Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

Ilipoishia

Baada ya Accountant kumaliza kazi yake Caryn aliniita na kunipa maagizo flani

Caryn: "Una mawasiliano ya Mr Michelle?"

BM: "Hapana"

Caryn: "Basi nitamuambia Secretary ampigie ili aje kuanza kazi tarehe 1 December"

Nikashusha pumzi kwanza, nikajua hapa sasa nimemalizana na Michelle ila kuna kitu nikamuuliza Caryn maana nilijua àmempotezea jamaa

BM: "Pamoja na kwamba nilikuwa nakushauri huyu jamaa umpe kazi Lakini sikuwahi kuwaza kama utakubali"

Càryn: "Wewe tulia mimi najua nini nafanya, kama ana akili timamu ataikataa hii kazi"

BM: "Kwanini akatae sasa?"

Caryn: "Wewe alikunyima kazi kwasababu tu aliona picha yangu, hiyo ina maana ya kwamba Mimi na yeye hatuko sawa, kama mimi ndio ningekuwa ni yeye ningejiweka katika taadhari sana kwa mtu ambaye anaonesha kunijari au kunipenda na wakati najua hatukuwa sawa, Mimi huwa naamini kuwa mtu mbaya akipanga kufanya ubaya hutanguliza wema kwanza"


Muendelezo

(Episode 17, SEASON 2)

Tarehe 1, December, siku ya Alhamisi Opportunist aliitikia wito jamaa alifika ofisini mapema tu, Wakati nipo ofisini kwa Caryn secretary alikuja kumpa taarifa kwamba Opportunist tayari ameshafika.

Sasa mimi nikataka niondoke kusudi nimpishe Caryn na mgeni wake ila Caryn akanizuia

Caryn: "Unaenda wapi wewe kaa hapo, huyu naongea nae na wewe ukiwepo"

BM: "Sio heshima bhana Caryn, vitu vingine vinahitaji privacy"

Caryn: "Nina maana yangu kutaka wewe ubaki hapa"

Ikabidi nifuatishe order, halafu kitu kingine nilichokisoma kwa Caryn ni kwamba nikionesha kama nipo upande wa bwana ake Michelle ana kwazika sana, basi jamaa akaitwa akatinga ofisini na confidence zote akatusalimia halafu jamaa akakaa kwenye kiti

Caryn: "I didn't ask you to sit"

Opportunist ikabidi asimame, na muda huo Caryn amechange kabisa sio yule niliyekuwa naongea nae Dakika 2 zilizopita

Caryn: "Anyways, you may sit"

Nilivyomcheki Opportunist usoni nikamsoma kama kamaindi vile, kwasababu alikuwa ameshakaa kwenye kiti halafu Caryn akamuamsha eti kisa hajamruhusu kukaa na jamaa hicho kitendo kimemuudhi facial expression yake tu ilidhihirisha, Sasa kama ndio atakuwa mtu wa kumaindi vitu vidogo kama hivi sidhani kama atatoboa

Wakaanza maongezi yao mimi nipo pembeni nawasikiliza

Caryn: "Mr ****, I believe you dropped your CV with us few weeks ago, well the vacant job is not what you applied for but it's something based on the fact that you have an interesting"

Caryn: "Here is your work description work hours schedules and payments so if you agree kindly sign and resume immediately"

Jamaa aka sign, baada ya Caryn kumalizana na Jamaa Secretary akaambiwa awape taarifa staff wote kwamba baada ya lunch time kuna kikao

Basi, baada ya lunch time kweli kikao kikaanza na lengo la kikao ni watu kupangiwa majukumu yao upya hasa kwa Opportunist pamoja na Utambulisho wake kama new staff

Kwa kifupi jamaa alipewa kazi ya ku deliver mizigo kwa wateja hapa Dar kwa wateja ambao wanataka huduma hiyo na kupakia mizigo kwenye mabasi kwa wale wateja wa mikoani

Kwa haraka haraka kazi aliyopewa jamaa unaweza kuona ni ya kiseng* lakini ni moja kati ya Kazi ambayo mtu akiifanya basi atakutana na tip za kutosha, nasema hivyo kwasababu Mimi ndio nilikoanzia huko na nilikuwa napata vi tip sana japo si kwa wateja wote kama mnavyojua watu hawafanani,

Ila pia ina changamoto yake hii kazi, hasa kwenye hii mizigo inayoenda mikoani, ukijikoroga ukapoteza mzigo wa watu ujue Ofisi ndio inalipa na Ofisi hailipi hivi hivi tu itakukata kwenye mshahara wako.

Sasa Caryn alivyomaliza kumtambulisha mfanyakazi mpya na kumpangia majukumu, akaanza kumsomea kila mtu mashtaka yake coz pale ofisini kuna kisanduku Cha maoni au complaints kwa wafanyakazi

Caryn: "I have some grievances here in my desk....

Caryn: "Accountant you have treated as lot of your colleague here with disrespect, I get complaints all the time but I overlook them because of friendship between your Mom and Dad, I'm giving you a second chance to redeem yourself, I want to see if you can change for the better or if you remain this person that you are"

Accountant: "So correcting people's mistakes at work is that act interpreted as Disrespect?

