Hatua za kukabiliana na joto la Dar es Salaam

Hatua za kukabiliana na joto la Dar es Salaam

Matajiri hawachomwi na jua labda waamue. Gari kiyoyozi ofisi kiyoyozi nyumbani Kiyoyozi jua linamchoma sangapi!!??
Hao masikini mbona wako Dar huko tangu miaka ya 80 wamekufa? Shughuri za nchi hii nyingi ni za kuwa maeneo ya wazi unataka wafanyeje wafunge biashara zao?
 
Tuoteshe miti, faida na nyingi kuliko hasara, kuna nyumba zimejengwa kisasa zimewekwa na paving block chini, paving huongeza joto ni nafuu uweke majani (ukoka)
Mambo ya kuigana mkuu,
 
Kuna wengine wakikaa na feni wanaanza kuumwa kifua, AC majumbani sio kwa asilimia kubwa kutokana na gharama za umeme, cha msingi tuhimizane kuotesha miti, hali inazidi kua mbaya
Tuanze kuchukia mkaaa, nchi hii uharibifu wa mazingira ni wa kutisha mno cha ajabu si viongozi wala raia wanao chukizwa na hili
 
Sema dar tupo tropical area joto ni kawaida Kwa sehemu za ukanda wa pwani watu wa milimani ndio wanafaidi baridi mbeya, iringa,njombe huku sisi tushazoea ila pia inachangiwa na kutokana mwaka Jana dar na nchi NZIMA joto halikuwa kali sana kwaiyo ni watu tu usahaulifu ila hii HALI ya hewa ndio HALI ya HALISI ya dsm ni joto
 
Back
Top Bottom