aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 798
- 1,178
Kesho ni siku ambayo, kesi ya Madai ya Uhalali wa Muungano iliyofunguliwa na Wazanzibari wapatao 40,000 itasikilizwa. Waswahili wana maneno yao wanasema "Bora kua na adui alieelimika utanufaika, kuliko kua na Swahib mjinga".
Msemo huu unaakisi hasa dhana ya Uswahib wa Zanzibar na Tanganyika kupitia Muungano huu ambao uliundwa tarehe 26 April 1964.
Hata hivyo, ni muhimu baada ya miaka kadhaa iliyopita ya Muungano, leo tukaangalia khatma ya Muungano wetu, hasa kwa kuzingatia kua, kesho tarehe 8 March 2018 kesi ya Muungano itasikilizwa ndani ya Mahakama ya Afrika Mashariki - Arusha.
Ni vyema sasa tukaonyeshana njia ya eidha, kama Wazanzibari wanazo sababu na ishara za kushinda kesi hiyo au laah?
Mapema miaka ya 1960 kabla ya Uhuru wa nchi za Afrika Mashariki kupatikana, kuliibuka vuguvugu la kuundwa Shirikisho la Afika Mashariki (East African Federation - EAF). Katika Shirikisho hilo, nchi ambazo zilitarajiwa kuunda Shirikisho hilo zilikua ni Kenya, Uganda, Tanganyika na Zanzibar.
Marehemu Mwalimu J.K Nyerere alitangaza kua, endapo nchi hizo zote zingepata kua huru kwa pamoja angeghairisha adhma yake ya kupigania Uhuru wa Tanganyika ili kuunda Shirikisho hilo la Afrika Mashariki. Hata hivyo, hilo halikufanyika.
Miezi minne kabla ya Zanzibar kupata Uhuru wake wa tarehe 10 December 1963, Washirika hao wa Afrika Mashariki walimtuma Marehem Tom Mboya kutoka Kenya kuja kuiuliza Serikali ya Zanzibar, kama iko tayari kuanza majadiliano kuhusu kujiunga na Shirikisho hilo (EAF) na Zanzibar ikakubali.
Hata hivyo, mara baada ya Mapinduzi ya Zanzibar kutokea, Raisi J.K Nyerere pasi na kushauriana na wenzake aliamua kulifuta wazo hilo la kuundwa kwa Shirikisho la Afrika Mashariki na badala yake akaunda Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na hapo ikawa ndio mwanzo wa kile kinachoitwa "Kero za Muungano".
Inasemakana kua, chanzo cha Mwalimu J.K Nyerere kulifuta wazo hilo pasi na kushauriana na wenzake ni kwamba, Kenya na Uganda walikua wakisita kujiunga katika Shirikisho hilo kutokana na kua na mashaka/hofu na nia ya Mwalimu J.K Nyerere ambapo, hadithi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar imethibitisha ukweli wa hofu yao hiyo.
Pamoja na Mwalimu J.K Nyerere kutumia fursa ya hali ya ulinzi mkali Zanzibar haraka baada ya Mapinduzi, Mwalimu J.K Nyerere pia alitishia kuwaondosha askari wake wapatao 300 aliowatuma kumlinda Raisi Abeid A. Karume, endapo Raisi Karume angelilipinga wazo la Muungano lililotolewa na Mwalimu J.K Nyerere.
Hata Baraza la Mapinduzi ambalo ndicho kilichokua chombo pekee cha utendaji na cha kutunga sheria halikufahamu kuhusu wazo la kuwepo kwa Muungano, mpaka siku mbili kabla ya kutangazwa mnamo tarehe 26 April 1964, siku mia moja baada ya Mapinduzi.
Hivyo, hoja ya kwanza ya Wazanzibari katika kesi hiyo kama ilivyo, ni Uhalali wa Muungano, hasa kwa kuzingatia kua, kwanza Raisi Karume aliingizwa katika Muungano huu kwa ushawisho usiofaa (Vitisho) ambapo, licha ya hayo niliyoyaeleza juu, Raisi Karume pia alidanganywa na kuaminishwa kwamba alikua anasaini mkataba wa Shirikisho la nchi mbili huru zenye mamlaka sawa. Udanganyifu huo ulifanywa baada ya aliekua Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kulazimishwa kundoka katika shughuli hiyo ya utiaji saini.
