Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuondoka nyumbani

Kabisa mkuu .thank u
 
Sasa wewe kama familia yenu mnakaa kwenye nyumba ya kupanga mpaka leo utakaeje hapo?acha kuwaonea wivu watoto wa wenzio Wazazi wao waliojipanga na kujenga nyumba ili kuwasitiri watoto wao mpaka pale watakapofanikiwa kimaisha,wewe mlaumu Baba yako wakati wenzie wanasoma yeye alijifanya mjanja kuwa chimbo na kuvuta bangi na kunywa mataputapu.
 
mtoa hoja upo sahihi kabisa familia nyingi wa kina mama ndio hawaamini kwa mtoto kutoka na kwenda jitafutia wanahisi kama anakwenda teseka.
wenzetu wazungu ukifikisha miaka 18 hata kama unaishi kwa wazazi unatakiwa kuchangia chakula nyumbani au kulipa kodi hapo kwa wazazi maana yake uanze kutafuta kazi.
vijana wa kiafrika anakaa kwa mzazi anakataa kufanya kazi za kusafisha barabara kufanya usafi maofisini kulea wazee amemaliza form 4 anakataa kuosha magari au hata kujitolea sehemu yoyote.

cha ajabu tukienda ulaya tunagombea kazi hizi hizi ambazo huku tunazikataa mwenye masters anaenda soma phd ulaya anasafisha vyoo vya public, analea wazee na walemavu, anasafisha mifugo ili apate pesa ya kujikimu na bado tulio africa tunamwomba omba wakati kazi afanyazo kule huku zipo ila tunadharau
 
[emoji121]
MKUU
WEKA PICHA YA UTHIBITISHO KWANZA!

VINGINEVYO HUU UZI NI WA KICHOCHEZI KABISA HUU!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…