Ilipoishia
Pia katika maongezi Mzee akaniambia kuwa kwa vile ahadi za kuja kupaona kwangu zimekuwa nyingi bila mafanikio akaniahidi na kunihakikishia atakuja siku ya Pasaka kula sikukuu kwasababu siku hiyo Bi Mkubwa Yani mke wake atakuwa yupo mkoani
Hivyo Ukiachana na Annie, Mzee pia ameingia kwenye list yangu ya wageni nitakao wapokea siku ya Pasaka japokuwa Annie alisema atakuja before Pasaka
Muendelezo
(Episode 24, SEASON 2)
Hii siku nilivyorudi nyumbani nikamjulisha Caryn kuhusu Mchina (Hili Jina kalitoa member wa hapa Jf wakuitwa [emoji1542]Tajiri Kichwa) Mchina ni huyu jamaa ninayemfanyia Mpango wa kwenda China, basi nikamuambia kwamba jamaa inabidi awe anakuja ofisini pale akiwa anasubiria process za visa zianze kufanyika
Caryn: "Ofisini anakuja kama nani? na kufanyaje? majukumu yake yeye si ni huko China"
BM: "Anakuja kwa lengo la kujifunza ili akifika kule (china) at least awe anajua baadhi ya mambo"
Caryn: "Wewe ni nani aliyekuambia sisi tunaajili wanafunzi wa kuja kujifunza kazi"
BM: "Aysee, hii sio amri yangu, ni kutoka kwa Mzee"
Caryn: "Na mm ndio nakuambia hatuajiri wanafunzi, tafuteni mtu mwenye Experience"
BM: "Kama ni hivyo acha niende mwenyewe"
Caryn: "Unajua BM unapenda sana kufanya vitu kwa mazoea, hii tabia hata Dad anayo"
BM: "Hiyo tabia ya mazoea unayoiana kama ni kasoro ndio imemfikisha Mzee pale alipo"
Caryn: "Back then, kwasasa huwezi kutoboa ukiwa una apply hiyo tabia mara kwa mara"
BM: "Tatizo lako unapenda ku complicate sana mambo... anyways kwa uchache wa siku zilizobaki according to Mzee, ni Either Mimi au Jamaa"
Caryn: "What's for dinner?"
BM: "Hujaniambia msimamo wako kama ni Mimi au Mchina, kama ni Mchina nimuambie Jumatatu aanze kuja job"
Caryn: "How does that answer my dinner question"
Caryn bhana, ukiwa unabishana nae kuhusu kitu fulani na ghafla ukaona ame switch topic basi ujue ameshakubaliana na wewe, hawezi ku admit directly, ikitokea basi ni mara chache sana.
Jumatatu ya mwisho ya mwezi wa 3, nakumbuka ilikuwa date 27 kama sikosea Mchina ndio alianza kuja pale ofisini, kabla hajaja nilimpanga kabisa kuwa mtu anayekuja ku-Deal nae ni kichefu chefu so ajue namna ya kuishi nae coz akisema NO basi ujue ni NO kweli hadi Mzee anaipitisha ila kwa Mzee anaweza kukutamkia YES lakini kwa Caryn ikawa NO na Mzee akabadilisha YES yake kuwa NO kwa Caryn
Yani nilichokuwa najaribu kumuambia Mchina ni kwamba katika kuruka ruka kwake kote awe makini tu asimkanyage Caryn kwasababu ndio mambo yote, ukijua kwenda nae sawa mambo yana floo yenyewe
Mchina nikampeleka Ofisini kwa Caryn kumtambulisha, baada ya kutambuana Caryn akaanza kumfanyia Oral interview
Caryn: "Okay, tell me have you ever exported....I mean What experience do you have in exportation of goods"
Mchina: "No, I don't have any, I'm looking forward to gain some here"
Caryn: "Impressive! I really like straight forward guy like you"
Caryn baada ya kumaliza kumuulizia Mchina maswali ya yanayohusiana na kazi akaanza na Personal questions
Caryn: "Una familia?"
Mchina: "Ndio ninayo"
Caryn: "Una watoto wangapi? na uliezaa nae bado unaishi nae?"
