Hatua na maandalizi muhimu ya kujenga nyumba

Hatua na maandalizi muhimu ya kujenga nyumba

King snr

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
1,165
Reaction score
1,470
Wakuu karibuni tujuzane hatua na maandalizi muhimu ya kufuata wakati wa kuanza ujenzi wa nyumba
Nina eneo langu nataka kuanza ujenzi Sasa nimepitia thread nyingi humu zinazoelezea ramani nimeshindwa kuelewana ile michoro hasa ya ground floor.

Hivi wazee wetu zamani wakati wanajenga walikua wanachora ramani ngumu Kama hizi? Mbona huko kijijini fundi anaitwa tu anaanza ujenzi na nyumba inatoka Kama ilivyokusudiwa. Anyway tuachane na hayo. Kwa ambao mmejenga nyumba zenu tupeni hatua na mambo muhimu ya kuandaa ili kuimaliza nyumba mapema.

Mfano nyumba yenye vyumba vitatu vyote master, public toilet, jiko, sebule, dinning,library(na Cha maombi hicho hicho),store.

Michango yenu ni muhimu sana kupata makadirio ya gharama na ushauri juu ya hii nyumba yangu.
 
Wakuu karibuni tujuzane hatua na maandalizi muhimu ya kufuata wakati wa kuanza ujenzi wa nyumba. Nina eneo langu nataka kuanza ujenzi Sasa nimepitia thread nyingi humu zinazoelezea ramani nimeshindwa kuelewana ile michoro hasa ya ground floor...
Omba msaada direct usizunguke mbuyu
 
Unaweza kunipa maelekezo unavyotaka na ninaweza kukushauri ikiwa hauko sahihi pia.
Ushauri ni bure kabisa mkuu
Una maanisha jinsi ramani yangu navyotaka iwe si ndio
 
Elezea basi hizi pwenti mkuuu hasa apo 2, aina ya paa
1. Ramani ni ule mchoro unaoelezea idadi na ukubwa wa vyumba kwa ndani.

2. Paa...hapa nazungumzia aina ya paa aitakayo Paa za kawaida au Paa za kuficha?...
3. Makadirio ni idadi na gharama ya majenzi/vifaa vya ujenzi ambavyo kimsingi vinatokana na ukubwa na aina ya nyumba
 
1. Ramani
2. Aina ya paa
3. Makadirio
Screenshot_20230312-130326.png

Screenshot_20230312-130312.png

Nahitaji nyumba Kama hii
Ramani nimeitoa tu sehemu Ila kitu Kama hiki ndo kipo kichwani mwangu

Vyumba 3 masters,library,jiko, dining,sebule,choo,store
 
View attachment 2547359
View attachment 2547360
Nahitaji nyumba Kama hii
Ramani nimeitoa tu sehemu Ila kitu Kama hiki ndo kipo kichwani mwangu

Vyumba 3 masters,library,jiko, dining,sebule,choo,store
Marekebisho kidogo...
Hii sio ramani...tunaita elevation yaani muonekano halisi wa nyumba.

Ramani ni mchoro unaoonyesha mpangilio wa ndani...ukubwa na idadi ya vyumba japo nimekuelewa
 
Hapo mbili sawa kabisa ndipo nilihitaji kumbe paa la kawaida na hidden.

Kuna nyumba zile kama madarasa wanapaua mgongo wa tembo napenda sana. Formular ni 1/3*kipimo cha hiyo section ya kuweka ^____^ mkuu mimi napenda sana paa fupi kwaio naona kiformula yaani 1/3 bado kenchi ni refu ningependa lipungue zaidi. Kwani kuna tatizo likiwa fupi kama nilivyoeleza apo?
 
Yes kuna tatizo.
Paa likilala sana litapata kutu mapema.

Tofauti ya paa lenye slop kali na slop ndogo;
Slop kali hutiririsha maji haraka na kukauka
Slop ndogo huchelewa kukauka ndio mwanzo wa kupata kutu.

Unajua kwanini hiden roof zinavuja?
Slop zake ndogo...kwa mjenzi asiye na ufahamu atakuharibia nyumba
 
Mfano nyumba yenye vyumba vitatu vyote master, public toilet, jiko, sebule, dinning,library(na Cha maombi hicho hicho),store.
Kuna mkuu hapo juu amekuuliza kama utamudu gharama za kujenga nyumba yenye master rooms tatu na nnavyohisi hujamuelewa.
Kwanza unatakiwa ujue kutofautisha kati ya master bedroom na self contained room.
 
Naomba tofauti zake,nikiri tu sijui kuzitofautisha
Nachojua tu Ni kuwa Zina choo ndani
 
Back
Top Bottom