Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Caryn ana dharau sana sijaona sababu ya yeye kumdhihaki dada yake vile tena mbele za watu wasiowafahamu anamshusha na mzee pia hajamtendea haki michelle eti kisa kapenda kijana wanayemuona sio hadhi yao.

Mwisho wa siku wanakuandaa kuifahamu biashara uje umuoe caryn ambayae hatakuheshimu kamwe. Sijaona akili zake zaidi ya kebehi tupu.

Mwisho ukimuweka annie mbele utapoteza kazi maana mshadanganya kwa mama accountant pia utampoteza mzee maana anakuandaa kuwa kijakazi wake kupitia caryn
Kuna muda nakuelewa sana
 
Sikiliza kuna mtu kukushauri biashara nzuri tu hapo juu, amesema fungua duka la spare za pikipiki na bajaji, tafuta mafundi wazuri hata wawili kwenye hii biashara mafundi huwa wanajilipa kwa kufanya ufundi ila wewe unauza spare, sasa mi naongezea kwenye hili wazo kalifanye njee ya mji kidogo, kule unapanga nyumba nzima mbele ya nyumba utaweka kiosk cha hiyo biashara, pili utakuwa hiyo nyumba unalaza bajaji na pikipiki so utamwajili mlinzi , na ukipata kaeneo kaziada hapo mbele ya nyumba unaongezaa na mashine ya kuosha pikipiki na bajaji.

Upande wa mapenzi tumia formula inaitwa delay method, yaani unaendelea kubuy time huku unasongesha goals zako, Ongea na Mama yake Accountant kuwa kuna mambo unataka kuweka sawa ndio umvalishe pete, omba akupe muda kidogo, huo muda ukipita unaangalia jambo lingine la kulata delay, siku zote visingizio haviishi mkuu, utakuwa unatengeneza visingizio mpaka mwaka unaisha.

Hii ndo delay method.
Hii ndio JF ya zamani ninayoipenda mimi yenye vichwa namna hii
 
Ushauri:

1. Mapenzi
Wote wamekusaidia kwenye nyakati ngumu ila Annie unamuonea huruma zaidi, Accountant ana madhaifu ya kibinadamu ya kuropoka hii inatokana na familia na malezi, ila sioni sababu kubwa ya yeye kukosa point…..sometime inabidi udanganye ili mambo yaende sawa, Accountant anajua moyo wako uko wapi.

Anyway go for Annie naona ndio mnaelewana vile unataka.

Mfanye Annie ajue walau ndoto yako ya kutaka kiwa mfanyabiashara na fanya ajue uko na unalenga kuutengeneza mtaji kutoka kwenye hiyo kampuni, ila usikubali nafasi kwa masharti ya kuoa mtu usiyempenda.

2. Mzee na familia
Kuna muda unashuka sana mpaka inakuwa noma, hasa kwenye conversation na hako katoto, mpaka hapo nadhani huo mtihani wa mzee na huyo mtoto wa buguruni itakuwa umeshinda ila hako katoto Karen ki design ni type wale hawakupi ushindi kirahis rahisi.

Kukuza biashara ndani ya miezi sita kwa mtu ambaye hajawahi na imletee pesa zaidi ya 100,000 kwa mwezi plus majukum ya wadogo zake.Tengeneza link zaid na mzee huyo dogo anaweza kuja kuwa kirusi
Hii ndio JF pendwa yenye vichwa vya namna hii.
 
kupitia michelle na jamaa yake kweli mboo sio mchezo tuzitumie vizuri jamani
bm caryn usiharakishe nae demu haeleweki,lakin kitendo cha kumdanganya mzee wake kuhusu gari kinatia hamasa sana
 
Hakuna upande wa kubaki...

Kwanza umekosea sana kuingiza mapenzi sehemu za kazini, Acha kabisa...
Accountant atakuharibia kazi...

Hivyo huna kazi...

Pili umekuwa umekuwa unapenda vya bure, wewe mtoto wa kiume pambana kwa jasho...

Mzee anakupelekesha tu ka mtumwa...kama anataka kukusaidia mbona masharti...

Pia msaada angetoa yeye mwenyewe kwa hao watoto wa mtaaani...

Anataka kitu kutoka kwako mwishoe utaambiwa uoe mtoto wake...

Mi nafikiri Acha vyote ufanye biashara yako mwenyewe achana na Mzee na Achana na kazi ya mama Accountant
Mmmh....! Acha kumdanganya. Kila mtu ana njia zake za kufanikiwa kimaisha.
Na huyu kijana njia zake za kufanikiwa ziko hapa. Huwezi kumwambia aache kazi,aache kwa mzee ajue atakavyojua,kisa?

Kuna wengine pia huko juu wamecomment kwa nini iwe wewe BM tu uwe na bahati ya kukutana na familia bora?. Yeye hapo amehadithia familia hizo tu hajahadithia maisha yake yote hata familia zingine alizokutana nazo hata zile ambazo sio bora. Lakini souce ya hii story ni hizo familia tu alizohadithia
 
Na kwann umfanye Annie mnyonge?? Kisa leo unacho..kisa hupendi kusikia ukweli..au kisa ni mnyenyekevu na mpole and she loves you dearly... Au ni kwamba kujikuta mi ndo mwanaume huku ukiwa kwa accountant na mama ake unachutama na kwa Caryn mwenyewe unasalute ngoma isambee....

My take fanya maisha yako. Hapo ofisi ulioko ni shetan alipomuonesha Yesu vingi akamwambia ukinisujudia....if you can be ready kutoka hapo. Kwa mzee kuna mtu katoa ushauri mzuri sana i think Dona..kuwa anaweza aje kukufanya his puppet...not actively rather passively so every time you be submissive..usije jikuta waabudu mwanadamu..just be careful wit this option too...

Ushajifunza meng up to now mkuu its high time you get a life. And dont treat Annie like a clown simply coz she is too weak to get back to you. If you lose her one day you will wish you treasured her more...thamini mwanamke mzuri na good thing kila mtu anaesoma uzi huu kamcommend so akili kumkichwa. She is a woman and a half..usijitie alpha male kwake...ukastep on her beautiful and submissive heart...

Actually fanya uonavyo maisha ndo haya haya...
Ndugu kumfanya mnyonge kama alivyomaanisha mnyonge wangu Anie sio kwa maana uliyoitafsiri wewe. Anamaanisha Anie hamuogopi ana uwezo kumuamlisha chochote kama mke. Au kwa lugha nyingine wanaweza kukubariana ktk mambo mengi wakaenda sawa.
Hata hivyo oa mwanamke unaeweza kumuonea,na kusema chochote kwake. Ndoa nyingi zimevunjika ksbb ya mwanaume kuwa mnyonge kwa mke. Hasa hawa wanawake wanaopenda kuwa juu na kuongea sana. Kwa hiyo mkuu anamtaka Anie asiwe mnyonge,awe juu?. Akiwa hivyo kesho tu anaachika
 
BM tunakuskilizia mzee? Au mshua kajua Carry anakutaka kwahyo kakufukuza job?[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Back
Top Bottom