Caryn: "But you don't correct people by being rude to them you speak to them nicely and with love no matter who they are"

Caryn: "Nadhani tumeelewana Accountant, na BM naomba kama hauko Zanzibar nikuone Ofisi, Habari za kupotea na kuonekana siku za safari hiyo tabia ife tafadhali yani unafanya kazi kama vile we ni Agent na wakati umeajiriwa"

Hatimaye na mimi sikuachwa salama nikachanwa mbele ya kadamnasi

Caryn: "Last but not least, naomba tufanyeni kazi kwa bidii, Watanzania tuna utamaduni wakupoteza sana muda, tunajifanya na kujionesha tunapenda sana kufanya kazi lakini kiuhalisia hatufanyi kazi kama tunavyoonekana. Mimi sitalipa mtu kwa kuonekana anafanya kazi, nitakulipa kwa matokeo ya Kazi uliyoifanya"

Tukafunga kikao, masaa yakaenda hatimaye na muda wa kufunga Ofisi ukafika tukafunga, Usiku wa siku hiyo Wakati nipo kwangu nataka kulala Mzee akanipigia simu akanambia kwamba Asubuhi ya jumamosi ya kesho kutwa nijitahidi tuonane,

Ilivyofika Jumamosi mapema tu nilikuwa nyumbani kwa Mzee, kumbuka jumamosi ni siku ya kazi pia japo ni nusu siku lakini sikwenda ofisini nimekuja kwa Mzee moja kwa moja (Kosa hilo, a very Big one)

Nilivyofika kwa Mzee nikamkuta nikamsubiria sitting room alivyomaliza kujitayarisha tukaanza safari wakati tunaondoka nyumbani sikujua tunaenda wapi hadi tulipofika tulipokuwa tunaenda, sema hapa naomba nisiingie deep sana Incase Uzi huu ukaja kusomwa na family member

Tukatoka kule tukarudi mjini tukaenda hoteli flani ipo maeneo ya Mikocheni, hii hotel ndio kwa mara ya kwanza naenda na Mzee lakini nilishaenda na Caryn mara kadhaa

Tukatafuta Mahali tukaketi akaja muhudumu akatusikiliza Mzee akanambia niagize chochote nikaagiza then yule muhudumu akaambiwa na Mzee amuite Manager

Manager alivyokuja ndio nikajua sasa kuhusu Ile hotel, kumbe Ile hotel ni ya Mzee bhana na tunakujaga na Caryn hata hakuwahi kuniambia, Manager alivyoondoka ikabidi nimuulize Mzee

BM: "Mzee kumbe hapa ni kwako?"

Mzee: "Ndio lakini nimepanunua juzi juzi tu hapa, kama miezi 7 iliyopita"

BM: "Ooh! ndio maana hata wahudumu hawakujui sababu naona wanakuhudumia kama mteja wa kawaida tu"

Mzee: "Na Mimi ndio nataka iwe hivyo, ukiwa unamiliki sehemu kama hii Kuna faida kubwa kama wafanyakazi watakuwa hawakujui sababu ni rahisi kuona madudu yanayofanyika"

BM: "Sasa Mzee huyu manager hawawezi kuwaambia wafanyakazi ili mradi wawe makini pindi wewe unapokuwepo hapa"

Mzee: "Kwenye mkataba wake kuna kipengele kinambana kufanya hivyo"

Mzee: "Hata wewe Mungu akikubaliki na Mali za kutosha usipende kuwa front kila sehemu hata kama Mali zako ndio zitakupa umaarufu"

Basi tulivyomaliza kula tukaondoka tukaenda masaki kule kwenye Appointments zake ambapo nilishawahi kwenda na Caryn pia, Mzee akakagua kagua pale then akampigia simu Caryn nikamsikia anamuomba namba za msimamizi wa zile Apartments

Mzee: "Nina Mwaka sijaja huku, naona Binti aliamua kubadilisha rangi za kuta"

BM: "Yeah, management mpya iliyowekwa inajaribu kufanya vitu tofauti"

Mzee: "Na sijui mtu mwenyewe anafanyanana aje, asije akawa adui yangu ndio anasimamia Mali zangu"

BM: "Mzee Kwani wewe una maadui?"

Kabla ya kunijibu Mzee akacheka kwanza

Mzee: "Unajua kwenye ridhiki adui hakosekani, tena hasa ukiwa na ukwasi wa kutosha sio binadamu wote watakuangalia kwa jicho zuri, kumiliki utajiri inakubidi uwe na roho ngumu sana, sikutishi lakini ndio uhalisia kama roho yako ni nyepesi na huruma huruma nyingi hutoboi"

Saa hiyo tunashuka ngazi huku tunaongea, tumetoka rooftop kuangalia matank ya Maji

BM: "Mzee mbona wewe una huruma bhana na umetoboa"

Mzee: "Kwa bahati mbaya umenijua uzeeni, Mimi Wakati najitafuta hii huruma unayoniona nayo sikuwa nayo kabisa"

Mzee: "Hata spirit ya kutafuta pesa sio kama Ile niliyokuwa nayo zamani, nimekuja kupunguza speed baada ya kujua kwamba tunapambania vitu tusivyozikwa navyo na tunazikwa na vitu tusivyo vipambania, lakini hii kauli isikufanye ubweteke na maisha ikupe tu angalizo katika njia unazochagua katika kutafuta hayo maisha"


Sasa wakati tunaendelea kuzunguka zunguka kwenye compound ya zile apartments manager akatokea nikawaacha na Mzee wanaongea, mm nikatoka nje ya fence kabisa tulikopaki Gari (Jeep Wrangler) Mzee alivyomalizana kule ndani akatoka tukasepa tukarudi nyumbani

Kikawaida kama ukitoka na Mzee mkianzia safari nyumbani kwake mkimaliza Mizunguko yenu huwa anataka mrudi wote nyumbani halafu ndio uondoke, hawezi mkatoka wote nyumbani halafu akakuachia juu kwa juu, hapa ndio huwa simuelewagi

Sasa wakati tumefunguliwa Geti ndani Parking tukakuta gari ya Michelle Audi, Mzee akaniambia

Mzee: "Ivi ulianza kile nilichokuagiza?"

