Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Ilipoishia

Nadhani nimemaliza Accountant Please after this meeting set up another meeting with Sales Team for me and I really need you to supervise them, Mnaweza kuendelea na shughuli zenu BM wewe baki sijamalizana na wewe bado

Basi watu wote wakatoka nikabaki mimi na Caryn ofisini

Caryn: "BM nimetumiwa Parking list ya mizigo inayoingia kesho kwahiyo jiandae kwaajili ya safari

BM: "Sawa ila itabidi niende na mtu mmoja maana nikisema niende mwenyewe nitashindwa kujigawa mwisho wa siku mzigo utachelewa kufika Dar"

Caryn: "Okay lakini huyu mtu uliyekuwa unaenda nae hapo awali sitaki uende nae tena acha abaki store nikiendelea kukutafutia mtu wa kusaidiana nae"

BM: "Basi mteue mtu ambae nitaenda nae kwa muda"

Caryn: "Utaenda na Mimi"


Muendelezo

(SEASON 2 Episode 10)

Alivyosema tu Utaenda na Mimi nikaduwaa kwanza kama nimepigwa ganzi, nikaona hii Sasa miyeyusho nitaendaje na Boss Zanzibar anataka kwenda kujua nini?

Yani kifupi nikawa sijamuelewa ila nikaitikia tu kwasababu yeye ndiye mwenye mamlaka sasa hivi na ndio anaamua Nini kifanyike

Basi nikamuitikia tu kwamba sawa tutaenda wote lakini michezo yangu inabidi niicheze smart sana this time around,

Sasa wakati tunaendelea kupanga safari ghafla Accountant akaingia ofisini akawa anamjulisha Caryn kwamba kile kikao alichomuambia akiandae tayari ameshakinga na muda unakaribia

Accountant: "Kila Kitu kipo sawa pamoja na watu wa sales nimesha waandaa tunakusubiri wewe tu"

Caryn: "Ooh sorry! Unfortunately I'm not going to be available for that meeting so you're going to have to move it to the day after tomorrow, I'm not even available tomorrow either"

Accountant: "Okay, so should i reschedule the meeting up to Wednesday or?"

Caryn: "Yeah but nitakujulisha kama Kuna mabadiliko, Cha kufanya sasa hivi muwekee BM pesa kwenye Account yake, Pesa ya matumizi ya Zanzibar ya watu wawili"

Accountant: "Okay"

Accountant akaondoka wakati huo muda unasoma ni saa 4 pm akili yangu haipo nawaza kuingia mtaani

BM: "Caryn kila kitu si kipo sawa, mimi naweza kwenda"

Caryn: "Kwenda wapi?"

BM: "Si nyumbani kwangu"

Caryn: "Kwani sasa hivi ni saa ngapi?"

BM: "Saa kumi"

Caryn: "Na muda wa kutoka ofisini huwa ni saa ngapi?"

BM: "Saa kumi na moja" (5:00 pm)

Caryn: "Sasa kumbe muda wa kutoka ofisini unaujua kwanini kuondoka Sasa hivi"

BM: "Sasa Caryn mimi hapa sasa hivi nafanya nini, hakuna issue"

Caryn: "Kwahiyo kama hakuna issue ndio uondoke tu muda unaotaka? unajua BM sijui hukunielewa mara ya kwanza nilipokuambia kuwa Ushkaji kwenye kazi sitaki ivi unadhani nikikuruhusu ukaondoka na sio kwamba una dharura ya msingi na wafanyakazi wengi wakuona umeondoka na wao Bado wapo kazini unadhani watajisikiaje"

BM: "Mbona Mama alikuwa ananiruhusu bhana, unajua mm majukumu yangu mengi ni ya nje ya Ofisi ndio maana humu mimi Sina Ofisi"

Caryn: "Sasa ushasema Mama ndiye aliyekuwa anakuruhusu, huyo mtu hayupo kwasasa, Sasa hivi unadili na mimi so acha tu kutaja watu kutaka kujitetea, Mama kukuruhusu wewe kutoka kazini kabla ya muda ya kufunga Ofisi haujafika haimaanishi kwamba alikuwa sahihi, hii kwa wafanyakazi wengine haileti picha nzuri"

BM: "Caryn una complicate sana mambo, sasa nikuulize mm nikibaki hapa nafanya kazi gani au nakaa wapi?"

