Hatua ya msingi imeisha naomba tathimini

Nimeipenda ramani yako boss tunaweza kushare.
 
Hapo
Tofali si chini ya 2000 mpaka top koz
 
Hapo

Tofali si chini ya 2000 mpaka top koz
Room3

Moja master

Public toilet na sebule

Hapo kila room inakula tofali 300×3= 900

Chukulia sebule ni room ya nne jumla zinakiwa 1,200

Master moja na public chukulia ni room nyingine jumla 1,500

Tofali 2000 ni nyingi sana
 
Ujenz sio mrahisi kama mnavyoandika hapo juu.
Alaf Kuna mtu kasema Nondo 6[emoji23][emoji23][emoji23].

Kwa uzoefu tu,
hapo sio chini na Nondo 20 , * 21k. = 800k
Kuna kokoto roli 1 hapo, 200k+.
Kuna trip 2 za Mchanga 200k
Matofali hapo weka 2,000 * 1,250 ni 2.5 Mill
Cement ni mifuko 20 kujenga ,(20*17k ) ni 340k
Cement ya nguzo na lenta weka 10 ni 170k
Mbao, maji weka 200k
Ufund weka 1.5 mill
Gharama usafiri vifaa + misumar weka 100k

Andaa 7 mill kufikisha kwenye Lenta

Na Hapo hujajaza vifus vyumban.

Ukitaka kuamia hapo hamna hamna bila umeme andaa 20mill.
 
Kwenye ujenz wa Nyumba hiyo ya kupandisha matofali ndio hatua rahisi.

Ukishamaliza hapo kuezeka standard ni pagumu. Coz unatakiwa ufanye yote wakat mmoja,
Wakat kwenye kujenga unaweza pandisha kozi 5 kwanza.

Pia baada ya kuezeka,
finishing ndio ngumu.

Ogopa sana vifaa unavyonunua vikawa na majina ya kiingereza. Vikaitwa kwa kingereza.

Mfano Wiring, skimming, gypsum, tiles, plundering .
 
Hapo ulipo vifaa vipo juu kuliko alipo mtoa mada

Angalia bei za kwao hapo juu

Kwingine sikupingi ufundi unatofautiana

Mfano lenta mwingine anaweza suka nondo tatu mwingine mbili
 
Yan mie pia nimeshangaa kuona nondo 6
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…