BM: "Yeah" (ilibidi nimdanganye)

Mzee: "Jitahidi, watoto wa kike hawa sio wa kuwaamini sana hasa huyu Michelle"

BM: "Sawa Mzee nimekuelewa"

Tukaingia ndani, Tukakuta sitting room ipo tupu hakuna mtu, Mzee akamuita Michelle alikuwa chumbani kwake then akamuagiza Michelle aniletee kinywaji halafu yeye akaenda chumbani kwake

Nikamwambia Michelle aniletee juice, akaleta juice

Michelle: "Usipende kunywa kunywa majuice haya sio mazuri hasa kwa mwanaume yana masukari mengi"

BM: "Sasa kama sio nzuri mbona mnaendelea kuzitengeneza?"

Michelle: "Huu ni ushauri tu kama uliopo kwenye pakti la sigara, shauri yako utashindwa kunanii"

BM: "Kufanyaje?"

Michelle: "Umenielewa....umetoka wapi na Mzee?"

BM: "Town tu misele misele ya hapa na pale"

Michelle: "Ooh, naona mmempatia mtu wangu kazi ila katika nafasi zote ndio mmeamua kumpa Ile?"

BM: "Ile si kazi mbaya kama unavyofikiria, Iko na pesa kama akijua ku deal na wateja, huko Mimi ndipo nilipoanzia"

Michelle: "So kwasababu wewe ulianzia huko chini basi unataka watu wote waanzie ulipoanzia wewe sio"

BM: "Hapana sina maana hiyo, ila kama nafasi nyingine ingekuwepo angepatiwa ni vile tu hakukuwa na nafasi na Ile ndio iliyokuwepo"

Wakati tunaendelea maongezi Caryn akafika, mida hiyo ni ya jioni, amefika hata hajasalimia

Caryn: "BM Kwanini hujaja kazini Leo?"

BM: "Aah nilikuwa na Mzee leo ndio tumerudi tu muda sio mrefu"

Caryn: "You can't be serious, nikajua unaumwa kumbe ulikuwa katika mishe zako!"

BM: "Nimekuambia nilikuwa na Mzee"

Caryn: "Hata kama ulikuwa na Rais, ulinipa taarifa?"

BM: "Sasa hata hivyo kulikuwa na ulazima gani wa Mimi kuja? maana najua hakuna kazi inayohitaji uwepo wangu pale"

Caryn: "Unajua wewe nilishakusoma kitambo sana, linapokuja swala la kazi unachukulia poa sana, hata juzi kwenye kikao nilikusema makusudi mbele ya watu kuhusiana na hii issue nikijua utachange.....sasa usije kabisa ofisini mpaka nitakapo kupigia simu"

Halafu huyoo akaelekea chumbani kwake

Michelle: "Ashavurugwa huyo huko alipotoka"

BM: "Aah atajua mwenyewe bhana, anamtisha nani sasa"

Michelle: "Mwenzako alichokiongea kamaanisha, we kwani bado hujamjua Caryn?

BM: "Aah uzuri nilikuwa na Mzee na Mzee mwenyewe anajua"

Michelle: "Sasa ukitaka usiharibu zaidi kwenye hii issue usiende kushtaki kwa Mzee kwasababu Dad hawezi kuingilia maamuzi ya Caryn namjua yule Mzee, na Caryn akijua tu umemshtaki atakukazia zaidi ili ku prove kwamba ana power"

BM: "Dah! nishakosa mood ya kuendelea kukaa hapa, kama vipi tutoke basi unisogeze sogeze na gari yako"

Michelle: "BM nimechoka, unajua nilianza kulala wewe na Mzee ndio mmeniamsha"

BM: "Twende bhana hata ukashangae shangae mlimani City"

Michelle: "Sasa mlimani City nikashangae Nini ambacho sijawahi kukiona? wewe sema tu unataka kwenda mlimani"

Akakubali akaenda kujiandaa Sasa alivyenda kumuaga Mzee nadhani Caryn alimsikia, Michelle akaja ameongozana na Caryn

Caryn: "Count me in guys kwenye hiyo Outing yenu, sijisikii kula chakula Cha nyumbani leo"

Michelle: "But sisi hatuendi kula"

Caryn: "Mnaenda Kufanya nini?"

Michelle: "Original request BM alitaka nimsindikize, kwenda mlimani ni idea tu ya kwenda ku buy buy time"

Caryn: "Ni sawa, wewe msindikize unayemsindikiza na wakati mki buy-time mm nakula"

Michelle: "Okay, let's go"

Tutatoka na (Audi) gari ya Michelle na Dereva alikuwa ni yeye mwenyewe Mimi nimekaa kushoto kwake mbele Caryn kakaa Back left yani nyuma yangu

Tukafika mlimani City tukaenda hadi kuku kuku wote tukajikuta tumeagiza chakula

Caryn: "Si mlisema hamli nyie?"

Michelle: "So ulitaka tukuangalie ukila, tumeamua tu kukusupport isingeleta picha nzuri kwenye mezani ya watatu mtu mmoja tu ndio anakula....au unasemaje BM"

BM: "Yeah, true"

Michelle: "BM"

BM: "Yes"

Michelle: "I feel like you want to say something but you're scared"

Hii sasa michoro, Michelle kaamua kunichoresha

BM: "Something to say? to who?"

Michelle: "Maybe to Caryn

Simu yangu ikaita katikati ya maongezi kucheki alikuwa ni Annie nikaenda kuongea pembeni kule parking kabisa, baada ya Dakika kama 4 nikarudi nikakuta mhudumu kaanza kuleta Cutlery kiashiria Cha kwamba msosi unakaribia kuja

Michelle: "So Madam, you hired my man yes I appreciate for that, but you put him into a cheaper position! really!?"

