Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Tokea nimenza harakati za utafutaji sijawahi kukanyaga kwa mganga na maisha yangu sio mabaya sana, sitarajii kuwepo siku nitaenda kwa mganga kwa sasa nipo njiani kuulekea utajiri, japo utajiri una mapana na marefu yake ila tujuwe tu upo uwezekano wa kuwa tajiri bila nguvu za giza.
Uwezekano wa kuwa na maisha mazuri au tajiri kwa kupitia kwa waganga ni sawa na ngamia kupenya kwenye tundu la sindano.
 
Acha upumbavu,wewe una mambo mengi ya kufanya na upo hapa?.

Huu upumbavu mtaacha lini?

Aliyekwambia hili ni jukwaa linahusu stori za briefly ni nani?
We jamaa mbona unawaka sana utafikiri hii stori ni yako! Mwandishi mwanzo alianza vizuri na sasa analazimisha stori iwe ndefu kwa kuweka mambo yasiyo ya msingi kisha hutaki watu waseme?

Kuona kwamba wengine ni wapumbavu na hawana akili haikufanyi wewe kuwa na akili...mwandishi anapoanza kuleta maelezo ya ovyo itaondoa hata ule uhalisia alioanza nao Kisha stori nzima itaonekana ya kutunga tu.
 
Acha upumbavu,wewe una mambo mengi ya kufanya na upo hapa?.

Huu upumbavu mtaacha lini?

Aliyekwambia hili ni jukwaa linahusu stori za briefly ni nani?

Nyie ndio wale watu mnaoshinda kutwa mitandaoni kitafuta habari za umbea hamna kazi za kufanya sisi wengine tunakuaga na time limit za kuperuzi hatutaki story za Itaendelea
 
Huwa nasema kila siku ya kwamba,baadhi ya watanzania wana matatizo ya utindio wa ubongo lakini sieleweki,yaani mtu kavurugwa na maisha huko anataka hasira zake aje azimalizie kwenye nyuzi za watu hapa Jamii forum,Kwanini hambadiliki?

Kila stori zinapoletwa hapa Jamii forum ziwe za maisha ya kweli au zile za kutunga basi lazima hao watanzania baadhi niliowataja hapo juu wataanza vituko,iwe kupinga,iwe kukatisha tamaa,iwe kukejeli,iwe matusi n.k,huu ni utindio wa ubongo kwasababu hakuna mtu aliye na akili timamu akawa kila uzi ni kupingapinga tu na kukejeli bila sababu za msingi.
Hebu badilikeni,acheni haya mambo ya kipumbavu.

Kama unaona ni chai na wewe nenda kachemshe yako ukanywe na familia yako!.

Kama unaona stori inawekwa mambo mengine yasiyokuwa na ulazima nenda kaanzishe ya kwako na ukaweke mambo ya msingi ili wanaopenda mambo ya msingi waje wasome.

Mleta mada kaamua kuweka kila kitu ili kupunguza maswali ya baadhi ya watu ambao huwa wanapenda maswali yasiyokuwa ya msingi,lakini bado pamoja na hilo kuna wajinga hawataki!.

Bado mtu anatumia muda wake mwingi kuandika stori yake akiwa na maana watu wajifunze lakini baadhi ya wapumbavu wanakejeli na kukatisha tamaa!

HIVI NYIE WAPUMBAVU MTABADILIKA LINI?,MBONA MENGI YENU NI MAJITU MAZIMA LAKINI AKILI MNAZIDIWA NA KUKU?

HAMTAKI KUSOMA PITENI KUSHOTO LAKINI SIYO KUMPANGIA MWANDISHI NINI AANDIKE NA NINI AKIACHE!.

BADILIKENI WAPUMBAVU NYIE!

#USIPOBADILIKATUTAKUBADILISHA
Unajua kuandika kwa herufi kubwa ni upumbavu wa kiwango cha SGR!!??
 
