Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sijaruka kipande lakini sidhani kama nimemgonga[emoji848] acha tuone episodes zijazo
Watu mna mbinu za kijasusi kabisa,....Huyo caryn usimtongoze fanya hivi, mwekee mitego sana usimchukulie kama dada yako mwangalie kwa staili kali za kumtamani mtongoze kwa macho jifanye kama unaangalia sana mwili wake mpaka akushtukie lakini usimtongoze , hiyo ni mbinu ya kivita ya kumshusha confidence , alafu potezea usimwambie chochote , mwanamke ni mwanamke tu
Niko paleee nakusikiliza.Ilipoishia
Mzee: "Kabla sijafanya uamuzi, nataka kujua sababu zilizokufanya BM uache kazi"
Ghafla nilihisi joto wakati ndani full AC watu wote kimya mimi ndio natakiwa kuongea kwa wakati huo halafu Caryn akanipiga jicho flani hivi akakunja na mikono kifuani yani Ile kwamba "TUNAKUSIKILIZA"
Inaendelea
SEASON 2, Episode 2
Turudi nyuma kidogo tulipoishia
Ile siku Caryn alivyoniacha pale hotelini sikuchukua muda na Mimi nikasepa, zilipita kama siku mbili hivi sijawasiliana na Caryn, akaja kunipigia siku kama ya 3 ivi
Caryn: [emoji338]"Hey"
BM: "Mambo"
Caryn: "Poa, vip mbona kimya! umefikia wapi?"
BM: "Bado sijapata nyumba, nipo kwenye michakato"
Caryn: "So wale watoto wanaishi wapi kwasasa?"
BM: "Si wanaishi walipokuwa wanaishi"
Caryn: "Naona unaenda kufeli hili zoezi kabla hata jlhujalianza"
BM: "Kwanini? ni kama unataka nifeli sio?"
Caryn: "Hapana, ila kwa akili ya kawaida tu unadhani wale watoto wakiondoka kule unakowakutaga utawapata wapi tena? coz ulisema pale sio makazi yao permanent"
BM: "Dah! halafu kweli nilikuwa sijawaza upande huo kabisa"
Caryn: "Just act fast, you're wasting too much time" [emoji3513]
Caryn sometimes ni mzinguaji ila leo ameongea kitu Cha maana ambacho hata sikukifikiria, nikaona hapa nikisema niendelee kusubiri nyumba nikipata ndio nikawachukue wale madogo naweza nikafeli, Nikapata wazo, nikamvutia waya sister angu flani anaishi Yombo, nikampanga kwenye simu lakini hakupangika ikabidi jioni niende kwakwe nikamuelezea kwa kina zaidi, Lengo ni kutaka aishi na wale madogo kwa muda huku nikiendelea kutafuta nyumba ili nisije kupotezana nao
Kwa bahati nzuri sister akaelewa japo kishingo upande, maana anajua angenikatalia na mimi ningemfungia vioo kwenye mambo yake, na Mimi sikupoteza muda kesho yake tu nikaibuka Buguruni kuwacheki madogo, nikaenda hadi pale maskani yao lakini sikuwakuta nikazunguka mitaa yote karibu na lile eneo lakini hola, ikafika hadi mchana narudi yale maeneo bado sikukuta mtu, nikampigia sister kumuuliza kama ameshaandaa kila kitu maana Jana nilimuambia chakula Cha mchana aongeze kipimo kidogo atuhesabie na sisi chakula, nikamuambia kwamba huku madogo sijafanikiwa kuwaona
Ikabidi nitafute mahali nipate msosi, nimemaliza kula saa hiyo ni saa tisa kasoro na tangu asubuhi nipo Buguruni, ilivyofika saa 15:00 ikabidi niende Kinondoni Mkwajuni kwa mshkaji wangu flani maana tulipanga kuonana siku kadhaa sema ratiba zinavurugika kila tukipanga
Nikaibuka Kinondoni tukaenda kuchill Kitambaa Cheupe jamaa popote atakapokuwa utamkosa na vyote lakini sio laptop, ni wale wenzetu wa kufanya deal za Online, ila huyu mshkaji wangu yupo karibia kila sehemu kuanzia Forex, Cryptocurrency, ni freelancer pia hadi kubeti ana beti, na mchizi anaishi fresh mjini, anapokea kodi ya nyumba huko maeneo ya Goba lakini yeye kaamua kupanga Kino
Mshkaji anajua mambo mengi kuhusu mimi na mm Najua ya kwake Yani ni best friend, Nakumbuka hii siku nilivyoenda mchizi analikuwa ananishauri kutokuacha kazi, maana nilimuelezea situation niliyokuwa nayo
Mshkaji: "BM Unajua njia uliyochagua wewe kutafuta pesa inataka uwe na mahusiano mazuri na watu, so inabidi ucheze na akili zao ili uweze ku win"
BM: "Unamaanisha nini?"