Caryn: "Unatakiwa Appreciate pia kwa hiyo kwa nafasi ambayo ameipata kwasababu nimefanya kama favor tu, nilikuwa na uwezo wa kumuweka mtu mwingine bila kuulizwa na yeyote"

Michelle: "Sawa, lakini kumbuka hata hizo favors unazoziongelea hata mimi nimekufanyia sana tu mdogo angu"

Caryn: "Niache nile tafadhali"

Msosi ukaja tukaufinya, tulivyomaliza kula tukaachana pale pale mlimani City, hiyo siku ilikuwa Jumamosi Jumatatu yake nikaingia job nilichelewa kama Dakika 20 ivi nikapita ofisini kwa Caryn kusaini ile kwanza hakutegemea

Caryn: "We vipi! kwani juzi hukunielewa?"

BM: "Nilikuelewa, Ina maana hadi Leo umemaindi?"

Caryn: "Narudia tena usije kazini hadi nitakapokupigia simu, kama mimi na wewe tunaheshimiana utanisikiliza ninachokiongea"

Nikaona mambo yasiwe mengi nikaondoka, ila nikawa nimemaindi yani kumbe Caryn ndio ana mambo ya kiduanzi hivi!

Nikarudi nyumbani, kesho yake Jumanne nikaenda kule manzese kwa kijana wa Buguruni anapojifunzia ufundi furniture nilikuwa nimewapa kazi ya kunitengenezea kitanda lakini nilitaka Kijana wa Buguruni ndio akitengeneze mwenyewe chini ya uangalizi wa mwalimu wake ili kumpima kama amekwiva?

Basi nilivyofika manzese nikakuta Bed ndio inapigwa polish, na kufanyiwa finishing hiyo siku niliimalizia pale manzese jioni mida ya saa 11 jioni nikarudi zangu home, kwa kifupi kijana amekwiva maana kitanda amekitoa fresh.

Sasa katika siku ambayo nilikuwa nategemea simu ya Caryn ni leo lakini simu haijaita kwasababu ndio siku ambayo huwa naenda Zanzibar, Yani nisipoenda Jumatatu basi nitaenda Jumanne halafu usiku wa Jumanne nageuza na mizigo Asubuhi ya Jumatano inanikutia Bandarini

Kwahiyo kama hadi sasa hivi simu haijaita hiyo ina maanisha kwamba kuna mtu mwingine ndio ameenda kufuata mizigo sio! atakuwa ni nani? hapo ndio sijui

Jumatano Asubuhi nikiwa nawaza niende wapi, Nikapata wazo la kumcheki Michelle, nikampigia simu akanambia yupo job nikamuibukia,

Uzuri wa Michelle ha complicate mambo office hours unaweza ukapiga nae story fresh tu lakini sio kwa Caryn

BM: "Nikajua utakuwa umeenda site"

Michelle: "Hapana leo sio siku ya kwenda site, vipi ww hujaenda kazini kwani?"

BM: "Mdogo wako si ndio kashaamua, me nikajua Ile siku anazingua tu kumbe alikuwa serious"

Michelle: "Ooh dah nilisahau, lakini nilikuambia kwamba Mwenzako yupo serious...lakini nyie watu huwa mnanishangaza sana"

BM: "Kwanini?"

Michelle: "Anyways acha nisifikirie vitu ambavyo pengine hata havipo, ila ngoja me nitaongea nae japokuwa najua kwasasa ww unammudu Caryn ila Hujataka tu kuongea nae vizuri"

BM: "Achana nae bhana, vipi Shemeji yangu hajambo?"

Michelle: "Hajambo, mzima kabisa wa afya"

BM: "Ooh nice, ila muambie asichelewe kuleta Mahali kwasababu watu wanaokutaka ni wengi"

Michelle: "Nilienae ananifaa kwakweli, labda aamue kuniacha yeye"

BM: "Ivi mshkaji anakupenda kama wewe unavyompenda?

Michelle: "BM Ebu niache, naona umeishiwa na story"

Nilivyoona hayupo interested kuendelea kumuongelea jamaa wake nikachange topic tukaendelea na story baada ya muda kidogo akapokea simu kwamba kuna mgeni anamsubiri ikabidi nimuache maana mgeni mwenyewe alikuwa ni wa kiofisi zaidi

Ikafika weekend siku ya Jumapili nimemaliza kufanya usafi

(Kuna mtu aliniambia eti jumapili sio siku ya kufanya usafi, nitafute Hela)

Sasa nimetulia zangu sina hili Wala lile simu ikaita kucheki ni Accountant anapiga

Accountant: [emoji338]"Vip Boss unaumwa na hausemi!"

BM: "We nani kwakuambia kama mimi naumwa"

Accountant: "Si kaniambia Boss wako sijui Demu wako, mnapendana wenyewe hadi mkiumwa mafua tu mnapeana off"

BM: "Sijaelewa madhumuni ya hii simu yako, umenipigia kunijulia hali au kuninanga?"

Accountant: "A na B yote majibu, halafu nikuulize huyu mtu wenu mmemtoa wapi?"

BM: "Mtu gani?"

Accountant: "Si huyu Mfanyakazi wenu mpya"

BM: "Nani? Opportunist au?" (Nilimtaja kwa Jina lake halisi)

Accountant: "Mm sitaki kujua anaitwa nani, ila mwambie aache mazoea na mimi"

BM: "Haya kafanyaje tena?"

Accountant: "We nishakuambia muambie aache mazoea na mimi"[emoji3513]

Moja kwa moja nikawa nishaelewa kwamba Opportunist atakuwa alijaribu kuchapa verse na kwa bahati mbaya verse zikadunda kwa Accountant,

Ila sikushangaa sana ni kawaida yetu sisi wanaume ila jambo lililonishangaza ni hili la Caryn kuwaambia watu kuwa naumwa akati kanipiga stop kwenda kazini

Nikampigia Michelle kumpeleleza maana aliniambia ataongea na ndugu yake kuhusu mimi

BM: [emoji338]"Mambo"

Michelle: "Poa, nambie BM"

BM: "Vip uliongea na hako ka Boss lady?"

Michelle: "Yeah, niliongea nae lakini kaniambia mambo yenu nisiyaingilie mtamalizana wenyewe"

BM: "Ooh"

Michelle: "Kwani wewe hukuongea nae tena?"

