Hatma ya mradi Stiegler’s Gorge: Hatakama hatukubaliana kiitikadi, tukubaliane katika Ushauri wa kitaalam

Nchi yetu ,mradi wetu,fedha zetu , halafu tugombane na washirika wa maendeleo?,huo ni ukoloni wa wazi kabisa.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona mwenye mikosi yuko wazi na hata wewe mwenyewe wamjua?? Wewe ndege zako unazifungia uwani inakwenda kuwapa tenda majirani zako kama sio mikosi inamuandama ni nini?? Au ulifikiri hakupenda kupeperusha twiga wake??

Yuko anajaribu kuoga na maji ya chumvi ziwani kutwa mara tatu labda yaweza kutowesha mikosi.

Mkuu ukibarikiwa umebarikiwa na ukilaaniwa umelaaniwa. Kila mtu utamuona ni adui. Kila siku kulialia eti anahujumiwa na mabeberu hadi kwenye corona wakati ni janga la kidunia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajamvi heshima sana kwenu hasa kipindi hiki ambacho Covid 19 inatesa ulimwengu.

Nimsifu pia Mheshimiwa Yerico kwa andiko lake zuri linalofikirisha ingawa pia limejaa mashaka kibao,na hoja nyingi zikiwa zimewekwa nakshi pengine kumfurahisha msomaji au kumzubaisha asifikiri nje ya box.

Awamu ya 4 chini ya Mheshimiwa Kikwete ulianzishwa mradi mkubwa wa ujenzi wa bomba la gasi kutoka Kusini hadi Dar es Saalam.WaTanzania wengi walihoji kwanini bomba lijengwe kwa gharama kubwa wakati tungeweza kujenga mitambo ya umeme huko Mtwara.Jambo hili lilifinyangwa finyangwa pasipo majibu ya kuridhisha.Badala yake ubabe ukatumika na bomba likajengwa kwa matumani makubwa na maneno mazuri kwamba tatizo la umeme lingekwisha kabisa na lingekuwa historia.

Baada ya ujenzi wa bomba la gesi kukamilika ghafla tumehamia Striegler's Gorge huku tukisahaulishwa kimkakati na ghilba za kijasusi eti sasa mradi huu ndio ukombozi wetu ?.Najiuliza hivi bomba la gesi tumelitumia kwa kusafirisha gesi kwa asilimia ngapi hadi leo hii !.

Miradi yote hii inatafuna budget kubwa sana na hivyo kusababisha miradi mingine kuwekwa kando au kuachwa kabisa.Hii si dalili nzuri hata kidogo,tunaweza kujikuta tunatumia fedha nyingi katika miradi ambayo itakwamisha maendeleo ya taifa kwasababu tayari ipo miradi mingine ambao ilitarajiwa ingeongezewa nguvu kidogo na kuweza kutuletea tija na faida kubwa kwa taifa.Tatizo hapa ni kuweka akili za watanzania wote chini ya mtu mmoja au kikundi kidogo sana ambacho kinaangazia maslahi ya kisiasa ya muda fupi tu.

Angalia manunuzi ya ndege leo jiulize tumeingiza kiasi gani na tumetumia kiasi gani.Leo tunashuhudia shehena ya minofu ya sangara ikisafirishwa na Rwandair kwanini Air Tanzania haifanyi kazi hiyo wakati ndege zipo ?.Huo ujasusi mbona siuoni katika mambo madogo kama haya ambayo hata form four lever angeweza kufikiri vyema na kutoa maamuzi mazuri.
 
Wataliwekea maji?

Leo sudan kagoma
 
Sio watanzania, sema midomo ya CHADEMA na Zitto Kabwe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi kuwa na world heritage sites kunawasaidia nini mnaowaita mabeberu? Hivi mradi ukijengwa watapata hasara gani mpaka washupae usijengwe? Nielimishe...
 
Tunapaswa kutii mikataba tuliyoingia. Leo hii rais akija na mapendekezo ya kujenga jiji kubwa ndani ya Serengeti dunia haiwezi kukaa kimya. Selous game reserve ni urithi wa dunia na tunalazimika kuulinda. Inashangaza kwamba tunaharibu urithi huu wakati ni wetu tulipaswa kuulinda sio kuuharibu, aibu sana.
 
Nyie mnamuunga mkono jiwe kwasababu uelewa wenu wa mambo ni finyu sana kama wa kwake. Ona kila kitu afanyacho kipo hovyo na hayo yanadhihirika wazi kila kukicha na nchi inaabika sana kwasasa.
 
Nyie mnamuunga mkono jiwe kwasababu uelewa wenu wa mambo ni finyu sana kama wa kwake. Ona kila kitu afanyacho kipo hovyo na hayo yanadhihirika wazi kila kukicha na nchi inaabika sana kwasasa.


Mti utupiwao mawe, Tanzania is rising na ndio maana majirani wote wana wivu na chuki tu, ...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…