Mshkaji: "Si namaanisha hicho nilichokiongea, Yani kama Mimi ningekuwa ni wewe kazi nisingeacha na kumgonga ningekuwa na mgonga kama kawa (Accountant) kwani wewe unachubuka wapi ukimgonga yule Demu?"
Huyu jamaa kwanza ni mtu wa mademu sana ndio maana sijashangaa hiki anachonishauri
BM: "Nikifanya kama unavyoniambia ndio nitazidi kumpa matumaini kitu ambacho mimi sitaki kukifanya"
Mshkaji: "Unajua the fight is against poverty, ukiendekeza sana Mapenzi Utaumia, mpe anachokitaka ili na wewe upate unachokitaka, huko mbeleni mambo yakinyooka ndio una nafasi ya kuchagua nani awe nani"
BM: "Kwa tafsiri nyingine hapa una maanisha nimuache Shemeji yako Annie sio?"
Mshkaji: "Hapana! Mimi sijasema hivyo ila huyo ambaye upo tayari kuacha Kazi ili tu uwe nae nina uhakika mambo kama yatakuendea hovyo atakuja kukuacha wewe"
BM: "Inawezekana lakini sio kwa yule mtoto"
Nilivyomuambia hivyo jamaa akacheka sana huku akitingisha kichwa left-right, nikaona huyu acha nimuage pengine zishaanza kumuingia, nikarudi zangu nyumbani, Sasa Wakati wa kurudi nipo kwenye daladala si tukapita Buguruni nikatamani nishuke nikacheki wale madogo lakini nafsi ikasita kwamba pengine nitapoteza tu muda kama nilivyopoteza mchana
Nimefika mjengoni nawaza kumpigia Caryn nimjulishe kwamba madogo sijawaona, nikaona huyu hata nikimjulisha hata nisaidia chochote zaidi ya kunisema, nikapiga zangu usingizi kesho yake nikatinga tena Buguruni, raundi hii nimeenda Asubuhi sana kama saa 2 na Dakika zake lakini nikakuta bila bila tena
Sasa yale maneno alioongea Caryn ni kama yanatimia ivi, nikarudi zangu home, unajua kipindi hiko sina ratiba maalum nipo nipo tu, siunajua tena ukipatiwa likizo ambayo hata hukuiwazia wala kuipanga unatamani kusafiri lakini huwezi juu ukisafiri kuna mambo yatasimama
Ilivyofika mida ya jioni nikarudi Mungu sio Mandonga nikamkuta yule Dogo wa kiume na mdogo wake wa kike Kaka yao alikuwa hayupo, Nikamuuliza yule Dogo janja Asubuhi mlikuwa wapi, na Jana pia nilikuja lakini sikuwakuta, Akanambia kama hawapo pamoja na kaka yao basi huwa wanakwenda kushinda na watoto wenzao huko mitaani,
Dogo akanielekeza Kaka yake anapopatikana kwa muda huo ambapo ni Ilala kuna mtaa unaitwa Ya Mungu Mengi
Ipo hivi, kumbe Kaka mtu asipopata kibarua Cha kumuingizia pesa basi humlazimu kwenda kuomba kazi kwenye migahawa ya kusafisha vyombo na malipo yake huwa ni Chakula
Basi nikaenda hadi kwa huo mtaa mgahawa kwa mgahawa sikufanikiwa kumuona nikarudi kule kwa madogo tukachoma sana mahindi tukimsubiria kaka yao hadi giza linakaribia kuingia ndio Kaka mtu anafika
Kaka mtu alikuja na kifuko ambacho alibebea msosi, Sasa muda wote nipo pale kumbe madogo walikuwa wamepiga pasi ndefu yani mchana hawajauona, kikatolewa kitu Cha wali pale kilikuwa kimefungwa kwenye foil, nikaacha wamalize kula baada ya kushiba nikawaambia Leo mnahama makazi hii sio sehemu sahihi ya kuishi
Nikawaelekeza Kila Kitu madogo wakaelewa, nikampigia simu sister kumjulisha kuwa madogo nimewapata, sisi hao tukafunga safari hadi Yombo tukafika kwenye saa mbili kasoro usiku