Mchina: "Sina mtoto, kwa kifupi sijaoa"
Caryn: "Kwanini ulijibu Ndio kwenye swali langu"
Mchina: "Nilidhani una maanisha familia ya Baba, Mama na ndugu niliozaliwa nao"
Caryn: "Hiyo sio familia yako, ni familia ya Baba yako na Mama yako"
Caryn: "Wewe na BM mna muda gani tangu mfahamiane?"
Mchina: "Karibia Mwaka sasa"
Càryn: "Be specific"
Mchina: "Ni ngumu kukumbuka siku tuliyofahamiana, so I can't be specific"
Caryn: "Wow, this is the level of confidence and boldness we want to see moving forward...anyways kesho utaniletea Barua mbili za udhamini"
Kusikia hivyo nikajua 'hapa mchezo ushaisha' tulivyotoka nje nikamuambia Mchina "Mwanangu kumbe unaweza kuwa kauzu"
Mchina: "Oya, unajua ulivyoniambia tabia za demu mwenyewe nikasema piga ua hata kama Sina Confidence nitakuwa nayo tu hata kama ni ya kuigiza"
BM: "Na kama ulimsoma, Kuna maswali alikuwa anakuuliza ili tu ujikanyage"
Mchina: "Ila unajua nini mwanangu, umetisha sana, sitakuangusha, Boss wako mm nitaenda nae anavyotaka tutarekebisha mbeleni, Ujanja sio kua bora, ujanja kupata"
Jioni yake wakati tupo nyumbani Caryn akawa kama Bado ana mashaka
Caryn: "BM yule jamaa ni rafiki yako kweli? I mean mnajuana vizuri?"
BM: "Ndio, kwani kuna tatizo?"
Caryn: "Nop, hakuna tatizo, anaonekana smart kiasi chake ila confidence inambeba"
BM: "Sawa sawa Mwana saikolojia"
Caryn: "Kebehi tu lakini naongea fact"
BM: "Uko sasa ni kujishtukia mm sijakebehi mtu"
Caryn: ".....wewe una uwezo mkubwa, you're smart ila ujasiri unakuangusha"
BM: "Hii sasa ni compliment au?"
Kwenye hii Convo nilikuwa namletea Caryn masihara mengi na utani wa kutosha, watu walivyoanza kusikia njaa ilibidi utani tuuweke pembeni
Caryn: "Bro, Body warms in my stomach are already screaming"
BM: "Sasa mm nifanyaje?"
Caryn: "It's your turn to cook today"
BM: "I'm not in the mood"
Caryn: "So you're in the mood to be hungry then"
BM: "Mimi nilishaji-sort (nilishakula)
Caryn: "BM you know this is not the first time you've doing this each time is your turn to cook you choose to eat out"
Caryn: Wait... you want me to do the cooking just for myself while you continue to eating out ... right? that's what you want?"
BM: "Hiyo pia si mbaya, mm nitarudi kwa nyumba nikiwa nimejipanga kabisa"
Nikaingia zangu chumbani, ukweli ni kwamba nilikuwa sijala ila nimemjibu tu vile kukwepa kukatakata vitunguu, Wakati naingia chumbani Caryn akaingia jikoni kukorofisha mambo,
Baada ya lisaa limoja kupita nikagongewa mlango eti chakula kimeiva naitwa nikale, nikaona kabisa huu ni mtego japokuwa nina njaa lakini nikavunga, nikamuambia we tangulia nakuja, hadi yeye anamaliza kula mimi sijatoka chumbani akanifuata tena akaniambia "BM chakula kinazidi kupoa, na hakuna Microwave kusema uta warm"
Sikwenda hata kula kwa kujishtukia, asubuhi naamka nimeingia jikoni kufuata ndizi (Kila asubuhi ni lazima Nile ndizi) nikakuta chakula alichoniwekea Caryn kakifunika na sahani kumbe msosi niliwekewa kweli ila kwa ego nikaamua kulala nayo
Wiki moja kabla ya Pasaka Annie akanicheki akaniambia Mpango wake wa kuja Dar unaweza usiwezekane kwasababu kuna mfanyakazi mwenzao amefiwa na Mama yake so kama huyo mfanyakazi mwenzake akiwahi kurudi kutoka mazishi ndio anaweza akaja na kama akichelewa itabidi tu Pasaka ailie huko huko Mwanza akisubiri safari ya mwezi wa sita
Hii ilikuwa Habari njema kwangu kwasababu mwanzo nilipanga uongo ambao sikuwa na uhakika kama Annie angeniamini au lah!
