Dah! Shukrani mkuu umeenda deep sana, I appreciate [emoji1545]
Nilikuwa na Mpango wa kuleta muendelezo tarehe 5 mwezi wa 3 yani jumapili ya wiki ijayo lakini kwa comment yako nitajitahidi kuleta muendelezo jumamosi ya kesho kutwa, nikichelewa sana jumapili
Aaaaaah kumbe mkuu swala la kuamua kuleta humu story ni wewe tu na wala sio ubize wala nini.. Maana hapo unasema ulikuwa na MPANGO wa kuleta hiyo story tarehe 5 March ila kwa kuwa umeguswa na comment ya mwamba unasema utaiwahisha.....Safi. Ila hapa chini nina barua yako ya wazi
With all Due respect, siamini kama wewe ni the most busiest person humu ndani. Naheshimu muda wako unaotumia kuandika hii story ila imekuwa too much.
So inaonekana unakaaga nyuma ya keyboard afu unaenjoy vile watu wanakuw craving na story yako. Mnapata raha gani nyie jamaa kuona watu wanahangaika kuingia na kutoka kwenye nyuzi zenu ili kuona kama kuna updates?
Hata kama haulipwi, kwanini uliamua kuanza kuiandika wakati unajua ni ndefu na hauna muda wa kuandika? Najua watakusaidia kunipopoa kuwa sijalazimishwa kuisoma ila inabidi ujue, the first time mtu yeyote anaamua kupublish story humu ndio first time anapoteza umiliki wa ile story...inakuwa ni mali ya wote.
Afu kuandika sio kazi kama hivyo ambavyo huwa mnajaribu kuexaggerate humu ndani. Hakuna episode hata moja kati ya zote ambazo umeziandika humu ndani ambayo ulitumia zaidi ya dakika 20 kuiandika. HAKUNA!!
Kwahiyo kati ya masaa 24 kwa siku unakosa dakika 20 kuwapa watu wako kitu ambacho kitawasaidia kuua addiction yao ambayo umewapatia?....Let's assume we ni mwanamme na unapenda soka, pamoja na kuwa busy sana lakini hukosi dk 90 za kuangalia games za soka....Unataka kuniambia huangalii mechi na kila kitu chako kimestop kisa ubusy?
Sasa kwanini ukose dk 20 tu basi kwa siku 2 kuandika episode ndefu?....
In long run nashauri Moderators waweke condition mtu yeyote anayeanzisha humu story asiipublish hadi awe ameitimiza yote.
Hii tabia ya watu kuona raha wenzao wakimtag tag kwenye uzi wake ni ya ajabu sana.
Ila watoa story daily nyenyenye ubusy ubusy....NONSENSE!!!
Mimi napongeza watoa story wengine kama Kigakoyo.....Jbourne96.....SinganoJr....pamoja na umughaka....wanajitahidi sana sana sana.
Sio nyie wengine ambao kiepisode chenyewe unatumia siku 15 kuandika na hapo umeliliwa sana.
Kuna mwenzako mwingine aliletaga story yake, baada ya kuona attention ya watu imekuwa kubwa...akaanza kuvimba na kuona raha kubembelezwa....matokeo yake kuna siku akalopoka "leo nilipanga niwape episode 3 ila kwakuwa taifa limepata msiba naomba tuendelee kwanza na maombolezo" 😄😄
Najua utasoma hapa. Vyovyote utakavyochukulia na kutafsiri ni sawa tu as long as naelewa nakwambia ukweli na inabidi ubadilike....
1. Ni either usiendelee nayo na uishie hapa hapa maana sio kwamba ni special kiviiiiile kuliko kunata kiasi hiki.
2. Or uendelee nayo na uwe na consistency kuliko kuwakosea watu hivi. Eti hadi sahizi bado hujamaliza matukio ya November mwkaa jana 😀😀😀
Maswala ya kuleta excuse kuwa ooooh kuandika ni kazi sana kuliko kusoma mara sina muda....HATUKUKULAZIMISHA KUILETA.
Wale watakaokusaidia kunipopoa kuwa sikulazimishwa kuifatilia wajue tu kuwa HII STORY HAINIONGEZEI WALA KUNIPUNGUZIA CHOCHOTE. Ila nipo hapa kuwakilisha watu wanaokereka ndani kwa ndani. Mnawapa addiction kwa sababu za kipuuzi.
NB: Hii barua nimeiandika kwa dk 6 tu....Assume ningeandika kwa dk 20 si ingekuwa ndefu kama episodes 4 za nyie masimuliaji....
Afu eti mtu bila aibu anaanza oooooh tatizo muda wa kuandika nakosa....ULILAZIMISHWA KUILETA? au ulitegemea nini wakati ulijua huna muda?
Acheni kutaka umuhimu/trending isio na faida.
Kuna mwamba anaitwa SINGANOJR.....anasimulia story yake ya jamaa naitwa ROMA. Hadithi ni ndefu hadi sahizi kafika episode ya 320....Episode yake moja ni kama episodes 3 za hii story yako lakini jamaa hazingui....Yeye ni Jumanne anakupa episodes 3....Jumamos anatoa episodes 3....Safi kabisa maana anatimiza wajibu wake. Ndiyo, ni wajibu kwasababu yeye ndio aliianzisha. Hakuna mtu aliyejua wala kumuomba. So anatimiza wajibu wake.
BM acha visinvizio. Acha kutafuta trending na cheap popularity....Acha kujifanya uko busy zaidi ya nini sijui. Acha dharau kwa mashabiki zako. Huwezi kukosa dk 10 kila siku za kuandika hii story kwenye kifaa chako. Then baada ya wiki unaituma episode moja ndefu sana iliyotumia dk 70 kuiandika.
Lakini haya maswala ya kuwaweka watu onhold kwa wiki 4 halafu unakuja na kiepisode kimoja cha maneno 950 ni USHAMBA!!!