Sister katika harakati za kuandaa chakula kama mnavyojua familia zetu za hali ya chini kwenda na mahesabu ni lazima, sister akaniuliza kama nitakula ili anihesabu nikamjibu "hapana, hata hivyo nawaacha muda si mrefu, pia sidhani kama hawa wenzenu watakula" kusema hivyo yule dogo wa kiume akadakia "watuhesabu tu na sisi kaka"
Nilidhania wako sawa, basi sio kesi sister utawahesabu, Mimi sikupoteza muda nikahepa zangu japokuwa sister alisisitiza kesho niende kwaajili ya kumpeleka yule Dogo wa kike hospital maana afya yake ilikuwa hairidhishi,
Kweli kesho yake mapema tu nipo Yombo, nikamchukua Dogo nikampeleka hospital akakutwa na mataifodi malaria [emoji3082] nikaandikiwa dawa nikamrudisha nyumbani, tukashinda wote pale kwa sister mida ya jioni nikarudi zangu kwangu
Jumapili kama kawaida ni siku ya kwenye kwa Mzee ila kwa kipindi hiki ambacho amesafiri huwa naenda hata mara mbili kwa wiki, sasa hivi nikiwa nimeshazoeana na Caryn kidogo nikampigia simu kumuuliza kama yupo home akanambia kuwa ametoka ila anarudi muda sio mrefu nyumbani yupo Mama na Michelle
Nikaenda kweli nikamkuta Michelle na Mama yake, nilichogundua ni kwamba Michelle na Mama yake wanapatana sana halafu Caryn yeye kwa Mzee ndio humuambii kitu, hata kwenda Kazini Bi mkubwa anaongozana na Caryn kwasababu ya heshima ya Mzee tu ila kipenzi Cha Bi Mkubwa ni Michelle
Niliwakuta wanapiga story kama mtu na rafiki yake, nikawajoin japokuwa sikuwazoea kivile kama ilivyo kwa Mzee mwenyewe au Caryn japo kwa uchache.
Ilivyofika mida flani hivi ya jioni Caryn akafika kama kawaida yake yupo na Jeep Wrangler ya 2020 Diesel Engine akalipark, akatukuta mimi na Michelle tunapiga story Mama alituacha na kwenda kusaidiana na Dada wakazi jikoni
Caryn: "BM nilijua sitokukuta"
BM: "Hata hivyo ndio nataka kuondoka muda sio mrefu"
Michelle: "Leo itabidi ulale BM, Kila siku unakuja tu na kuondoka"
BM: "Dada Michelle nitalala siku nyingine wala usijali"
Basi nikamuaga Bi Mkubwa, Michelle akanisindikiza hadi nje getini nikaondoka
Zikapita kama wiki 2 ivi Caryn akanitafuta ilikuwa weekend akaniomba tukutane Morocco mida ya mchana, mimi ndio niliwahi kufika akanipitia, tulivyokuwa Morocco akapinda na ile njia ya kuelekea Kawe mbele tukaingia Barabara ya Masaki
Tulienda hadi kwenye Apartments flani akapark gari parkings za nje, tukaingia ndani tukamkuta mlinzi, Sasa kile kitendo Cha kuingia tu ndani ya geti Caryn akachange ghafla
Caryn: "BM naomba niletee simu yangu kwenye Gari"
Nikafata Simu lakini kinyonge sana nilihisi kama vile kanikosea heshima, huyu Binti nimempita miaka mitatu three good years nikampelekea simu yake ni kama kuna mtu alikuwa anataka kumpigia
Caryn: [emoji338]"Tell me where are you now, is this how you work
You call yourself an estate manager but you're nowhere you are managing, Nothing
Look at the whole compound so messy, look at trash everywhere, people are packing anyhow"
Kwa maongezi hayo nikajua tu kwamba huyu anayeongea na Caryn atakuwa ni Manager wa hizi apartments, kwa maana hiyo hizi apartments zitakuwa za Mzee, maana nilisikia Mzee ana apartments Masaki ila sikuwahi kuziona, muda huo Caryn anaendelea kuongea na huyo manager ila sikuwa namsikia manager anachokijibu
Caryn: "Get yourself another job because I no longer consider you fit to be my estate manager"[emoji3513]
Caryn akakata simu, nikamuuliza kwani kuna tatizo?
