamboni?"

BM: "Nahamia kwenye vi appointment tu, pesa ya kujenga natoa wapi Mimi sasa hivi"

Caryn: "If I were you ningekuwa nishajenga, kazi unayofanya ina pesa sana the problem is, you don't know where to stand"

BM: "Ila Caryn bhana huwa unanifurahishaga sometimes, sasa mimi na wewe Kuna tofauti gani au ni nani anastaili kumcheka mwenzake?"

Caryn: "Mimi kama sio Biashara ningekuwa nishajenga, nilitaka kwanza Biashara yangu ikomae vizuri"

Majibu mdomoni yakaniisha, najibu nini tena hapo, ghafla nikawa mnyonge, moyoni nikasema hii chance safari hii sitaki kuichezea, yani hadi Caryn kajua ninapopiga kazi kuna hela na hadi sasa hivi sijafanya jambo la maana

Nikapata wazo la kumshirikisha Caryn kwenye kipengele nilichonacho kazini nione kama anaweza nishauri jambo ingawa tayari nishampanga Accountant akapangika, nimepata ujasiri na kuhisi ni salama kumshirikisha Caryn kwasababu nae naona ananishirikisha kwenye baadhi ya mambo yake


Nilichokifanya Sasa nikamuelezea Caryn mkanda mzima, jinsi nilivyopata kazi kupitia huyo mwanamke na kuniwekea kizingiti Cha kutokurudi kazini hadi nimkubalie, kifupi nilimueleza Kila kitu kasoro upande wa Annie Ndio sijamueleza chochote, Baada ya kusikiliza maelezo kwa makini Caryn alianza kwa kuniuliza tena swali ambalo kwenye maelezo lilishajijibu

Caryn: "Do you love her"

BM: "I don't love her"

Caryn: "So you have no feelings for her and you've been sleeping with her!?"

BM: "We've been sleeping together for fun, there's no attachments it's called friends with benefits"

Caryn: "Well she got attached while you were playing your game of friends with benefit she fell in love with you

BM: "That girl is not close to what I want in a wife, not mentally, not educationally, not psychological"

Caryn:"So what do you want?"

BM: "Your advice"

Caryn: "Quit"

BM: "Una maanisha niache kazi?"

Caryn: "We fanya kama nilivyokuambia"

Huu Ushauri umekuja too late wakati ambao nimeshafanya maamuzi, sasa kulikuwa na haja gani ya kumruhusu Annie kwenda Mwanza mbaya zaidi nishajishusha kwa Accountant na mambo yalikuwa yashanyooka,

Wakati naendelea kuongea na Caryn, Michelle akapiga simu, Sasa vile simu ilivyokuwa nikaiangalia halafu nikamuangalia na Caryn, Caryn akahisi kitu akaniuliza "ni nani?" nikamjibu ni Michelle anapiga, akanambia "Achana nae utaongea nae badae"

BM: "Labda Kuna emergency anataka usaidizi"

Caryn: "Usaidizi gani bhana mtu nimemuacha yupo nyumbani"

BM: "Dah! we si umeniambia ametoka wewe, au sio wewe?"

Caryn: "Sasa ulitaka kwenda kushinda nae nyumbani mkifanya nini?"

BM: "Alinipigia simu bhana alitaka mazungumzo na Mimi huwezi jua alitaka kunambia nini"

Caryn: "Mimi namjua Michelle vizuri kinachomsumbua sasa hivi ni Mapenzi hana anachowaza pale mwenzako zaidi ya hicho"

BM: "We umejuaje? usipende kumuongelea mtu pengine mwenzako ana mambo yake mengine"

Caryn: "Unajua wewe umetujua juzi tu hapa, Mimi yule sio Dada yangu tu, we used to be very close, we used to be friends, so nikikuambia kitu kuhusu yeye Jua Nina uhakika nacho

BM: "Sasa kwanini Sasa hivi hamna ukaribu huo tena?"

Caryn: "Alinikosea, Alinikosea sana Yani pakubwa mno"

BM: "Alikukosea nini?"