BM: "Sikumtafuta mimi tangu nilipotoka ofisini Ile siku"

Michelle: "Tatizo wewe sijui unamuogopa, au unavimba? unamvimbia Boss? shauri yako, mtafute ametoka hapa muda sio mrefu"

BM: "Sawa"[emoji3513]

Nilivyokata simu ya Michelle nikampandia hewani Caryn

BM: [emoji338]"Hello...Mambo"

Caryn: "Poa"

BM: "Vipi uko wapi"

Caryn: "Niko town, sema una shida gani"

BM: "Nimekumiss, nilikuwa nataka nikuone"

Caryn: "Niko busy kidgo kwasasa nitakutafuta mwenyewe"[emoji3513]

Imefika majira kama ya saa Tisa alasiri kweli Caryn akanipigia simu akanambia anakuja mjengoni Uzuri nilikuwa mtaani tu maeneo karibu na nyumbani,

Nikarudi home fasta nikafanya usafi kwa mara nyingine tena, nikabadilisha hadi mapazia yale aliyoyasema kwamba ni ya kichaga

Nika make sure kila kitu kipo sawa, after one hour ivi nikamsikia mtu anabisha hodi, kufungua mlango kumbe ni Caryn

BM: "Kwani haukuja na Gari?"

Caryn: "Nimekuja nalo nimelipaki nje hapo"

BM: "Kwanini sasa?"

Caryn: "Acha tu likae huko si kuna usalama pia au?"

BM: "Yeah, usalama upo"

Caryn: "Nisaidie na Maji please"

Nikaenda jikoni kumchukulia Maji nikamletea alivyomaliza kunywa kama kawaida yake akaanza na swali

Caryn: "BM Ivi una side hustle nyingine unafanya au unategemea tu kazi moja kukuingizia pesa"

BM: "Kwasasa nina kazi moja tu, vipi kwani?"

Caryn: "Hiyo kazi moja ni ipi sasa?"

BM: "Si ya pale ofisini"

Caryn: "Sasa mbona huichukulii serious, kama ndio kazi pekee unayoitegemea?"

BM: "Sijajua Sasa ww kwa upande wako ili mtu awe serious na kazi unataka aweje"

Caryn: "Halafu ivi unajua kama una dharau? sijui kwasababu tumezoeana sana, I don't know ila unadharau aise"

BM: "Dah! labda ni kweli siwezi jua"

Caryn: "Ndio ujue sasa, labda nikuulize kama wewe ndio ungekuwa katika nafasi yangu halafu mtu anajiamulia kutokuja kazi na hatoi hata taarifa, wewe kama wewe ungechukua uamuzi gani juu ya huyo mtu"

BM: "Kiukweli sijajua ningechukua hatua gani kwa kitu ambacho ni Assumption hadi hiyo circumstance ini face ndio ningejua nini Cha kufanya"

Caryn: "Ooh nice, jibu zuri sana...Mimi maamuzi niliyoyachukua nilikusimamisha kazi, unajua ni kwanini nilikusimamisha kazi?"

BM: "Hapana, sifahamu"

Caryn: "Pengine ulikuwa na mentality ya kwamba bila ya wewe mambo hayataenda pale ofisini, so niliamua kukusimamisha makusudi ili kukuonesha kwamba bila ya uwepo wako mambo yanaweza kwenda tena vizuri tu"

Caryn: "We unadhani kwanini nilitaka kwenda na wewe Zanzibar? Kama ulikuwa hujui mimi nilienda kule kwa ajili ya kutengeneza Back up, kila ninachokifanya mimi lazima niwe na Backup plan"

Dah! sikuwaza hili Jambo, Aisee kumbe Ile trip ya Zenji niliyoenda na Caryn kumbe mwenzangu alienda kutengeneza network yake, so kwenye Ile trip alijuana na maagent na maafisa wa TRA, hadi ZBS kote huko mawasiliano anayo, Yani Dah niliishiwa nguvu nyie nikakosa hata cha kuongea

Caryn: "Halafu mm najua kama unaiibia Kampuni ila nilijifanya mjinga nikatulia, kona zote unazopita mimi nazijua, kama utabisha mimi ushahidi ninao"


Itaendelea
Mzee akaniambia

Mzee: "Ivi ulianza kile nilichokuagiza?"

BM: "Yeah" (ilibidi nimdanganye)

Mzee: "Jitahidi, watoto wa kike hawa sio wa kuwaamini sana hasa huyu Michelle"

BM: "Sawa Mzee nimekuelewa"

Naomba ukumbushie hapa, ni maagizo gani?
 
Mzee akaniambia

Mzee: "Ivi ulianza kile nilichokuagiza?"

BM: "Yeah" (ilibidi nimdanganye)

Mzee: "Jitahidi, watoto wa kike hawa sio wa kuwaamini sana hasa huyu Michelle"

BM: "Sawa Mzee nimekuelewa"

Naomba ukumbushie hapa, ni maagizo gani?
Hayo maagizo sikuyaweka wazi ila episodes zijazo nitaelezea

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee akaniambia

Mzee: "Ivi ulianza kile nilichokuagiza?"

BM: "Yeah" (ilibidi nimdanganye)

Mzee: "Jitahidi, watoto wa kike hawa sio wa kuwaamini sana hasa huyu Michelle"

BM: "Sawa Mzee nimekuelewa"

Naomba ukumbushie hapa, ni maagizo gani?
Mzee anataka either kijua anapokaa Careen au mtu wa Careen. Kaa humo
 
Nilishamtoa hofu baada ya kumuambia sasa hivi Accountant sio incharge tena

Uzuri ni kwamba yupo mbali so hamjui Incharge wa sasa hivi, na akija kumjua sijui itakuwaje

Ivi unajua kama Caryn naishi nae lakini as a Housemate
Bro kula mali safi hiyo
 
EPISODE 01, SEASON 01

Wakuu nahitaji ushauri wenu ili niweze kufaulu katika huu mtihani, nimepewa kazi kubwa ambayo nikifaulu basi milango mingi itafunguka huko mbeleni.