Caryn: "Huyu mtu anajiita manager lakini hana anachokifanya, ona kulivyokuwa hovyo, na Baba ndio anamuendekeza sasa mimi namuondoa hapa natafuta mtu mwingine"
BM: "Lakini Caryn mm naona ungewasiliana na Mzee kwanza kabla hujafanya maamuzi pengine anaweza kukushauri jambo"
Caryn: "Namjua yule Mzee hana atakachonishauri zaidi ya kunambia nimuache, hizi huruma zake ndivyo zinafanya watu wamuharibie kazi"
Wakati tunatoka nje ya Geti yeye akabaki sijui alikuwa anaongea Nini na mlinzi hata maongezi yao sijayasikia, tukaiacha Masaki tukaenda hadi Sinza tukaingia kwenye Duka kubwa la nguo za kike na za kiume
Hii siku nilikuwa kama mkia kila anapoenda Caryn mimi nipo nyuma yake, tulivyoingia kwenye lile Duka Caryn alienda moja kwa moja kwenye meza ya Muuzaji (Mdada) na mimi nikamfuata
Caryn: "Boss find your corner and hang yourself there"
Nikatafuta sehemu nikakaa nikamuacha na yule mdada wa Dukani, zimepita kama Dakika 15 akanifuata nilipokaa ikabidi nimchane
BM: "Caryn, this habit of yours has to stop"
Caryn: "I don't understand, what are you talking about?"
BM: "We jua tu sijapenda, nisiongee sana"
Caryn: "Achana na hizo habari, tujadili nilicho kuitia hapa"
BM: "Ushanikata mood, we ongea nakusikiliza"
Akagundua nipo off mood na sikuwa comfortable tena pale Dukani, akanambia basi tuondoke tutafute sehemu tunywe hata juice, tukaondoka pale Dukani tukaenda maeneo ya Mlimani City lakini sio kule ndani, hii inakuwa ni mara ya pili kuja hapa, mara ya kwanza tulitoka wote out kuanzia Bi Mkubwa, Mimi, Michelle pamoja na Caryn
Nikaagiza juice na msosi, Caryn akaagiza juice tu, maongezi yakaanza
Caryn: "BM umeliona lile Duka, ule mzigo wote ni kutoka Uturuki, nataka nichanganyie nianze kuagiza mizigo kutoka china"
BM: "Sasa si uagize mbona ni simple tu"
Caryn: "Ndio maana nikakuita ili unisaidie, nataka kuagiza mizigo kupitia Kampuni unayofanyia kazi Najua wewe ndio unaepokea mizigo ila Baba asijue"
BM: "Kwann hutaki Mzee ajue, unajua Kuna maamuzi mengine unayoamu ni muhimu sana kumshirikisha Mzee kwasababu huwezi jua risk itakayotokea badae"
Sasa mm nimeongea hivyo nikijua lile Duka nalo ni la Mzee ambapo Caryn ameambiwa asimamie
Caryn: "Tatizo unaongea sana halafu hutaki kufuatisha ninachokuelekeza, kwanza lile Duka ni la kwangu, ndio maana nimekuambia sitaki Mzee ajue, na sio Mzee tu, hadi Michelle na Mama"
Nikawa kama vile nimezubaa hivi, maana hilo Duka analodai ni la kwake nikahisi ni kamba napigwa
BM: "Bado hujanishawishi, kama Duka kweli ni la kwako kwanini umeniamini mimi nilijue halafu Mzee umemficha, nikivujisha Siri je?"
Caryn: "Siri Najua huwezi kuvujisha, na wewe kulijua duka haimaanishi wewe ni mtu spesho sana kwangu, bali imetokea tu kwasababu nataka tufanye kazi,"
BM: "Kazi gani?"
Caryn: "Kuna Suppliers kutoka china nimewapata lakini bei zao sio nzuri sana, so nilikuwa nakuomba unitafutie supplier mwenye bei Nzuri, Najua kwako itakuwa rahisi kwasababu kazi yako una deal na wafanyabiashara"
BM: "Sawa, acha tuone"
Caryn: "Kwani kazini una report lini?"
BM: "Bado kama wiki 2 ivi"
Tushamaliza kula, ule muda pendwa wa kulipa bill umefika, Dah! hapa Caryn aliniacha hoi, muhudumu kaja kuchukua pesa eti anamuuliza juice 2 ni shillings ngap? muhudumu akamuambia 10k, Caryn akatoa elfu 10 Kama ilivyo
BM: "Sasa mbona unalipia juice tu, na chakula?
