Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuondoka nyumbani

Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuondoka nyumbani

Kukaa kwa wazazi siyo kigezo cha kumzuia mtu kuendelea
Wabongo tuna akili finyu na kudhani kukimbia kwenu ndio kwenda kutafuta maendeleo, hebu tuangalie jamii za Waasia na waarabu wengi hupenda kuishi katika familia kubwa, unamkuta babu, mtoto na wajukuu wanakaa kwenye mansion moja na bado wametuzidi mara hamsini kwenye maendeleo.
 
huu ni uchochezi

Mods naomba huyu apewe ban , nyinyi mna mamlaka ya kumpa ban huyu hata masaa 24

Hahahaah mkuu kama vile ulikuepo .

Swali la kizushi wewe hukai home?
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kwani jamii za Asia wote ni matajiri ?
Mkuu umeongelea watu wa Asia na Mimi nine base kwa jamii za Africa ambazo nyingi ni masikini na pia zina utamaduni tofauti..... Sasa kuna faida gan kukaa familia yenye watoto kumi afu bado familia ni ya hali ya chini
 
Wabongo tuna akili finyu na kudhani kukimbia kwenu ndio kwenda kutafuta maendeleo, hebu tuangalie jamii za Waasia na waarabu wengi hupenda kuishi katika familia kubwa, unamkuta babu, mtoto na wajukuu wanakaa kwenye mansion moja na bado wametuzidi mara hamsini kwenye maendeleo.
Wewe ni mu Asia?
 
Kurudisha mpira kwa kipa sio shida, shida ni wewe striker kuganda golini na kipa
Hao ndio wale wanajifanya kuiga kila kitu, unakimbia home bila kujiandaa sawa sawa unaenda zako huko baada ya muda maisha yanakupiga mdogo mdogo unaanza kwenda home kula mara Bi Mkubwa nitumie hela mwisho wa siku unarudi tena pale pale home kwa aibu.
 
Maish ni vyovyote lighte wazee wangu wangekuwa nauwezo mm nisingetoka nyumbani niende wapi
Unakuta mtu baba yake ananyumba tano lakini yeye kapanga huo upuuzi mm nisingefanya ila kwakuwa wazazi wangu hawakuwa na uwezo nilianza kujitehemea nikiwa na miaka 15 mpaka leo bado hata nyumba yangu sijaezeka.
Shukuru Mungu hata hilo boma ulilonalo, kwa maelezo uliyotoa kama ungebaki nyumbani hata begi la nguo bado ungekua unatumia uliloachiwa na mzazi wako
 
Kuhama nyumbani hasa Kwa vijana inawaandaa kukabiliana na majukumu
Ukiwa umepanga ukiangalia huna kitanda kabati friji tv chakula na mengineyo akili itakaa sawa
Unarudi nyumbani chumba kinakuangalia unatakiwa ulipie umeme maji na chakula chako hapo lazima uchakarike upate mahitaji yako ya lazima
Tofauti na uko kwenu unarudi unakuta ugali unakula unaeda kuoga unarudi unaangalia TV ukitoka hapo kulala yani nakuambia mtu kama huyu akioa anapata shida sana hawezi majukumu anaona mzigo
Anakuwa hawezi kumtunza mke
Wadogo zangu amkeni mkajitegemee msiwe kama watoto Wa kike
 
Hi wana Jf,
Nimejaribu kuchunguza hasa hizo nchi zetu za Africa hususani (East Africa) limekuwa ni jambo la kawaida kukuta kijana ana miaka takribani 30 na bado anaishi kwa wazazi wake bila aibu anasubiri ugali wa shikamoo.
Hili jambo ukiliangalia kwa mapana utagundua linasababishwa na vitu Vingi..

Mfano mfumo wetu wa elimu nao unachangia kwa sababu elimu mtu anayopata mpaka chuo kikuu haimjengi muhusika katika kuwa na mawazo ya kujiajiri . Tatizo linakuja pale mtu kamaliza chuo alafu kakosa kazi ..utashangaa mtu anakaa nyumbani mpaka anaoa/kuolewa akiwa nyumbani.