Kuna Mzee flani huwa tunashirikiana kikazi na mara nyingi mizigo yake huwa anaiagiza kupitia Kampuni yetu, ni Mfanyabiashara na ameanza Biashara miaka ya 90s alivyomaliza tu O level, Sasa huyu Mzee kijana (1971) huwa tunaongeaga mambo mengi kuhusu Biashara huku nikitaka anipe miongozo ili na mimi nielekeze nguvu na akili huko

Huyu Mzee akijaga Ofisini ni lazima nionane nae japokuwa muda mwingi Mimi huwa nakuwa nje ya ofisi kutokana na majukumu yangu mengi si ya kufanyia Ofisini nimesema ni lazima nionane nae ni kwasababu zangu Binafsi na si za kiofisi, Huyu Mzee ndio ameni inspire mm kutaka kufanya Biashara si kimafanikio tu bali hata lifestyle yake, Yani kifupi ana enjoy mafanikio yake anafanya kazi huku amerelax nyakati za kujituma usiku na mchana kwake zilishapita, sio kama wazee wengine wenye Utajiri lakini Bado anajitesa siku nzima kama yeye ndio kaajiriwa jambo ambalo ni tofauti kwa huyu mzee, huwezi kujua ratiba yake muda wowote yupo Ofisini na muda wowote pia anaweza akawa nyumbani, Ni siku ya Ijumaa tu ndio Najua kwamba haendagi ofisini kwake labda kuwe na jambo muhimu sana ambalo linahitaji uwepo wake.

Sio mtu wa mitandao sana hasa kama hii Jf pengine hata haijui, Kuna siku nilimuuliza kuhusu mitandao akanambia anatumia Twitter na Whatsapp tu, so hii story Najua itakua ngumu kwake kuiona, maana hata kwa codes nitakazoweka kama akiiona atajua tu ni Mimi na ndio mchongo mzima utaishia hapo

Sasa nikibahatikaga kukaa na huyu Mzee mtu mbili huwa namuonesha shauku ya mimi kutaka kufanya biashara lakini kila nikimgusia swala hilo ni kama anaona sipo serious, anahisi nataka kufanya biashara kwa kufuata mkumbo tu, Kwasababu nakumbuka aliniuliza nataka kufanya Biashara gani mimi nikamwambia nataka kufanya Biashara kama ya kwake, aliishia kucheka tu

Nakumbuka siku moja nimetoka Zanzibar kupokea mizigo ya ofisi ya wateja, nimefika Dar Huyu Mzee akanipigia simu kuniomba kwamba mzigo wake nisiupeleke store Bali niende nao Ofisini kwetu ili nikitoka kazi nimpitishie kwake, na ndio ilikuwa mara ya kwanza kufika kwa huyu Mzee, Asee vile nilivyokuwa namdhania ni robo yake, Kuna watu wanaishi acheni nyie

Basi Mzee alinikaribisha vizuri sana mjengoni mjengo mjengo kweli! Wakati naingia kwenye Parking sijaona Gari yake niliozoea kumuona nayo siku zote (Land Cruiser ZX V8) nilimkabidhi vitu vyake Mzee akapanda juu Nadhani ni Bedroom kwake alivyorudi akanipeleka Backyard tukakaa, Sasa tulivyokuwa mule ndani sikuona mtu mwingine yeyote ikabidi nimuulize Mzee nyumba yote hii unaishi peke yako? akanambia "hapana mabinti zangu na Mama yao wameenda Kibaha watarudi Jumapili" (Siku hiyo ilikuwa Ijumaa)

Story zikaendelea pale Mzee akanambia "Kijana wangu nilikuambia uniletee mzigo kwa makusudi, mm kila Ijumaa huwa na utaratibu wa kupata chakula Cha jioni na familia yangu ya ndani na ya nje hivyo nilitaka na wewe uwepo" alivyosema familia ya nje niliwaza mbali, nikamuuliza kwani Mzee wewe una wake wa ngapi? kabla hajajibu alitabasamu "mmoja tu na Najua umeuliza hivyo kwasababu gani, nilivyosema familia ya nje nilimaanisha watoto wa mitaani ambao hawana makazi maalum, kwahiyo badae tutatoka kwenda kuwachukua" nikasema sawa ni jambo zuri Mzee

Wakati tumekaa na kuendelea na story Mzee akanambia kama nitataka kunywa chochote niende kwenye fridge nijihudumie, Nikamwambia haina shida, Mara ghafla Mzee akapokea simu Wakati anazidi kuongea akachange ni kama kapokea Taarifa mbaya, yule Mzee aliinuka pale alipokuwa amekaa akiwa bado anaongea na simu huku akiingia ndani, alivyotoka alikuwa kashika funguo mkononi akanambia "Kijana wangu nimepata dharula itabidi nikuache kidogo ila nitajitahidi niwahi kurudi ili tufanye lile jambo nililokuambia, in case of anything utanipigia simu" Nikamwambia sawa Mzee

Tukatoka kule backyard hadi Parking pale kulikuwa na Magari mawili ambayo sikuwahi kumuona nayo akaingia kwenye Jeep, Yale majeep yenye muundo kama wa Benz G Wagon, Mzee alifungua geti na Remote control akasepa, Mtu mzima nikachoma ndani, nikajiachia kwenye Sofa huku nikiperuzi, Giza likaanza kuingia na saa Ile Mzee anaondoka ilikuwa ni around saa kumi jioni.