Pili; Kifungu cha (viii) cha Mkataba wa Muungano ambacho ndio hati ya kuzaliwa kwa Muungano, kimesema kua, Mkataba huo ulipaswa kuridhiwa na Bunge na Baraza la Mapinduzi. Wakati vifungu hivyo vikiridhiwa kwa upande wa Tanganyika na kuhalalishwa kupitia Gazeti la Serikali la Tanganyika, hakuna makubaliano yaliyofikiwa kwa upande wa Zanzibar, kwa kua hakuna Sheria iliyopitishwa na Baraza la Mapinduzi ili kuidhinisha kama walivyoidhinisha Tanganyika na hakuna taarifa yoyote iliyotolewa katika Gazeti la Serikali ya Zanzibar.
Tatu; Jina rasmi la Muungano katika Mkataba wa Muungano lilikua ni "Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar". Miezi sita baadae, kwa mara ya pili, Mwalimu J.K Nyerere bila ya kushauriana na mwenzake, aliamua kubadili jina hilo kutoka jina lililokua ndani ya Mkataba wa Muungano na kua "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" ambalo lilipitishwa rasmi na Bunge la Tanganyika lakini halikupitishwa na Baraza la Mapinduzi. Huu ulikua ukiukwaji mwengine wa wazi wa Mkataba wa Muungano.
Nne; Mkataba wa Muungano Vifungu (vii(b) vimeeleza wazi kua, Bunge litakutana ndani ya mwaka mmoja kutengeneza Katiba ya kudumu, lakini mwisho wa mwaka wa kwanza, Mwalimu J.K Nyerere kwa mara ya tatu pasi na kushauriana na yoyote, aliamua kughairisha kupitishwa kwa Katiba ya kudumu kwa miaka 13 hadi mwaka 1977 baada ya mauaji ya Raisi Karume na kuunganishwa kwa Vyama vya TANU na AFROSHIRAZI na kua Chama kimoja (CCM). Hapo ndipo pakapitishwa Katiba ya sasa tena bila ya kushauriana na Wazanzibari.
Hivyo, licha ya hoja hizi nne kutoa ishara ya namna gani Wazanzibari wanavyoweza kushinda kesi hiyo au laah! Swala la Muungano pia limekua na ukakasi mkubwa ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano hasa baada ya mfumo wenyewe wa Muungano kushindwa kujieleza kama ni mfumo wa Muungano wa nchi moja au Shirikisho. "Although it's 22 years of the Union, the natural and content of the Union has presented considerable confusion both in Tanzania and abroad. It is not clarified wether the Union is a federation or unitary state".
Pia; Swala la Mambo ya Muungano (Union Matters) ni swala ambalo limekua likiibua mjadala mkubwa. Wachambuzi wanadai kua, ndani ya Mkataba wa Muungano, mambo yaliyokubaliwa kama ni mambo ya Muungano ni 11 tu, lakini idadi ya mambo hayo yamekua yakiongezeka mara mbili zaidi baada ya miaka 50 ya Muungano na kupelekea Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kudhoofika siku hadi siku.
Swala la kuondoshwa kwa nafasi ya Raisi wa Zanzibar kua Makamo wa raisi wa Tanzania kinyemela ni sawala jengine linalotoa taaswira mbovu ya adhma ya Tanganyika dhidi ya Zanzibar.
Swala la Raisi wa Muungano kuchaguliwa kwa kura nyingi za Tanganyika bila ya mahitaji ya kura chache za Zanzibar kama vile Wazanzibari hawana sauti ama hawahusiki na Muungano huu, pia linaonyesha jinsi Muungano huu inavyokosa uhalali zaidi.
Chini ya kifungu cha 98 cha Sheria ya Umoja wa Mataifa (UN), Sheria yoyote iliyotungwa juu ya jambo lolote la Muungano inapitishwa na zaidi ya nusu ya kura/wajumbe (Simple Majority). Hivyo, Bunge ambalo idadi yake ya Wabunge kutoka Zanzibar haizidi asilimia 20% haihitaji ushahidi zaidi kuthibitisha kua Muungano huu ni Muungano wa kilaghai.
Haya na mengine mengi, ndio mambo ambayo Wazanzibari wanapaswa kuyajua wanapoenda kuamua khatma ya Muungano wao, hasa katika kipindi hichi ambacho kesi yao ya madai ya Muungano imeshafunguliwa na inaanza kusikilizwa.