Ukweli mchungu ambao Mzee Nyerere aliona lakini alikataa kuukiri ni kwamba siku ambayo Zanzibar inatoka kwenye huu Muungano kutakuwa na machafuko makubwa sana huko Zanzibar. Lakini baada ya muda Zanzibar itatulia na kuwa taifa moja tajiri sana Afrika ya Mashariki, siyo tajiri kwa kubahatisha bali tajiri haswaaa na kitakuwa ndicho kitovu kikubwa cha dini ya Uislamu kusini mwa jangwa la sahara. Itafika kipindi hata kama tunaweza kuwawekea vikwazo vya kiuchumi wao wanaweza kuishi vizuri kabisa bila bughudha ya Tanganyika.
Kardinali Pengo na baadhi ya viongozi wa dini wanaujua sana huu ukweli,
Mzee Nyerere alilijua hili ndiyo maana "akasema ukiwaacha Wazanzibari watapewa mapesa mengi kutoa kwa waarabu"
Ukikaa na Wazanzibari utakuja kugundua mbali na tofuati zao, wana kitu cha ziada ambacho sisi Watanganyika hatuna kabisa: Kwenya maslahi mapana ya Zanzibar CUF na CCM visiwani wote huwa na sauti moja.
NB: Kimkakati Zanzibar kutoka kwenye Muungano kunaweza kuwanufaisha sana kwasababu eno lao limekaa vizuri sana kijographia. Hasa hasa ukiangalia Maritime Silk Road inapita hapo baada ya Kutoka The Strait of Malacca kwa upande wa Bahari ya Pasifiki na Suez Canal ukiwa umetoka Ulaya. Kama wataamua kutanua bandari yao basi wanaweza kujihakikishia kuwa na soko kubwa sana la biashara za kimataifa kama ilivyo Dubai. Pia inaweza kuwapunguzia sana kutegemea Tanganyika kwasababu bidhaa zao wanaweza kuzipata kutoka Asia, Ulaya, Uarabuni na Mombasa (Haya yatafanyika kama watapata viongozi wenye akili na upeo mkubwa wa kufikiri bila kutumiwa kama vibaraka wa Tanganyika ili kuwagawanya Wazanzibar kama ilivyo sasa hivi)
Tanganyika wakiacha siasa za kidini na kibaguzi basi wanaweza kuitumia Zanzibar kama moja ya kitega uchumi kikubwa,
Pia Zanzibar inaweza ikaongezewa uhuru (Commercial Autonomy) kwenya masuala ya kibiashara kama Bandari na Kodi ili kuutenga mfumo wa kodi wa Muungano ili kuweza kutengeneza soko la kimtaifa ambapo wafanya biashara wa Tanganyika na Zanzibar wanaweza kupata bidhaa nyingi kwa bei ndogo kutoka Ulaya, Asia ya Mbali na Ghuba ya Uajemi. Haya yanawezekana kama tu, tutaamua kukaa kama Taifa na kuweka siasa na udini pembeni......ZANZIBAR INAWEZA KUUINGIZIA MUUNGANO PESA NYINGI SANA....
LONG LIVE THE UNION.............
THE FUTURE IS VERY BRIGHT FOR BOTH TANGANYIKA AND ZANZIBAR!
Mungano ukivunjika sifikirii kama wazanzibari wenye akili timamu watapigana au kuleta vurugu,hofu yangu kubwa ni hawa vibaraka wa CCM watakaosadiwa na Watanganyika ndio wataleta vurugu ili kulinda masilahi yao..
Wakati Dubai warabu wanakula vumbi la jangwa Zanzibar ilikuwa imeshapiga hatua mbali sana kimaendeleo,warabu wa nchi tafauti walikuwa wanakuja kufanya makaaza na biashara
Zanzibar,Waoman,Wayemen,Waurani.wachina na mataifa mengine wote wanapatikana Zanzibar wamechanganyika na kuunda kabila la waswahili,Mwafika kama kawaida yetu tulipopata Uhuru mwaka 1963,ndio ikawa mwisho wa uchumi wa Zanzibar,ikawa ndio kaburi la Zanzibar..
Mfano wa waafrika kuzizika nchi zao na kuzipeleka katika umasikini wa ufukara baaada ya kupata Uhuru sio kwa Zanzibar tu,tazama Zimbabwe na nchi nyengine chini ya jangwa la sahara,mfano mzuri sana ni nchi mpya ya Sudan Kusini,hii nchi watu wake walipigana vita miaka na miaka ili kudai wajitenge na Sudan ya Kaskazini,lakini baada ya kupata uhuru wao kutoka kwa Sudan Kaskazini wameanza kupigana wenyewe kwa wenyewe vita vinavyoendelea hadi leo..
Ni aibu kubwa sana kuiona nchi kama Zanzibar ipo hapo ilipo kisiasa,kimaendeleo,kiuchumi nk,waafrika hatuwezi kujitawala,waafrika maamuzi yetu yako kiushabiki,tunaamua kihisia sio kiuhalisia...Naamini kama Zanzibar inaongozwa na mtu asie na asili ya kiafrika ingelikuwepo mbali sana kwa kila kitu,sio vizuri kwangu mimi kama mwafika kusema hayo lakini ukweli ndio huo...,nawakilisha