Raphael Thedomiri
JF-Expert Member
- Sep 1, 2019
- 442
- 729
Mtazamo mpya wa NATO ni kwamba, ili amani irejee katika huu mzozo, ni lazima Putin akatishwe tamaa kabisa kwamba hataweza kuidhibiti Ukraine kabisa, kwa kumuongezea Ukraine msaada zaidi wa silaha.
Katibu wa NATO anaamini hiyo ndio njia bora ya kumshawishi Putin aone anachokihitaji ni kama mlima mkubwa ambao hataweza kuupanda, na hivyo aachane na vita.
=====================
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg ametoa wito wa kupelekwa silaha zaidi nchini Ukraine. Katika mahojiano yake na shirika la habari la Ujerumani, DPA, Stoltenberg amesema msaada wa kijeshi kwa Ukraine ni njia ya haraka ya kupatikana kwa amani. Amesema Rais wa Urusi, Vladimir Putin anapaswa kushawishiwa kwamba hatoweza kufanikiwa katika lengo lake la kuidhibiti Ukraine. Ameongeza kusema kuwa kila nchi ina haki ya kujilinda. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa NATO, panaweza kuwepo suluhisho la mazungumzo ya amani kuhakikisha kwamba Ukraine inashinda kama taifa huru la kidemokrasia. Stoltenberg ameweka wazi kwamba anayachukulia mashambulizi ya hivi karibuni ya Ukraine dhidi ya maeneo ya kijeshi nchini Urusi kuwa halali.
DW