Ilipoishiaa[emoji1484]

Imefika Lunch time najiandaa kwenda kupiga Menu yule Mzee nikamuona anaingia Ofisini halafu ana hasiri amekunja sura, nikajisemea hapa kimeshanuka nikaanza ku recall matukio ili nijue ni wapi nimekosea hasa kule nyumbani kwake, kote nilicheza safe na mara ya mwisho kuongea na huyu Mzee ilikuwa ni Ile Jumamosi akinipa mabadiliko ya ratiba yake huku akinipatia option mbili za yeye kupata gari yake, na Mimi nilivyochagua kubaki na Gari hadi Jumatatu sikumpigia tena simu kumjulisha uamuzi niliouchukua....nikapata majibu kwamba inawezekana hapo ndipo nilipo haribu, alikuja kwenye desk langu na kuniambia "nipatie funguo ya Gari na ukimaliza kazi nitafute" hata hakunisalimia akatoka nje ya ofisi akaondoka....

Muendelezo [emoji1484]

Ilivyofika saa tisa alasiri nikawa nishafunga makashabrasha yangu, nikamcheki Mzee, akanambia nimkute hoteli flani, kweli nilivyofika kwenye Ile hoteli nikakuta ile Alphard imepark kwa nje nikampigia simu, akanielekeza nikachoma ndani nikamkuta Mahali amekaa anakunywa Cappuccino, akamuita muhudumu akanambia niagize mm nikaitisha Passion Juice, Mzee akaanza kwa kuniuliza maswali "Nyumbani unaishi nani?" Nikamwambia peke yangu Mzee "Nakumbuka uliwahi kunambia kwamba Wazazi wako pia wanaishi hapa mjini, Ukiachana na Wazazi wako una ndugu wengine wanaishi hapa Dar?" nikamjibu ndio wapo wengi tu

"Okay! unajua ni vigumu kuyafanya maisha magumu kuwa rahisi lakini ni rahisi kuyafanya maisha rahisi kuwa magumu, ww upo tofauti na vijana wengi wenye umri kama wa kwako, nakuambia haya kwasababu Mimi vijana nawajua vizuri na wafanyakazi wangu wengi ni vijana, inawezekana wewe unalijua hili lakini vijana wengi hawajui kwamba ikitokea mtu amekuamini kwa haraka ujue kashaandaa mazingira flani ya kupambana na matokeo hasi, Ile siku Wakati nakuacha nyumbani kwangu Ile nyumba ilikuwa na Pesa nyingi sana, baadhi ya pesa zilikuwa sehemu ya wazi kabisa ila kwa haraka niliyokuwa nayo nilisahau hata kuzihifadhi mahala sahihi, kabla ya kukupigia simu wewe na kukupa maagizo ya kuingia chumbani kwangu nikakumbuka kwamba sijaweka mazingira sawa hivyo nilimpigia mmoja wa vijana wangu ninaowatumia katika kazi zangu za mjini nikampa maagizo aje maeneo ya nyumbani kwangu alivyofika ndio nikakupigia wewe, kwahiyo maeneo yote uliyokuwa unazunguka na gari Mimi taarifa nilikuwa nazipata huku nikihakiki kwenye system, Kitu nilichokipenda kutoka kwako ni kwamba ulifocus na maelekezo niliyokupa kuanzia nyumbani kwangu yani hukutaka kugusa hata heleni ya mke wangu, unajua unaweza ukawa sio mdokozi lakini kama ungeanza kugusa hiki mara kile tayari ningeanza kukutilia shaka, kila mtu ana tamaa lakini wachache wanaweza kujicontrol, Ukiachana na tamaa kingine nilichokipenda kutoka kwako ni sio mtu wa kurahisisha mambo, Nilipokupa kazi ya kugawa chakula kwa wenye uhitaji ulifanya kwa moyo wote kama vile nakulipa pasipo usimamizi angekuwa mtu mwingine angerahisisha hata kwa kugawa kwa watu anaowajua yeye"

