Hatua za kukabiliana na joto la Dar es Salaam

complex31

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2016
Posts
421
Reaction score
1,289
Kwa hali ilivo Dar es Salaam wakati huu sio ya kawaida. Joto lililopo wakati huu linatukumbusha kufanya vitu vingi sana kwanzia kwenye miili yetu mpaka maeneo tunayoishi au kushinda.

Unapaswa kunjwa maji mengi ya kutosha, kama hauendi haja ndogo mara kwa mara na ukienda mkojo unakua na rangi ya njano na afya yako ni nzima hicho ni kipimo ya kwamba maji unayokunywa hayatoshi mengi yanatoka kwa njia ya jasho.

Kwa hali hii ya hewa jamani tukumbuke kuotesha miti, naongelea miti sio maua. Miti huweza kusaidia kivuli na kufanya ardhi kua na unyevu nyevu.

Embu jiulize mpaka sasa umewahi kupanda miti mingapi? Kama jibu na hakuna ni wakati sasa wa kuanza kupanda miti, ukipita barabara ya Shaban Robert (Posta) ni mfano mzuri kua miti inamsaada mkubwa sana kukabiliana na hii hali.

Tukirudi majumbani weekend hii walahu tukumbuke kupanda mti mmoja kwa kila mtu kuokoa hii hali ya joto kwa miaka michache ijayo

Kwa hali hii ya Joto na mabadiliko ya tabia nchi kiujumla tutegemee kwa wakazi wa Dar kupata mgao wa Maji majira ya usoni kaka hatutachukua hatua za mapema kukabiliana na hii hali.
 
Kwa hali ilivo Dar es Salaam wakati huu sio ya kawaida. Joto lililopo wakati huu linatukumbusha kufanya vitu vingi sana kwanzia kwenye miili yetu mpaka maeneo tunayoishi au kushinda...
Mateso yamezidi hivi.

Bora sisi wakazi wa chato,

karibuni sana Kuna warembo huku.
 
Ac na feni zipo mkuu ishi nazo

Ila naunga mkono hoja ya kupanda miti
 
Wabongo wengi wana visa na miti... unakuta mtu anakata miti kisa unamchafulia kwake... mwingine anasema anasafisha... inabidi kuondoa hii Dhana na kuhimiza upandaji wa miti sana.
 
Tuoteshe miti, faida na nyingi kuliko hasara, kuna nyumba zimejengwa kisasa zimewekwa na paving block chini, paving huongeza joto ni nafuu uweke majani (ukoka)
 
Ac na feni zipo mkuu ishi nazo

Ila naunga mkono hoja ya kupanda miti

Kuna wengine wakikaa na feni wanaanza kuumwa kifua, AC majumbani sio kwa asilimia kubwa kutokana na gharama za umeme, cha msingi tuhimizane kuotesha miti, hali inazidi kua mbaya
 
Kwa hali ilivo Dar es Salaam wakati huu sio ya kawaida. Joto lililopo wakati huu linatukumbusha kufanya vitu vingi sana kwanzia kwenye miili yetu mpaka maeneo tunayoishi au kushinda.

Unapaswa kunjwa maji mengi ya kutosha, kama hauendi haja ndogo mara kwa mara na ukienda mkojo unakua na rangi ya njano na afya yako ni nzima hicho ni kipimo ya kwamba maji unayokunywa hayatoshi mengi yanatoka kwa njia ya jasho.

Kwa hali hii ya hewa jamani tukumbuke kuotesha miti, naongelea miti sio maua. Miti huweza kusaidia kivuli na kufanya ardhi kua na unyevu nyevu.
Embu jiulize mpaka sasa umewahi kupanda miti mingapi? Kama jibu na hakuna ni wakati sasa wa kuanza kupanda miti, ukipita barabara ya Shaban Robert (Posta) ni mfano mzuri kua miti inamsaada mkubwa sana kukabiliana na hii hali.

Tukirudi majumbani weekend hii walahu tukumbuke kupanda mti mmoja kwa kila mtu kuokoa hii hali ya joto kwa miaka michache ijayo

Kwa hali hii ya Joto na mabadiliko ya tabia nchi kiujumla tutegemee kwa wakazi wa Dar kupata mgao wa Maji majira ya usoni kaka hatutachukua hatua za mapema kukabiliana na hii hali.
Mnafurahia kutumia mikaaa mnaona haiwahusu ndio matokeo yake hayo, nchi raia hadi viongozi hawana uchungu na uhalibifu mkubwa wa mazingira
 
Back
Top Bottom