Caryn: "Si ukakae store huko, kwani wenzako wanaokaa stoo kule sio watu? halafu wewe kwenda Zanzibar haimaanishi kwamba kazi za stoo usifanye"

Dah! Caryn hapana kwakweli kwa mwendo huu hii kazi itakuwa chungu sana, sikutaka hata kumjibu tena nikatoka zangu nikaelekea stoo nikawakuta wana wanapiga story halafu ni kama walikuwa wanamzungumzia

Storekeeper: "Oya BM haka ka Boss lady ni mtoto wa Magufuli nini?

BM: "Kwanini?"

Storekeeper: "Naona kaanza mikwara sana, hope ni nguvu ya soda tu"

Storekeeper 2: "Nakumbuka hata Mama alikuja na mikwara kama hii ya huyu Demu ila mikwara ya Mama ilikuwa sio heavy weight hivi kwanza Mama alitumia kiswahili kwenye introduction yake, Demu katoa mikwara na lugha ya kikoloni hapo ndipo alipotumaliza zaidi"

Sasa mimi nikawa nawasikiliza tu kwasababu mtu wanaemuongelea ameshanitibua, wana wakaendelea kupiga story mimi nipo Busy na simu

5:00 ikafika office ikafungwa Wakati nipo chini parking si nikaiona Bimmer imepark, nikatamani kumsubiri Caryn maana alikuwa bado hajashuka nikasema hapana acha nisepe hizi shobo nizi balance maana nilimaindi kuniweka hadi saa kumi na moja nimechelewa kwenye mitikasi yangu

Kesho yake mapema tu nikawahi ofisini sikutaka mambo mengi, nimefika ofisini kabla hata ya 8:00 pm Ofisi haijafunguliwa,

Ila hii siku kama ingekuwa ni enzi za Mama yake Accnt Unajua ningeunga juu kwa juu nisingepita ofisini ningeenda Zanzibar moja kwa moja kutokea nyumbani ila Caryn kabadilisha mfumo, kasema ni lazima nilipoti ofisini ndio niondoke

Basi ilipofika kama saa 8:06 Caryn akawa amefika akaniita ofisini kwake

Caryn: "Huyu Accountant yupo wapi mbona simuoni kwani hajafika?

BM: "Kwakweli sifahamu, mpigie simu"

Caryn: "Lakini pesa amekuwekea"

BM: "Bado"

Wakati Caryn ananiuliza hayo maswali alikuwa anapitia kitabu cha wafanyakazi cha kusaini muda waliofika kazini, akanambia

Caryn: "nina Access ya kutoa pesa kwenye Account ya Kampuni lakini sitaki kuingilia majukumu ya mtu ni bora tuchelewe lakini ajue atalipia gharama ya sisi kuchelewa"

Ilivyofika 8:36 pm Accountant ndio anaingia job, nikatulia ili nicheki vizuri movie itakayoendelea kati ya Caryn na Accountant Yani mtu na Boss wake

Accountant: "Morning guys"

Caryn: "Accountant ulimuwekea BM pesa niliyokuambia umpatie?"

Accountant: "Dah! nilisahau nimekuja kukumbuka leo Asubuhi hata hivyo Niko na Cash"

Caryn: "Peana hiyo Pesa muda huu tunaondoka"

Caryn akawa anaweka vitu vyake sawa mezani akamuita na Secretary muda huo Accountant ananihesabia Pesa

Caryn: "I need the details of every stuff and the time the reported to work today"

Caryn alivyomaliza kutoa hayo maagizo kwa Secretary Accountant akaacha kuhesabu pesa kwa sekunde kadhaa akamuangalia Caryn, Yani alihisi Yale maelezo yametolea kwaajili yake kwasababu amefika amechelewa, Caryn mwenyewe ndio kwanza yupo serious yani akiongea tu unajua kabisa hii kweli ni sauti ya mamlaka

Accountant akamaliza kunihesabia pesa akanikabidhi huku Caryn anatutazama tu

Caryn: "Accountant naomba huu utaratibu wa kutoa pesa Cash uwe mwisho leo, sitaki kuona hiki kitu kinafanyika tena"

Sisi hao tukaelekea Bandarini tukakata tiketi tukasepa hadi Komekongwe, tulivyofika Zanzibar tukaenda hadi kwenye hotel ambayo huwa nafikiaga kila nikija, tulivyofika tu pale hotelini Caryn akaniuliza

Caryn: "Hapa ndipo unapolalaga kila ukija huku?

BM: "Ndio"

Caryn: "Kulala kwa siku ni bei gani?"