Simu ikaita, kucheki ni Mzee, akanambia "Kijana wangu ni kama nitachelewa kurudi Sasa wewe Fanya hivi, umeiona hiyo gari hapo parking?" nikamjibu ndio "Sasa panda juu mkono wa kulia chumba Cha mwisho fungua mlango ingia ndani nenda hadi kwenye dressing table utakuta funguo ya Gari ichukue, si unajua kuendesha gari?" nikamwambia ndio lakini Sina leseni Mzee "Wachana na mambo ya leseni, kwani Driving licence ndio inaendesha gari? Sasa si umesema unajua ku drive, nenda jikoni kachukue hicho chakula pakia kwenye gari wapelekee wenye uhitaji sababu ninaweza nisirudi halafu hicho chakula kikaharibika" nikamjibu sawa Mzee akakata simu

Nikawa najiuliza pa kwenda kuwapata hao watoto, Basi bhana Mimi nikapanda juu kuchukua funguo ya Gari, nikazama hadi chumbani asee ni noma, Chumba kama sebule nikawa sielewi dressing table Iko wapi, kilichonisaidia ni kioo, nilivyoona kioo nikajua tu hii ndio yenyewe hadi kesho sijaelewa Ile dressing table imetengenezwaje, kweli nikakuta funguo pale juu Ile kupiga jicho pembeni nikakuta maburungutu ya pesa elfu tano tano, hata sijayagusa maana nilijua nyumba kama Ile haiwezi kukosa CCTV camera, me nikabeba funguo kikashuka chini hadi jikoni nikakuta mahotpot yana msosi wa kutosha (Wali njegere maini) nikayabeba hadi kwenye Gari (Alphard) nikarudi jikoni kucheck sahani zote za dongo nikaachana nazo nikarudi kwenye Gari nikafungua Geti nikasepa ila sasa nimetoka na sijui naelekea wapi nikicheki saa ni saa moja kasoro, nikaenda hadi Mwenge, nikapark kando ya Barabara nikawa nawaza hao watoto nitawapata wapi, mawazo yakaja niende kwa sister angu flani anakaa uswahilini huko ndiko nikagawe hiki chakula, nikapiga mahesabu ya masaa nitakayo tumia hadi kufika huko muda utakuwa umeenda hata hivyo nitakuta watoto wengi wapo majumbani mwao na watakuwa washakula nikaona nikifosi kufanya hivyo nitaendelea kuipa nguvu ile kauli ya "mwenye nacho huongezewa"

Nikatoka pale Mwenge nikaenda Buguruni, nimepitia Ile footbridge na Mataa nikaingia Barabara ya kama naelekea Ilala, sijafika hata mbali nikapark pembeni kusikilizia, sijakaa sana nikaona madogo wawili nikawasimamisha Nikawauliza wanapoishi hawakunijibu, nilivyoona hivyo sikutaka story nyingi tena niwaambia ninachakula nataka niwapatie lakini nyie wawili hamtakimaliza mnaweza kuwaita na wenzenu? mmoja akaniuliza "kiko wapi hiko chakula chenyewe?" nyie kawaiteni wenzenu mkija mtakiona chakula, nitawaambia hivyo wakaondoka nikakaa kama Dakika 8 nikaona wale madogo wanakuja na rundo la madogo wenzao nikajisemea Leo kazi ipo maana kwa Ile idadi niliyoiona ya wale watoto na nikipiga mahesabu ya kile chakula nilichobeba ni kama hakitatosha kabisa halafu saa hiyo hiyo nikakumbuka nilibeba tu chakula na sikubeba sahani nilipanga nipitie supermarket ninunue zile sahani za karatasi nikasahau

Madogo wakafika hadi kwenye gari, nikawauliza mgahawa wa karibu uko wapi?wakanionesha lengo nikwenda kununua chakula ili niongezee na hapo hapo nitapata sahani za kutumia kwasababu kwa kile chakula kilichopo kinatoshea kwa watu kama 9 ivi na kile kikosi Cha madogo 15 wamefika, nikalock gari nikawaacha madogo pale kwenye gari nikavuka Barabara hadi upande wa pili nikaulizia chakula nikaambiwa kipo, saa hyo ni saa 2 usiku na madakika yake, Nikwambia Mama ntilie nataka chakula Cha watu kama kumi, Yani sahani kumi za wali, akanipakulia akaniwekea kwenye ndoo, nikatumia ujanja wa kumwambia kila sahani ifunike ili chakula kisipoe ili nipate sahani excess, alivyomaliza nikampatia 20k Nikamwambia siendi mbali sana sahani nitakuletea mwenyewe, akakubali bila wasi na sijui kwanini aliniamini kiwepesi vile

Nikafika kwa madogo nikafungua gari nikatoa Yale mahotpot ujinga mwingine ambao niliufanya sikubeba vijiko vya kupakulia na kule kwa Mama ntilie sikuchukua Maji ya kunawa, Sasa ule msosi wa Kwenye hotspots nikaupakua kwa kutumia sahani nikakigawa kile chakula wengine ilibidi wale wali wa mama ntilie na baadhi yao wakala ule niliokuja nao ila ngegere na maini nilizigawanya katika Kila sahani, sasa nikawa nawauliza madogo mtanawa wapi mikono?, dogo mmoja akasema blaza haina haja mikono yetu misafi[emoji3] basi nikawaruhusu wafinye msosi na mm nikichukia sahani moja, walivyomaliza Nikaingiza mahotpot kwenye gari nikalock nikamchukua dogo mmoja Nikamwambia abebe ndoo yenye sahani anifuate wale wengine niliwaambia watusubiri, tukaenda hadi kwa mama ntilie nikampatia sahani zake akanirudishia balance yangu elfu 5, nikamuomba chenchi ya elfu 10 buku buku, akanipatia, tukarudi hadi kwenye gari na yule dogo, Nikawaambia Sasa Mimi na nyie tushamaliza nikampatia Kila mmoja buku buku angalau kesho Asubuhi wawe na uhakika nikaagana nao pale nikasepa, Wakati nipo Njiani nikampigia Mzee kumjulisha kwamba nishafanya kile alichoniagiza akanambia "sawa Sasa wewe unaweza kwenda na hilo gari kesho utalileta nyumbani, si ulifunga vizuri nyumba?" aliniuliza Nikamwambia ndio na funguo Niko nazo, "Haina shida ww unaweza kwenda kupumzika Sasa" okay Mzee, Sasa wakati huo naongea nae kwenye simu Mimi nilikuwa nishapita Ubungo Interchange naitafuta Mwenge, nikielenda nyumbani kwake, ilibidi nigeuze gari nilirudi nilikotoka sababu mm naishi Tabata, Yani kama ningewahi kumpigia simu basi nisingejisumbua kufika mbali kote huko

