Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuondoka nyumbani

Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuondoka nyumbani

Lakini ni kweli ukiondoka nyumbani akili inafunguka sana kupambana na maisha,angalia wachaga walio wengi wameendelea coz walihama kutoka moshi kuja Dar,Moro,Mbeya etc na wamefanikiwa
Ndugu hii mada inaweza kuwa pana kuliko tunavyoichukulia juujuu, kwa upande mmoja naungana nawe kuhama mkoa hata nchi kwenda kutafuta ni jambo jema na la kupongeza.
Ila tukirudi kwenye maudhui ya mleta mada kuwa ili ufanikiwe ni lazima uondoke nyumbani mimi hapo ndipo tutakapopingana, mfano uliouleta wa wachaga kuhamia mikoa mingine hebu ujiulize mfano vijana wote wa kichaga wakiondoka nani atakayebaki kuendeleza mji na vijiji vyao? Maendeleo hayana formula ya moja kwa moja useme ulipopita wewe nami nikikufata nitafanikiwa big NO.
Cha muhimu ni kuwahimiza vijana wachape kazi waache kuwa tegemezi kwa kila kitu, haijalishi anakaa kwa wazazi, shemeji, shangazi au mjomba.
 
Maish ni vyovyote lighte wazee wangu wangekuwa nauwezo mm nisingetoka nyumbani niende wapi
Unakuta mtu baba yake ananyumba tano lakini yeye kapanga huo upuuzi mm nisingefanya ila kwakuwa wazazi wangu hawakuwa na uwezo nilianza kujitehemea nikiwa na miaka 15 mpaka leo bado hata nyumba yangu sijaezeka.
 
ugali wa shikamoo..
hauna nidhamu kabisa, mara utasikia kapasue kuni, kachume mboga hadi sokoni kununua nyanya utaenda!!
mmh mimi siiutaki hata bure aaseee
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] dah kwel inakera saaaana
 
Wakati mwingine ni bora ukaishi kwenu

2m za kodi ukanunua hata kiwanja cha 20x20

Ukapanga tofali....


Ila kila mtu ana maono yake

Au kodi ambayo ungelipa ukaizungusha na faida ukawekeza
Wabongo tuna akili finyu na kudhani kukimbia kwenu ndio kwenda kutafuta maendeleo, hebu tuangalie jamii za Waasia na waarabu wengi hupenda kuishi katika familia kubwa, unamkuta babu, mtoto na wajukuu wanakaa kwenye mansion moja na bado wametuzidi mara hamsini kwenye maendeleo.

Kukaa nyumbani si tatizo, shida ni pale mtu unapokaa nyumbani bila kujishughulisha na chochote. Kuna wengi nawajua bado wako kwao na wanajishughulisha kuhudumia pia wazazi wao.

Mi siondoki home,takufa njaa bure!kwani dhambi kukaa kwa wazazi?na nina miaka 36 sasa
 
Hi wana Jf,
Nimejaribu kuchunguza hasa hizo nchi zetu za Africa hususani (East Africa) limekuwa ni jambo la kawaida kukuta kijana ana miaka takribani 30 na bado anaishi kwa wazazi wake bila aibu anasubiri ugali wa shikamoo.
Hili jambo ukiliangalia kwa mapana utagundua linasababishwa na vitu Vingi..

Mfano mfumo wetu wa elimu nao unachangia kwa sababu elimu mtu anayopata mpaka chuo kikuu haimjengi muhusika katika kuwa na mawazo ya kujiajiri . Tatizo linakuja pale mtu kamaliza chuo alafu kakosa kazi ..utashangaa mtu anakaa nyumbani mpaka anaoa/kuolewa akiwa nyumbani.

Lakini upande wa pili hata kama mtu hajasoma pia bado utakuta anaishi nyumbani kwa wazazi akiwa na umri mkubwa..mi nadhani pia sisi wa Africa uvivu unatupeleka pabaya.

Tumezoea kukaa vijiweni muda mwingi tukijadili mambo yasiyo na msingi na tumekuwa watu wa kutojali muda kabisa... Wala hatuna ratiba ..