Nikamtajia kiasi ninacholipaga

Caryn: "Na kama mkija watu wa nne Kila mtu anachukua chumba na mnalipia hiyo pesa"

BM: "Ndio, lakini hatujawahi kuja watu wa nne huku, labda wa 3 lakini pia hazidi mara 4 kuja watu wengi hivyo huku"

Basi tukapelekwa vyumbani, Sasa mimi nikifikaga hapa kwenye hii hotel huwa Kuna chumba changu hicho huwa ndio napenda kukitumia ila kama nikikuta hakijachukuliwa, nikaanza kwenda kwenye hiko chumba nikaacha mzigo wangu nikamuambia Caryn ngoja nikupeleke chumbani kwako.

Basi tukaenda hadi room nyingine akaniuliza

Caryn: "So what next?

BM: "Hapa nasubiri Kuna documents moja haijamalizwa kutengenezwa, nimewasiliana ameniambia alimaliza tu atanishtua so akimaliza ndio tunaenda huko"

Caryn: Lakini ndege si ishafika?

BM: "Ndio ishafika na ishashudha lakini sisi hatuwezi kwenye kuchukua mizigo bila hizo Documents"

Caryn: "Hebu kaa kwanza hapa....na Ile Document uliyonionesha kwenye simu ni ya Nini?"

Nikaa kitandani yeye akiwa amekaa kwenye kakochi (one sitter)

Caryn: "Hebu nielezee utaratibu huwa unakuwaje, kwasababu Mimi Ile Document kwenye simu nikajua hiyo pekee ndio inatosha

BM: "Ile niliyokuonesha ni Airways bill Iko hivi, Ukishapandisha Mzigo kwenye ndege kuna kitu kinaitwa Airways bill unapewa, hii Airways bill anapatiwa mtu ambaye amepakia mzigo China baada ya kuulipia"

"Hiyo Airways bill inaonesha mizigo iliyopo yani ni mizigo ya aina gani, Sasa mtu wa china akishapewa Airways bill na yeye anamtumia mtu wa huku Tanzania ambaye ni Mimi au mtu yeyote yule ambaye atakuja kupokea mzigo"

"Sasa Airways bill ikisha scaniwa nikatumiwa Mimi ndio naenda kutengeneza Documents kupitia Airways bill, Documents nitakazotengenezewa Mimi zitaonesha mzigo ulipotoka, Mji, Ghorofa gani? Room namba ngapi? na inaonesha vitu ambavyo vipo Mfano labda smart watches, sijui Hereni na takataka zote na bei zake za china"

"Nikishamaliza kutengeneza hizo Documents naziambatanisha pamoja na Airways bill halafu naenda ZBS, shirika la viwango yani ni sawa na TBS kwa kule Bongo, ZBS wanaenda kunipigia hesabu"

Caryn: "Slow down bro, unanitajia tu Document na hunifafanulii ni ya aina gani ya Document

BM: "Okay, labda niite Invoice"

Caryn: "Sasa hiyo Invoice na Ile Airways bill vinatofauti gani? maana naona kinachoelezwa kwenye Airways bill ndio kile kile kilichopo kwenye Invoice"

BM: "Kivipi sijakuelewa"

Caryn: "Umesema Airways bill inaonesha aina ya mzigo na Invoice pia inaonesha aina ya mzigo, Sasa kwanini upoteze muda kwenda kutengeneza Documents zingine badala yake ungeweza kutumia hiyo hiyo Airways bill maana inaonesha kila kitu"

BM: "Nisikilize basi, Iko hivi Airways bill unaweza kuchekecha ukaandika mzigo una vitu viwili Mfano Hereni na Vioo vya simu lakini kiuhalisia mzigo hauna vitu viwili tu pengine labda vipo zaidi ya vi5 kwahiyo Ile invoice inakuja kueleleza vitu ambavyo vipo"

Niliendelea kumuelezea Caryn jinsi kazi zinavyoendeshwa ila nikawa na Jitahidi kutokumuelezea kila kitu maana yeye hatokuja kufanya hii kazi ila anataka tu kupata experience ya mambo yanavyokuwa, ila alikuwa ananichosha kwa maswali, na maswali yenyewe ni yale ambayo yanataka majibu ya maelezo ila nilijitahidi kwenda nae sawa

Caryn: "Sasa kwanini mizigo iwe mingi halafu kwenye Airways bill iandikwe michache?"

BM: "Ahh Caryn bhana, si watu wanachezesha mtu unakuta hataki mambo mengi, na hata hivyo hii invoice niliyokuambia inaonesha kila kitu pia watu wanachezesha vile vile, mizigo mingine wanairuka hawaiandiki hasa hasa Ikiwa mizigo ya hatari"

Caryn: "Mizigo ya Hatari ni ipi? Cocaine au?"

