Hatma ya mradi Stiegler’s Gorge: Hatakama hatukubaliana kiitikadi, tukubaliane katika Ushauri wa kitaalam

Mada zako ni bora ila unakosea kuweka matangazo ya biashara! Kitabu tulishasoma na kila mtu anajuwa njia ya kukipata ebu leta mada bila kuwa na mlengo wa kibiashara Yeriko
Nilivyoanza kusoma Uzi huu, nikajua nitapata mawe makubwa,
Ghafla napelekwa kununua kitabu na hata bila ABC za alichotaka kutuambia leo.

Inaonekana Soko haliendi vizuri ameamua kuja kiaina ili kupromote soko la vitabu vyake.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuna Uhuru wa kuwafanya chochote wanyama wetu tukawala au tukawapiga kibiriti
Mpelekeni Selemani Nchambi tu mbona mnajifanya kumuhifadhi kelele ziiishe

Ili iwe Arabs contractors ya kwelikweli
 
Mimi Mimi niliahidi kikifika bei ya buku, ndio nitakinunua!
 
Hujambo ndugu, mengine hayana maana, naomba kidogo tuchombezi juu ya kisa cha bomba la gesi kuyeyuka.

Tanzania ilifanikisha kwa 💯, hili apongezwe Jasusi mkuu aliyeongoza vita Marehemu mzee Mahiga. Kenya walisanda kabisa.

Majasusi wa kimataifa kutoka USA, Ufaransa na Uchina wapigana vita wao kwa wao kupigania nani ajenge, nani asafirishe, na nani awe Sub-Contractor.

Mwenye tenda ya mradi alikuwa Mfaransa (Total), dili la kusafirisha akalishika USA, Sub Contractor akaidaka mchina, sasa vita vikaanzia hapo kwamba mchina kaingizwa na Mfaransa huku USA hajashirikishwa kumkubali. Hii inamaana kuwa USA alitaka alete mtu wake yule mjomba wale kutoka kutoka Cambridge. Mvutano ulipokuwa miubwa Mfaransa mwenye dili akasema sitoi mpunga na sijengi.... Hivyo sisi wengine tunasubiri wanyukane kisha mshindi tutajenga nae.... Tatizo ni je msindi atatoa hela?
 
Vitu vingine tunaandika humu naonaga ni delusions tu. Sioni role yoyote ya TISS kwenye huo mradi, kwa mfano TISS wamepambana na nani ili huo mradi uendelee au wameshauri nini.
Wataalam wa ndani na nje ya nchi waliandika na kusema huo mradi haufai, utaharibu mazingira na hata kuvuruga maisha ya watu downstream.
Global warming na uharibifu wa mazingira pia umeathiri kiwango cha maji kwenye mito mingi ikiwamo Rufiji.
Kimsingi huo mradi haufai, utaishia kuwa the only white elephant in Selous game reserve.
Halafu hapo ulipoandika realised documents nafikiri unamaanisha declassified documents. Tutaendelea kuelekezana taratibu jasusi Yericko Nyerere.
 
Mwenye Tenda ya mradi upi?

Kampuni inayozalisha gas nyingi inayosafirishwa ni kampuni ya Uingereza.

Aliyeshinda tenda ya kujenga bomba ni kampuni ya Kichina na kwa mkopo kutoka benki ya Exim ya China,bomba limejengwa na gesi inasafirishwa.

Hivyo visa vyako vya vita ya majasusi umevipata wapi kama sio stori za kutunga?
 
Huyu ni jasusi uchwara anayetumia ujinga wa wabongo wengi kujipatia kipato kwa kuuza vitabu anavyoandika kwa kukusanya stori uchwara za mitandaoni na kufanya hadaa kwamba ni mambo halisi ya kijasusi.
 
Labda sijui jambo hapa. Hizi pongezi kwa TISS zina maana gani huku ukimsifia Rais dhidi ya wenzake walioshindwa??

Tumechemka kwenye mtadi huu, tulipaswa kuutumia kama kigezo cha kuwalazimisha kufanya uwekezaji katika eneo lingine!! Tungeweza hata kupata umeme wa nyuklia. Iran na North Korea zimetumia vitu kadhaa kulazimisha haya mashirika ya kimataifa kufanya mambo kadhaa.

Ninadhani hukupaswa kupongeza TISS, ulipaswa kushauri vyombo vya serikali vitafute njia za kujadiliana ili kuwe na win-win situation. Katika swala la umeme, tunaonekana kama kuna zero sum!
 
Mkuu ninavyomjua jemedari wetu alivyojasiri wakigoma atawaweka wanajeshi wajenge! Piga kazi baba mabeberu hawawezi kukushinda.
 
Tutawasingizia mabeberu..bila wao mradi ungekamilika.

Wananchi watatuelewa.

Sent using iphone pro max
 
..tunahitaji umeme wa maji lakini siyo kwa style na utaratibu huu aliotumia bwana mkubwa.

..kwanza, mradi wa stieglers ni mkubwa sana, unatumia fedha nyingi, na muda mrefu kukamilika.

..pili, ni mradi ambao unatugombanisha na marafiki na wadau wetu wa maendeleo.

..kwa maoni yangu, serikali ilipaswa kujenga miradi ya ukubwa wa kati. Na miradi hiyo ijengwe ktk vyanzo ambavyo havina migogoro na wafadhili wetu.

..advantage ya hatua hiyo ingekuwa kuingiza umeme kwa awamu bila kusuburi muda mrefu kama tunavyofanya kwenye mradi wa stieglers. Pia tusingekuwa na ugomvi na marafiki na wafadhili wetu. Zaidi tungekuwa na fedha za kugharamia miradi mingine muhimu kama viwanda, kilimo cha umwagiliaji, etc etc.

..Stieglers inatumia fedha nyingi, na imesababisha miradi mingine muhimu ikose fedha. Waswahili wana msemo kuwa " tumeweka mayai yote ktk kikapu kimoja ."
 
Unajua gesi ipi inayoongelewa ni liquified natural gas project likong'o na mchinga, sio iko kibomba Cha hapo kinyerezezi, usijifanye mjuaji alafu hujui vitu
 
'iko kibomba Cha hapo kinyerezezi' kinatoa gesi gani,kutoka wapi kwenda wapi?
Unajua gesi ipi inayoongelewa ni liquified natural gas project likong'o na mchinga, sio iko kibomba Cha hapo kinyerezezi, usijifanye mjuaji alafu hujui vitu
 
'iko kibomba Cha hapo kinyerezezi' kinatoa gesi gani,kutoka wapi kwenda wapi?
Tofauti kinyerezi na mradi wa likongo na mchinga ni miradi miwili tofauti, usipende lig kwa mambo ambayo yako wazi utaonekana mjinga
 
Kati ya miradi inayothibitisha ujinga wa serikali yetu ni pamoja na huu wa umeme...
Huu mradi una madhara makubwa sana siku zijazo kuliko Covid-19...
Najua wengi hawajui thamani ya mazingira... Na wengi zaidi hawajui madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabia ya nchi...
Majuzi hapa si mlishuhudia mafuriko yaliyodumu wiki kadhaa kule RUMAKI na kule Mikumi? Basi ile ni trela... Majanga yajayo yanatisha....!!
Kifupi tu ni kuwa mtu yeyote mwenye akili timamu hawezi kuunga mkono ujenzi wa hilo bwawa...!!
Mwana kulitafuta.... Mwanakulipata!!
 
Kazi ipo!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…