Hatua ya kwanza ya MO iwe kumuondoa Manara

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Manara atamchafulia MO kutokana na mahaba yake kwa Simba yaliyopitiliza kiasi cha kusahau kanuni na taratibu za mchezo huo na sheria za nchi.

Manara anapaswa kujua kuwa kila lalamiko lina utaratibu wake wa kuliwasilisha kwenye mamlaka za kutoa maamuzi sio kukurupuka kama anavyofanya jamaa yetu na yule mwenzake aliyekuwa upande wa pili.

Kwa bahati mbaya ndivyo alivyo hakanyiki. MO kazi kwako, nadhani ungependa kuona bidhaa zako zinanunuliwa na watu wote bila kujali ushabiki wa mpira, lakini kwa Manara hilo linaweza kuwa gumu.
 
akifukuzwa unazani utapewa kazi hiyo wewe
Kufa kufaana, vinginevyo apunguze kukurupuka. Mbona watu wanawafurahia Maso Bwire na Kifaru wanapozisifia timu zao? Atenganishe kazi na mahaba ya timu.
 
Kufa kufaana, vinginevyo apunguze kukurupuka. Mbona watu wanawafurahia Maso Bwire na Kifaru wanapozisifia timu zao? Atenganishe kazi na mahaba ya timu.
Hakuna lolote yule jamaa kama anachamsha tu sasa tatizo liko wap?
 
akifukuzwa unazani utapewa kazi hiyo wewe
Unadhani MO atataka mtu atakaewakera kijingajinga watu wa aina fulani wasinunue MO juice zake? Uwendeshaji huu wa mpira ni wa kibiashara zaidi kuliko utani wa jadi na mahaba yasiyozuilika.
 
Kufa kufaana, vinginevyo apunguze kukurupuka. Mbona watu wanawafurahia Maso Bwire na Kifaru wanapozisifia timu zao? Atenganishe kazi na mahaba ya timu.
huyo masau bwire angekuwa simba au yanga ungekuja na maneno km hayahya
 
Unadhani MO atataka mtu atakaewakera kijingajinga watu wa aina fulani wasinunue MO juice zake? Uwendeshaji huu wa mpira ni wa kibiashara zaidi kuliko utani wa jadi na mahaba yasiyozuilika.
ubora na bei zake ndo ushawishi tosha WA kupata Wateja sio manara
 
Ikiwezekana aongezwe Manara mwingine wawe wawili kabisa. Otapendeza zaidi!
 
Umeongea point sana mkuu... Japo kuna unazi lakin upande wa pili kuna Biashara pia...
 
ubora na bei zake ndo ushawishi tosha WA kupata Wateja sio manara
Mbona Raila aliwaambia watu wake wasusie bidhaa za makapuni fulani na wakafanya hivyo bila kujali bei na ubora wa bidhaa?
 
Aondolewe kvp Manara yuko right kutetea klabu iliyomuajiri.We pambana na hali yako acha wivu huo.Mwenzeko akitaka kuonana na MO fasta,au unamuonea wivu anavyokuwa Oman anavyotafuna mpunga.
Manara ndio msemaji bora mpaka sasa waliokuwa Simba anajua kuhamasisha mashabiki,ulikuwepo Simba DAY jibu umngelipata umuhimu wa Haji Manara.
 
atatafutiwa kitengo kingine labda cha ushabiki lakini sio kazi kama zile. by the way ulaya msemaji wa timu ni manager na sio kila mtu.
msemaji wa timu lazima awe skills na sense za entrepreneurship, sio kuropoka tu chochote na namna ya kufanikisha kuwaudhi wengine. Kwenye biashara kila mtu ni muhimu.
 
Sio mtu mbaya ki vile, anahitaji maboresho machache tu ili aendane na mfumo wa kibiashara wa sasa, vinginevyo timu itapigwa faini kila siku na watu wengine kususia bidhaa za mheshimiwa sokoni kwaajili ya maneno na tabia yake. Pamoja na burudani ya mpira lakini mwekezaji anatarajia kupata faida, hivyo atawahitaji watu wote sio wale wa Simba tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…