BM: "Hapana! Ukiachana na madawa, mizigo ya hatari ni Ile ambayo haitakiwi kuingia nchini Tanzania, kama yale ma dildo madawa ya kuongeza shepu, Vitenge vya China haviruhusiwi pia japokuwa watu wanavusha"

Caryn: "Ooh kumbe!"

BM: "Yeah, Sasa ukienda ZBS watakupigia hesabu ya mzigo wako then utalipia, na hapa ZBS kupita ni muhimu kwasababu huwezi kupata Documents za TRA kama hujapita ZBS"

"Ukishamalizana na ZBS Unarudi tena kwa watu waliokutengenezea Documents kule mwanzoni wakafanye attachment ya Airways bill, Invoice, Fomu ya ZBS pamoja na risiti za malipo za ZBS ulizolipia baada ya hapo unaenda TRA huko ndio wanaangalia wanakupangia kodi Mfano wanaweza kukuambia kwa kilo ulipie Tsh 1,500 au 1,800 itategemea Sasa na wewe utakavyo bargain nao"

"Sasa kama wata ku-charge kwa kilo 1,500 utapiga mahesabu una kilo ngapi, Mfano labda una kilo 500 katika mzigo wako kwahiyo utapiga 1,500×500 = 7500,000 inamaana mzigo wako utalipia laki Saba na nusu"

"Ukishakubali kulipa hicho kiasi unamrudia tena yule mtu aliyekutengenezea Documents mwanzoni kule kwenye system akubali Yani a-accept kile kiwango Cha Kodi kilichopigwa pale, akishakubali anaziprint zile karatasi za TRA unazichukua unaingia nazo Airport ukiwa ushalipia"

"Moja kwa moja unaenda kwenye Ofisi zao za TRA ndani ya airport unawaonesha Documents kama zimelipiwa wanakugongea muhuri"

"Ukishagonewa muhuri unaenda ZAT, ZAT kazi yao ni kutoa mizigo kule ndani ya Airport unawaonesha Documents wenyewe watajua kwamba mzigo wako ni namba flani flani umekuja siku flani na ndege flani, wao Sasa wataenda kuangalia labda walishaitoa ipo kwenye ma Godown yao, watakutolea nje kazi yako ni kuichana ukimaliza unaita mapolisi unaita ZFD pamoja na TRA kuja kukagua"

"Mzigo unakaguliwa kimoja baada ya kingine, wanaangalia sasa kwenye Ile invoice yako kama vilivyomo vimo? au kuna vya ziada? na vikikutwa vya ziada ambavyo havijaandikwa kwenye Documents unapigwa tena Kodi nyingine hapo hapo Airport"

"Ila ukiwa mjanja ukiona kodi inaenda kuwa kubwa unaweza kumuwahi na kitu kidogo, labda unaona Kodi inaenda kwenye laki 5 unamshikisha laki 2 mnamalizana"

Caryn: "So kumbe unaweza kutoa pesa ili mzigo usikaguliwe"

BM: "Aahwapi! Mzigo ni lazima ukaguliwe, lakini hiyo kagua inakuwa kama ushahidi tu wa mtu kufanya kazi yake ila wewe unakuwa ushamalizana nae nyuma ya pazia, kwasababu anayekukagua ndio anajua kakutana na nini katika mzigo ofisini kwao hawajui kinachoendelea"

"So akishamaliza kukukagua anakutolea release ya wewe kutoka baada ya hapo unaenda ZAT unapewa Manifesti ukipewa document Unarudi TRA inagongwa muhuri halafu unalipia ZAT, Ukishalipia ZAT unapata release unafunga mzigo wako unapakia kwenye gari kuelekea Bandarini"

"Ukifika Bandarini kuna TRA mlangoni unamuoneshea Documents, Lakini hapa pia kuna Document ya kusafirisha mzigo huwa inatakiwa, mara nyingi watu wengi wanaosafirisha mizigo huwa hawana hii Document, huwa inaitwa M8, Sasa ikitokea huna hii Document unawaacha na elfu 10

Caryn: "Subiri kwanza....ni kwanini watu wanakosa hiyo Document, yani kwanini upambane huko koote na ma-document ya TRA sijui ZAT halafu uje kukosa hii"

BM: "Tatizo ya hii Document ukisema uifuatilie itakucheleweshea muda, kama unaweza kupita kwa elfu 10 ya nini sasa kupoteza masaa mawili kufuatilia karatasi"

Caryn: "So ukitoa hiyo elfu 10 hakuna usumbufu utakutana nao juu ya kukosa hiyo karatasi?"

