Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuondoka nyumbani

Hatua ya kwanza ya mafanikio ni kuondoka nyumbani

Hi wana Jf,
Nimejaribu kuchunguza hasa hizo nchi zetu za Africa hususani (East Africa) limekuwa ni jambo la kawaida kukuta kijana ana miaka takribani 30 na bado anaishi kwa wazazi wake bila aibu anasubiri ugali wa shikamoo.
Hili jambo ukiliangalia kwa mapana utagundua linasababishwa na vitu Vingi..

Mfano mfumo wetu wa elimu nao unachangia kwa sababu elimu mtu anayopata mpaka chuo kikuu haimjengi muhusika katika kuwa na mawazo ya kujiajiri . Tatizo linakuja pale mtu kamaliza chuo alafu kakosa kazi ..utashangaa mtu anakaa nyumbani mpaka anaoa/kuolewa akiwa nyumbani.

Lakini upande wa pili hata kama mtu hajasoma pia bado utakuta anaishi nyumbani kwa wazazi akiwa na umri mkubwa..mi nadhani pia sisi wa Africa uvivu unatupeleka pabaya.

Tumezoea kukaa vijiweni muda mwingi tukijadili mambo yasiyo na msingi na tumekuwa watu wa kutojali muda kabisa... Wala hatuna ratiba ..

Yangu ni hayo tuu kama kuna mwingine mwenye mawazo tofauti na mimi anaweza akaongeza au kunipinga kwa hoja lakini...
Nawasilisha
Umeandika kwa mtazamo mfupi angalia watanzania wengi hatuwezi kuondoka nchini tupo mikelele kushabikia chadomo cheki nchi za wenzetu walivyojaa nje ya nchi kusaka keki angalia Leo kuna wakenya laki tano America tu watz ndio Kwanzaa tupo laki moja sembuse hao unaosema waliopo kwa baba zao .....
 
Vipi ambao bado wanaishi kwao ila wamepanga mageto kwa ajili ya kugongea mademu. Yaani mtu yupo home na ana geto bado lina kila kitu anaamua tu alale wapi
 
Huyo hawezi kuanzisha mji wake mpaka aanzishiwe aukute yeye afanye kuhamia tu na akileta mchezo anatimuliwa anakaribishwa mwingine
[emoji28][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Ila kwel adse
 
Hao tayari tunawahesabia kua hawako nyumbani kwao cz tayari Ana mji wake .so swala la kurud hm n option tuu
Vipi ambao bado wanaishi kwao ila wamepanga mageto kwa ajili ya kugongea mademu. Yaani mtu yupo home na ana geto bado lina kila kitu anaamua tu alale wapi
 
Umeandika kwa mtazamo mfupi angalia watanzania wengi hatuwezi kuondoka nchini tupo mikelele kushabikia chadomo cheki nchi za wenzetu walivyojaa nje ya nchi kusaka keki angalia Leo kuna wakenya laki tano America tu watz ndio Kwanzaa tupo laki moja sembuse hao unaosema waliopo kwa baba zao .....
Mkuu kuondoka nyumbani n neno pana kwa mfano ukiwa nchi za watu ... Bhac ujue nchi yako n nyumbani. ... So nlilenga kule kule Ila km ningekuja na mada kua ili ufanikiwe n lazima uondoke nchini kwako ... Bhac mada isinge balance
 
Mkuu [emoji817] nakubaliana na hoja yako hii

One love
 
Mi siondoki home,takufa njaa bure!kwani dhambi kukaa kwa wazazi?na nina miaka 36 sasa
Hapana mkuu kwa sasa una miaka 41 sio 36...ukiangalia kuna vijana wameanza kushika million wakiwa na 23.....toka hapo kwenu nenda katafute wewe mtoto wa kiume...au wazazi wataishi milele??...
 
Wabongo tuna akili finyu na kudhani kukimbia kwenu ndio kwenda kutafuta maendeleo, hebu tuangalie jamii za Waasia na waarabu wengi hupenda kuishi katika familia kubwa, unamkuta babu, mtoto na wajukuu wanakaa kwenye mansion moja na bado wametuzidi mara hamsini kwenye maendeleo.
Mansion yenu iko mbagala maeneo gani???....usijifananishe mswahili wa kwenye nchi masikini na watu ambao nchi zao tayari ni matajiri...
 
Waasia na waafrica wote ni binadamu,na wanafanana kwa mahitaji ya msingi,hakuna kasoro yoyote kuchukua mfano kutoka kwao,jambo zuri unajifunza kutoka popote no matter the race.
Haya endelea kujifananisha huku unaendelea kuzeeka.....muda haukusubiri....ukistuka 50 huna hata bakuli....
 
Uko waliko endelea ulaya na america ndio wanaongoza vijana kuishi nyumbani tena sio kuchelewa kuondoka wanaisha nyumbani maisha yao yote.ni maskini tuu ndio ulazimika kuondoka nyumbani.mfano akipeleka mtoto shule anarudi kuboresha biashara au shamba la baba ,na hili sio wazungu tuu njoo Arusha wamasai ,waarusha wachaga ,wagogo ,wasukuma ,karibu makabila yote Tanzania .vijana wanaume awaondoki nyumbani wanaishi nyumbani. wanajenga nyumbani .ni maskini tuu usiekuwa ataa na shamba na mjini nae umepanga ndio inabidi kufukuzaniana nyumbani,sana sana naona umeleta huu uzi bila ya kuwa na utafiti .
Na kama unabisha muulize RAIA namba moja pale Chato kama sio kwa baba na mama yake ,
Jobless kwenye ubora...
 
Sasa wewe kama familia yenu mnakaa kwenye nyumba ya kupanga mpaka leo utakaeje hapo?acha kuwaonea wivu watoto wa wenzio Wazazi wao waliojipanga na kujenga nyumba ili kuwasitiri watoto wao mpaka pale watakapofanikiwa kimaisha,wewe mlaumu Baba yako wakati wenzie wanasoma yeye alijifanya mjanja kuwa chimbo na kuvuta bangi na kunywa mataputapu.
Watoto wako watajengewa na Nani??...
 
Back
Top Bottom