Hatimaye Pasaka ilifika lakini Annie hakufika Dar, ila Mzee yeye Alifika kwangu, alikuja mapema tu yale masaa ya breakfast but Mzee hanywagi chai, nikamuandalia kahawa, Wakati naendelea kunywa chai huku Mzee akipiga kahawa yake akauliza
Mzee: "Hapa unaishi mwenyewe?"
Unajua kuna swali mtu anauliza Kwa maana ya kwamba hajui kitu anataka umfahamishe, na kuna swali mtu anauliza kutaka kujua akili yako inaishia wapi kupitia majibu yako huku yeye tayari akiwa na majibu yake, ilibidi ninyooshe maelezo huku nikiwa na wasiwasi mno
BM: "Hapana, naishi na Caryn japokuwa mara nyingi huwa anakuwa kwa Dada yake"
Mzee: "Najua kama unaishi na Caryn, niambie kitu kipya ambacho sikifahamu"
BM: "Mzee mimi nilihisi unajua, kwakudhani Caryn alikuambia"
Mzee: "Hisia zako zipo sahihi, nilikuwa najua lakini kwa njia zangu mwenyewe hata huyo Caryn hajaniambia, hata hivyo wewe ndiye uliyepaswa uniambie, ukaribu wangu Mimi na wewe unashindwa kuniambia jambo nyeti kama hili kweli? unataka mimi nikufikiriaje, ivi ingetokea huyu Binti kakufia usiku na Mimi sifahamu kama yupo kwako unadhani Mama yake angekuelewa?"
BM: "Mzee kosa ni la kwangu naomba unisahame"
Mzee: "Unajua kuna makosa unaweza ukahisi ni madogo lakini yanavunja uaminifu kwa kiasi kikubwa sana"
Hiyo kauli ya Mzee ndio ikanimaliza nguvu, sasa namna alivyojua hii issue ndio nilichoka kabisa
Iko hivi, Mzee gari zake zote kazifunga tracker kasoro Gari ya mke wake, ninaposema Gari zake zote namaanisha hadi hizi za kina Caryn na Michelle, Sasa Ile siku ananipa Jeep mm nikijua narahisishiwa usafiri kumbe ule ulikuwa mtego,
Kwanini nasema mtego, ilikuwa hivi, Wakati Mimi naondoka Mzee alikaa chini na hiyo simu yake specific kwaajili ya hizo mambo, akaona Jeep lake hadi Mahali lilipo park, aliyekuja kuharibu ni Caryn maana Mzee anajua Caryn yupo kwa Michelle na atalala huko lakini baada ya muda akaona BMW limepark maeneo yale yale lilipopark Jeep
Hapo ndipo alipoanza kupata mashaka japokuwa tulimuambia sisi ni majirani lakini kupitia alichokiona yeye mwenyewe akawa kashajijazia kichwani kwake ni kitu gani kinaendelea
Baada ya Mzee kumaliza kunielezea kilichokuwa kinaendelea nyuma ya Pazia bila Mimi kujua Mzee akaniuliza swali
Mzee: "Nakumbuka ushawahi kuniambia kama una mchumba, na hiki ndio kipindi kizuri Cha kuishi nae ili mjuane vizuri kitabia lakini badala yake unaishi na Caryn, Kwani wewe na Caryn mna mpango gani?"
Hili swali ni muendelezo wa yale maswali ya Mzee ambayo anakuuliza ili kujua akili yako inapoishia na uwezo wako wa kufikiria, ila safari hii hajaniachia gepu la kumjibu, Wakati nataka kumjibu akaniambia kitu ambacho hadi kesho nakitafakari lakini nakosa majibu
Mzee: "Unajua...ngoja nikuambie kitu kijana wangu, kwenye huu ulimwengu ukitambua wenye manufaa maishani mwako usiwape umuhimu, hawatakuumiza*. Wenye umuhimu maishani mwako usiwafanye wenye manufaa, Utaumia"
Itaendelea