BM: "Hamna, Ukishalipia elfu 10 ndio imetoka hiyo unaenda kulipia na wharfage mzigo wako then unachukua tolori unaingiza kwenye meli mzigo unavuka Maji shughuli imeishia hapo"

Caryn: "Na mzigo ukishafika Dar inakuaje, process ni kama za huku Zenji?"

BM: "Dar hakuna ZAT utalipia tu ushuru wa Bandari wharfage, TBS wapo ila wajanja huwa wanawawahi kabla hawajafika"

Caryn:. "ZBS na TBS si ni kama kitu kimoja unataka kunambia huwa unalipia huku ZBS na ukifika Dar unalipia TBS?"

BM: "Ndio maana ake ila Sasa hivi nimesikia wanataka kuweka mfumo kwamba ukishalipia ZBS Zanzibar ukifika Dar unapita tu ila utakaguliwa na TRA tena, lakini hukaguliwi kama vile mzigo umetoka china straight"

Caryn: "Duh! kazi yako nilikuwa naichukulia simple lakini ni ngumu sana hasa kwangu, hii kazi inataka mtu wa kujishusha muda wote kitu ambacho Mimi siwezi, na hawa watu wa serikalini wanavyopenda kuabudiwa dah! mm sidhani kama nitapelekana nao sana"

BM: "Unajua kama Document leo zingewahi kutoka tungegeuza na mzigo leo leo usiku hata tusingelala na tukiikosa Sealink leo basi kesho tutageuza na meli za kawaida ambazo kupakia mizigo kwenye hizo meli huwa ni expensive"

Caryn: "Hata kama ni Expensive Wacha tu turudi kesho, Habari za kusafiri usiku kwenye Maji sizitaki"

Basi ikafika mida mida ikabidi tutoke hivyo hivyo japokuwa Documents zilikuwa hazijakamilika ilibaki document ili kukamilisha documents zote, na ubaya wa Airport Sasa wanakutolea mizigo kwa Documents ambazo unazo, kama Kuna mizigo yako mingine halafu huna document hawakutolei

Sasa kwasababu muda ulikuwa unazidi kwenda nilichokifanya nilienda na documents ambazo nimefanikisha kuzitoa na kuzilipia kwahiyo baadhi ya mizigo sikufanikisha kuitoa

Sasa nikamuambia Caryn "Hapa inabidi hii mizigo tuliofanikiwa kuitoa isafiri Leo na Sealink halafu mizigo ya kesho ndio tuondoke nayo na boti ya kawaida kwasababu itakuwa imebaki michache tutakuwa tumekwepa Gharama"

Caryn: "Hapana hiyo ni ku Risk, mizigo ya watu ikipotea je?


BM: "Haiwezi kupotea bhana mm sometimes huwa nafanya hivi, kwasababu tukisema tusafiri nayo kesho itakuwa ni gharama"

Caryn: "Hapana, huko ni kufanya kazi kwa mazoea ni bora tu tugharamike na hizi gharama unazoziona ni kubwa ila tuwe na uhakika na mizigo ya watu kufika salama kuliko kukwepa gharama halafu tukajikuta tunakuja kulipa gharama kubwa zaidi kuliko hata hii ambayo tunataka kuikwepa Sasa hivi"

BM: "Dah, haya bhana lakini nilikuwa nashauri tu kwasababu gharama tutakazolipia kusafirisha mizigo kwenye meli ya Abiria ni kubwa kama tutaiachia hii meli ya mizigo iondoke"

Caryn: "Labda nikuulize swali, ukipakia mizigo kwenye hiyo meli unayoisema na ikatokea mizigo ya watu ikapotea unadhani utakuwa ni uzembe wa aina gani? Kampuni hapo ndio itaingia gharama kulipia mzigo uliopotea na sio wewe ndio maana naona unafanya maamuzi ya kurahisisha sana"

Ikabidi tu nimuelewa japokuwa anachokiongea kina make sense ila naona kama ana complicate sana mambo, tukaweka Kila kitu sawa Ilivyofika saa mbili kasoro tukarudi hotelini

Tukapiga msosi tukamaliza tukaelekea vyumbani, chumba changu hakipo mbali na chumba Cha Caryn, nilivyofika tu kwenye room yangu nikaingia bafuni kuoga, natoka bafuni namkuta amekaa kitandani nikajua tu huyu amekosa usingizi anataka tukeshe tukipiga story

BM: "Vip kwema?"

Caryn: "Itabidi tulale wote humu, mimi ugenini siwezagi kulala peke yangu"


Itaendelea
Kama boss hajaliwa kimasihara itakua chai !🤪
 
Bado hakijaeleweka tu...!!! Ngoja niweke kambii hapaa kusubirii
 
Back
Top Bottom