Sawa Mzee Nimekuelewa lakini kama sijakuelewa pia, Yani maelezo yote haya yanamaanisha kwamba hukuniamini? "Hapana kijana wangu nilikuamini sana na umezidi kuweka mizizi ya kuendelea kukuamini, Nilichokuwa nakifanya nikujitengenezea mazingira ya kutojilaumu badae kwa chochote ambacho kingetokea kwasababu sisi ni Binadamu tuna madhaifu lolote linaweza kufanyika, unajua hata Ugonjwa unapoanza ni rahisi kuutibu lakini si rahisi kuugundua. Lakini kadri unavyokua, inakuwa ni rahisi kuugundua lakini ni vigumu kuutibu." Kiukweli nilikuwa nishaingiza baridi sikutegemea maneno haya kutoka kwa Mzee kwa vile nilivyomuona Ofisini nilijua kuna mahali nimeharibu,

Kumbe saa Ile Mzee anaingia Ofisini Dakika kama mbili nyuma Mzee alitoka kupokea simu iliyomkasirisha sana, na hakuwa comfortable kunielezea ni nini kimetokea, alinambia tu "Leo nilikuwa najua kabisa siku yangu inaenda kuisha vibaya, acha niende nyumbani kupumzika ni refresh akili nijue nakabiliana vipi na hili jambo, Kila Kitu kikiwa sawa nitakutafuta tuongee mengi zaidi ikiwemo Biashara lakini kuna mtihani hadi ufanye na ufaulu ndio nitakuonesha ulimwengu wa kibiashara wenye mafanikio, kwasababu sio wote Wanaofanya Biashara wanafanikiwa, wengi wanafeli na wanafelishwa na mambo ambayo pengine wanayajua ila wanayapuuza, kila mafanikio yanajumuisha maelfu ya vitendo vya ujasiri"

Nikajisemea moyoni haya ndio mambo niliyokuwa nayataka ila sasa huu mtihani ni mtihani gani tena, Mzee kakaa ki CIA CIA nitatoboa kweli huo mtihani?

Hayo ni mambo niliyokuwa najiuliza kichwani Wakati Mzee ana clear bill pale hotelini, tukaagana mzee alinichukulia moja ya tax zilizokuwa zimepark nje ya Ile hoteli, yeye akaingia ndani ya Alphard akaondoka na Mimi nikashika njia ya kuelekea Tabata

Sasa huo mtihani ndio umesababisha kuanzisha huu Uzi, naona episode zinaenda kuwa 3 badala ya 2 kama nilivyopanga mwanzo hii nikutokana na pressure za baadhi ya memba humu imenibidi niipost hivyo hivyo bila kuikamilisha yote

Muendelezo soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
Ohoooooooo
 
We jamaa mbona unawaka sana utafikiri hii stori ni yako! Mwandishi mwanzo alianza vizuri na sasa analazimisha stori iwe ndefu kwa kuweka mambo yasiyo ya msingi kisha hutaki watu waseme? Kuona kwamba wengine ni wapumbavu na hawana akili haikufanyi wewe kuwa na akili...mwandishi anapoanza kuleta maelezo ya ovyo itaondoa hata ule uhalisia alioanza nao Kisha stori nzima itaonekana ya kutunga tu.
......ya hovyo wapi?,acha ujuaji.

Ina maana anachosimulia mwandishi ni mambo ya hovyo?,kwanini usipite kimya kimya kama umeona kuna mambo ya hovyo?

Hivi huu ujinga mtaacha lini?
 
Nyie ndio wale watu mnaoshinda kutwa mitandaoni kitafuta habari za umbea hamna kazi za kufanya sisi wengine tunakuaga na time limit za kuperuzi hatutaki story za Itaendelea
Huu ndiyo upumbavu umeandika hapa na wewe unaona umeandika point?,hutaki habari za itaendelea unajua kuandika kunavyochosha? kama wewe hushindi mitandaoni kwahiyo unataka mwandishi ashinde mitandaoni ashindwe kufanya shughuli zake akuandikie tu wewe ucheke na kukenua meno yako hayo yaliyopandiana kama mahindi mabovu!


Badilika, acha upumbavu
 
Asante kw mwendelezo mkuu si bado tumeunga folen hapa fanya uje umalizie
 
'
1657230384-picsay.jpg
 
Back
Top Bottom