Yangu ni hayo tuu kama kuna mwingine mwenye mawazo tofauti na mimi anaweza akaongeza au kunipinga kwa hoja lakini...
Nawasilisha
Uko waliko endelea ulaya na america ndio wanaongoza vijana kuishi nyumbani tena sio kuchelewa kuondoka wanaisha nyumbani maisha yao yote.ni maskini tuu ndio ulazimika kuondoka nyumbani.mfano akipeleka mtoto shule anarudi kuboresha biashara au shamba la baba ,na hili sio wazungu tuu njoo Arusha wamasai ,waarusha wachaga ,wagogo ,wasukuma ,karibu makabila yote Tanzania .vijana wanaume awaondoki nyumbani wanaishi nyumbani. wanajenga nyumbani .ni maskini tuu usiekuwa ataa na shamba na mjini nae umepanga ndio inabidi kufukuzaniana nyumbani,sana sana naona umeleta huu uzi bila ya kuwa na utafiti .
Na kama unabisha muulize RAIA namba moja pale Chato kama sio kwa baba na mama yake ,
 
Hakuna cha aibu kukaa kwenu mkuu, mbaya ni kuwa tegemezi wa kila kitu. Kuna ambao wamekimbia kwao kwenda kupanga na bado wanategemea kulipiwa chakula na pango na ndugu au wazazi wao.
Huyu nadhani ajui anacho ongea .hao ndugu zetu wenye asili ya India .anajua jinsi wanavyo mzidi maarifa wameama nyumbani kwa wazazi wao !!??
 
Hiv hyo elimu ya wenzetu huko ulaya na marekani inafundisha vip watu kujiajiri? mm naona ni uoga wa walio wengi kuogopa kujaribu, na uvivu wa kuona fursa, naamini mtu anayesoma mfano mechanical eng oxford hafundishwi kujiajri ila pindi anapomaliza anatafuta fursa,, vyuo ving hapa tz wanafunzi wanasoma entreprenuership tusisubri elimu ya kujiajiri zaidi ya hyo wakuu, ni maoni yangu tu hayo
 
Hi wana Jf,
Nimejaribu kuchunguza hasa hizo nchi zetu za Africa hususani (East Africa) limekuwa ni jambo la kawaida kukuta kijana ana miaka takribani 30 na bado anaishi kwa wazazi wake bila aibu anasubiri ugali wa shikamoo.
Hili jambo ukiliangalia kwa mapana utagundua linasababishwa na vitu Vingi..

Mfano mfumo wetu wa elimu nao unachangia kwa sababu elimu mtu anayopata mpaka chuo kikuu haimjengi muhusika katika kuwa na mawazo ya kujiajiri . Tatizo linakuja pale mtu kamaliza chuo alafu kakosa kazi ..utashangaa mtu anakaa nyumbani mpaka anaoa/kuolewa akiwa nyumbani.

Lakini upande wa pili hata kama mtu hajasoma pia bado utakuta anaishi nyumbani kwa wazazi akiwa na umri mkubwa..mi nadhani pia sisi wa Africa uvivu unatupeleka pabaya.

Tumezoea kukaa vijiweni muda mwingi tukijadili mambo yasiyo na msingi na tumekuwa watu wa kutojali muda kabisa... Wala hatuna ratiba ..

Yangu ni hayo tuu kama kuna mwingine mwenye mawazo tofauti na mimi anaweza akaongeza au kunipinga kwa hoja lakini...
Nawasilisha
mi nadhani hatua ya kwanza ni kutokua tegemezi kabisa kwa watu wote,na kujitambua
 
Mkuuu hom sihami ng'oh bora wao wazaz wanikimbie wenyew maana mi ni mtoto wao na inabid nieategemee had pale nitakapo pata uhakika wa kuish mwenyew tofaut na hapo hom siondok na siham
bora wewe uko kwa wazazi wako kuna wengine wa age km yko wanakomaa kukaa alipo olewa dada...manina kweli...
 
Siwezi kusema kipi ni sahihi, ila ni mazingira ya familia uliyotoka yanayoweza kukufanya either kuzidi kukaa nyumbani or ukimbie nyumbani ukapange. Ni mazingira ya family yako yatayo determine choice ipi ina payoff kubwa.

Kama wazazi ni matajiri na wana uwezo mkubwa tu sioni ubaya hata kwa kijana kukaa home hata akiwa na 30 years. So asubuhi unaenda zako kazini unarudia home sio mbaya sema una uhuru utakuwa unaukosa maana bado upo na wazazi.

Vivo hivyo kama familia yako ni masikini, hakuna maana ya wewe kijana kuzidi kubana nyumbani kwanza ile hali itakuwa inakuumiza kisaikolojia so hapo ni bora hata uende mbali na home hata ukifa njaa poa tu lakini ujue una hustle. Ila sio kukaa hapo hapo home unaangalia wazazi wako wanavyochapika, itakuuma roho.

Conclusively, siwezi moja kwa moja kukubaliana na mtoa mada ila pia siwezi kumpinga. Inategemeana na mazingira. Na isionekane kukukaa mbali na nyumbani kwa wazazi ni ujanja na wala tusiwalaumu wanaokaa na wazazi wao nyumbani. kila kitu kina sababu zake za msingi kabisa.
 
Back
Top Bottom