Kwa mara ya kwanza nafika mtaani kwangu na Gari, siku zote Mimi niwakufungua kale kageti kadogo Leo nafungua Geti lote kubwa ili kuingiza ndinga, maana nilipopanga tunakaa watu 3 nyumba zinajitegemea ila tunashea Compaund, nikapark gari nikaingia ndani kulala, kukakucha, Jumamosi mara nyingi huwa siendagi ofisini labda itokee naenda Zanzibar, so nikawa Sina ratiba ndefu nikafua nguo kadhaa nikaingia mtaani kupiga chai, nilivyomaliza nikarudi home direct nikakuta missed call ya Mzee maana nilivyotoka simu niliiacha, nikampigia akanipa maelekezo fulani pale ya kwamba atarudi Jumapili Pamoja na familia yake hivyo kama Nina muda nilipeleke Gari kule nyumbani au nibaki nalo hadi Jumatatu aje alichukulie Ofisini, nikamjibu sawa yote yanawezekana ila acha niangalie lipi litakuwa rahisi zaidi

Baada ya kukata simu nikapiga hesabu kurudisha hili Gari hadi kule mwisho wa mji, nikaona uvivu isitoshe gari lenyewe lilikuwa rafu mavombo machafu humo ndani, Yani ukifungua mlango wa gari Gari lote linanuka wali, nikatoa vyombo vyote, nikajikaza kuviosha hakuna Kitu kinanikera kama kuosha vyombo ndio maana huwa sipikagi mara kwa mara. nilivyomalizana na hiyo Kero nikalipeleka Gari Car Wash nikalirudisha kulipark home, hamuwezi amini nilishinda ndani hiyo weekend yote hadi inaisha na Gari limepark tu uwani

Jumatatu hii hapa, Asubuhi na mapema nikawa najianda kwenda kazini, Nikaingiza vile vyombo kwenye gari ila Sasa nikawa nawaza hao police huko Barabara kwasababu Sina Driving licence, nikasema potelea mbali nikatekenya mchuma hadi kazini nikalipark kimya kimya kama sio Mimi nikaingia Ofisini kwaajili ya kuchapa kazi

Imefika Lunch time najiandaa kwenda kupiga Menu yule Mzee nikamuona anaingia Ofisini halafu ana hasira amekunja sura, nikajisemea hapa kimeshanuka nikaanza ku recall matukio ili nijue ni wapi nimekosea hasa kule nyumbani kwake, kote nilicheza safe na mara ya mwisho kuongea na huyu Mzee ilikuwa ni Ile Jumamosi akinipa mabadiliko ya ratiba yake huku akinipatia option mbili za yeye kupata gari yake, na Mimi nilivyochagua kubaki na Gari hadi Jumatatu sikumpigia tena simu kumjulisha uamuzi niliouchukua....nikapata majibu kwamba inawezekana hapo ndipo nilipo haribu, alikuja kwenye desk langu na kuniambia "nipatie funguo ya Gari na ukimaliza kazi nitafute" hata hakunisalimia akatoka nje ya ofisi akaondoka....

Inaendelea badae acha nipate msosi.....story yangu ina episode 6 tu, episode ya kwanza na ya mwisho (1 & 6) ndio muhimu zaidi Sababu ushauri wako ndio unahitajika hapo

1. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

2. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

3. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

4. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

5. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

6. Muendelezo Soma Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni
The story is good, but I always ask myself' is this fiction or none fiction story maana unavoelezea, kwanza najiuliza unawezaje kukumbuka visa vidogo vidogo haswa Kwa matukio yaliyopita! Hata hata dialogue umekumbuka umeandika as if ulikuwa unatembea na daftari na peni Kila siku unaandika yanayoendelea Kwa wakati huo! Kwa akili yangu mm nimeona hii ni story ya kutungwa! Yaan Mzee ulikaa ukafikiria sana mwisho wa siku ukaandika story in an organised way
 
The story is good, but I always ask myself' is this fiction or none fiction story maana unavoelezea, kwanza najiuliza unawezaje kukumbuka visa vidogo vidogo haswa Kwa matukio yaliyopita! Hata hata dialogue umekumbuka umeandika as if ulikuwa unatembea na daftari na peni Kila siku unaandika yanayoendelea Kwa wakati huo! Kwa akili yangu mm nimeona hii ni story ya kutungwa! Yaan Mzee ulikaa ukafikiria sana mwisho wa siku ukaandika story in an organised way
Ni true story na matukio sio ya kitambo sana, ni ya miezi 3 nyuma

Na kuhusu kukumbuka siandiki popote labda ninapokuwa naongea na Mzee zile Conversation huwa narekodi kwenye simu bila yeye kujua lakini, maana najua huwa anatema nondo japokuwa sio mara zote nafanya hivyo,

Halafu pia kuhusu kusahau mbona nasahau sana tu maana kuna sehemu nyingi sana sijaziandika, na mara nyingine unakuta baadhi ya sehemu nazikumbuka nikiwa nishapost episode yenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom