Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuondoka nyumbani

Nini lengo la kwenda shule?..
 
Ebu fanya maisha yako ya kwao waachie wenyewe [emoji124][emoji124][emoji124]

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
Hahah mkuu humu kuna watoto wa kiume wapo kama dada zao...yani mtoto wa kiume over18 alafu kwao masikini bado anafagilia kukaa kwa wazazi na hana mchango wowote kama anasubiri kuolewa nayeye au wazazi wake wataishi milele...
 
Hakuna cha aibu kukaa kwenu mkuu, mbaya ni kuwa tegemezi wa kila kitu. Kuna ambao wamekimbia kwao kwenda kupanga na bado wanategemea kulipiwa chakula na pango na ndugu au wazazi wao.
Kwenu unaweza kukaa kama una nafasi kubwa pia, ila kama unavyosema usiwe tegemezi kabisa pengine wewe unaweza kujipa majukumu kadhaa ukawa unahudumia baadhi ya vitu ili kupunguza mzigo kwa mzee wako pia.
Kuna watu nimeona mpaka wameoa wakiwa kwao ili mradi hawachangamani na wazazi wao nyumba moja yaani anaishi chumba cha nnje na mke wake na anajitegemea kula kitu na wazazi wake anawasaidia baadhi ya mambo pia.
 
Mkuu kukaa nyumbani umri kuanzia 25+ ..ni uzembe huo
 
Unaondoka nyumbani ukiwa na nini?Mtaji,bidhaa?Ufafanuzi tafadhali.
 
Na Hakuna kitu unatufanya
 
Nimefarijika sana kuona Mada nlioianzisha ...2016 ..Leo ikipewa platform katika page kubwa ya jamii forum ..huko mjini fb wataijadili

Real recognize real [emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Mkuu ukiwa unajitambua sio mbaya sana ..Ila sisi wa Africa tunajuana tulivyo ...ndo maana nkasema kwa Africa Bora kuondoka nyumbani
 
Mi siondoki home,takufa njaa bure!kwani dhambi kukaa kwa wazazi?na nina miaka 36 sasa
Hapo mkuu unakwama sio vizuri maana ukikaa sana nyumbani na akili inakuwa haichangamki (passive) maana inajua chakula kipo tu but ukiwa away from home akili inakuwa active kutafuta ili wewe ule pamoja na familia yako
 
Thanks for that I agree with you
 
Mada imenikuta nimeweka mgongo kwny godoro macho kwa dari, natafakari nawaza mbali.. npo mji wa watu takribani 6 months najitegemea kwa heka ya TAESA, kijana niliemaliza chuo mwaka jana na mtaa hausomi.. 26 ndio age yangu lakn natafakar sijui nirudishe mpira kwa kipa😅
 
Ni bora kuanza kujitegemea ukiwa nyumbani kwa wazazi vijana wengi walioondoka home asilimia kubwa bado ramani hazisomi
 
Mkuu kukaa nyumbani umri kuanzia 25+ ..ni uzembe huo
Napingana na wewe. Mimi nimekaa home mpaka naoa nikiwa na umri wa miaka 30+ Baada ya kuoa nikahama nyumbani nikahamia kwenye nyumba niliyojenga na ninayoishi mpaka leo. Sikuona kwa nini nitoe pesa kulipa kodi badala ya kuipeleka kwenye ujenzi wa nyumba yangu mwenyewe.
Tatizo la vijana wengi ni kuwa na mienendo ambayo inakua vigumu kuishi na wazazi (ulevi, umalaya, u-popo, n.k). Kama unaishi kistaarabu, unachangia pesa ya matumizi nyumbani, utapewa heshima zote na hakuna atakayetamani uondoke.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…