Caryn: "Chakula analipa aliyekula, mimi nimetoka na hesabu ya juices mbili tu, kama ulikuwa na njaa ungesema mapema"
BM: "Kwahiyo unataka kuniambia hapo ulipo unakosa elfu 15 ya kulipa sahani moja ya chakula?"
Caryn: "Naweza kuamrisha mwenye hii hotel atoe watu wote humu ndani ubaki wewe tu na uagize unachotaka halafu wanilipishe kwa Kila meza na nikalipa bila shida, ila siwezi kufanya huo upuuzi coz haikuwa katika ratiba zangu"
Nikanote kitu kingine kipya kutoka kwa Caryn, Yani kila ninavyozidi kuwa karibu nae ndio nazidi kumsoma ni mtu wa aina gani, nikawa Sina budi kulipa Ile 15k ya msosi tukaondoka, Cha ajabu sasa tukapitia petrol station [emoji618] akaweka mafuta ya laki 2, nikashindwa kuvumilia
BM: "Ila Caryn hapa ndio sijakuelewa kabisa! kule restaurant umeniachia bill ya elfu 15 nilipe, hapa petrol station umeweka Diesel ya laki 2, na hii safari ni wewe ndio umeniita"
Caryn: "Yani bado ume catch! sikiliza nikuambie, Wakati natoka nyumbani nilitoka nikijua nitapita petrol station kuweka mafuta, so niliandaa pesa yake, na wakati tunatoka pale Dukani kwangu nilitoka na budget ya kunywa juice tu, elfu 15 ni pesa ndogo sana lakini haifai kutumia pesa eti kwasababu tu uko nayo"
BM: "Ni kweli lakini hujafanya poa, sijapenda kabisa...kama ningekuwa sina pesa je?"
Caryn: "Next time utajipanga, we Mwanaume utafikaje sehemu na kuanza kuagiza huku ukijua huna pesa"
BM: "Madam niache hapa hapa, na Asante kwa treatment"
Ilikuwa ni Tabata reli, nikashukia hapo maana niliona miyeyusho tu, Kesho yake mapema sana Annie akatinga mjengoni, wenzake wanakuja usiku yeye anakuja Asubuhi Sasa sijui ana maana gani, akanikuta nilikuwa bado sijaamka
Annie: "Babe ivi una matatizo gani? kwanini unanifanyia hivi lakini?"
(Annie aliongea hiyo sentensi kwa hisia za hudhuni sana)
BM: "Haya kumekucha! nimefanya nini tena?"
Annie: "Sikujua kama unaletaga Wanawake zako humu ndani nikiwa sipo, mwenyewe unajikuta mjanja kuwahi kuwatoa Asubuhi Asubuhi"
BM: "Unajua sikuelewi!"
Annie: "Hunielewi kitu gani Wakati humu Leo umelala na Mwanamke, Jana usiku nimepiga simu yako akapokea huyo mwanamke"
Duh! huyo atakuwa ni Caryn, si nilisahau simu yangu Jana kwenye Gari yao asee, sasa nikawa nawaza jibu la kumpa Annie huku nikiwaza kwann Caryn amepokea simu yangu na atakuwa amemjibu nini Annie hadi amepanic hivi
Itaendelea...
Hizi mbinu hazitolewagi kizembe mkuu , ni muhimu sana kushinda vita na mwanamkeWatu mna mbinu za kijasusi kabisa,....
Mkuu kama ulisomeaga Cuba vile[emoji23]
Na isipofanya kazi hii mbinu, huoni italeta majanga zaidi? Though lengo langu kuu sio kupita naeHuyo caryn usimtongoze fanya hivi, mwekee mitego sana usimchukulie kama dada yako mwangalie kwa staili kali za kumtamani mtongoze kwa macho jifanye kama unaangalia sana mwili wake mpaka akushtukie lakini usimtongoze , hiyo ni mbinu ya kivita ya kumshusha confidence , alafu potezea usimwambie chochote , mwanamke ni mwanamke tu
Kinachonipa uvivu ni kwamba story nilishaiandika yote halafu ikafutika, so hapa najitahidi kuandika tena, halafu kuandika sio kazi sana ni kupata tu muda na kuvuta kumbukumbu za matukio na hadi maongezi, japokuwa story nai minimize siandiki kila kitu kinachotokeaSeason 1 aliweka kila siku ila hii anavyoipeleka sasa daaaah. Haileti munkari wa kuifuatlia kabisa sijui tatizo limekuwa ni nini?