Caryn: "Kama nilivyokuambia Mimi yule sio Dada yangu tu Bali alikuwa rafiki yangu pia, na unaijua sifa ya urafiki? So siwezi kukuambia alichonifanyia ila we Jua tu alinikosea"

BM: "Ila yeye kanambia, kanielezea kila kitu

Caryn: "Sasa yeye ni sawa kufanya hivyo kwasababu yeye ndio mkosani ila nikianza mimi kuongea kwa kila mtu atajisikia vibaya"

BM: "Lakini wewe si ulimsema kwa Mzee"

Caryn: "Lini? na saa ngapi?"

BM: "Kuna siku ulimsema bhana tena nikiwepo hiyo sijahadithiwa Wala nini, ulimsema kuhusu huyo Mwanaume wake mbele ya Mzee

Caryn: "Sasa vile ndio kumsema? vile si ni vitu vya kawaida tu, je ningeamua kusema vyote? and I'm sure hata wewe hajakuambia mambo yote"

BM: "Sioni Ubaya wa Sister Michelle ni kuteleza tu ameteleza, unajua sister ako yuko humble sana hana mambo mengi na ni muelewa"

Caryn: "Eti eeh! Okay"

Ilivyofika jioni nikamuacha Caryn Dukani kwake Mimi nikaenda kwa sister Yombo nikapiga na msosi huko huko nikarudi zangu Tabata

Kesho yake Jumatatu nakumbuka ilikuwa Nanenane hii siku sikutoka kabisa ndani ila mida ya jioni akaja Mshkaji wangu wa Kinondoni, alikuwa katika mishe mishe zake huku huku Tabata alivyomaliza akapitia mjengoni, akanikuta nabrash viatu

Mshkaji: "Nakubali mwanangu, kesho kazini sio"

BM: "Kama kawaida"

Mshkaji: "Nakubali, angalau siku hizi ushauri wangu unauzingatia....hujapika Mzee nina njaa kiseng*"

BM: "Mm huwa sipikagi, kwani hoteli zimefungwa huko ulipotoka?"

Mshkaji: "Hapo ndipo unapofeli"

Hii siku mshkaji aliangusha kwangu, mida mida tulienda kufinya msosi tukarudi mjengoni tukalala, ila sasa jamaa akagoma kulala chumbani akaenda kulala Sebuleni kwenye kochi

Tarehe 9 mwezi wa 8 (Jumanne) siku ya kuripoti kazini mapema tu nikajiandaa nikamuamsha na mshkaji sababu alitaka tutoke wote

Wakati nipo njiani nimeshaachana na mshkaji naelekea kazini kichwani nawaza kipi Cha kufanya na kipi Cha kuacha, kichwani wananijia watu wawili Caryn na mshkaji wangu, Caryn kanambia niache kazi huku Mshkaji kanambia niendelee na Kazi, Hadi nafika Ofisini Bado nipo njia panda

Nikasalimiana na staff wenzangu Accountant muda huo alikuwa hayupo nimeambiwa kaenda Bank ila Mama yake yani Bosi yupo Ofisini kwake, Mnyamwezi nikachoma ndani

Mama Accnt: "Karibu mwanang, Hujambo?"

BM: "Sijambo Mama Shikamoo"

Mama Accnt: "Marhaba mwanangu tulikumiss sana na umekuja Wakati muafaka huyu mwenzako uliyemuachia majukumu anaelemewa na Kazi?"

BM: "Bado haja Master tu? sababu akikwama huwa ananipigia simu namuelekeza"

Mama Accnt: "Tatizo ni kwamba mwenzako hajui kuongea na TRA kabisa, na hajui kubagain, kabla sijakuachia majukumu yangu itabidi uendelee kwenda nae trips kadhaa hadi atakapokuwa sawa"

BM: "Ni sawa, lakini Mama unajua Mimi nimekuja kukuaga, nimeona nikafanye majukumu mengine kwahiyo nilikuwa naomba ruksa yako"

Mama huwa anavaa miwani, kusikia hivyo akavua kwanza na mawani yenyewe, kuna vitu alikuwa anaandika akaacha akaweka peni chini yani ni kama vile hakutarajia kusikia nilichomuambia

Itaendelea
 
Caryn anakupoteza.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…