WanaJF ilibidi nilete hizi njia kwa ajili yenu baada na kuniambia niwaandikie. Nimeongea na watu mbalimbali kuhusu experience yao kwenye mahusiano na Leo nimekuja na kisa Cha kweli ambacho huenda kitakuelimisha hasa kabisa linapokuja suala la mahusiano. Lakini kwanza kabisa, nitaziandika njia zitakazofanya wewe usahau mahusiano yako ya zamani yaliyovunjika.
Kuachwa au kuachana huwa haitegemei mlipendana au lah! Ila Yale mazoea humfanya mtu apate maumivu mazito sana wakati anaachana na mwenza wake, Hivyo basi hizi ni njia ambazo ukizifuata Moyo wako utapona kwa haraka sana;-
1. Kubali kwanza kwamba ni ukweli mmeachana.
- Ni ngumu sana kukubaliana na matokeo kama haya hasa pale wawili nyie mlipodumu kwa muda mrefu na mkawa na ndoto nyingi za pamoja. Hivyo tiba ya kwanza kabisa ni ukubaliane na matokeo kwamba it's over.
2. Kwenye simu yako futa mazungumzo yenu yote ya zamani, voice, picha lakini zingatia usimblock. Kumblock mtu uliempenda na mkaachana huonesha kutojiweza kwake na ukomavu mdogo wa mahusiano. Ila kufuta mazungumzo yenu itakusaidia kutorudi rudi kurejelea mazungumzo yenu ya zamani.
3. Usiweke hasira moyoni mwako kumuhusu Ex wako wa zamani ikibidi umuone tu kama rafiki.
Ugomvi usidumu kwenye maisha yako, mpaka wawili nyie mlipofikia kwenye uamuzi wa kuachana basi lazima kulikuwa na sintofahamu Kati yenu basi usidumu. Samehe lakini kama kunajambo unahitaji msaada kutoka kwake usisite kusema akikusaidia ni yeye na asipokusaidia basi ni yeye. Ni vyema umchukulie Kama rafiki ili kuweka mipaka na amani Kati ya mioyo yenu.
4. Usimfatilie mitandaoni(stalking). Haijalishi ni unampenda kiasi gani Ila ili kuweka usawa wa kihisia na akili yako mwenyewe usimfatilie aliekuwa Mpenzi wako mitandaoni.
5. Usitafute mahusiano ya haraka ili kumove on maana kama sio kujuta basi utaziumiza zaidi hisia zako. Kutafuta mtu mwingine ili uponye majeraha sio njia sahihi ya kujitibu maumivu yako ya zamani.
Angalizo kwa waliopo kwenye mahusiano au wanatarajia kuingia kwenye mahusiano,
Kama ikitokea mmegombana epuka Mambo haya 3 ;-
i. Usitumie maumivu yake ya zamani aliyokushirikisha kumuumiza zaidi.
ii. Usimlinganishe na ex zako wa zamani haijalishi yeye amekufanyia kosa gani.
iii. Usitumie maneno ya ukali au lugha ambazo zinamdharirisha.
Kitu Cha kuweka kwenye akili yako, mahusiano sio lazima yadumu, muda mwingine kuachana hutokea kwa sababu na hatima. Huenda sio mtu sahihi kwako au muda sio sahihi, Hivyo basi muachane kwa heshima ili kutoharibu mbele ya mwenza wako kwa kumkashifu.
P.p ;- samahani hii article imekuwa ndefu sana, kisa nilicho waahidi nitakiandaa alafu nikitume kwenu.
~rayamikhal