Lakini upande wa pili hata kama mtu hajasoma pia bado utakuta anaishi nyumbani kwa wazazi akiwa na umri mkubwa..mi nadhani pia sisi wa Africa uvivu unatupeleka pabaya.

Tumezoea kukaa vijiweni muda mwingi tukijadili mambo yasiyo na msingi na tumekuwa watu wa kutojali muda kabisa... Wala hatuna ratiba ..

Yangu ni hayo tuu kama kuna mwingine mwenye mawazo tofauti na mimi anaweza akaongeza au kunipinga kwa hoja lakini...
Nawasilisha

Nimeshuhudia Watu wengi walioondoka makwao kwenda kutafuta Maisha (hasa mijini), na bado hawakutoboa.

Hawawezi hata kununua Kijiko cha Chai, achilia mbali kua na mke ndani. Na umri unaelekea Jioni. Ni mara mia wasingeondoka, wangebaki kuwasaidia wazazi kulima ili mkono uende kinywani.
Haya mambo myatazame kwa mapana yake .
Nadhani swala ni namna unavyoondoka nyumbani badala ya kukazania Kuondoka Nyumbani.
Na Elimu ya Digrii, mastazi, Diploma haina uhusiano wowote na Mtu kuja kuishi decent life.

Tunaina Familia za Waarabu na wahindi wengi tu wanaishi na wazazi wao maisha mazuri tu. Kikubwa ni kuishi maisha mazuri.
 
Hi wana Jf,
Nimejaribu kuchunguza hasa hizo nchi zetu za Africa hususani (East Africa) limekuwa ni jambo la kawaida kukuta kijana ana miaka takribani 30 na bado anaishi kwa wazazi wake bila aibu anasubiri ugali wa shikamoo.
Hili jambo ukiliangalia kwa mapana utagundua linasababishwa na vitu Vingi..

Mfano mfumo wetu wa elimu nao unachangia kwa sababu elimu mtu anayopata mpaka chuo kikuu haimjengi muhusika katika kuwa na mawazo ya kujiajiri . Tatizo linakuja pale mtu kamaliza chuo alafu kakosa kazi ..utashangaa mtu anakaa nyumbani mpaka anaoa/kuolewa akiwa nyumbani.

Lakini upande wa pili hata kama mtu hajasoma pia bado utakuta anaishi nyumbani kwa wazazi akiwa na umri mkubwa..mi nadhani pia sisi wa Africa uvivu unatupeleka pabaya.

Tumezoea kukaa vijiweni muda mwingi tukijadili mambo yasiyo na msingi na tumekuwa watu wa kutojali muda kabisa... Wala hatuna ratiba ..

Yangu ni hayo tuu kama kuna mwingine mwenye mawazo tofauti na mimi anaweza akaongeza au kunipinga kwa hoja lakini...
Nawasilisha
Ninaunga mkono asilimia zote.
 
Mimi home sihami na niataolea hapa hapa.
Mimi ntatoka nikipata uhakika wa maisha , mtu unakuta anatoka home hajui hata anaanzaje maisha
Anaenda kubangaika mtaani hata hajui baadae yake atakula nini , si bora ufanye hustle zako ukiwa home unatoka ukiwa fit
 
Acha uongo unasema elimu ya Tanzania haimjengi mtu kuwa na mawazo ya kujiajiri,una takwimu za kutuonyesha graduates wangapi wameshindwa kujiajiri,kujiajiri kunategemea na kujifikirisha kwa mtu kama mkichwa wako umelala ndio hivo utakaa tu nyumbani kusubiri kuajiriwa.

Tusisingizie elimu tuvilaumu vichwa vyetu vilivyolala,wapo watu wengi tu wamejiajiri baada ya kumaliza chuo sasa na hawa wamesoma elimu gani kama sio hii hii tunayoisoma wote
 
Back
Top Bottom